MKAPA ndio kaimalizia Tanzania

MKAPA ndio kaimalizia Tanzania

Sasa kikwete angefanyaje . Kakuta kila kimeuzwa. Hadi posta na simu. Nyumba za oysterbay. Watu walichukua hela bot EPA . Watu watamuhukumu kikwete bure. Ndio maana kaamua kuwa mzururaji

Hapo kwenye nyekundu aliyechukua hizo pesa ni Kikwete na kundi lake. Vile vile kwenye upande wa mdini mkataba wa Buzwagi umesainiwa gizani London na waziri rafiki wa Kikwete aitwaye Karamagi. Miradi ya gesi je? Richmond je? Leseni nyingi za makampuni ya madini zimeisha wakati wa Kikwete na wakapewa leseni kwa uhuni ule ule ulioanzishwa enzi za Mkapa. Kwahiyo wote ni hovyo tu.
 
Ni kweli kabisa yeye ndiye alieimaliza Tanzania, Alifanikiwa kukusanya kodi kwa wingi na akazihamishia kwake na rafiki zake. Wanaomlaumu Kikwete hawaangalii mambo kwa mapana yake!!!

Linganisha hali ya maisha ya sasa na kipindi cha Mkapa. Labda kama una ajenda nyingine. Mkapa apewe heshima yake. Hakuwa perfect, alifanya makosa kama walivyo wengine. What more, he was a decision maker, which makes him a leader. Alifanya vitu vilivyoonekana, sio mpaka mawaziri wazunguke nchi nzima kujaribu kuwashawishi wananchi waliopigika kuwa serikali imewaletea maisha bora, na kuwa kupigika walikonako ni kwa dunia nzima, hivyo ni haki yao. But guess what, kama atagombea leo hii Mkapa, I bet you, HAKUNA WA KUSIMAMA NAYE TANZANIA NZIMA!!! Painful reality ladies and gentlemen.
 
Why aliuza oysterbay
 
Suruhisho ni kujitoa muhanga tuwapoteze mafisadi wote na familia zao adabu itakuwepo humu nchini
 
Mkapa kafanya mengi,kikwete ndo usiseme mazuri mengi mno!stop living in the past ndugu,wake up!!
 
Dawa ya hawa mafisadi miakina mikapa ni kubadirisha katiba kuwafanya viongozi kama wafanyakazi na si viongozi kutufanya sisi kama wafanyakazi wao. ANABAHATI SANA HILI FISADI LINGEKUWA LINATAWALA CHINA LINGENYONGWA,ACHANA NA WACHINA!
 
Hivi Jk ni Mgogo? na wanaundugu wowote na Marehemu Mzee Matonya? na kama kunza ubishi anaweza ruhusu kipimo cha DNA. Maana Mambo mengine yana Asili haya si bure
 
Anyway, many Tanzanians are not able to analyse things critically. The just blabber! They will say this and that but if you ask them the reason behind their saying they will just have a gaze at you! I think we have a long way to go!!!
Samahani !hivi kulikua na umuhim wa kuandika kwa lugha hii ya kigeni kwa ajili ya kuchangia hili???acha hizo ndugu ungeeleweka zaidi kama ungetumia lugha halisi ya kiswahili.asante
 
mtu aliyeimaliza na kuliangamiza kabisa taifa hili ni jakaya mrisho kikwete. Hakuna mwingine zaidi yake. Historia itamhukumu kwa hili.

Bwana asifiwee! Isiwe sababu! Udini hoyeee!
 
Mtu aliyeimaliza na kuliangamiza kabisa taifa hili ni Jakaya Mrisho Kikwete. Hakuna mwingine zaidi yake. Historia itamhukumu kwa hili.

Mnyonge na anyongwe lkn HAKI yake mpeni. Huyo jamaa amechangia 80% kuimaliza Tz, sema kwa vile hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari hivyo yalikuwa yakinenwa chinichini. Huyu Mkere anajaribu kukomba na yeye sbb apate fadhila japo kdg ametoka mbali na Nchi hii. Pamoja na anayoyafanya na hkk kama waliopita waliweka vyema kwa huyu jamaa ni mwema kuliko Dr. Omar Ali Juma (Hayati) M/Mungu ailaze ROHO yake mahali pema PEPONI. Kikwete si mbaya hivyo ila wema wake umemponza, sasa kugeuka amechelewa hivyo amekuwa mtu wa Vituko.
 
Lkn kwa asili huyu Mnyamwezi. Hivyo mizigo lawama ndiyo utamaduni wake. Anadondokewa na Nchi, na Tanzania na mbaya zaidi Muungano wkt wwt Tamko linatoka. EAC mambo si mambo. Looh! Jamani Mnyamwezi Mkere !
 
Hakuna asiye kuwa na mapungufu sema wanazidiana,ila utendaji wa mkapa ufisadi ulikuwa wa kutisha,upande wa jk tatizo undugu na urafiki mwingi kazini ndo maana mambo hayaendi.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
kuwa ombaomba ni tabia ya mtu, anayeamini katika kusaidiwa, Nchi hii bado ipo na ni tajiri sana, tatizo viongozi wetu hawajajua uongozi ni sayansi, na ili mtu afanikiwe lazima utaratibu ufuatwe.
 
Nenda LUSHOTO TANGA ndo utalijua JIJI.Ukimaliza nenda kiwira
 
Kuuza kwa bei ya kutupa migodi, bandari, mashirika ya uma, viwanda etc ....kuingia mikataba na wachina ni kama ameimalizia nchi . Sasa kamfanya kikwete awe ombaomba

We hujui hata unachokiandika,aloimaliza hii nchi ni JAKAYA KHALFANI MRISHO KIKWETE,Mungu atamlaani huyu.
 
Na watu wengine kupenda kuabudu lugha za kigeni kuliko lugha yako ni utumwa.
Samahani !hivi kulikua na umuhim wa kuandika kwa lugha hii ya kigeni kwa ajili ya kuchangia hili??? ungeeleweka zaidi kama ungetumia lugha halisi ya kiswahili.asante
 
Si aliingia madarakani kwa gia kubwa ya "ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" "mkinichagua nitaipitia tena mikataba ya uchimbaji wa madini ili kuhakikisha inakuwa na maslahi kwa Tanzania na Watanzania" na usanii chungu nzima mwingine. Kwenye swala la EPA na Richmond/Dowans akawa upande mmoja na mafisadi hadi leo hii wahusika wakubwa wa EPA bado wanatesa mtaani kwa raha zao na mafisadi wa Richmond/Dowans bado wanasubiri na bakuli lao ili wakusanye mgao wao karibu $100 millioni pamoja na kuidanganya Serikali kumbe hawana uwezo wowote wa kufua umeme.

Kwenye swala na Kagoda na Meremeta pia angeweza kusimama kidete ili kuona Watanzania tunaujua ukweli wa kile kilichojiri na hatimaye wahusika wote wa ufisadi ule wanapandishwa kizimbani lakini akazembea tena kwa kisingizio cha "siri za Serikali." Huyu ni chaguo la mafisadi naye anastahili lawama zote za kuingiza nchi kwenye mkenge sawa na maamuzi mbali mbali ya Mkapa ambayo yameigharimu sana nchi yetu na yataendelea kuigharimu kwa miaka mingi ijayo.


Sasa kikwete angefanyaje . Kakuta kila kimeuzwa. Hadi posta na simu. Nyumba za oysterbay. Watu walichukua hela bot EPA . Watu watamuhukumu kikwete bure. Ndio maana kaamua kuwa mzururaji
 
Kuuza kwa bei ya kutupa migodi, bandari, mashirika ya uma, viwanda etc ....kuingia mikataba na wachina ni kama ameimalizia nchi . Sasa kamfanya kikwete awe ombaomba

Acheni unafiki, hao ni walewale kasoro majina,MKAPA or JK wote .....zi tu.
 
Back
Top Bottom