Mkapa na Gazeti la RAI

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,944
703
Nimetembelea gazeti la Rai kusoma habari za nyumbani baada ya kukosa magazeti niyapendayo kwenye mtandao. Mimi si mpenzi wa gazeti la RAI kwa sababu baadhi waandishi wa gazeti hili hawapendi kuzungumzia habari ambayo inamhusu kwa njia moja au nyingine Mmiliki wa gazeti hilo. Nitatoa mfano: Hivi karibuni kulikuwa na Warsha/Semina iliyokuwa ikizungumzia kuhusu maboresho ya utawala bora katika kupambana na rushwa. Hii semina ilikuwa ikiendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la African International Political Risk Analysis (PORIS). Rai ilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa PCCB Bw. Hosea kuhusu kesi kubwa za rushwa ambazo wanazifanyia kazi na haya ndiyo majibu ya Hosea na ninanukuu hapa chini.

“Tumejiwekea malengo ya kuchunguza na kukamilisha kesi 10 kila mwaka. Mwaka huu kufikia Julai tutakuwa tumekamilisha kesi tano za kwanza… hizi ni kesi za rushwa kubwa kubwa. Na tabia ya kesi za rushwa kubwa ni kwamba inakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, wahusika huwa ni watu wakubwa, kiasi cha rushwa kinachohusishwa ni kikubwa, eneo la uchunguzi wake huvuka mipaka ya ndani na nchi za nje, zinahusisha maandiko mengi, zinahitaji kiasi kikubwa kwa uchunguzi na huvuta hisia za jamii.

“Hatujapotea njia na tunaomba wadau wote kutuunga mkono sisi kama PCCB, kwani mapambano ya rushwa si kazi ya PCCB na serikali pekee. Ni mapambano yanayohitaji wadau wote, kwani inatuathiri sote kijamii, kiuchumi na kisiasa,”

Kama mtaona hapo kwenye majibu ya Hosea hakudiriki kutaja hata mtu au kampuni mojawapo iliyomo katika hizo kesi 10. Lakini Rai ilisema kutokana na uchunguzi imebaini katika kesi hizo kuna ile ya mgodi wa dhahabu uliopo Kahama wa Buzwagi, kampuni ya Tangold, Meremeta, Mwananchi Gold, Alex Stuart (ilikuwa inakagua madini), maghorofa pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Deep Green, Kiwira Coal Mines na ununuzi wa Rada kutoa kampuni ya BAe Systems ya Uingereza.
Ukihesabu hapo unaona ni kesi 9 tu badala ya 10. Sasa sielewi kama wameacha hiyo ya 10 kwa makusudi au vipi. Na ya 10 itakuwa ni RICHMOND na kwa kuwa Bosi wao anahusika basi hawakuona umuhimu wa kuijulisha jamii kuwa hata RICHMOND ni mojawapo ya kesi 10 ambazo zitafanyiwa kazi kabla ya 2010.

Hiyo ni moja ya kasoro ambayo inanifanya nisitegemee kupata habari za nyumbani kupitia gazeti hilo.

Anyway, nirudi kwenye KIINI cha HEADING yangu "MKAPA NA GAZETI LA RAI"
Katika gazeti hili hili na toleo hili hili (1712 EAT) kuna habari yenye kichwa kisemacho "WANANCHI WAHOFIA MKAPA KUCHUNGUZWA" Yaani hii imenishangaza sana kwa gazeti hilo kuandika kitu kama hicho. Ukisoma kwa undani zaidi utaona watu waliohojiwa ni 3 na kati ya hao 2 ni makada wa CCM yaani Kakobe na huyo mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe. Sasa mie sielewi kama hao 3 wanawakilisha majority ya watanzania.
Watanzania wa leo si wa mwaka 1922, watu wanaelewa ni nini kinaendelea. Leo huwezi kuja kutueleza kuwa kuchunguzwa kwa MKAPA kutazua machafuko na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tanzania hatuna dola ya KIFALME, mtu akitenda kosa na ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Zambia au Malawi yalitokea machafuko gani baada ya kuwafikisha waliokuwa watawala mbele ya sheria?? Hiyo RAI haijawahi kufanya tathmini nchini kuona ni madhara gani ambayo wananchi wanapata kutokana na UFISADI wa MKAPA na vilevile tathmini ya kuona ni watanzania wangapi wanaunga mkono hoja ya MKAPA kuchunguzwa.

Kwa mtazamo wangu naona gazeti hili la RAI wanajaribu kutumia taaluma yao kuwaogopesha wananchi kuwa yatatokea machafuko wakimchunguza MKAPA. RAI wanajaribu kuangalia INTEREST za MAFISADI akiwamo na BOSI wao. Ndiyo nimesema akiwamo na BOSI WAO. Yatakuwa yaleyale oh tukiwa na mfumo wa vyama vingi yatatokea yale ya RWANDA, shut the hole.
Sheria haina mkubwa wala mdogo, Rais au Katibu tarafa, Jenerali au Koplo wote ni watanzania sawa na ukitenda kosa unatakiwa uwajibishwe kwa mujibu wa sheria na si kuanza kuwaogopesha wananchi eti kutakuwa na machafuko. Watanzania wanaelewa sana ni nini kinaweza kuleta machafuko eg. Kukalia kimya UFISADI, NJAA, UKABILA, UDINI na takataka zingine zinazofanana na hayo.

RAI KUWENI MAKINI NA HABARI ZENU NA ANDIKENI YA UKWELI YANAYOMHUSU HATA BOSI WENU ROST-TAMU AZ-IZ
 
Ndugu yangu nakuunga mkono kwa asilimia 100, Mkapa ni raia kama raia wengine, awajibishwe kama wanavyowajibishwa raia wengine. Ametuingiza kwenye matatizo makubwa, Yeye pamoja na genge lake la mafisadi wamekomba kila kitu na sasa wamekaa kimya wanajifanya MABUBU. Huyu Mkapa si ndiye alikuwa bingwa wa kuongea wakati alipokuwa madarakani??? Inakuwaje sasa hawezi kuongea hata sentensi moja??? Angalau aseme "HAPANA MIMI SIKUIBA, MNANISINGIZIA" Je mmemusahau yule aliyetuambia watanzania "HATA IKILAZIMU WATANZANIA KULA MAJANI, LAKINI NDEGE YA RAIS ITANUNULIWA" Jiulize huyu Mramba alipata wapi hiyo jeuri kama si kwa Mkapa???

Naomba Hosea na timu yake waendelee na uchunguzi na waongeze kasi ili siku ikidhibitika kwamba hawa watu wana makosa sheria ichukue nafasi yake, ADHABU YA KWANZA NI VIBOKO 12 KWA KILA MMOJA PALE UWANJA MPYA WA TAIFA, BAADAE JELA.
 
Indume Yene, mbona unapigia mstari majibu? Haya yote watanzania wa kawaida wanayajua, hamna kitu mpya hapoo, lakini nashukuru kwa kutumia muda wako kuwakumbusha kumbusha wenye kujisahaulisha. Huyu Rutashobya anamuomba Hosea na PCCB waendelee na uchunguzi, hawapaswi kuombwa bali kufanya kazi ambayo wanalipwa pesa nyingi za walalahoi. siyo maombi hapa, kwa sababu na wao tutawachunguza. Unakumbuka kuwa wanalo deni la kujisafisha kwa kutuambia uongo hapo nyuma karibu tu?
Big up wasema ukweli kwa sauti kubwa!!
 
Huyu Hosea katika ripoti ya Mwakyembe kuhusiana na Richmond si walitoa ushauri huyu fisadi Hosea aondolewe hapa TAKUKURU sasa bado anangoja nini hadi hii leo? Yaani kkuna vitu vingine vinasikitisha mpaka unakasirika. Tume iliundwa na mwenyewe muungwana inatoa mapendekezo kuhusiana na kazi waliyotumwa lakini mapendekezo hayo hayafanyiwi kazi na siku zinayoyoma tu! Halafu wakiitwa wasanii wanalalama!
 
Unasema?..
 
Nimetembelea gazeti la Rai kusoma habari za nyumbani baada ya kukosa magazeti niyapendayo kwenye mtandao. Mimi si mpenzi wa gazeti la RAI kwa sababu baadhi waandishi wa gazeti hili hawapendi kuzungumzia habari ambayo inamhusu kwa njia moja au nyingine Mmiliki wa gazeti hilo. Nitatoa mfano: Hivi karibuni kulikuwa na Warsha/Semina iliyokuwa ikizungumzia kuhusu maboresho ya utawala bora katika kupambana na rushwa. Hii semina ilikuwa ikiendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la African International Political Risk Analysis (PORIS). Rai ilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa PCCB Bw. Hosea kuhusu kesi kubwa za rushwa ambazo wanazifanyia kazi na haya ndiyo majibu ya Hosea na ninanukuu hapa chini.

“Tumejiwekea malengo ya kuchunguza na kukamilisha kesi 10 kila mwaka. Mwaka huu kufikia Julai tutakuwa tumekamilisha kesi tano za kwanza… hizi ni kesi za rushwa kubwa kubwa. Na tabia ya kesi za rushwa kubwa ni kwamba inakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, wahusika huwa ni watu wakubwa, kiasi cha rushwa kinachohusishwa ni kikubwa, eneo la uchunguzi wake huvuka mipaka ya ndani na nchi za nje, zinahusisha maandiko mengi, zinahitaji kiasi kikubwa kwa uchunguzi na huvuta hisia za jamii.

“Hatujapotea njia na tunaomba wadau wote kutuunga mkono sisi kama PCCB, kwani mapambano ya rushwa si kazi ya PCCB na serikali pekee. Ni mapambano yanayohitaji wadau wote, kwani inatuathiri sote kijamii, kiuchumi na kisiasa,”

Kama mtaona hapo kwenye majibu ya Hosea hakudiriki kutaja hata mtu au kampuni mojawapo iliyomo katika hizo kesi 10. Lakini Rai ilisema kutokana na uchunguzi imebaini katika kesi hizo kuna ile ya mgodi wa dhahabu uliopo Kahama wa Buzwagi, kampuni ya Tangold, Meremeta, Mwananchi Gold, Alex Stuart (ilikuwa inakagua madini), maghorofa pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Deep Green, Kiwira Coal Mines na ununuzi wa Rada kutoa kampuni ya BAe Systems ya Uingereza.
Ukihesabu hapo unaona ni kesi 9 tu badala ya 10. Sasa sielewi kama wameacha hiyo ya 10 kwa makusudi au vipi. Na ya 10 itakuwa ni RICHMOND na kwa kuwa Bosi wao anahusika basi hawakuona umuhimu wa kuijulisha jamii kuwa hata RICHMOND ni mojawapo ya kesi 10 ambazo zitafanyiwa kazi kabla ya 2010.

Hiyo ni moja ya kasoro ambayo inanifanya nisitegemee kupata habari za nyumbani kupitia gazeti hilo.

Anyway, nirudi kwenye KIINI cha HEADING yangu "MKAPA NA GAZETI LA RAI"
Katika gazeti hili hili na toleo hili hili (1712 EAT) kuna habari yenye kichwa kisemacho "WANANCHI WAHOFIA MKAPA KUCHUNGUZWA" Yaani hii imenishangaza sana kwa gazeti hilo kuandika kitu kama hicho. Ukisoma kwa undani zaidi utaona watu waliohojiwa ni 3 na kati ya hao 2 ni makada wa CCM yaani Kakobe na huyo mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe. Sasa mie sielewi kama hao 3 wanawakilisha majority ya watanzania.
Watanzania wa leo si wa mwaka 1922, watu wanaelewa ni nini kinaendelea. Leo huwezi kuja kutueleza kuwa kuchunguzwa kwa MKAPA kutazua machafuko na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Tanzania hatuna dola ya KIFALME, mtu akitenda kosa na ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Zambia au Malawi yalitokea machafuko gani baada ya kuwafikisha waliokuwa watawala mbele ya sheria?? Hiyo RAI haijawahi kufanya tathmini nchini kuona ni madhara gani ambayo wananchi wanapata kutokana na UFISADI wa MKAPA na vilevile tathmini ya kuona ni watanzania wangapi wanaunga mkono hoja ya MKAPA kuchunguzwa.

Kwa mtazamo wangu naona gazeti hili la RAI wanajaribu kutumia taaluma yao kuwaogopesha wananchi kuwa yatatokea machafuko wakimchunguza MKAPA. RAI wanajaribu kuangalia INTEREST za MAFISADI akiwamo na BOSI wao. Ndiyo nimesema akiwamo na BOSI WAO. Yatakuwa yaleyale oh tukiwa na mfumo wa vyama vingi yatatokea yale ya RWANDA, shut the hole.
Sheria haina mkubwa wala mdogo, Rais au Katibu tarafa, Jenerali au Koplo wote ni watanzania sawa na ukitenda kosa unatakiwa uwajibishwe kwa mujibu wa sheria na si kuanza kuwaogopesha wananchi eti kutakuwa na machafuko. Watanzania wanaelewa sana ni nini kinaweza kuleta machafuko eg. Kukalia kimya UFISADI, NJAA, UKABILA, UDINI na takataka zingine zinazofanana na hayo.

RAI KUWENI MAKINI NA HABARI ZENU NA ANDIKENI YA UKWELI YANAYOMHUSU HATA BOSI WENU ROST-TAMU AZ-IZ
Rostam Aziz. ..TUMWACHIE MAULANA. .
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom