Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Mnyenz

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
4,881
Reaction score
13,217
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.

Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.

KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).

Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.

VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.

Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.

ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??

MCHANA MWEMA.
 
Polisi wetu na uzembe wetu!

Polisi anapofika hasa mda usio wa kazi na hana uniform ni lazima ajitambulishe na atoe ID ndipo afanye kaZi yake. Hapo kwa vile wengine tuna uoga basi nao wanachukulia huo upenyo na kutubabaisha. Ungemuuliza hizo detail, ndipo afanye yake.

Polisi wanatumia sana ujinga wetu kutunyanyasa 'vile tu ana cheo cha upolisi' wakati ni kazi ka kaZi zingine tu. Pole sana, pia ukute hiyo pisto ilikuwa toy tu, kwa sbabu polisi hawezi fanya huo upuuzi wa kuload ammo kwa ajili ya leseni. Next time jua haki zako kabla ya arrest
 
Pole sana mkuu,kuna alituchomolea bastola hivo boss alikua na s.mg ilibid awe mpole ka sh. Mia
 
Jtahidi siku nyingine anakupa kitambulisho usome namba!ndo muanze kuchenjiana Hongera kwa ujasili.
 
DUI huyo alikuwa tapeli tuu askari mwenye maadili na miiko ya kazi hawezi Fanya hivyo
 
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014. Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.
KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni)
Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.
VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.
Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.
ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??
MCHANA MWEMA.

Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.
 
Nilipokuwa nasoma nilikuwa natetemeka sana sijui hasira!!! daah aisee pole sana, nadhani hukulala siku hiyo mkuu kwa hasira.Ila ulimvimbia kinoma,alikoenda alijua amekutana na kidume.Wajinga sana hawa jamaa.
 
Kwanini alivyokuomba lesseni hukumuomba na wewe Kitambulisho ili ujue kuwa kweli alikuwa Askari..?
 
Wewe una gari na unatembea sehemu kama hizo usiku huna bastora!! hata sime?

Mambo ya kutishiana kwangu no. Na nnapiga picha kama ingekuwa ni mimi angekiona cha moto.

Huyo alikuwa ni polisi sio jambazi kwani ingekuwa jambazi angekuomba leseni kwa kazi gani? tena anashika na kukurudishia!! hao ni vijana wa mangu hawana kipya.
 
Last edited by a moderator:
Polisi wetu na uzembe wetu!

Polisi anapofika hasa mda usio wa kazi na hana uniform ni lazima ajitambulishe na atoe ID ndipo afanye kaZi yake. Hapo kwa vile wengine tuna uoga basi nao wanachukulia huo upenyo na kutubabaisha. Ungemuuliza hizo detail, ndipo afanye yake.

Polisi wanatumia sana ujinga wetu kutunyanyasa 'vile tu ana cheo cha upolisi' wakati ni kazi ka kaZi zingine tu. Pole sana, pia ukute hiyo pisto ilikuwa toy tu, kwa sbabu polisi hawezi fanya huo upuuzi wa kuload ammo kwa ajili ya leseni. Next time jua haki zako kabla ya arrest

Cooking up a Story vilaza mupo wengi
 
Kama muvi vile....

Ngumu kumesa anyway.
 
Next time usiwe unavimbia bunduki na kijisifu "eti"ukamkomalia ni ujinga,sasa hivi ungekuwa marehemu kwa kiburi cha kumwona demu wako pembeni.

Swala la bunduki kuwa toi au ya ukweli unatakiwa kujuwa baada ya kutii amri ya mwenye moto!!!!
 
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014. Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.
KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni)
Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.
VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.
Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.
ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??
MCHANA MWEMA.

hii stori ngumu kuamini....COCO beach monday to monday mida hio upande huo wa kitimoto kuna magari kibao yanapaki watu hawashuki mimi nikiwa mmoja wao tukio kama hilo haliwezi kutokea....na polisi pale wapo na wanakuwa na defender yao au wanapatrol kwa miguu wala hawahangaiki na watu ndani ya magari....kwanza kuna watu wengi sana hilo tukio lingejaza watu,huyo polisi mjinga kiasi gani akutolee bastola,tena akuwekee kichwani??!!
 
Cooking up a Story vilaza mupo wengi

Sasa hapa ukilaza wangu ni nini? Humu Jf kuna vitu vingi vingine vya kweli ama vya kutunga. Wajibu wa memba ni kufanya uwezalo, ushauri ama kusaidia.

Sasa wewe unaposema mimi kilaza kwa kushauri fake story hunitendei haki.
 
Back
Top Bottom