Mkasa wa kweli: Kibuyu cheusi

Mkasa wa kweli: Kibuyu cheusi

SEHEMU YA SABA (07)

ILIPOISHIA; “mkazie macho kisha funga ngumi yako ya kushoto”. Sauti ya baba ilisikika ininipa maelekezo kwakua nilikua nimebanwa sikutaka hata kuhoji kwamba ile sauti imetokea wapi, zaidi nilifanya kama nilivoelekezwa.

SASA ENDELEA;Bila kusita nilianza kumkazia macho mzee Yule na kisha kufunga ngumi yangu a kushoto kama nilivyoelekezwa na sauti ya baba, ambabi taratibu nilianza kumuona mzee Yule akianza kutetemeka mdomo kisha naye kijasho chembamba kilianza kumtoka.

Sikuweza kuachia mkono wangu wa kushoto wala sikuacha kumtazama Yule mzee ambapo katika hali nisioitarajia, mzee Yule alidondoka chini na kuanza kutapatapa kama mfa maji au laa kama mtu aliyepandwa na mashetani.

Kisha niliachia mkono wangu wa kushoto na nilirudi nyuma kwa hatua chache kisha nikageuka nyuma ambapo nilikutana na mzee moja mweusi, mwenye macho mekundu yaliyomfanya awe na mwonekano wa kutisha sana.

Mzee Yule alinitazama pia kama alivofanya Yule wa awali ambaye nilifanikiwa kumuangusha chini, kwakua nilishajua jambo la kufanya, sikusita kumkazia macho lakini bado hirizi yangu ilionekana kunibana, kengere ya hatari ilishaanza kulia kwenye kichwa changu kwani tayari nilishaanza kusikia kizunguzungu.

Lakini nilikumbuka kwamba sikufunga ngumi yangu ya kushoto hivyo nilikunja ngumi hio kwa nguvu huku nikimazia macho Yule mzee na safari hii nilimuona nae akizidiwa na mwisho aliishia kufyonya tu na kuondoka huku akiwa ameinamisha kichwa chini.

“mfyuuuu, bahati yako kijana mjinga sana wewe”.

Alisikika akiongea mzee huyo kwa sauti ya kukoroma huku akionesha hasira za wazi za mimi.

Baada ya mzee Yule kuondoka, niliwaona watu watatu nyuma yangu wakininyooshea vidole kisha ilionesha wanazungumza jambo kunihusu.

Sikutaka kabisa shari na mtu, niliaza kuzipiga hatua ili niondoke katika eneo lile la msiba, nilipotazama kwa nyuma niliona watu wanne wakinifuata nyuma ambapo wawili kati ya hao niliwatambua.

Walikua ni wale nilowazidi nguvu Na wengine ambao sikuweza kuwafahamu.

Kengele ya hatari iliweza kulia kwenye kichwa changu ambapo niliogeza mwendo lakini watu hao waliendelea kunifuata, mwisho niliamua kukimbia kabisa na kuvuka barabara kuelekea kwenye mashamba ya mahindi ya kanisa la pentekosti.

Nilichanja mbuga lakini watu hao hawakuonesha hata dalili ya kuchoka kunikimbiza kabisa, na hatimaye tulimaliza shamba la mahindi na tukaanza mashamba ya kahawa yaliyokua yakimilikiwa natajiri wa kizungu.

Lakini watu hao bado hawakuniacha kabisa, na tayari nilishaanza kuchoka.

Nilikaa chini huku nikihema kwa nguvu na jasho lilinitoka sana.

“leo utajuta kuhudhuria msiba ambao uchawi mweusi umehusika kumuua marehemu, vua nguo zako zote kisha uanze kukimbia na urudi ulikotoka”.

Ilikua ni sauti ya baba ambayo ilisikika vilivyo kwenye ngoma za masikio yangu, hakika sikumuelewa hata kidogo baba inakuaje nirudi nilikotoka tena.

“hivi baba ana kusudi gani”.

Nilijiuliza lakini sikua na jibu kabisa, na nilipowatazama wale watu walikua washanikaribia kabisa.

Haraka nilivua nguo zangu na kubaki kama nilivozaliwa kisha nikaanza kuchanja mbuga kurudi nilipotoka, hakika nilishangaa sana baada ya kupishana na wale watu ambao walikua wakielekea mahali nilipotoka.

Nilifika mbali na kugeuka nyuma ambapo niliwaona wakiwa wamesimama kwenye eneo ambalo nilivulia nguo zangu

Nilicheka kimoyomoyo na kisha kuendelea na safari nilikatiza barabarani bila kuangalia pande zote mbili , kwenye moja ya vijiwe ambavyo madereva bodaboda wanapaki.

Bila kutarajia nilimvamia dereva aliyekua akikatiza mahala pale name sikujali niliendelea na safari yangu lakini kishindo kikubwa ndicho kilichonishitua na kunifanya nigeuke nyuma.

Sikuamini macho yangu baada ya kushuhudia ajali kubwa sana ambapo dereva Yule alikufa hapo hapo.

Hilo sikulijali japo moyo uliniuma sana, kwakua bado palikua na umbali mrefu kutoka kijiji cha igamba hadi kijiji cha msia, niliongeza mwendo hadi niliporudi nyumbani majira ya saa moja usiku nikiwa nimechoka sana.

Nilifika na kumkuta baba sebleni ambaye alinikata jicho la hasira
sana mimi sikujali nilimsalimu na kupitiliza chumbani.

“justice hebu njoo sebleni hapa”. Nilisikia kuitwa nami sikua na pingamizi nilitoka na kuketi sebleni ili nisikilize alichoniitia baba

“ulichokitafuta umekipata sasa, wale watu wangekuua”. Aliongea baba na hata sikustuka kwani nilijua dhahiri wale watu walitaka kuniua lakini sikujua ni kwanini.

Ni kama baba alijua swali nililokua najiuliza moyoni.

“kosa ulilolifanya ni kuhudhuria msibani, ilhali uchawi wao na uchawi wetu vinapingana”.

Baba alianza kuongea vitu kwa mapana zaidi na kunifanya niwe makini pia siuacha kumhoji pale ambapo nilionesha kutoelewa.

“hii inakuaje sasa”. Nilihoji

“asia anatumia uchawi mweusi ambao kazi yake ni kuua na kuwafanya watu waishi maisha magumu milele ambao huuu hutumiwa na mataifa kama kongo Malawi na mataifa ya maghaibi”.

Aliongea baba kwa kirefu sana na kufanya nibaki mdomo wazi.

“uchawi wetu unapatikana unatumika sana na mataifa ya afrika ya kati, Nigeria, Ghana, na mali. Kamwe hutakiwi kuhudhuria msiba wowote ambao mchawi mweusi amehusika”.

“umenielewa?” aliongea baba.

“ndio baba nimekuelewa”. Nilijibu

“unajua nini hatma ya dereva bodaboda uliyemgonga? Amekufa na umefanya kosa kubwa sana, na adhabu zake ni kali sana, leo usiku utajua tu. Ila kaa ukijua mkuu amekasirishwa na kitendo chako cha kwenda msibani”.

Je nini kilifuata
 
SEHEMU YA NANE (08)

ILIPOISHIA; “unajua nini hatma ya dereva bodaboda uliyemgonga? Amekufa na umefanya kosa kubwa sana, na adhabu zake ni kali sana, leo usiku utajua tu. Ila kaa ukijua mkuu amekasirishwa na kitendo chako cha kwenda msibani”.

SASA ENDELEA; moyo wangu ulipasuka kama risasi ambayo ilimlenga mtu ikamkosa

Paaaaaaah!

Maana maneno ya baba yalikua ni makali mno na yalinitisha hakika, moyo wangu haukuweza kutulia kabisa mapigo ya moyo wangu yalienda mbio sana.

Hapo nilianza kujilaumu sana kwa uamuzi wangu wa kwenda msibani bila ruhusa na pasina kujua namna ya kuzitumia nguvu zangu. Akili yangu likua kwenye adhabu ambayo nilitakiwa kupewa siku hiyo.

Niliinuka nikiwa mnyonge kabisa kisha nikachukua maji na kwenda bafuni ambapo nilifika na kujipaka sabuni mwili mzima kisha kujimwagia maji yote yaliyokua kwenye ndoo, nilifanya hivyo kwa sababu ya kuhofia ubaridi wa maji.

Nilifungua macho yangu na kutazama chini ambapo nilipigwa na butwaa na ilinilazimu nifikiche macho yangu kwani niliona kama mawenge tu!

Lakini suala la kufikicha macho yangu halikubadili chochote kile, damu iliyotapakaa ndani ya bafu lile ilikua vile vile.

Hakika hali hii ilinishangaza sana, kwani sikuwahi kuona maji yakigeuka kuwa damu zaidi ya kusikia mambo hayo kwenye misaafu na vitabu vya dini juu ya watawala waliokua wakaidi.

Nilitoka na taulo langu na kumwambia baba juu ya jambo hilo ambapo aliniambia nimfuate ambapo yeye alienda chumbani na kisha kurudi na funguo za chumba chake maalumu kwaajili ya tiba zake na mambo yake ya kiganga.

Baada ya hapo tuliingia na kisha akanipaka unga mweusi kwenye paji langu la uso, kisha akatoa majani makavu yaliyokua kwenye kontena na kuniambia niyatafune kisha mate nikayateme kwenye maji ya kuoga.

Hakika mwenye kuweza kuvumilia uchungu wa majani yale ni Yule mwenye shida ambazo zimemfika hadi shingoni bado tu kuzitapika.

Nilitamani kuyatema majani yale kabla hata sijafika huko bafuni, na kwa bahati nzuri nilikuta maji hii iliniepushia kazi ya kuvuta kisimani.

Haraka niliyaweka maji yale kwenye ndoo ya kugoea na kisha haraka nilienda bafuni kisha kutema mate yaliyokua na dawa kwenye maji ya kuogea.

Hali ya ukavu ghafla ndiyo iliyonishangaza sana kwani bafu lilikua kavu kana kwamba halijatumika siku nzima wakati ni mudda mfupi nimetoka kuoga.

“ina maana niilioga hewa ama”. Nilijihoji swali hilo ambalo halikua na mtu wa kunijibu hhivyo niliamua kuendelea kuoga tu kisha nilipomaliza nilienda moja kwa moja chumbani na kuvaa nguo zangu.

Nilipotoka nilikuta chakula kiko tayari na walikua wakinisubiri mimi tu maana mboga ilikua kidogo siku hiyo.

Tulikaa na tulijumuika pamoja kupata chakula kisha kila mtu alienda kupumzika.

Majira ya saa nane usiku nilishushwa na hali ya ubaridi ulioambatana na upepo mkali ambao ulifanya nywele zangu zisimame.

“justiceee, amkaaaaa!”.

“justice mkaaaaa”. Sauti ile ya kunong’ona ilijirudia mara nyingi na ghafla usingizi mkali ulinipitia kisha nilijikuta tayari nipo kwenye eneo ambalo nililikumbuka vema sana, wachawi wengine walikua wakitua mmoja mmoja na mwisho nilimuona mzee ambaye aliniapisha kuwa mchawi siku ya jana.

Uso wake haukua na furaha na nilijua dhahiri ni kwasababu ya makosa yangu kwani baba alishaniambia kila kitu.

“okaaa,bandugu”. Mzee huyo alisalimia kwa lugha ambayo sikuifahamu wala sikuwahi kuisikia mahali popote

“okaaaaa, baba gwetu mukulu”. Watu wote walijibu kwa unyenyekevu mkubwa sana, waliinamisha vichwa vyao mpaka mzee huyo alipochezesha usinga wake kuashiria wainuke.

Baaada ya hapo moto mkali uliwaka na kisha ngoma zilianza kuchezwa kwa dakika kadhaa huku nyimbo zikiimbwa kwa furaha sana mpaka mzee huyo alipoamuru ngoma zizimwe ambapo wachawi wote walitii.

Ndugu kama kuna watu wana heshima na wanatii sheria duniani basi ni wachawi tambua hilo.

Mzeee Yule aliguna kama ishara ya kuweka koo lake sawa kabla ya kuanza kuzungumza

“mwanachama wetu mpya, amefanya makosa makubwa sana, na kwa hili mizimu imekasirika na inahitaji sadaka ya damu kwaajili ya kupunguza hasira na gadhabu
yao”.

Hakika nilistaajabu sana kwa ni stori za uchawi nilizokua nikizisikia kabla ni tofauti kabisa na ninachokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu.

Baaada ya hapo walikuja kina mama wawili ambao nilikua nikiwafahamu kabisa, walikua wamebeba maiti mbili za watoto wachanga.

Kilka mtu alishangilia kwani damu ya watoto wachanga zilikua zikipendwa na kila mtu hata mizimu pia inapenda sana.

Baada ya hapo tulikula nyama na kisha mkutano ukavunjwa hapo hapo na kila watu walitawanjika kwenda makwao.

Kwakua muda ulikua bado kwani hatukukaa sana siku hio, baba aliniambia anahitaji kunifundisha jinsi ya kutega mitego ya ajali kwani ninahitajika kuwa mchawi aliyekomaa, na pia alinisisitiza kuwa makini sana na nisirudie makosa.

Pia baba alinomba radhi kwa kosa la kutonielekeza jinsi ya kutumia nguvu pamoja na mambo mengine kuhusu uchawi.

Nilimwelewa sana baba kwani alikua akinielekeza kwa upole wa hali ya juu kisha nilifunga macho na ghafla nilijikuta eneo lingine ambalo sikulitambua lakini ilikua ni katikati ya barabara ya lami.

“huu ni msitu wa karasha, tunatakiwa kutengeneza ajali hapa”.

Aliongea baba kisha aliniambia nimfuate na safari yetu ilikomea mndani ya msitu huo.

“umeona huu mti? Uchimbe na utafute mizizi mitano Kisha utahamia kwenye mti mwingine na kuchimba mizizi miwili”.

Aliongea baba huku akinisisitiza kuchimba kwa kutumia mkono wangu wa kushoto.

Baada ya kumaliza kazi hiyo ya kuchimba mizizi baba alinielekza kuifunga mizizi mitatu kwa kamba maalum kisha mizizi mitatu mingine niliifunga kwa kamba maalum pia.

Maelekezo hayo niliyapata kwa baba ambaye alinipa maelekezo name nilifanya kama nilivoagizwa.

Baada ya hapo baba aliniambia niende upande wa pili wa barabara kisha ni weke mizizi nilioifunga kwenye oande mbili za barabara na mmoja ninuie ajali.

Baada ya muda nilianza kusikia ngurumo za gari kisha baba aliniamuru nikitupe barabarani kijiti nilichokishika.

Kishindo kikubwa kilisikika

itaendelea
 
SEHEMU YA TISA (09)

ILIPOISHIA; Baada ya muda nilianza kusikia ngurumo za gari kisha baba aliniamuru nikitupe barabarani kijiti nilichokishika.
Kishindo kikubwa kilisikika

SASA ENDELEA; “kazi nzuri kijana wangu, nenda ukachukue maiti ya mtoto ndani ya gari”. Aliongea baba na nilimsikia barabara japo yeye alikua msituni mbali kabisa na eneo la barabara, name sikusita na kwenda moja kwa moja mahali gari dogo lilipoangukia.
Hakika nilishangaa kukuta watu wengi sana eneo lile, lakini nilichogundua wengi hawakua viumbe wa kawaida walikua viumbe wa ajabu ajabu tu wenye sura zilizotisha na miguu yao ilikua na kwato za punda na wanyama wengine wenye miguuu mine.
Niliwaona wakikazana kuzoa viiugo vya watu waliopata ajali siku hio, wengi walikua wakigombania mifupa na wengine wakilamba damu zilizotapakaa chini.
“uma meno yako ili uwatishe viumbe hao, wakupishe hapo”. Aliongea baba name nilifanya hivyo na nilishangaa kuona viumbe wale wakitokomea msituni, baada ya kuuma meno yangu.

Taratiu nilizipiga hatua zangu na kulisogelea gari lile lililokua limeharibika kabisa, ambapo nilifungua mlango na kisha kutoka na maiti ya mtoto aliyekua na umri kati ya miaka mitano hadi saba hivi.
Pumzi zake zilikua zikielekea ukingoni kwani alikua akihema kwa taabu sana, na pumzi zake na mapigo yake ya moyo havikusikika tena.
Nilifika msituni alipo baba ambaye alinipongeza sana kwa kazi niliyoifanya.

“natumai mkuuu atafurahishwa sana na kazi uliyoifanya”. Aliongea baba na kisha aliniamuru niuweke mwili wa mtoto Yule chini ambao ulikua ni mwepesi sana.
Baada ya kufanya hivyo baba alichora duara kutuzunguka na kisha aliamuru nikae na kisha nifumbe macho yangu.
Baada ya sekunde chache nilisikia sauti ya baba ikiniamuru nifungue macho ambapo nilijikuta sehemu nyingine kabisa ambayo ilikua na joto sana, na si joto tu bali kulikua na moto mkali ambao uliwaka na kufanya eneo lile liwe na rangi nyekundu pekee kama gongo la mboto kipindi cha mabomu.
Mikononi mwangu ulikuwepo mwili wa mtoto Yule na mbele yangu alikuwepo baba ambaye alikua akiniongoza name nilimfuata nyuma hadi tulipofika sehemu moja ambayo ilikua na kiti cheusi tii!
Mandhari ya eneo lile ilitisha kwa kweli. Na laliti kamasiku umelala na ukaamka ukajikuta katika eneo hilo basi tambua kwa,mba utakufa kwa presha kama si joto la mahali pale.

Ghafla ulitokea mwanga mweupe kisha kilitokea kiumbe cha ajabu ambacho sikuweza kukitazama mara mbili lakini kwa haraka nilivokiangalia kiumbe kile, kilikua na jicho moja jekundu kwenye paji la uso pia ngozi ngumu na mkia mrefu
“mkuu amenituma nipokee sadaka yenu, na pia amesisitiza kwamba kijana asirudie tena kosa alililifanya”.
Aliongea kiumbe Yule kwa sauti ya kukoroma ambayo ilijirudia mara mbili
“piga magoti kisha fumba macho yako”. Aliongea kiumbe Yule ambapo niltii wakati huo baba alikua kimya tu akiangalia picha linaloendelea kati yangu na yule kiumbe.
Nilipiga magoti na kufunga macho, kisha nikafungua macho yangu kama nilivoelekezwa.
Lakini nilishangaa kujikuta eneo lingine kabisa ambali lilikua jekundu kama volcano, huku baba akiwa pembeni yangu na Yule kiumbe mwenye jicho moja akiwa mbele yetu lakini yeye alikua hakanyagi chini, kama sisi bali alikua anapaa kama ndege.

“miimi ni malaika wa adhabu kuzimu, nataka kukuonesha yatakayokukuta pindi ukikosea sheria”.
Aliongea kiumbe Yule kauli ambayo ilinifanya nijute kuwa mchawi kabisa, lakini ni kama aliingia kwenye mawazo yangu na kugundua ninachokiwaza.
“usijute, shetani sio mbaya kama utafuata sheria zake”. Aliongea kiumbe Yule na kutoa kicheko cha kutisha na kuufanya moyo wangu ushituke sana.
Baada ya kutembea kwa muda mfupi tulifika eneo ambalo lilikua linatisha sana, hakuna kilichosikika zaidi ya kelele za watu waliokua wakiungua na moto lakini hawateketei, tena moto wa safari hii ulikua ni mkali mithiri ya bomu la nyuklia.
Hakika niliogopa sana na nilijikuta nikihema kwa kasi na nilitamani tuondoke hapo hapo
“omba ukutane na mimi kwenye adhabu ila sio hao wengine sita waliobaki, naitwa uchochoro na kwa l eo umesamehewa adhabu yako ila siku nyingine usirudie, ziara yetu inaishia hapa kwaheri”.
Aliongea kiumbe Yule aliyejitambulisha kwa jina la uchochoro na kisha kupotea ghafa tu

Nilikuja kuzinduka majira ya asubuhi kukiwa kumekucha kabisa na jua la asubuhi lilikua likiwaka.
Kwakua ilikua siku ya jumapili sikumkuta mama, alikua kashaenda ibadani na alikua anakaribia kurudi.
Mooyo wangu uliiuma sana na nilijikuta nikitamani kujua hatma ya kijana Yule ambaye nilimtegea mtego wa ajali na siku hio nilipanga kwa namna yoyote ile niende kwenye mazishi na si msibani kwani nilitambua kwamba hilo lilikua kosa kubwa sana.

Baada ya kufanya shughuli zangu ikiwemo usafi binafsi nilimuaga baba kuwa ninakwenda kwa rafiki yangu katika kijiji kingine cha igamba.
Baba aliniruhusu na kunisihi nisitumie nguvu zangu vibaya kuwanyanyasa watu, ni kama alijua lengo langu kwani sikua na rngo la kwenda kwa rafiki yangu bali hata kidogo.
Lengo langu lilikua ni kwenda karasha ambako ndiko ajali ilipotokea, nilitoka nyumbani vizuri na kisha nilipofika mbali na nyumbani niliingia pembeni ya msitu na kisha nikapotea na ndani ya dakika moja nilikua karasha vijiweni ambapo nilifika na kwenda kwenje duka moja kubwa lililopo maeneo yale
Nilipofika niliulizia maji kwani jua lilikua linawaka sana
“hakuna maji hapa kwanza ondoka”. Aliongea mzee Yule na kunifanya nishangae sana kwani niliyaona maji mengi tu kwenye shelve za duka lake.
hirizi yangu ilinibana na kunai taarifa kwamba nilikua nimesimama na mtu ambaye hana nia nzuri na mimi na nilipomuangalia mzee Yule alikua amekunja ngumi yake ya kushoto na alipojua nimemgundua aliishi kusonya tu kisha kuondoka.
Nami nilicheka na kisha nikamuuliza dereva mmoja wa boda boda mahali ajali ilipotokea ambapo alinijibu
“ni hapo tu dogo unataka nikupeleke?”
“hapana kaka ntafika tu sina pesa”. Nilijibu na kisha kuondoka
Nilitembea taratibu na kwa mbali nilianza kuona watu wakiwa wamejikusanya na nilijua lazima tu itakua ndo hapo
“ila watu wana roho mbaya jamani, mtoto Yule alikua na heshima sana tena amekufa mdogo sana”. Alisikika mama mmoja akizungumza
“tena ni bora walivokufa wote tu maana lingekua pigo kubwa sana”. Aliongea mwanamama mwingine lakini nilisikia kelele upande wa nyuma ya mwana dada aliyekua amepandisha mashetani.
Kisha hirizi ilinibana na jasho kuanza kunitoka

itaendelea
 
SEHEMU YA KUMI (10)

ILIPOISHIA“tena ni bora walivokufa wote tu maana lingekua pigo kubwa sana”. Aliongea mwanamama mwingine lakini nilisikia kelele upande wa nyuma ya mwana dada aliyekua amepandisha mashetani.
Kisha hirizi ilinibana na jasho kuanza kunitoka

SASA ENDELEA; tayari nilishahisi jambo ja hatari linakwenda kutokea na nilijua dhahiri kuna mtu ananipima na lengo lake ni kuniumbua kwani kwa siku chache tangu nimekua mchawi nimegundua kwamba uchawi ni mchezo mchafu tena wa kuumbuana.

Hakuna mchawi atakaekusaidia pindi uwapo na matatizo labda awe mzazi wako au mtu anaekujua au huenda ndiye aliyekufanya uwe mchawi, mbali na hapo kila mtu ataubeba msalaba wake.
Niligeuka na kumuona mzee mmoja akinitazama huku amebana vidole vyake, safari hii hirizi yangu ilizidi ilibana kwa nguvu sana na hio ni ishara mbaya sana kwa mchawi na hio inaashiria kwamba mtu unayeshindana nae ana nguvu nyingi zaidi yako.

“mkazie macho, kisha bana vidole vyako alafu kunja ulimi wako kurudi nyuma”. Sauti ya baba ilisikika ikinielekeza namna ya kufanya name sikusita nilifanya kama baba alivonipa maelekezo na nilishangaa mzee Yule akianza kujikuna mwili mzima kisha akaanza kukimbia kama kichaa kuelekea ndani ya msitu wa karasha nami sikumjali zaidi nilendelea na safari yangu hadi nilipofika eneo la tukio ambapo nilisababisha ajali usiku wa kuamkia siku hiyo.

Nikiwa katika eneo hilo nilipata ushawishi wa kwenda kwenye msiba lakini nilipokumbuka vitisho vya Yule kiumbe niliyekutana nae kuzimu nilipata uoga ghafla na kuamua kusitisha zoezi langu kwakua nilisharidhika niliamua kuondoka eneo lile lenye ambalo asilimia kubwa ya watu waliokueppo pale ni wachawi sema wanatofautiana uwezo.

Sikutaka kurudi na barabara kuu huku nikihofia kupimwa na wachawi wenzangu kama wasemavyo wahenga kwamba;
“waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba”.
Vivyo hivyo wachawi nao hujuana kwa hirizi
Taratibu nilianza kuzipiga hatua zangu kuelekea msituni huku nikiacha mjadala mkubwa sana kwa watu waliokuwepo nyuma.
“huyu kijana ni mchawi na anajiamini sana”. Aliongea mzee mmoja akijadili na wenzake
“eee tena amevamia anga ila ana nguvu sana, mzee simbeye alitaka kumpima na amezidiwa nguvu sijui nini hatma yake mzee wetu”. Aliongea mzee mwingine na kufanya muda uzidi kusogea pasipo mzee simbeye kurudi.

“au tumfuate tumchangie nguvu”. Mzee mmoja alitoa wazo ambalo kila mmoja aliliunga mkono kisha wazee watatu walianza safari ya kwenda ndani yam situ wa karasha kwa lengo moja tu!
Kuhakikisha wananikamata.

Hirizi yangu iliweza kunipa taarifa kwamba kuna hatari mbele yangu kisha nikasikia sauti ya baba ikiniambia nikimbie bila kugeuka nyuma hadi nitakapoikuta reli kisha nivue viatu vyangu na kuokota kokoto kisha kuirusha nilikotoka.
Haraka nilianza kukimbia hadi nilipotokezea kwenye uwanja wa mpira wa miguu
“kimbia haraka kabla hawajatuma bomu la kichawi likupige kwani hapo upo kwenye uwanja wao wa mikutano”.
Sauti ya baba ilisikika ikinihimiza name niliendelea kutimua mbio kama fisi wanaogombania mfupa, kabla sijaumaliza uwanja huo nilishangazwa na hali ya kuchoka ghafla kisha tumbo liliniuma sana lakni sikuacha kukimbia na hahtimaye nilifanikiwa kuikuta reli na kisha nilifanya kama nilivoagizwa na baba.
Nilichukua moja ya jiwe lililokua reline kisha nikalitupa kama nilivoelekezwa.

Hakuna kulichosikika zaidi ya kishindo kikubwa sana kikifuatiwa na moshi mweusi ambao ulipelekea eneo lile kuwa na wingu la ghafla kisha mvua kubwa yenye kuambatana na ngurumo za radi ilianza kunyesha.

Nilikaa nikiwa nimeduwaa tu na nisijue kitu cha kufanya zaidi nilimsubiri baba anipe maelekezo lakini hadi mvua inakata ukimya wa hali ya juu ulitawala sikupata kusikia neno lolote toka kwa baba hali iliyonifanya nijiongeze.

Nilivaa viatu vyangu na kisha kusogea pembeni kidogo ya reli ambapo nilichora duara kisha kuketi ndani ya duara hilo.
Baada ya hapo nilifunga machu yangu na baada ya sekunde kadhaa nilitua ndani ya msitu uliokua nyuma ya nyumba yetu.
Kisha taratibu nilianza kuzipiga hatua zangu kuelek ea nyumbani ambapo nilikuta mama amesharudi lakini baba sikumuona.
Nilimsalimu mama na kuingia ndani ambapo pia sikumuona baba lakini harufu kali ya udi ilitosha vema kutambua kwamba baba alikua kwenye chumba chake maalum kwa shughuli zake za kitaalamu.

Nilipitiliza moja kwa moja chumbani ambapo nilikaa kitandani kisha usingizi ulinipitia kwani nilichoka sana na safari ya kwenda karasha.

“unajifanya kimbelembele eeeh, sasa nitakunyoosha mimi ndo asia binti wa mwashilindi mfyuuu”.
Alisonya asia kwa hasira sana huku machozi ya damu yakimtiririrka.
Macho yake yalikua yakifanana nap aka na kumfanya awe na muonekano wa kutisha.

“ghafla alikuja baba akiwa na mkuki unaowaka moto ambapo aliusimika chini kisha akachukua usinga wake na kunikabidhi huku akiniambia maneno ya kishujaa

“mwanangu pambana, usikate tama utampiga tu huyu asia”. Aliongea baba kisha kicheko kikali kikafuata kutoka kwa asia.

“ndivyo mnavodanganyana na baba yako kwamba mtaweza nipiga mimi? Hilo msahau na sio muda mrefu nitakwenda kuwa mchawi ninaetikisa dunia”.
Aliongea asia kwa majigambo.
Maneno ya asia yalimchukiza mno baba ambapo aliuchukua usinga wake na kuurusha kama anarusha jiwe, moto mkali ulitokea kama kombora na kwenda kumpiga asia kwenye mguu wake ambapo alianguka chini.
Kisha akainuka na kurusha kombora ambalo almanusura linipige kisha baba akanikinga kwa kutumia mkuki wake.

Nilishtuka ghafla na kumkuta baba akiwa pembeni yangu huku jasho jingi likiwa linanitoka mwilini
“pole mwanangu, na ndoto mbaya”. Alongea baba na kunifanya nishushe pumzi ndefu kisha kumtazama usoni kabla ya kumjibu huku kichwani nikiwa na maswali mengi sana
Nilikaa kitako na kumtazama baba usoni kwa uso wa maswali mengi sana.

Je nini kilifuata?
Toa maoni yako mdau
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)

ILIPOISHIA; Nilishtuka ghafla na kumkuta baba akiwa pembeni yangu huku jasho jingi likiwa linanitoka mwilini
“pole mwanangu, na ndoto mbaya”. Aliongea baba na kunifanya nishushe pumzi ndefu kisha kumtazama usoni kabla ya kumjibu huku kichwani nikiwa na maswali mengi sana
Nilikaa kitako na kumtazama baba usoni kwa uso wa maswali mengi sana.

SASA ENDELEA; “vita ndiyo imeanza, jitahidi usitumie nguvu zako vibaya usiwanyanyase watu wala usiwe na kiburi kwani nguvu huisha taratibu na kufanya mwisho wa siku ufedheheke, na hakuna mtu yeyote atakaekua upande wako hata mimi sitakuepo kwenye fedheha yako na wewe kuwepo kwenye fedheha yangu”.
Aliongea baba jambo ambalo nililiona ni la msingi sana katika maisha yangu, sipaswi kumdharau mtu eti kwa sababu nina jicho la tatu, au eti kisa nimemzidi uwezo.

“tumefanikiwa kumdondosha asia lakini hajaridhika na ameenda kujipanga kwaajili ya kisasi, hivyo basi leo nitakuelekeza namna ya kupigana kutumia nguvu za giza”.
Alionga baba na kunifanya nishushe pumzi ndefu kisha kuamka na kwenda sebleni ambapo niilimkuta mama akiwa anamalizia kuandaa chakula cha usiku.

Baada ya hapo tulipata chakula kisha nilikwenda chumbani na kwenda kulala, lakini baba nilimuacha akiwa anafungua chumba chake cha dawa kisha harufi kali ya udi ilisikika na kunifanya nipate kizunguzungu kikali sana ambacho kilinipelekea nipoteze fahamu zangu na baada ya hapo nilijiona kama napaa hewani huku baridi kali ikinicharaza.

Mbele yangu nilimuona baba aliyekua amevalia kanzu nyeupe na kilemba cheusi kuku akiwa amevaa skafu nyekundu, hakika alikua na mwonekano wa kutisha sana mboni za macho yake zilikua nyeusi tii! Hakika alitisha sana baba.
Nilistuka na kujikuta nikiwa katikati ya msitu ambao sikujua ni sehemu gani, baba alinipa kitambaa cheusi na chekundu na kuniamuru nijifunge kama yeye lakini nilitikisa kichwa kuashiria siwezi kujifunga kwani nilishapewa onyo kwamba sitakiwi kuongea jambo lolote mpaka nitakapo ruhusiwa

Baba alisogea na kunifunga kisha akanipa tunguri kubwa nyeusi kisha akanipa ishara nimfuatishe atakachokifanya name nilikua makini na nilihakikisha hakuna hatua inanipita.

Baba aliinama na kisha kupiga magoti akianza na goti la kushoto name nilifanya hivyo kisha baba alitanua mikono yake na kutazama juu angani huku tunguri yake akiwa ameishika kwa mkono wake wa kushoto nami nilifanya hivyo ghafla wingu kubwa lilitanda na kufanya mbalamwezi iliyokua ikituangazia ipotee kisha kiza kikali kilitanda na mvua kubwa ilianza kunyesha ikiambatana na ngurumo za radi kisha nilishangaa kujiona nikipaa tena na mbele yangu walikua kina mama wawili waliovaa kaniki nyeusi,

Baba alinipa maelekezo jinsi ya kufanya
“hao ni wachi kutoka jamii ya uchawi mweusi, wamekuja kupima nguvu zao, jitahidi uwashinde la sivyo utashindwa kurudi nyumbani na tutakuzika na utishi kama mzimu na itakuchukua miaka miasita kurudi tena ulimwenguni”.
Aliongea baba maneno yaliyonifanya niogope sana, hofu na woga viliitanda nafsi yangu
Ghafla nilishangaa kuona kombora la moto likija upande wangu toka kwa kina mama wale
“jikinge na kibuyu kisha puliza itatokea barafu na kuuzima moto huo”. Nilisikia maelekezo toka kwa baba kabla ya kombora kunifikia amba[o nilifanya kama nilivoelekezwa kisha nilishangaa moto ule ukizima kabla hata ya kunifikia.

Vicheko vikali kutoka kwa kinamama wale vilisikina na ghafla walikuja kunguru wengi walitokea kusikojulikana na kuja uoande wangu kisha nyuma niliona kombora la moto.

“mimina maji toka kwenye kibuyu kisha yarushe kuelekea upaande wao”. Aliongea baba name nilifanya kama alivonielekeza
Nilishangaa kuona kina mama wale wakiziba macho yao na kuanza kuyafikicha huku kunguru nao wakigeuka na kwenda kuwadonoa wenyewe.

“sasa hapo bado kumaliza kazi tu, rusha kibuyu hicho kitaenda kuwagonga na kisha kurudi kwako, hapo unaweza kuwaamuru kila kitu unachokitaka”.

Aliongea baba ambapo nilifanya vivyo hivyo ambapo nilishangaa kibuyu kikirudi na kina mama wale kisha nilijikuta nipo chini kweny e ozi lile lile la kupiga magoti huku mbele yangu wakiwepo kina mama wale ambapo walikua kama mazezeta

“kazi kwako kuwaamuru, na hawa adhabu yao huwa ni kuogelea kwenye bwawa la mbozi mission, baridi iwapige hadi wafe”.

Aliongea baba na kisha kuchora duara kutuzunguka ambapo ghafla tulijikuta tuko pembezoni ya bwawa kubwa linalotegemewa na vijiji viwili igamba na mbozi.

“haya ingieni bwawani”. Niliongea ambapo kina mama wale walitii na walianza kuzipiga hatua kuelekea bwawani, tulisubiri hadi makelele ya kutapatapa yalipoisha kisha tuliondoka na kwenda moja kwa moja kwenye makaburi ya msia.

“huku tumekuja kufanyeje”. Nilihoji
“Yule bodaboda uliyesababisha kifo chake, maiti yake inatakiwa itolewe kafara na iliwe nyama siku ya leo, cha kufanya wewe utalala juu ya kaburi kisha nitakuelekeza jambo la kufanya”.
Aliongea baba name nilitii japo niligopa sana.

Baada ya kulala juu ya kaburi, baba alianza kuongea maneno ambayo sikuyaelewa, ghafla lilitokea shimo kubwa na kisha jeneza lilipanda juu na kisha kujifungua.
Baada ya hapo marehemu alitoka ndani ya jeneza na kuanza kunikata jicho kali sana, kisha alianza kuzipiga hatua kunisogelea huku macho yake yakiwaka moto.
Nilimfuata baba na kumshika kanzu yake nyeupe.
Kisha nishashituka kutoka ndotoni huku nikihema kwa nguvu sana na jasho likinitoka.

Nilipoangalia saa ilikua ni saa nane usiku hakina niliona kama hapakuchi kabisa, kisha nikalivuta blanketi langu na kujifunika gubigubi na baada ya muda usingizi ulinipitia na nilijikuta nipo katika uwanja wa shule ya sekondari wasa lakini ajabu baba hakuwepo.

Je nini kilifuata
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12)

ILIPOISHIA; Nilipoangalia saa ilikua ni saa nane usiku hakiKa niliona kama hapakuchi kabisa, kisha nikalivuta blanketi langu na kujifunika gubigubi na baada ya muda usingizi ulinipitia na nilijikuta nipo katika uwanja wa shule ya sekondari wasa lakini ajabu baba hakuwepo.

SASA ENDELEA;nilikuwepo mkutanoni na sikujua baba yuko wapi kwa wakati huo, huku hofu ikinitanda lakini nilipiga moyo konde na kuendelea kusikiliza kinachoendelea, ambapo baada ya muda alikuja mkuu ambapo wote tulipiga maguti na kusalimia kwa heshima huku tumeinamisha vichwa vyetu chini mpaka mzee huyo ambaye ndiye mkuu wa wachawi kwa ukanda wetu alipoturuhusu kuinuka.

“twambombo,vana vangu”. Aliongea mzee huyo kwa lugha ya kikabila
“twinza, baba gwetu”. (salama baba yetu) watu wote waliitikia salamu hio isipokua mimi ambaye nilikua sielewi vizuri hio lugha ya kilozi.

Baada ya salamu hio mzee huyo alikohoa kidogo kisha kuanza kuongea mambo mengi kuhusu uchawi na kuhusu chama chetu cha uchawi lakini ni kama alikua hawzi Kiswahili vizuri hivyo mambo mengi yalikua yakinipita kutokana na kuwa yakizungumzwa kwa lugha ya kikabila.

Akili yangu iliwaza hali ya baba kwa wakati huo kwani machale yalinicheza muda wote moyo wangu ulikua unaniuma sana hapo ndipo nilianza kukumbuka maneno ya baba ambayo alitoka kuniambia siku muda mfupi uliopita.

“vita ndiyo imeanza, jitahidi usitumie nguvu zako vibaya usiwanyanyase watu wala usiwe na kiburi kwani nguvu huisha taratibu na kufanya mwisho wa siku ufedheheke, na hakuna mtu yeyote atakaekua upande wako hata mimi sitakuepo kwenye fedheha yako na wewe kuwepo kwenye fedheha yangu”.

Sasa nilianza kuona kwamba maneno ya baba yakianza kutimia kwani mkuu alifunga mkutano pasipo kuzungumza jambo lolote kuhusu baba, zaidi alinipongeza kwa kafara niliyoitoa na aliniambia kwamba mizimu imefurahi sana na imeniambia nichague kitu kimoja kati ya utajiri na kuongezewa nguvu.

“sikua na yeyote wa kunishauri na mzee huyo alihitaji majibu muda huo huo, lakini kwakua nilishasikia jinsi utajiri wa kichawi ulivyo na mashariti magumu basi niliamua kuchagua nguvu”.

“kazi nzuri kijana, mizimu itakupa nguvu zaidi na utakua na uwezo wa kuona yaliyojificha kadha wa kadha”.
Aliongea mzee huyo kisha alishoosha usinga wake juu ambapo radi zilitokea kisha usinga huo akaugusisha kifuani kwangu ambapo ghafla nilianza kutetemeka, mikono na miguu vilikosa nguvu na kupelekea pia macho yangu kukosa nuru kisha nilipoteza fahamu.

Nilikuja kuzinduka nikiwa nyumbani majira ya saa kumi na moja alfajiri nikiwa nimechoka sana, moyo wangu uliniuma sana na nilijikuta nikishawishika kuingia kwenye chumba cha baba pasipo mama kujua.
Niliingia na kuukuta mwili wa baba ukiwa wa baridi sana, hakika nilishtuka sana

“ina maana baba ameshakufa?” nilijiuliza swali ambalo hapakua na mtu wa kunijibu na nisijue nini cha kufanya.
“nafsi yake imekwenda mbali sana unahitaji kufanya jitihada kabla wachawi weusi hawajaichukua, na kupelekea baba yako kupoteza maisha”.
Ghafla nilishangaa kusikia nikipewa maelekezo namna ya kufanya, sikutita kuuliza ni nani alikua akinipa maelekezo.

“nyie ni kina nani hadi mmeyajua haya yote”. Nilihoji
“sisi ni mizimu ya simangwa, tumekua tukiishi ndani ya mwili wa baba ako kwa takribani miaka ishirini sasa na tumekua tukimuongoza na kumlinda baba yako. Sasa hivi hatuna kwa kwenda kwa sababu mwili wake hauna uhai”.
Iliongea mizimu hakika nilishangaa sana
“usishangae, una muda mchache tu wa kulikamilisha jambo hili la sivyo utamkosa baba yako”.

Nilbaki nkiwa nimeduwaa tu kwani maneno waliyoniambia yalinitisha mno.
“sasa nifanyeje”. Nilihoji
“fanya tahajudi, ili uirudishe nafsi yake kupitia nafsi yako”. Iliongea mizimu lakini hata hio tahajudi nilikua siijui hivyo ilinielekeza kila kitu

“washa mishumaa kisha ondoa nguo zako na ukae chini kisha unganisha vidole vyako pamoja na miguu alafu angalia juu uwe unavuta pumzi kwa kutumia pua na kutolea mdomoni hadi utakapoona hali ya tofauti ikijitokeza, usishangae hapo ndio uta kua ukihama kwenda ulimwengu mwingine”.

Mizimu ilimaliza kunipa amaelekezo kazi ilibaki kwangu kufanya kama nilivoelekezwa, nilizivuta pumzi zangu kwa muda kama nilivoelekezwa kisha nilianza kuona hali ya ajabu ikinitokea.
Nilikua nimeganda kama barafu kisha nikaanza kujiona nikiwa eneo la makaburi ambalo tulienda na baba usiku wa kuamkia siku hiyo.

Nilifika na kuangaza huku na kule ambapo nilishangaa kumuona asia akiwa na Yule dereva bodaboda ambaye tulienda kwaajili ya kumfukua, kaburi lilikuwa wazi na jeneza lilikua juu kama tulivoliacha siku ya jana.
nilisogea taratibu huku nikinyata na kuwafanya wasiweze kuhisi chochote katika hali ya kushangaza nilimuona baba akitabasamu, nadhani alishatambua ujio wangu mahala pale.

“huyu tunamfukia na unakua ndio mwisho wake, damu yake itanisaidia kujaza kibuyu cheusi”. Yalikua ni maongezi kati ya asia ambayo niliyasikia barabara kabisa lakini sikutaka kuonesha uwepo wangu mahala pale.

“mbona kama nasikia harufu ya udi maeneo haya?”. Aliongea dereva bodaboda ambapo sikutaka kuchelewa, nilimchapa konde la kichwa na kumfany adondokee kaburini kisha kaburi likajifukia moja kwa moja.

Kisha nilimsogelea asia moja kwa moja ambaye alianza kurudi nyuma taratibu huku akitetemeka kwani hakua na nguvu yoyote ya kunizuia.
“leo nimekukamata, utakufa na utafufuka baada ya miaka elf moja au usifufuke kabisa, kwani damu yako nitaiweka kwenye kibuyu cheusi pia kwahio hizo nguvu usahau kuzipata”.
Niliongea kwa kujiamini sana kisha nilinyoosha mkono juu ambapo kilitokea kibuyu cheusi wakati huo asia akiwa ameduwaa kama zezeta ambapo niliweza kumuongoza afanye chochote nitakacho.
“haya jiue mwenyewe, kisha damu yako iweke humu alafu ujizike mwenyewe hapa hapa na kibuyu chako”.
Niliongea ambapo bila kutarajia nilishangaa kuona mvua kubwa ikinyesha kisha asia aliganda kama sanamu.
Kisha ardhi ilijichimba na mwili wa asia ulipotelea chini ya ardhi, nilihamaki kuona pia kibuyu cheusi kikiteketea kwa moto mwisho kilipotea tu kisha mvua iliyokua ikinyesha ilikoma na kukawa shwari kabisa lakini kaburi la asia lilibaki kuwa historia kwani lilikua likionekana usiku pekee na mchana halionekani.
Asia anatazamiwa kurudi baada ya miaka elf moja kwani alikosea mashariti ya uchawi mweusi.

Baada ya hapo nilimshika mkono baba kisha kupotea na ghafla baba alizinduka na kunikuta nikiwa pembeni yake kisha nilimpa pole naye alinipa hongera kwa kufanikisha zoezi la kumteketeza asia kwani alibakiza watu wachache tu ili aweze kuwa mchawi hatari sana.

Ilikua siku ya jumatatu, ambapo sikwenda shule badala yake nilitoka na kwenda mjini kwenye kanisa moja lililopo katika mji mdogo wa mlowo.
Nilifika na kuwaeleza kila kitu na baada ya kumaliza mchungaji aliniombea na niliamua kuachana na uchawi moja kwa moja kwa moyo mweupe.
Haukupita muda mrefu baba nae alitangaza kuachana na uchawi ambapo aliniomba nimpeleke kwenye kanisa nililoenda kupokea wokovu name sikusita nilimpeleka baba ambapo alisalimisha vikorombwezo vyote kisha vikachomwa moto na chungaji peter nyika wa kanisa la presibyterian mlowo.

Baada ya hapo familia yetu ilifungua ukurasa mpya toka maisha ya kichawi hadi maisha ya utakatifu na hatimaye baba na mama waliongeza familia na kufanya tuwe watu watano kwani hata tatizo la ugumba alilokua nalo mama lilipona kutokana na kufunguliwa vifungo vya kichawi.

Nimeandika simulizi hii ili utambue kwamba uchawi upo tena una nguvu sana na asitokee yeyote akakudanganya uchawi haupo lakini mungu ndiye muweza wa yote.

Karibu katika visa vijavyo, kama una mkasa wa kweli unaweza kuanitafuta kwa namba tajwa hapo juu

mwisho
 
Asante kwa simulizi, je n kitu gani mtu anaweza kufanya Ili kuepuka kupata hzo ajali za kichawi?
 
Back
Top Bottom