Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 17,796
- 32,148
MKASA WA KWELI; KIBUYU CHEUSI
MWANZO
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Kwa majina naitwa justice simangwa mkazi wa mkoa wa songwe katika wilaya ya mbozi kijiji cha msia, nilizaliwa katika familia ambayo naweza kusema ni masikini ijapokua tulikua na uhakika wa kupata chakula na kula milo mitatu kabisa.
Suala la kula halikua tatizo kwani kwa maisha ya kijijini ukikosa chakula basi wewe ni mzembe kupitiliza, yaani hata kula kwa jirani umeshindwa.
Kijumba cha nyasi cha vyumba vitatu ndicho kilichonikuza hadi kufikia umri wa miaka kumi na tano na hapo nilianza kujiona ni mkubwa kwani hata shuleni tulifundishwa kwamba unapoanza kubalehe basi ndio dalili ya kuuanza ukubwa.
“hivi utakua lini wewe”. Ni sauti ya baba akiongea kwa ukali na kunifanya nikasirike sana, kwani kila siku baba huniambia mimi ni mtoto ilhali nilijiona nimeshakua sasa
“kwani nimefanyeje baba?” nilihoji kwa mshangao kwani sikuona sababu ya baba kunikoromea kiasi kile na ukizingatia ndio nikwanza nilikua narudi kutoka shuleni.
“hivi ni mara ngapi nakukanya kuhusu kuongea na asia, Yule binti wa mzee mwashilindi?” aliongea baba na safari hii macho yake yalishaanza kuwa mekundu ma ishipa yake ilimtoka kuashiria amekasirika sana na hapendi mambo ninayoyafana.
Kwa vile, namtambua baba akiwa amekasirika, sikutaka kuendelea na majibizano zaidi nilikua mpole kama nimenyeshewa na mvua kisha nikachukua begi langu na kwenda chumbani moja kwa moja.
Ambapo nilifika na kulirusha kitandani na kisha nami nilifuata na haukupita muda tangu nilipouweka mgongo wangu juu ya kitanda usingizi ulinipitia, hii ni kutokana na kuchoka na umbali kati ya shule ya sekondari wasa na makazi yetu yalipo.
Nishituka baada ya kuhisi nimeguswa na kitu Fulani, na nilipofungua macho yangu tayari nilikutana na baba ambaye aliniamuru niamke haraka kwani kulikua na kazi ya kuhamisha vitu kutoka kwenye nyumba ya nyasi na kuvipeleka kwenye nyumba yetu mpya.
Sikua na namna na nilipoangalia nje kulikua kweusi lakini giza lilikua halijatanda kabisa, na kwa kukadiria ilikua ni saa moja usiku.
Nilijiuliza sana kwanini baba hakusiema tuhamishe vitu mchana mpaka aseme tuhamishe muda ule, maswali yangu hayakuweza kuishia moyoni tu na moja kwa moja niliamua kumuuliza baba swali hilo ambaye alinikata jicho kali hadi niliogopa.
Baba hakunijibu hilo swali wala mimi sikuhitaji tena jibu la swali lile kwani nilishatambua kuwa baba hapendi.
Baada ya kumaliza kazi hio ya kuhamisha vitu mama alipika chakula na kisha tulikula, name baada ya kula nilienda chumbani na kuchukua madaftari yangu kwa lengo la kujisomea , lakini nilishangazwa na uvivu niliokua nao siku hio, niliposhika daftari nilisinzia lakini nilipoliachia nilijiona nisie na uchovu wowote.
Niliamua kupuuzia hali hio na kuyarudisha madaftari yangu kwenye begi kisha kulivuta blanketi langu tayari kwa kulala tena na nilipanga ningeamka kusoma usiku wa manane kwani huo ndio muda akili inakua imetulia na kunakua hakuna vurugu.
Majira ya saa nane usiku nilistuka ghafla kutokana na bati za nyumba kupiga makelele sana kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha usiku huo.
Hakika mvua ile ilinishangaza sana, kwani ilikua ni majira ya kiangazi, sasa inakuaje mvua kubwa kiasi kile inyeshe majira ya kiangazi.
Nikiendelea kuwaza hayo nilishikia kishindo kikubwa maeneo ya sebleni, hakika kishindo hiki kilipelekea moyo wangu upasuke paa!
Kisha mapigo yangu ya moyo kuanza kudunda kwa kasi, kabla sijakaa sawa niliaza kusikia bati zikigonga gonga kana kwamba kuna vitu vilikua vikicheza.
Nilipata ujasiri kisha haraka niliinuka na kutoka kuelekea sebleni ambapo katika hali ya kustaajabisha niliona kibuyu cheusi chenye shanga zinazowaka kama taa na kukifanya king’ae.
Macho yangu yalinitoka pima na kisha kibuyu kile kikapotea, baada ya hapo kila kitu kilikoma, hata mvua iliyokua ikinyesha iliacha na kukawa swari kabisa.
Sikua na budi kurudi chumbani kwa hofu sana kwani nilichokiona yalikua ni maajabu kwa upande wangu na moyo wangu haukua na amani hata kidogo.
Nilifika na kuvuta shuka langu na kujifunika gubi gubi nikiwa na hofu sana yote hii ni kuufanya usingizi uwahi kunichukua.
Baada ya kupitiwa na usingizi nilikuaja kuzinduka majira ya alfajiri kama ilivyokua kawaida yangu kuwahi kuamka kabla ya wote na kuandaa kifungua kinywa kabisa kisha kuwahi shuleni.
Na wiki hio ilikua ni ya mwalimu mkali kuliko wote pale shuleni.
Nilijinyoosha na kisha kutoka nje kwa lengo la kuwasha moto lakini nilishangaa sana baada ya kukuta nyumba yetu ya zamani ikiwa imeanguka, haraka niliingia ndani na kumgongea baba ambaye alitoka na kuangalia hali halisi lakini hakuonesha kustuka na chochote.
“tukiwaambia mnakua wabishi”.
Aliongea baba na kisha kuingia ndani akiniacha na maswali mengi sana
Je nini kilifuata