Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,741
- 25,681
SEHEMU YA 01
Nilikuwa bado kijana na umri wangu ulikuwa wastani wa miaka ishirini na mitano. Sikuwa nimepata elimu ya kutosha baada ya wazazi wangu wote wawili kufariki dunia wakati nikiwa mdogo.
Nilianza maisha ya kuhangaika tangu nikiwa mdogo baada ya wazazi wangu hao kufariki dunia. Nilianza kuajiriwa kazi ndogondogo ili nipate pesa za kujikimu na nilipofikia umri wa miaka kumi na minane ndipo nilipopata ajira rasmi.
Ajira yenyewe ni ya kazi ya ulinzi. Niliajiriwa katika kampuni moja ya ulinzi, kazi yangu ikiwa ni kulinda zamu usiku. Kwa vile sikuwahi hata kupitia mafunzo ya mgambo nilifundishwa hapo hapo jinsi ya kutumia bunduki na jinsi ya kukabiliana na wezi na majambazi.
Lindo langu la kwanza lilikuwa katika eneo la Gofu. Unapoingia katika jiji la Tanga eneo hilo unakutana nalo mwanzo mwanzo. Halikuwa eneo la makazi ya watu isipokuwa viwanda vidogo vidogo na maghala ya makampuni mbalimbali.
Wakati wa mchana eneo hilo linakuwa limechangamka kwa sababu kunakuwa na pilikapilika za wafanya kazi lakini ikifika usiku mahali hapo hupooza na kuwa kimya kabisa.
Mimi nilikuwa ninalinda ghala la kampuni moja ambayo wamiliki wake walikuwa ni Waasia. Ghala hilo lilikuwa liko mbali kidogo na maghala mengine na unapoliacha ghala hilo unaelekea katika maghala ya zamani ambayo yalikwa hayatumiki tena.
Nilikuwa ninaingia kazini saa 12 jioni na kutoka saa 12 asubuhi. Kama si dhiki ya kimaisha niliyokuwa nayo nisingekubali kwenda kukesha usiku katika eneo hilo kwani lilikuwa linatisha sana.
Siku za mwanzo mwanzo nilipoanza kazi nilikuwa na hofu na wasiwasi lakini kadiri siku zilivyoendelea hofu ilinipungua.
Nikawa najiambia pengine ni kwa sababu sijaizoea kazi yenyewe ndiyo maana ninapata hofu, lakini nikiizoea hofu itaondoka.
Nilipata mshahara wangu wa kwanza ukanisaidia kununua vitu vidogo vidogo vya chumbani mwangu. Nilikuwa nimepangisha chumba katika eneo la Chumbageni ambalo halikuwa mbali sana na lilipokuwa lindo langu. Ofisi zetu ndizo zilikuwa katikati ya jiji.
Siku moja nilipokuwa katika lindo langu nikirandaranda huku na huku nilimuona msichana mmoja akipita katika barabara iliyokuwa karibu na lile ghala ninalolinda
Nilishituka kwa sababu kwanza ilikuwa ikikaribia kuwa saa nane usiku. Nilijiuliza yule msichana alikuwa anatoka wapi usiku ule?. Pili nilishituka kwa sababu mahali alikokuwa anaelekea hakukuwa na makazi ya watu bali kulikuwa na maghala ya zamani yasiyotumika tena na viwanda vilivyokufa.
Nikasimama na kumuangalia. Kwa vile barabara ilikuwa mbali kidogo, msichana huyo hakuniona au pia inawezekana aliniona lakini hakunijali. Alikuwa akitembea kwa hatua za haraka lakini bila kuonesha kuwa alikuwa na wasiwasi.
Alikuwa amevaa vazi jeupe la aina ya dera lililoficha kabisa miguu yake na alijitanda ushungi mrefu uliofanana na rangi ya dera alilovaa.
Wakati akitembea kulikuwa na mlio wa ko! ko! ko! uliokuwa ukisikika kwenye miguu yake. Nikahisi alikuwa amevaa viatu vya mchuchumio ambavyo vilikuwa vikitoa mlio kila alipopiga hatua.
Kwa vyovyote vile kitendo cha msichana huyo kuwa peke yake usiku huo na akitembea kwa kujiamini bila kuonesha wasiwasi kilionesha ujasiri.
Punde tu akawa amelipita eneo hilo na kupotea kwenye kiza. Hata hivyo niliendelea kuusikia ule mlio wa viatu vyake ko! ko! ko! japokuwa mwenyewe sikuwa nikimuona tena.
Nikawa najiuliza msichana yule alikuwa nani, anakwenda wapi na anatoka wapi. Lakini sikupata jibu.
Usiku wa siku ya pili yake muda kama ule nikaanza kuisikia tena ile sauti ya viatu ko! ko! ko!. Nilipotupa macho barabarani nikamuona yule msichana akitokea kwa mbali. Alikuwa amevaa mavazi yaleyale na akitembea kwa mwendo wake uleule wa harakaharaka lakini bila kuonesha kuwa alikuwa na wasiwasi.
Wakati huo nilikuwa nimeketi kwenye kiti baada ya kuchoka kurandaranda. Nikawa namtazama. Alipita karibu na lile lindo kisha akaendelea na safari yake. Punde tu akapotea kwenye kiza.
“Huyu msichana anakwenda wapi saa hizi?” nikajiuliza.. Hata hivyo kama ilivyokuwa usiku wa jana yake sikupata jibu.
Ilipofika saa 12 asubuhi nilibadilishana lindo na mlinzi mwenzangu, nikarudi nyumbani.
Kama kawaida yangu ya siku zote nilipofika nyumbani nilioga kisha nikalala. Sikuamka hadi saa sita mchana. Nilivaa nguo zangu za kiraia, nikaenda katika mkahawa uliokuwa jirani na nyumba niliyopanga chumba. Nikala ugali na maharage. Nilikuwa natamani nile nyama au samaki lakini uwezo nilikuwa sina..
Kila inapofika saa kumi jioni hununua kabisa chakula ambacho nitakula usiku. Chakula hicho hukiweka kwenye chombo kinachotunza joto. Kwa hiyo ninapokwenda kazini jioni ninakuwa na mfuko wangu wenye chakula changu cha usiku pamoja na chupa ya maji.
Lakini si chupa ya maji safi yanayouzwa madukani bali ni maji ya bomba ambayo huyatia kwenye chupa tena bila kuyachemsha.
Chakula ninachokwenda nacho hukila inapofika saa tatu usiku halafu naendelea na kazi yangu. Sikuwa nikivuta sigara kama ilivyo kwa walinzi wengine ambao huvuta sigara sana usiku kwa sababu ya baridi.
Nilikuwa na koti langu la mvua ambalo hulivaa usiku ili kujikinga na baridi. Ninapovaa koti hilo huwa sisikii baridi.
Tangu nilivyofika katika lindo hilo saa 12 jioni, niliona dalili za kunyesha mvua kwani wingu lilikuwa limejikusanya na kulikuwa na upepo mkali.
Hata hivyo hakukunyesha mvua lakini hali ya hewa haikuwa nzuri.
Ilipofika saa nane usiku nikausikia tena ule mlio wa viatu vya yule msichana, ko! ko! ko!. Nilipotupa macho barabarani nikamuona. Alikuwa amechanganya mwendo kwani matone ya mvua yalikuwa yameanza kuanguka
Msichana huyo alipokuwa karibu na lindo langu, mvua ikaanguka kwa kishindo. Nikamuona anakuja mbio kuelekea kwenye lile ghala kujificha mvua.
Alipofika alipitiliza moja kwa moja hadi karibu na lango la ghala hilo mahali ambapo nilikuwa nimesimama. Mvua ilikuwa hainipati kwa sababu palikuwa pamepauliwa bati.
‘Asalaam alaykum’ akanisalimia.
Nilikuwa Mkristo lakini nilikwishaizoea salamu hiyo ya kiislamu.
Nikamuitikia. ‘Alaykumu salaam’
Alinitupia jicho mara moja tu kisha akauelekeza uso wake chini. Alikuwa amejikunja kwa sababu ya baridi na nguo zake zilikuwa zimetota kwa mvua.
Ingawa alinitazama mara moja tu lakini uso wake niliuona. Alikuwa na pozi la kisomali. Na kama hakuwa msomali alikuwa chotara wa kiarabu. Alikuwa mweupe mwenye nyusi zilizopakwa wanja. Macho yake yalikuwa makubwa yenye mboni za kijivu, pia aliyakoleza wanja mzito na kuwa na mvuto wa kipekee.
Midomo yake alikuwa ameipaka rangi ya waridi. Ilikuwa na papi za ukubwa wa wastani. Alikuwa amevaa mkufu wa dhahabu kwenye shingo yake.
Mara moja eneo hilo likaenea hewa ya manukato ya udi wa mawaridi na manukato ya Al-uud na marashi alivyokuwa amefukiza nguo zake.
‘Hujambo?’ Nilijaribu kumsemesha ili niweze kumuuliza, anatoka wapi na anakwenda wapi.
‘Sijambo’ akanijibu bila kunitazama. Alikuwa akitetemeka kwa baridi iliyompata.
‘Pole sana. Unatoka wapi saa hizi?
ITAENDELEA