Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Mwisho mwa mwezi huu kutafanyika vikao vya NEC (CCM) kwa siku mbili kijijini Butiama ambako ndiko alikozaliwa Muasisi wa chama hicho Marehemu Mwl. Julius K. Nyerere. Baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuwa katika agenda ni:-
1. Mustakhabali na muelekeo wa chama hicho baada ya kukumbwa na gharika la mafisadi.
2. Muafaka kati ya CCM na CUF huko Zanzibar.
Sikutaja mengine kwa sababu nina hakika haya lazima yatajadiliwa. Kitu ambacho naamini kila mtu atakuwa na shauku kubwa kuona au kusikia ni jinsi gani hicho chama chini ya Uongozi wa JK kitakapoweza kukaripia au kutoa adhabu dhidi watu ambao kwa njia moja au nyingine wamehusishwa na hizo tuhuma za ufisadi.
Wajumbe wa NEC ambao wemehusihwa na UFISADI ni:-
1. Ben Mkapa (Rais mstaafu)
2. Rostam Aziz (Tabora)
3. Nazir Karamagi (Kagera)
4. Edward Lowassa (Kutoka viti 20 Bara)
Sasa utamu upo hapa kwa Ben Nkapa, naamini Mwl. Nyerere alipozunguka nchi nzima kumnadi Nkapa aliamini kuwa ni kijana wake swaaaaaaaaafi kabisa, kumbe ndani yake kulikuwa na kipande cha chuma chenye kutu. Akafanya kinyume na Mwl. Nyerere na watanzania wengine walivyofikiria kwa kuichukulia mali ya serikali au kufanya bizinee wakati akiwa bado ndani ya jumba Jeupe. Sasa katika kikao hicho ambacho kitafanyika huko alikozikwa Mwl. Nyerere sijui huyu jamaa ataweza kuji-feel guilty na kuja mbele ya Public nakueleza utumbo na ufisadi aliofanya na watu wake wa karibu i.e Yona, Anna Mkapa na wengineo. Maana kawa Bubu hata hataki kuzungumzia kile ambacho watanzania wanakipigia kelele.
Yeye alikuwa anajulikana kwa ubabe, NATAKA HIKI KIFANYIKE, NATAKA HUYU APELEKWE PALE, NATAKA HIKI KIWE CHANGU. Sasa kwa nini asitumie ubabe huo huo akasema "SASA NATAKA NIONANE NA WAANDISHI WA HABARI au SASA NATAKA KUJIBU TUHUMA" Naamini BWM naye ni mcha Mungu hivyo nafikiri hiyo nafasi ya kwenda Butiama angeitumia vizuri aungame kwa watanzania mbele ya kaburi la Mwl. Nyerere maana CCM kupeleka hicho kikao huko wana moja yao kichwani. Nahisi lakini sina uhakika, inawezekana wanataka kusafisha chama ingawa ninaona ni ngumu sana maana mafisadi humo wamo kibao na wana influence, vilevile EPA haiko mbali na mlango wao maana tunaambiwa kuwa baadhi ya hizo pesa zilisaidia kampeni ya Muungwana. Sasa sijui wataanza kusafisha kuanzia kwa nani. FISADI NI FISADI na alishazoea ufisadi, kuja kuuacha ufisadi pasipo kuacha maumivu kwa wengine itakuwa ni kazi. Labda wapewe karipio na si kufukuzwa uanachama maana watakwenda wengi kwa ule mtindo wa "SIFI PEKE YANGU"
Utamu wa pesa hizo za EPA anaujua JK, BWM, EL, RA na wengineo maana ndizo zilizowaweka hapo walipo. Oh eti Mkapa aachwe apumzike alishastaafu, Shut the hole. Fisadi tangu lini anastaafu na wakati anazidi ku-generate mapato yake na familia yake kupitia fedha za kiharamu. Hataki kumhoji maana wanajua kazi yake waliyompa afanye kutumia umafia na ufisadi wake kuhakikisha CCM na JK wanaingia madarakani kaimaliza na ndiyo maana unaona hata Chenge anazidi kupeta coz alijua hizo deals.
Anyway, naamini watanzania wanasuburi kwa hamu kusikia maamuzi yatakayotolewa na NEC ambayo itahudhuriwa na MAFISADI. Vilevile kuona Emotions gani ambazo Mkapa ataonyesha kwa kumsaliti Baba wa Taifa na watanzania wengine.
Mkuu hapa Bangusilo umemsahau au?Wajumbe wa NEC ambao wemehusihwa na UFISADI ni:-
1. Ben Mkapa (Rais mstaafu)
2. Rostam Aziz (Tabora)
3. Nazir Karamagi (Kagera)
4. Edward Lowassa (Kutoka viti 20 Bara)
kitakuwa ni matope tupu.Unafikiri mwizi ana aibu? Wao wanajiona ni wajanja na wala sio wezi. Tusitegemee makubwa kwenye hicho kikao juu ya ufisadi maana wote hao ni kundi moja. Labda suala la muafaka litapata ufumbuzi.
CCM wanamtumia tu Mwalimu Nyerere. Familia yake ingelikuwa na nguvu, ingewakatalia na kusema mpaka wahakikishe suala la ufisadi limeshughulikiwa.
Bahati mbaya hawawezi kusema hivyo maana hata wao wanafaidika na ulaji ndani ya Chama. Makongoro anaona hiyo ndio nafasi ya kutanua.
Bila kutoa report ya EPA na kushughulikia wahusika, kwa kweli hicho chama
Mkapa na wenzie mafisadi wakihudhuria NEC Butiama Itasikika sauti kutoka kaburi la Mwalimu ikitamka:
"Wewe Ben ulikuwa chaguo langu nika zunguka nchi nzima kukunadi baada kufariki mie kumbe umekuwa FISADI MKUBWA!
haya wewe na mafisadi wenzio ondekeni haraka Butiama sitaki muonakane hapa MAFISADI WAKUBA nyie"
"Na wewe Lowasa unatafuta nini hapa Butiama umewafilisi Watanzania na mikataba yako mibovu ya Richmond ondoka haraka FISADI WAHEDI"
"Na wewe Karamagi nini kimekuleta hapa Butiama unaitafuna nchi bila aibu kila scandal upo buzwagi upo,Richmond upo Tics upo!Potea haraka Butiama" FISADI USIYE KUWA NA HAYA"
"Na wewe Bwana Mdogo Rostam BABA WA MAFISADI huna hata sura ya aibu kuja hapa Butiama?Umechota pesa za watanzania huko benki kuu bila aibu?Umeshirikiana na huyo FISADI mwenzio Lowasa kuingiza nchi kwenye mkataba ya Richmond"Haya nawe usionekane hapa Butiama tiimka haraka!
"Na wewe Kijana Kikwete nitakuita Baadae nikueleze madhaifu yake"
Mkapa anaweza kutoa makucha yake butiama na kumgeuzia kibao JK. Nadhani ana hasira naye sana kwa sababu inaonekana wazi kabisa kwamba mashambulizi yote kwake kupitia media yana baraka za JK.
Halafu japokuwa sina takwimu lakini nadhani wajumbe kwenye vikao vyote viwili wakiwekwa kwenye makundi JK atakuwa na minority upande wake. Mkapa atakuwa na sauti zaidi kwa sababu ndani ya hivyo vikao majeruhi wa ufisadi ni wengi kuliko walio wasafi. JK atapewa onyo kali na kuambiwa asiendelee kamwe kukiweka chama kwenye vulnerable situation kama kilivyo sasa.
Mkapa na mafisadi watatoka kifua mbele. JK ambaye tayari ameonesha udhaifu wa kuwashughulikia mafisadi kwa nguvu atatoka dhaifu zaidi na zaidi.
Du Balahau. Hii kali. Ni ya kuitafakari.Mkapa anaweza kutoa makucha yake butiama na kumgeuzia kibao JK. Nadhani ana hasira naye sana kwa sababu inaonekana wazi kabisa kwamba mashambulizi yote kwake kupitia media yana baraka za JK.
Halafu japokuwa sina takwimu lakini nadhani wajumbe kwenye vikao vyote viwili wakiwekwa kwenye makundi JK atakuwa na minority upande wake. Mkapa atakuwa na sauti zaidi kwa sababu ndani ya hivyo vikao majeruhi wa ufisadi ni wengi kuliko walio wasafi. JK atapewa onyo kali na kuambiwa asiendelee kamwe kukiweka chama kwenye vulnerable situation kama kilivyo sasa.
Mkapa na mafisadi watatoka kifua mbele. JK ambaye tayari ameonesha udhaifu wa kuwashughulikia mafisadi kwa nguvu atatoka dhaifu zaidi na zaidi.
Alipotutukana kutwambia kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri na tuna wivu wa hali ya juu kwa kumuona kila aliye tajiri amepata utajiri kwa njia za haramu hakujua kama kibao kinaweza kikamgeukia. Sasa kibao kimegeuka hata kusema tena hataki anaishi kwa wasi wasi mkubwa na Watanzanai tutalala naye mbele mpaka kieleweke kuhusiana na ufisadi mkubwa alioufanya fisadi huyu.
Kama ningekuwa na uwezo hata huko Butiama asingehudhuria hicho kikao.
Sisi waTZ ni wavivu sana wa kufikiri,sidhani kama tungekuwa tunafikiri kwa bidii leo tungekuwa tunaishaabikia CCM.Na kama tungekuwa tunafikiri kwa bidii sidhani kama watanzania wangemuona Mkapa ni mbaya.
Mkapa anaweza kutoa makucha yake butiama na kumgeuzia kibao JK. Nadhani ana hasira naye sana kwa sababu inaonekana wazi kabisa kwamba mashambulizi yote kwake kupitia media yana baraka za JK.
Halafu japokuwa sina takwimu lakini nadhani wajumbe kwenye vikao vyote viwili wakiwekwa kwenye makundi JK atakuwa na minority upande wake. Mkapa atakuwa na sauti zaidi kwa sababu ndani ya hivyo vikao majeruhi wa ufisadi ni wengi kuliko walio wasafi. JK atapewa onyo kali na kuambiwa asiendelee kamwe kukiweka chama kwenye vulnerable situation kama kilivyo sasa.
Mkapa na mafisadi watatoka kifua mbele. JK ambaye tayari ameonesha udhaifu wa kuwashughulikia mafisadi kwa nguvu atatoka dhaifu zaidi na zaidi.
Mkapa anaweza kutoa makucha yake butiama na kumgeuzia kibao JK. Nadhani ana hasira naye sana kwa sababu inaonekana wazi kabisa kwamba mashambulizi yote kwake kupitia media yana baraka za JK.
Halafu japokuwa sina takwimu lakini nadhani wajumbe kwenye vikao vyote viwili wakiwekwa kwenye makundi JK atakuwa na minority upande wake. Mkapa atakuwa na sauti zaidi kwa sababu ndani ya hivyo vikao majeruhi wa ufisadi ni wengi kuliko walio wasafi. JK atapewa onyo kali na kuambiwa asiendelee kamwe kukiweka chama kwenye vulnerable situation kama kilivyo sasa.
Mkapa na mafisadi watatoka kifua mbele. JK ambaye tayari ameonesha udhaifu wa kuwashughulikia mafisadi kwa nguvu atatoka dhaifu zaidi na zaidi.
Re: Mkapa kuhudhuria NEC Butiama?
Majibu yangu naomba niyaelekeze kwa kichwa cha habari cha thread.
Rais mstaafu. Mh. Benjamini William Mkapa anahudhuria kikao cha CC na then NEC kwa kuwa ni mjumbe wa vikao hivyo, period.
Kikao hiki ni cha Kihistoria kwa sababu moja tu na ambayo imejileta yenyewe nayo ni issue ya Muafaka wa Zanzibar na Serikali ya Mseto.
Mengine ya ufisadi hayatajadiliwa kwenye NEC, CC kwa kuwa kamati za Serikali zinazoendelea na mambo ya ufisadi hazijamaliza kazi zake... na Mwenyekiti atasema tunasubiri mapendekezo ya task force ya waziri mkuu.
Mengine mtakayojadili ni marudio ya yale ambayo tumeshayasema kwa muda mrefu.