Mkasa wa kweli: Kibuyu cheusi

Mkasa wa kweli: Kibuyu cheusi

SEHEMU YA TATU (03)

ILIPOISHIA; Nilipokua nikiendelea kuwaza hayo ghafla nilimuona asia akiwa pembeni ya mkuu wa shule akicheka na kumzomea kwa kuweka mikono yake kichwani kisha kuichezesha kama popo na kutoa ulimi kisha kicheko kikali kilifuata nami sikuweza kuvumilia nilizimia papo hapo.

SASA ENDELEA; baba alikuja bila hata kuambiwa, na mambo yote nilikua nayaona lakini sikua na uwezo wa kusema yaani kwa kifupi nilikua kwenye ulimwengu mwingine kabisa ambao niliweza kuona killa jambo linaloendelea lakini sikua na uwezo wa kufanya kuongea jambo lolote.
Nikiwa katika ulimwengu huo nilimuona mwalimu chimota akiwa buheri wa afya tena akiwa amesimama eneo lile lile la shule ambako paredi ya wanafunzi ilikuwepo.
Nilitaka kujaribu kama nina guvu ya kifanya jambo lolote, niliinuka pale nilipolala na kisha nikaanza kuzipiga hatua zangu, lakini nishangazwa na hatua zangu kuwa ndefu sana yaani hatua moja ilikua ni sawa na hatua mia moja za kawaida.
Wazo langu lilikua moja tu, nipate kujua mwili wa mwalimu chimota ulipo ikiwa nafsi yake niliiona mahali tulipokusanyika.
Nilipowaza hivyo tu, ghafla nilijikuta pembeni kidogo ya shule, nyuma ya vyoo vya wasichana na chini ulikuepo mwili wa mwalimu chimota ukiwa unatoa machozi hakika niliona huruma sana name nilijikuta nikidondosha machozi kisha nikawaza kurudi ilipokua paredi ya wanafunzi.
Nilifika na kumkuta baba akiwa kashafika, na tayari niliona kachanganyikiwa kabisa kwani ilionesha nimepoteza maisha.
Hakika nilimuonea huruma sana baba name nilijikuta nikilia katika ulimwengu huo, lakininilishangaa kuona mwili wangu nao ukitoa machozi ambapo baba aliyafuta kupitia kitambaa chake.
Macho yangu yaliangaza huku na kule na hapo nilimuona mwalmu chimota, nililikuta nikimfuata mwalimu chimota lakini kadiri nilipomkaribia ndivyo nae alizidi kunikimbia, name niliongeza mwendo nae aliongeza mwendo vivyo hivyo. Nilipomkaribia nilianza kusikia makelele ya mwalimu chimota akilalamika kwamba anaungua, na nilipojiangalia niliona kweli nilikua nawaka moto.
Nami sikusita kumuamuru arudi kwenye mwili wake na apate kuamka.
Katika hali isiyo ya kawaida mwalimu chimota alitii, na baada ya muda aliinuka akiwa uchi wa mnyama na kuanza safari ya kwenda kwenye paredi.
Kisha akili yangu ikanituma nirudi tena, maeneo ya paredi ambapo sikuweza kuuona mwili wangu, wala baba yangu hakuwepo hakika nilichanganyikiwa sana na kisha nilianza kukimbia kwa nguvu na nilikua sikanyagi chini.
Nilifika nyumbani na kumkuta baba yangu akiwa kwenye chumba maalum ambacho hakumruhusu mtu yoyote kuingia.
Nilishangaa sana kukutana na mafuvu mengi na mifupa ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti, ac ha hivyo vyote ndani humo mlikua na vibuyu vingi sana ambayo sikuelewa baba aivitumia kwa kazi gani.
Baba alikua amekaa chini na pembeni ulikuepo mwili wangi, hapo nilimuona akiwasha udi pamoja na kufukizia ubani,.
Taratibu niliona nikianza kupoteza nguvu na kichwa change kilianza kuona marue rue tu. Nilipata wazo la kutoka nje ya nyumba ambako nilishangaa kumuona asia akiwa na kibuyu cheusi ambacho mara nyingi kinanitokea kwenye ndoto.
Hakika nilipata hasira sana kisha nilimsogelea asia ambaye aliponiona alistuka sana na nilimuona akitetemeka kisha akaninyooshea kibuyu cheusi lakini alishangaa kuona nikimfuata bila kumuogopa.
Taratibu nilimuona asia akianza kurudi nyuma na kisha kuanza kukimbia kuelekea porini. Hakika sikutaka kumuacha asia nilitaka kuhakikisha ananipa siri ya kibuyu kile na kwanini kila siku kinitokee ndotoni.
Taratibu nilianza kumuona asia akichoka na kisha alibadilika na kuwa popo mkubwa na alipotea kwenye upeo wa macho yangu.
Niliamua kurudi na kumkuta baba akiwa anaendelea na zoezi lake hukua akiongea maneno ambayo sikuweza kuyaelewa.
Nilisogea ulipo mwili wangu na kulala juu yake ambapo nilianza kupiga chafya nyingi mfululizo na kisha kufungua macho yangu, baada ya kuyafikicha kwa muda.
Hakina nilijiona ni mchovu sana na kwa mara ya kwanza niliongea na baba
“baba nasikia kiu naomba maji”.
Niliongea ambapo baba aimuita mama ambaye mara ya mwisho nilimuona akiwa ameshika tama sebuleni.
Haukupita muda mama alikuja na jagi la maji pamoja na kikombe name sikusita kunywa maji yote ambayo yaikua ni lita mbili mpaka wazazi wangu walishangaa.
Kisha niliketi na kuegamia ukuta, nilikua kimya kabisa na wazazi wangu walinitazama tu bila kusema chochote.
“nadhani sasa umeshatambua kwanini nilikua nakukataza kuwa karibu na asia tena ushukuru nyota yako inang’aa na kuwafanya wachawi wakuone unawaka moto, hio ndiyo pona pona yako”. Alianza kuongea baba na kunifanya niwe makini kumsikiliza na alipomaliza nilianza kumuhoji
“kwahio asia ni mchawi? Na mwalimu chimota je”. Nilihoji swali hilo ambapo baba aliguna kabla ya kulijibu

Je nini kilifuata
 
SEHEMU YA NNE (04)

ILIPOISHIA; “nadhani sasa umeshatambua kwanini nilikua nakukataza kuwa karibu na asia tena ushukuru nyota yako inang’aa na kuwafanya wachawi wakuone unawaka moto, hio ndiyo pona pona yako”. Alianza kuongea baba na kunifanya niwe makini kumsikiliza na alipomaliza nilianza kumuhoji
“kwahio asia ni mchawi? Na mwalimu chimota je”. Nilihoji swali hilo ambapo baba aliguna kabla ya kulijibu

SASA ENDELEA; baba aliniangalia usoni kabla ya kusema jambo lolote na wakati huo nilikua nimeegamia ukuta.
“hebu njoo hapa”. Aliniambia baba kama ishara ya kuwa nisogee mahali alipo name sikusita nilisogea.
“umeona haya maji? Angalia kwa makini, alafu utakachokiona litakua jiu lako”. Aliongea baba nami nilitii, na kisha kuyakaza macho yangu kwenye moja ya chungu kilichokua na maji ndani yake.
“mbona sioni kitu?” nilimhoji baba aliyekua amekaa pembeni yangu akinitazama ninachokifanya.
“angalia kwa makini, mbona mimi naona? Hautakiwi kuwa na mawazo mengine. Jitahidi kuweka akili yako yote kwenye tukio hili”. Baba alimaliza kunielekeza na kisha nilirudia kukitazama chungu kile kilichokua na maji.
Gafla zilitikea radi kwenye chungu kile na kisha nilianza kumuona asia akiwa anaongea na sauti ya ajabu ambayo ilimjibu pasipo mtu anayeongea kuonekana. Hakika nilishangaa sana kwani asia hakuonekana kuogopa chochote kile.
Asia alivaa nikabu nyeusi na vazi aina ya kaniki nyeusi pia na kumfanya awe na mwonekano wa kutisha na kuogofya pindi ukimtazama.
“unahitaji damu ya kujaza kibuyu hiki ili upate kuwa mchawi mwenye nguvu ya kufanya jambo loloote lile pasipo kuonekana na mwisho utapotea kabisa katika ulimwengu wa dunia hii”.
Mazungumzo hayo niliweza kuyapata vema kwani yalisikika barabara kwenye ngoma za masikio yangu, na kunifanya nichoke mwili hadi akili. Licha ya hayo yote nilifikiria sana kuhusu baba kwani mara nyingi amekua akiniambia kwamba yeye ni mtaalamu wa dawa za kienyeji, licha ya hivyo mara kadhaa tuliongozana porini kuchimba dawa ambapo alinielekeza mambo mengi sana kuhusu dawa za kienyeji a aliniambia angependa sana niwe mrithi wake ili niweze kuendesha mambo ya tiba za kienyeji pindi atakapokufa.
“vipi mbona umeduwaa?” alihoji baba baada ya kuona nimekaa muda mrefu bila kusema chochote
“hivi baba umewezaje kuyajua yote haya?” nilihoji swali ambapo baba hakunijibu zaidi ya kuanza kunisema tena kwamba mimi bado sijakua.
Na siku hio nilitaka kumdhihirishia baba kwamba nimekua na sitaki aendelee kunidharau tena
“nitamuua huyo asia kabla hajafanya jambo lolote”. Niliongea kwa ujariri
“huwezi kumuua pasipo kupata dawa ya ulinzi, na pia kama sio mchawi huwezi kumzuia asifanye anachokifanya”. Alingea baba huku akinitazama aone nitasema kitu gani name nilibaki kimya tu.
“sahizi kunywa hii kisha nenda kapumzike, usiku kuna mahali nitakupeleka ila tambua unahitaji kuwa na kifua kwani ni kazi hatari sana”. Aliongea baba akinisisitiza juu ya suala la kuwa msiri
Tulipomaliza mazungumzo nilitoka na kwenda moja kwa moja chumbani huku nikimuacha baba kwenye chumba kile, ambapo nilifika na kujilaza.

Mwalimu chimota alifika paredi akiwa hana wasi kabisa, huku kila mwanafunzi akimshangaa kwani alikua kama alivyozaliwa, alifika moja kwa moja na kusimama mbele ya wanafunzi na kisha kuanza kuongea mambo ambayo kila mmoja alionekana kuyashangaa na mwisho mwalimu chimota alionekana ni kama aliyechanganyikiwa.
“halafu hii tabia ya kurogana tutakuja kuonana wabaya jamani”. Aliongea kwa mikwara mwalimu chimota ambapo wanafunzi hawakuelewa kabisa ambacho mwalimu wao alikua anakizungumza.
Kisha alipomaliza kuyasema hayo maneno alienda kwa mkuu wa shule na kumnong’oneza jambo Fulani na kisha kuondoka.

Wazo alilokuanalo chimota kwa wakati huo ni kwenda kwa mtaalamu wa tiba asilia aliyekuwepo kitongoji jirani cha msia, alijiandaa haraka na kisha kuwasha gari lake kwa lengo la kuwahi kwa mganga.
Aliendesha gari kwa kasi sana chimota ambapo alitumia dakika kumi tu kufika msia,kisha alipaki gari maeneo ya zahanati na kuanza kutembe a mita kadhaa hadi alipofika nyumbani kwa mganga.
“mwakata?” (habari ya saa hizi) aliongea chimota kwa lugha ya kinyiha
“mwakata huli?”. (ni nzuri, habari yako) alijibu mke wa mzee simangwa ambaye ndiye mganga
“hansi! Nimemkuta mtaalamu”. Alihoji chimota
“ndio, yupo ndani karibu!”. Aliongea bi zulfa mke halali wa simangwa kisha alimkaribisha ndani mwalimu chimota.

“mzee nimekuja, niko na shida sana na ninahisi kuna mwalimu mwenzangu ni mchawi ananiroga”. Aliongea chimota akimweleza mganga
“sio mwalimu, ni mwanafunzi mchawi na msipokaa sawa walimu wote mtakufa kwani anachokitafuta ni nguvu ya kufanya mambo ya giza pasina kuonekana”.
Aliongea mzee simangwa kwa umakini wa hali ya juu kumfanya mzee chimota astuke sana na kutoa mguno ambao ulioonesha dhahiri amestuka.
“haaaaaaa!”.
“hapa nitakupa dawa lakini kuna kazi kubwa ambayo tutaifanya siku ya kesho majira ya usiku ili tuweze kuvunja mitego yake yote kwako, lakini nitahitaji jogoo mweupe na tetea mweusi kwa kazi hiyoo”.
Aliogea mganga.
“hilo sio tatizo mkuu”. Alijibu chimota kwa shauku, kwani alishachoshwa na mauzauza yaliyokua yanamtokea.
Baada ya mazungumzo hayo mganga alipekua vitu vyake na kutoa moja ya mzizi na kumkabidi chimota na kumwambia aupokee kwa mkono wa kushoto, nae alifanya hivyo.
“pindi utakapoweka mzizi huu kwenye mfuko wako wa kushoto, hakikisha hauogi wala kubadili suruali yako mpaka tutakapokutana tena”. Mganga alitoa maelekezo kisha mwalimu chimota aliacha kiasi cha pesa na kuahidi kutimiza masheriti yote kisha kutoka nje ya chumba kile.
Baada ya kuchoka kulala, nilitoka nje japo nipate kuotea jua la mchana, nje nilikuta gari ambalo nililifahamu kabisa na mara nyingi lilikua likiegeshwa nje ya nyumba ya mwalimu chimota.
Ni kama niliotea sahihi kwani haukupita muda mwalmu chimota alitoka nje na aliponiona alistuka sana, hata mimi pia nilishituka na kubaki na maswali moyoni.

Je nini kilifuata
 
SEHEMU YA TANO (05)

ILIPOISHIA; Baada ya kuchoka kulala, nilitoka nje japo nipate kuotea jua la mchana, nje nilikuta gari ambalo nililifahamu kabisa na mara nyingi lilikua likiegeshwa nje ya nyumba ya mwalimu chimota.
Ni kama niliotea sahihi kwani haukupita muda mwalmu chimota alitoka nje na aliponiona alistuka sana, hata mimi pia nilishituka na kubaki na maswali moyoni.

ENDELEA; “SHIKAMOO!” nilimsalimu mwalimu chimota naye alijibu bila wasi huku akiingia kwenye gari lake.
“marahaba dogo hujambo”. Alijibu
“sijambo tu mwalimu”.
Baada ya salamu mwalimu chimota aliondoa gari maeneo ya nyumbani na safari yake iliishia kwa mzee simfukwe aliyekua akisifika kwa ufugaji wa kuku kijijini pale.
Alifika na kukaribishwa mpaka ndani nae hakusita kuingia na kumuelekeza kuwa alikua na shida ya kuku, jogoo mweupe na tetea mweusi.
“wapo wengi tu unataka wangapi?” alihoji mzee simfukwe
“nataka kuku wawili tu, jogoo mweupe na tetea mweusi”. Aliongea mwalimu chimota
“kuku wameshatoka nje, naomba jioni uje wajukuu zangu watakukamatia”. Aliongea mzee simfukwe
Mzee wa makamo anaeendesha maisha yake kwa ufugaji wa kuku pamoja na kilimo.
Bada ya makubaliano hayo mwalimu chimota hakuweza kukaa tena nyumbani kwa mzee huyo zaidi aliacha pesa na kuwasha gari kisha kuondoka kwenda nyumbani kwake ambako ndiko shule ya wasa sekondari ilipo.
Alifika na kuwakuta wanafunzi wakiwa paredi, lakini kwa mbali aliweza kumuona kiumbe akiwa mrefu kuliko wanafunzi wote huku akipitiliza hata jengo la ofisi ya walimu.
Hakika walimu chimota alistuka sana na almanusura angonge ukuta wa darasa, mwalimu chimota alienda moja kwa moja nyumbani ambapo alifika na kukuta nyumba yake ikiwa chafu na yenye matakataka mengi nje.
Aliyapuuzia kwani alitambua huenda takataka zile zimeletwa na kimbunga ukizingatia yalikua ni majira ya kiangazi, alizipiga hatua zake kuelekea ulipo mlango wa kuingilia ndani, alipofika mlangoni alishangaa kukutana na ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi nyeupe na ilionesha dhahiri iliandikwa kwa damu.
Hakika maneno yaliyoandikwa kwenye karatasi ile ilikua na maneno mazito ambapo hata ungelikua wewe ungetetemeka baada ya kuyasoma.
“maandishi haya nimeyaandika kwa damu yako mwenyewe, achana na jambo hili kabisa la sivyo nitakumaliza na hilii ni onyo la mwisho kabisa”.
Chimota alistuka sana mstuko alioupata hauwezi kulinganisha na kitu chochote kwani almanusura azimie, tumbo la kuhara lilimpata ghafla na alijikuta akitamani kwenda uwani kwaajili ya kujisaidia.
Haraka alichota maji kwenye bomba lililokua pembeni ya nyumba yake na moja kwa moja kwenda maliwatoni, alistuka sana pindi alipoingia maliwatoni baada ya kuona moshi mweusi wenye harufu kali ukitoka kwenye tundu la shimo la choo.
Moshi ule ni kama ulikua na sumu kwani mwalimu chimota alizimia na kuanguka chooni punde tu baada ya kuivuta hewa ile.
Chimota alizinduka na kujikuta akiwa chooni majira ya jioni, viungo vilimuuma sana pia harufu mbaya ya kinyesi ndiyo ilimchefua kwani kila mahala alipoenda nzi walimfuata.
Alipokumbuka masheriti aliyopewa ya kutokuoga alichoka sana, kwani aliwaza angewezaje kufika siku ya kesho pasina kuoga wala kubadili nguo?
Akili yake ilimtuma kuangalia dawa aliyoiweka mfukoni, na alipopapasa tu hakuiona, na hakuishia hapo bali aliingiza mkono mfukoni na alikuta ujumbe badala ya ile dawa.
“huwezi zima moto kwa moto zaidi utachochea moto uwake na ukolee zaidi, chimota ni lazima ufe”.
Moyo wa chimota ulipasuka paaaaah! Kwani alijiona kwamba tayari ameshakufa japo yapo alikua buheri wa afya.
Mikono yake ilitetemeka kwa wasiwasi, mdomo wake pia ulianza kutetemeka kama mtu anayesikia baridi kali sana.
Chimota hakutaka kulala tena nyumbani kwake na aliamua kupiga simu kwa mganga, ambapo simu iliita na kisha kupokelewa.
“kosa ulilolifanya ni kupita kwa yule mzee”. Aliongea mganga kabla hata ya salamu kisha kukata simu na kumuacha chimota akiwa kwenye hali ya sintofahamu .
………………………………………………………………………………………………………………………………………………....................
“karibu sana justice simangwa kwenye ulimwengu huu jisikie uko nyumbani na haujapotea njia kabisa”.
Ilisikika sauti ya mzee mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabisa na alikua wa pale pale mtaani
“baba yako amenieleza kila kitu kuhusu wewe, name nitakupa nguvu ya kuweza kuangamiza uchawi mweusi ambao unatufanya wachawi wote tuonekane wabaya”.
Aliongea mzee huyo wakati huo mimi nikiwa kimya kabisa, mazingira tuliyokuepo niliyafahamu kwamba ni ya uwanja wa shule ya wasa.
Niliona aibu sana na muda mwingi nilikua nikificha jogoo wangu kwani tulikua uchi wa mnyama lakini hakukua na mtu aliyeonekana kujali mambo ya mwenzake.

Baada ya kusema maneno hayo mzee Yule alichukua usinga wake na kuanza kuupepeza kisha ghafla kilitokea kibuyu chenye angi ya njano kilichonakshiwa na shanga nyeusi.
Mzee Yule alinisogelea mimi na kuniamuru nisimame name nilitii, kisha akaanza kuupepeza usinga wake kwenye paji langu la uso huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa kabisa.
Alipomaliza kuyasema maneno hayo, alinyoosha mkono wake juu na kisha kikatokea chungu cheusi ambacho ndani kilikua na damu kisha akaniamuru ninywe.
Hakika ulikua ni mtihani mgumu sana, kabla ya kufanya jambo lolote nilimtazama baba yangu ,ambaye alinipa ishara ya kwamba ninywe na nisimuangushe.
Nilipiga moyo konde na kuinywa damu iliyokua kwenye chungu kile ambapo baada ya kumaliza, shangwe zilisikika si kina mama wala kina baba wote walishangilia kwa nguvu na ngoma zilipigwa.
“hatimaye tumekamilisha zoezi la kumpokea mwanachama mpya katika chama chetu cha uchawi, tutajipongeza kwa kula nyama na mwisho kila mmoja ataenda kwake”.
Baaada ya kusema maneno hayo moto mkali uliwaka na kisha kina mama wawili waliokua ndani ya vazi la kaniki walisogea mbele wakiwa wamebeba miili miwili ambayo sikuelewa ni ya kina nani lakini ilionesha ni maiti mbili za kiume.
Kisha bila huruma walikata vipande vipande na kila mmoja alokua eneo lile alipanga foleni kwaajili ya kupata kipande cha nyama.
Mzee Yule mwenye ndevu nyingi na mvi nyeupe aliniamuru niwe wa kwanza kupata kipande cha nyama.
ambapo nilisogea pia baba alifuata na alikua nyuma yangu alihakikisha nafanya kila jambo linalotakiwa kwa usahihi.
Baada ya kupokea kipande cha nyama nilikaa pembeni nikisubiri kuelekezwa ijapokua nilijua kabisa kinachofuata ni kula nyama ile ya binadamu mwenzangu.

Je nini kilifuata
 
SEHEMU YA SITA (06)

ILIPOISHIA; ambapo nilisogea pia baba alifuata na alikua nyuma yangu alihakikisha nafanya kila jambo linalotakiwa kwa usahihi.
Baada ya kupokea kipande cha nyama nilikaa pembeni nikisubiri kuelekezwa ijapokua nilijua kabisa kinachofuata ni kula nyama ile ya binadamu mwenzangu.

SASA ENDELEA; Mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi sana kwani sikutarajia kwamba siku hio inaanza na nyama ya kiumbe mwezangu tena si kiumbe tu bali ni binadamu mwenzangu kwani kiumbe anaweza akawa kuku au mbuzi.
Zilipita dakika kumi nikiwa sijafanya jambo lolote zaidi nilikua nimekishikilia kipande cha nyama,ile ambayo ilikua ikichuruzika damu kuashiria kwamba mwili ule bado ulikua mbichi kabisa na ulizikwa siku si nyingi kama sio moja.
Macho makali yam zee Yule ndiyo yalinishitua sana na nilijikuta nikitetemeka mikono yangu hadi kupelekea kibande cha nyama kudondoka bila kugusa chini kwani kabla hakijafika chini mzee Yule alikizuia kwa nguvu za kichawi na kukifanya kielee kisha akaniamuru kukichukua tena.
Mtihani ulikua kwenye kukipeleka kipande kile kinywani mwangu, safari hii kila mmoja alikua ameshamaliza kula na macho yake yalikua kwangu kwani ndiye niliyekua nikiwachelewesha
“fanya haraka kijana, tutachelewa asubuhi itukute hapa”. Aliongea mzee Yule kisha baba akadakia.
“mwanangu justice, jitahidi usiniangushe”. Baba aliongea kwa upole hadi nilishangaa sana kwani nilimjua baba na tabia yake ya ukorofi na kunikoromea mara kwa mara.
lakini nilishangazwa sana na upole wa baba siku hiyo
taratibu nilisokomeza pande lile la nyama mdomoni, hakika nyama ilikua tamu hadi nilishangaa ambapo nilitamani hadi kuongezewa lakini ilikua ishamalizika, zaisi niliishia kujilamba vidole huku wachawi wengine wakinishangilia.
“sasa umeshakua mchawi rasmi, maelekezo mengine utapewa na baba yako na utakau ukiendelea kujifunza kadiri siku zinavozidi kwenda”.
Aliongea mzee huyo kisha watu wote wakainamisha vichwa vyao ambapo mzee Yule alipepesa usinga wake kisha akapotea na wengine wakafuata, uwanjani tulibaki mimi na baba ambapo tulianza safari yetu kutokomea gizani.
Moto uliokuwepo mahala pale ulizima na ghafla nilijikuta chumbani peke yangu na nilipoangalia saa ilionesha ni majira ya saa kumi na moja alfajiri.
Nilijiona niko fiti kuliko siku zote tena mwenye kujiamini sana na sikujua hali hio nimeipata wapi, nilipotazama bega langu la kushoto nilikutana na hirizi nyekundu ambayo ilifungwa na kamba nyeusi ambayo ilikua ikipumua mithili ya pumzi zangu.
Moyo ulianza kunienda mbio sana kwani niliamini yaliyokua yanatokea ilikua ni ndoto, lakini haikua hibyo na sasa nilianza kuona kwamba ilikua si ndoto bali ukweli wenye kweli zake na usiofichika.
Yaani mimi justice nimekua mchawi rasmi! Hakika niliwaza sana hadi usingizi uliponipitia, baba ndiye aliyekuja kuniamsha majira ya saa tatu asubuhi chumbani kwangu.
“amka kumekucha, chai ipo mezani”. Aliongea baba kisha kuondoka akiniacha nikiendelea kujinyoosha na kuweka swa viungo vyangu
Baada ya kuamka nilimkuta baba akiwa sebleni akiwa anasoma kijarida Fulani, na aliponiona alitabasamu, kwakua ilikua siku ya jumamosi, sikuweza kwenda shule kabisa
“umesikia taarifa za kifo cha mwalimu wako chimota”. Alihoji baba na kunifanya nishangae sana
“hee amekufa lini, na jana tu alikuja hapa”. Nilihoji
“usiku wa kuamkia leo, watu wamemkuta kwenye njia ya kwenda ibandawe jirani na mashamba ya kahawa ya kijiji”.
Aliongea baba taarifa ambazo hata mimi nilikua sijizui pia hata sikutambua amezijulia wapi, hilo halikua tatizo lakini nilijikuta nataka kuujua undani wa mambo hususani kuhusu kifo cha chimota.
Na nilipanga kwenda nyumbani ambako ndio msiba huo unafanyika pasipo hata baba kujua.
Baada ya kunywa chai nilichukua nguo zangu za shule na kuzifua kisha haraka na kuzianika baada ya hapo nilivaa nguo yangu aina ya pensi na kandambili za umoja kisha nilitoka kwa kupitia mlango wa nyuma na nilihakikisha kwamba hakuna mtu aliyeniona nikitoka kwani baba alikua amesinzia kwenye kochi.
………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………….
Usiku haukua mzuri kwa chimota kwani licha ya kua alitimiza shariti la kutokuoga lakini alikua ameshakosea kuloanisha mzizi aliopewa na mganga.
“usiniueeee, tafadhali na…o..mbaaa”. aliongea chimota na asia ambaye hakutaka kabisa kumsikiliza kwani tayari alishakua na roho ya kishetani kucha zake zilikua ndefu na meno yake yalichongoka mithili ya mbwa mwitu huku macho yake yakitiririsha machozi ya damu.

“ni lazima ufe chimota, wewe ndiye utakua wa kwanza kukijaza kibuyu cheusi, kwani nilikukanya hukusikia”.
Aliongea asia bia chembe ya masihara kisha akachukua kisu na kumchoma mwalimu chimota tumboni kisha meno yake yalitua kwenye shingo ya mwalimu chimota na kunyonya tamu kisha kuitemea kwenye kibuyu cheusi.
Baada ya asia kumaliza tukio hilo alitoa kicheko kikali ambacho kilisababisha majani ya miti kupukutika kwa wingi licha ya kua ni mabichi lakini yalidondoka hivyo hivyo.
Baada ya kumaliza shughuli hio upepo mkali ulivuma kisha ilisikika sauti ikimpongeza asia
“safi sana”.
Kisha asia akapotea.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Nilifika eneo ulipo msiba, ambapo mita chache kabla ya kufika nyumbani niliona viumbe wa ajabu wakipigana sikutaka kuwajali, zaidi niliendelea na safari yangu hadi nilipofika eneo ambalo msiba ulikuepo.
Nilisikitika sana baada ya kuona hakukua na mtu bali ndugu waikua wakililia mgomba wa ndizi.
Moyo ulinipasika paaa! Kisha nywele zangu zilianza kusimama, na mwili ulisisimka ghafla na sikujua hali hio ilikua ikitokana na nini.
Kijasho chembaba kilianza kunitoka almanusura nianguke, nilipogeuka nyuma nilimuona mzee mmoja akinikazia macho kwa nguvu na sikujua ni kwanini lakini jasho bado liliendelea kunitoka kisha hirizi ikaanza kunibana na kufanya nianze kupoteza nguvu.
“mkazie macho kisha funga ngumi yako ya kushoto”. Sauti ya baba ilisikika ininipa maelekezo kwakua nilikua nimebanwa sikutaka hata kuhoji kwamba ile sauti imetokea wapi, zaidi nilifanya kama nilivoelekezwa.

Je nini kilifuata
 
Back
Top Bottom