Mkapa na kiswahili

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
pamoja na mapungufu yake yote, Rais mstaafu Ben Mkapa kutokana na kutumia kiswahili fasaha katika hotuba zake, alituachia maneno mengi ameyaingiza katika matumizi ya kila siku ya lugha yetu ya kiswahili ambayo uko nyuma yalikuwa hayatumiki.

Mfano: Miundombinu, mipango endelevu, mipango shirikishi, utandawazi, wigo wa uchumi na mengineyo.

Kilugha, hotuba za muheshimiwa huyu zilikuwa na mvuto sana iwe kiswahili au kiingereza.
 
Mkapa has an excellent command of the queens language. Ni comparison nzuri sana ya elimu ya university of east africa na udsm, Kikwete akiongea kiingereza sikai as comfortably kwenye kiti compared to when bm speaks
 
Hii lugha gani umeandika mkuu?
 
pamoja na mapungufu yake yote,Rais mstaafu Ben Mkapa kutokana na kutumia kiswahili fasaha katika hotuba zake,alituachia maneno mengi ameyaingiza katika matumizi ya kila siku ya lugha yetu ya kiswahili ambayo uko nyuma yalikuwa hayatumiki.

Mfano: Miundombinu,mipango endelevu,mipango shirikishi,utandawazi,wigo wa uchumi na mengineyo.

Kilugha,hotuba za muheshimiwa huyu zilikuwa na mvuto sana iwe kiswahili au kiingereza.

Mkuu Baba wa Tatu.
Hakuna binadamu awaye yote ambaye hana mapungufu.
Udhaifu wetu wanadamu ni kuwa tunaangalia mapungufu ya wenzetu tu bila kuangalia mazuri aliyoyafanya.

Mungu mbariki BW Mkapa.
 
pamoja na mapungufu yake yote,Rais mstaafu Ben Mkapa kutokana na kutumia kiswahili fasaha katika hotuba zake,alituachia maneno mengi ameyaingiza katika matumizi ya kila siku ya lugha yetu ya kiswahili ambayo uko nyuma yalikuwa hayatumiki.

Mfano: Miundombinu,mipango endelevu,mipango shirikishi,utandawazi,wigo wa uchumi na mengineyo.

Kilugha,hotuba za muheshimiwa huyu zilikuwa na mvuto sana iwe kiswahili au kiingereza.

usilisahau hili neno MAMBO

ndo salamu yake mkubwa hii 'the kitambi'
 
WaChina wangekuwa wanaangalia viongozi wao wanazungumza lugha gani ya kigeni wasingefika walipo.
 
Yaani inasikitisha sana watu wanavyojitahidi kutetea mambo hata yaliyowazi kabisa kwamba ni makosa. inakuwaje mtu unadiriki kumsifia kinara wa ufisadi. yaani inasikitisha sana. WaTz tuamke sasa.
Lugha ni jambo jingine hakika simnyimi haki yake kwamba amejitahidi kuendeleza na kukienzi kiswahili.
 
Wewe ndio bure kabisa, yaani mtu asisifiwe kwa mazuri yake? hao watanzania wenzako unaotaka waamke kwa style yako tuendelee kulala.

Mimi bwana Che Mkapa kwa lugha namuaminia sana CTERI PARIBUS
 
Kwenye hotuba na jinsi anavyojua kuongea excellent........labda na fani inamsadia maana nasikiaa ni mahiri sana kwenye fani yake uandishi wa habari...hasa za kiingereza
 
Kwenye hotuba na jinsi anavyojua kuongea excellent........labda na fani inamsadia maana nasikiaa ni mahiri sana kwenye fani yake uandishi wa habari...hasa za kiingereza

Kwamba "siliva Rweye" anaweza ata siku moja kufikia hata moja ya mia nane ya mheshimiwa Nkapa????
 
BM ni noma kwa lugha. iwe swahili au kimombo. uelewa wake wa mambo ni wakijivunia kama taifa. haiwezekani kiongozi mkuu wa nchii kujieleza mbele ya umma iwe ni issue. tutachanganua vp mstakabali bila kuteta kwa ufasaha
BIG UP CHENKAPAAAAAAAAAA......UKO JUUUUUUUUUUUUUU
 
Ni haki kusifu mazuri ya mtu. Mkapa alikuwa na mazuri mengi.

Neno "kurasimisha", yaani kufanya rasmi, hakulianzisha Mkapa? Ni neno linalokidhi maana inayokusudiwa vizuri mno!
 
Nadhani ni makosa kusema Mkapa ndio alianzisha haya maneno kama "kurasimisha" wakati neno "rasmi" lipo na lilikuwepo.

Leo mtu akisema "KLM imeambulisha Boeing 777" utasema yeye ndio kaanzisha neno "ambulisha" kwa sababu tu ni wewe ndio ulikuwa hujawahi kusikia neno "ambua" likitumika hivyo ?

Halafu sio lazima uwe muhariri wa Uhuru ndio ujue kutumia maneno kama hayo.

Tunaweza kusema Mkapa alikuwa anatumia Kiswahili kwa mapana kuzidi sisi lakini sio kusema ndio yeye alianzisha haya maneno.

Na hata kusema Mkapa alikuwa mzuri wa Kiswahili kuliko sisi bado haisemi lolote kuhusu umahiri wake mpaka ujibu swali, sisi tunajua Kiswahili kiasi gani ? Kwenye kundi la samaki papa huwa anaonekana ndio kilele cha uumbaji. Kizazi hiki cha "Saint Mary's Education," cha "Diaspora Generation" kumsifia Mkapa Kiswahili sio ajabu. Avumae baharini.
 
pamoja na mapungufu yake yote,Rais mstaafu Ben Mkapa kutokana na kutumia kiswahili fasaha katika hotuba zake,alituachia maneno mengi ameyaingiza katika matumizi ya kila siku ya lugha yetu ya kiswahili ambayo uko nyuma yalikuwa hayatumiki.

Mfano: Miundombinu,mipango endelevu,mipango shirikishi,utandawazi,wigo wa uchumi na mengineyo.

Kilugha,hotuba za muheshimiwa huyu zilikuwa na mvuto sana iwe kiswahili au kiingereza.

Kwa mazuri aliyotenda hatoacha kupokea sifa na kwa mabaya hatutoacha kumkosoa.
Mkapa alikataa ile dhana ya kuitwa MTUKUFU RAIS. Kweli hotuba zake zilikuwa fasaha katika lugha/matumizi ya lugha. Nakumbuka wakati moja alisema nanukuu "watanzania ni wavivu wa kufikiri" wadau wakaja juu wakati kwa tazamo wangu ni ukweli mtupu!
 
Former President Mkapa is individual intellectual we have in Tanzania for moment,regardless to the many allegations during his term in office,I do not know the current government will match this status.[Too much in their plate to handle]
 
Kawaida wanaotoa tafsiri sanifu ya maneno ya kiingereza kwenda kiswahili hapa Tanzania ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya UDSM. Hivyo basi, ni kawaida pia kwa taasisi za Serikali kuwasiliana na BAKITA pale ambapo kuna neno la Kiingereza ambalo kiswahili chake hakijulikani kwa ufasaha. Ninaamini ni BAKITA ndo inayofanya hiyo kazi. Kama mkapa alitumia msamiati wa kiswahili ambao wengi wetu ndo ilikuwa mara ya kwanza kusikia, ni wazi chimbuko lake ni BAKITA na maneno hayo huwa yapo na mtumiaji anatumia neno kwa kuwa tayari lipo kwenye misamiati.

Kwa hiyo maneno ya kiingereza kama Formalize (Rasimisha), Formalization (Kurasimisha), yalikuwepo. Maneno kama TAKRIMA (kwa maana ya kukarimu) yalikuwepo. Ukitaka kujua maneno haya kwamba yalikuwepo tafuta Kamuzi ya TUKI toleo la mwaka 1991 (?).

Ninakumbuka Marehemu Mwalimu J.K. Nyerere ndiye alileta msamiati wa neno "hodhi" (monopoly), "kuhodhi" (monopolization). Lakini pia baadhi ya maneno aliyatoa kwenye kizanaki kwa mfani neno Mkurugenzi (Director).

Tuendelee kujadili..............
 
Back
Top Bottom