MKAPA ndio kaimalizia Tanzania

So, what is new exactly here? Is this a topic to be discussed? I vehemently doubt.

Ni kweli JF ni Great thinkers?Wewe uliyeleta mada hii unaweza ukawa GT ingawa ninawasiwasi unalengo ambalo wachangiaji wanaweza kutolijua!Mimi naona ni sawa na kuwapumbaza watanzania washindwe kumfahamu adui wa maendeleo yao.Naamini GT wote wanaelewa na sidhani watachangia uzi huu kama jinsi ulivyowachezesha!
 
Kuuza kwa bei ya kutupa migodi, bandari, mashirika ya uma, viwanda etc ....kuingia mikataba na wachina ni kama ameimalizia nchi . Sasa kamfanya kikwete awe ombaomba

kupe hili halina shaka ndani yake,yeye ndo mwanzilishi na jk anaendeleza LIBENEKE
 
Last edited by a moderator:
Chinga ndo kaimaliza nchi hii kwa gia ya UWEKEZAJI,,JK lawama za bure tu mnampa ila kitakachomhukum ni ushkaji kazini. Yaan ni sawa na"Chumvi kwenye Chai",,,,na huyo jamaa aliyechangia kwa Kiingereza ni Mshamba halafu ni Mtumwa wa Fikra!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hakika tunalo lakuwauliza kama Mkapa alidhubutu kuwa mkali katika baadhi ya vitu ambavyo alikuwa na maslahi navyo vp waliopo leo wameshindwa kukemea badala yake wamebaki kukenua meno na kuanzisha misemo mingi isiyo na tija kwa taifa vp leo kila kona kuna migomo ya wafanyakazi kila kona unyama waufanyao polisi umezidi sana tena saanaaaaa. Usanii usanii umezidi sana mfano serikali inatangaza mwisho kununua magari mapya alafu bado PRADO mpya zipo nyingi sanaaaa wakati wananchi hawana hata panadol, gharama za maisha zimepanda sana vitu vimepanda bei sana kutokana na uzembe wakushindwa kuthibiti bei kwa vile wafanyao ni marafiki wao ndio wachangiaji wa pesa kipindi cha kampeni zao
 
Ki ukweli tunahitaji sana mapinduzi na sio mageuzi, tumpate kiongozi kama mwalimu au mugabe nk. Tuwafukuze makaburu, tuwakamate wahujumu uchumi, tuwanyang'anye kila walichoiba tujipange tuanze upya;
 
Tuanze na Nyerere
:huyu alikuwa mzuri sana lakini alisahau uzalendo yaani Nationalism na kuweka africalism maana ilifikia mahali akiambiwa huyo ni mkenya,mrwanda,mkongo,mmalawi etc anasema haina shida maana ni mwafrica na hapo ndiyo wakenya wengi waliingia TZ na kusoma mpaka chuo na baadaye wakamhujumu, na wakenya wengi kama wakamba walikuwa kwenye mashirika mengi na ndiyo walifanya uhujumu kwa taifa, kwa mfano hata Raila Odinga mgombea urais huko Kenya kwa sasa alishadhiriki kusema passport yake ya kwenda masomoni marekani alipata TZ kwa maana hiyo alipata scholarship ya TZ

Mwinyi
:Huyu naye alikuwa amejipanga vizuri kuleta maendeleo lakini mshauri wake Pr.Ibrahimu Lipumba huyu wa CUF na wenzake wakamshauri kuleta bidhaa za nje kama radio,matv nk na hapo akarusu ndiyo waarabu wakaanza kuleta bidhaa Tz na wakifika kulipia ushuru wanaenda wanaomba kwa rais tunaomba tuuze kwanza tutalipa ushuru maana bado hatuna hela na kwa kuwa walikuwa waislam aliamini watalipa na aliwajibu ishallal mujitahidi mlipe,wakimaliza mizigo wanajaza macontainer malighali na kurudi kwa rais na kumwambia mizigo yote tuliwapa watz na wamepotea na mali yote kwa hiyo tunarudi kutafuta tena anasema ishaal mungu atawarehumu, huo mchezo uliendelea mpaka ukaliweka taifa ktk hali mbaya kwa rais kuamini muislam hawezi danganya
:Mkapa
Huyu ndiye alikuwa rais mzuri sana ila baada ya kurudiana na mke wake Anna Mkapa ndiyo ilikuwa shida japo huyu mke wake hakuwa mwanasiasa ila aliwaingiza mashemeji na rafike zake kwenye system na ndiyo walioharibu kila kitu mfano Mramba,akina Yona na ikawa ndiyo hatari zaidi ambayo ndiyo inamfanya anaishi kwa wasiwasi kutokana na ufisadi alioupitisha mkewe na mashemeji zake wa Kiwila, EPA na NBC ukiachia mbali Net Group Solution iliyoletwa na shemeji zake kundi la Kilimanjaro.
:Kikwete
Huyu ndiyo mtawala wa sasa na mengi kuhusu yy kila mtu anafahamu
 
Wanabolonga kiasi kwamba wanashusha heshima zao na wanashindwa hata kuwa mstari wa mbele katika matukio ya kitaifa. Angalia Mkapa anavyopata shida katika matukio ya kitaifa ni tofaouti na Ally Hassan Mwinyi. shame on you Mkapa. Dhambi ya kuuza rasilimali za watamzania inakutafuna unashindwa hata kukaa nao vizuri sasa nakuhurumia sana kuwa kama mkimbizi katika nchi yako mwenyewe.
 
Sasa kikwete angefanyaje . Kakuta kila kimeuzwa. Hadi posta na simu. Nyumba za oysterbay. Watu walichukua hela bot EPA . Watu watamuhukumu kikwete bure. Ndio maana kaamua kuwa mzururaji

Mkuu Kikwete ndio alichukua fedha za EPA ili zimsaidie kwenye kampeni. Richmond, dowans, fedha za Urissi ni yeye na hakuna dalili zozote za kurekebisha yaliyopita bali kila siku kuna mapya.
 
Unapouza makampuni kama Saruji, beer, sigara na NMB kwa makaburu ambayo ndo yanatengeneza faida ya kufa mtu, unafikiri tutakaa tuendelee? kwa kukwepa kulipa kodi kwa makampuni yanayotengeneza faida kubwa! kwa sababu sheria zetu zipo legelege eti waziri/katibu/mkurugenzi anatuhumia kwa wizi anahamishwa kituo cha kazi au anasimamishwa ndo mambo yanaishia hapo! pangekuwa kuna kiongozi mmoja amenyongwa hadharani tungeshika adabu! au watuachie wananchi wenye hasira kali tuwasaidie!
 
Kuuza kwa bei ya kutupa migodi, bandari, mashirika ya uma, viwanda etc ....kuingia mikataba na wachina ni kama ameimalizia nchi . Sasa kamfanya kikwete awe ombaomba

Yote uliyosema ni sahihi kabisa, kasoro mwishoni. Kikwete aliingia madarakani hazina ya taifa ikiwa imenona vibaya sana. Ni kikwete ndiye alifuja hela alizoziacha Nkapa. Unakumbuka semina elekezi, n.k, n.k.?
 
Yote uliyosema ni sahihi kabisa, kasoro mwishoni. Kikwete aliingia madarakani hazina ya taifa ikiwa imenona vibaya sana. Ni kikwete ndiye alifuja hela alizoziacha Nkapa. Unakumbuka semina elekezi, n.k, n.k.?
Semina elekezi ni Sawa,sikulikuwa na malengo serikali iliyojiwekea.Embu twambie lengine kwa hili hatukuafiki ndugu.
 
Back
Top Bottom