Wema unalipa

Wema unalipa

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
339
Reaction score
743
Mzee Walter Swords (89), ambaye alikuwa mwanajeshi mstaafu wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alikuwa akila kwenye mgahawa huo kila siku.

Alikuwa na tabia ngumu, akifoka, kutukana, na kutaka chakula chake kiwe cha moto sana. Wafanyakazi wote walimkimbia.

Muhudumu mmoja wa kike aitwaye Melina Salazar, alimvumilia na kumhudumia mzee huyo kwa tabasamu kwa miaka saba.

Alihakikisha anapata chakula chake jinsi alivyotaka, licha ya tabia yake mbaya.

Mzee Walter alifariki mwezi Julai 2007. Kabla ya sikukuu ya Krismasi ya mwaka huo, Melina alishtushwa na taarifa kuwa mzee huyo amemwachia urithi wa dola 50,000 (zaidi ya shilingi milioni 130 za Kitanzania) pamoja na gari lake aina ya Buick (la mwaka 2000) kama shukrani kwa wema wake.
1789392708994.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom