Mkapa kuhudhuria NEC Butiama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa kuhudhuria NEC Butiama?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Indume Yene, Mar 19, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwisho mwa mwezi huu kutafanyika vikao vya NEC (CCM) kwa siku mbili kijijini Butiama ambako ndiko alikozaliwa Muasisi wa chama hicho Marehemu Mwl. Julius K. Nyerere. Baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuwa katika agenda ni:-
  1. Mustakhabali na muelekeo wa chama hicho baada ya kukumbwa na gharika la mafisadi.

  2. Muafaka kati ya CCM na CUF huko Zanzibar.

  Sikutaja mengine kwa sababu nina hakika haya lazima yatajadiliwa. Kitu ambacho naamini kila mtu atakuwa na shauku kubwa kuona au kusikia ni jinsi gani hicho chama chini ya Uongozi wa JK kitakapoweza kukaripia au kutoa adhabu dhidi watu ambao kwa njia moja au nyingine wamehusishwa na hizo tuhuma za ufisadi.

  Wajumbe wa NEC ambao wemehusihwa na UFISADI ni:-
  1. Ben Mkapa (Rais mstaafu)
  2. Rostam Aziz (Tabora)
  3. Nazir Karamagi (Kagera)
  4. Edward Lowassa (Kutoka viti 20 Bara)

  Sasa utamu upo hapa kwa Ben Nkapa, naamini Mwl. Nyerere alipozunguka nchi nzima kumnadi Nkapa aliamini kuwa ni kijana wake swaaaaaaaaafi kabisa, kumbe ndani yake kulikuwa na kipande cha chuma chenye kutu. Akafanya kinyume na Mwl. Nyerere na watanzania wengine walivyofikiria kwa kuichukulia mali ya serikali au kufanya bizinee wakati akiwa bado ndani ya jumba Jeupe. Sasa katika kikao hicho ambacho kitafanyika huko alikozikwa Mwl. Nyerere sijui huyu jamaa ataweza kuji-feel guilty na kuja mbele ya Public nakueleza utumbo na ufisadi aliofanya na watu wake wa karibu i.e Yona, Anna Mkapa na wengineo. Maana kawa Bubu hata hataki kuzungumzia kile ambacho watanzania wanakipigia kelele.
  Yeye alikuwa anajulikana kwa ubabe, NATAKA HIKI KIFANYIKE, NATAKA HUYU APELEKWE PALE, NATAKA HIKI KIWE CHANGU. Sasa kwa nini asitumie ubabe huo huo akasema "SASA NATAKA NIONANE NA WAANDISHI WA HABARI au SASA NATAKA KUJIBU TUHUMA" Naamini BWM naye ni mcha Mungu hivyo nafikiri hiyo nafasi ya kwenda Butiama angeitumia vizuri aungame kwa watanzania mbele ya kaburi la Mwl. Nyerere maana CCM kupeleka hicho kikao huko wana moja yao kichwani. Nahisi lakini sina uhakika, inawezekana wanataka kusafisha chama ingawa ninaona ni ngumu sana maana mafisadi humo wamo kibao na wana influence, vilevile EPA haiko mbali na mlango wao maana tunaambiwa kuwa baadhi ya hizo pesa zilisaidia kampeni ya Muungwana. Sasa sijui wataanza kusafisha kuanzia kwa nani. FISADI NI FISADI na alishazoea ufisadi, kuja kuuacha ufisadi pasipo kuacha maumivu kwa wengine itakuwa ni kazi. Labda wapewe karipio na si kufukuzwa uanachama maana watakwenda wengi kwa ule mtindo wa "SIFI PEKE YANGU"
  Utamu wa pesa hizo za EPA anaujua JK, BWM, EL, RA na wengineo maana ndizo zilizowaweka hapo walipo. Oh eti Mkapa aachwe apumzike alishastaafu, Shut the hole. Fisadi tangu lini anastaafu na wakati anazidi ku-generate mapato yake na familia yake kupitia fedha za kiharamu. Hataki kumhoji maana wanajua kazi yake waliyompa afanye kutumia umafia na ufisadi wake kuhakikisha CCM na JK wanaingia madarakani kaimaliza na ndiyo maana unaona hata Chenge anazidi kupeta coz alijua hizo deals.

  Anyway, naamini watanzania wanasuburi kwa hamu kusikia maamuzi yatakayotolewa na NEC ambayo itahudhuriwa na MAFISADI. Vilevile kuona Emotions gani ambazo Mkapa ataonyesha kwa kumsaliti Baba wa Taifa na watanzania wengine.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,137
  Trophy Points: 280
  Alipotutukana kutwambia kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri na tuna wivu wa hali ya juu kwa kumuona kila aliye tajiri amepata utajiri kwa njia za haramu hakujua kama kibao kinaweza kikamgeukia. Sasa kibao kimegeuka hata kusema tena hataki anaishi kwa wasi wasi mkubwa na Watanzanai tutalala naye mbele mpaka kieleweke kuhusiana na ufisadi mkubwa alioufanya fisadi huyu.

  Kama ningekuwa na uwezo hata huko Butiama asingehudhuria hicho kikao.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Unafikiri mwizi ana aibu? Wao wanajiona ni wajanja na wala sio wezi. Tusitegemee makubwa kwenye hicho kikao juu ya ufisadi maana wote hao ni kundi moja. Labda suala la muafaka litapata ufumbuzi.

  CCM wanamtumia tu Mwalimu Nyerere. Familia yake ingelikuwa na nguvu, ingewakatalia na kusema mpaka wahakikishe suala la ufisadi limeshughulikiwa.

  Bahati mbaya hawawezi kusema hivyo maana hata wao wanafaidika na ulaji ndani ya Chama. Makongoro anaona hiyo ndio nafasi ya kutanua.

  Bila kutoa report ya EPA na kushughulikia wahusika, kwa kweli hicho chama
  kitakuwa ni matope tupu.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  asihudhurie kwa nini?
  yeye anakwenda kule kukutana na mafisadi wenziwe. na atakaemnyooshea kidole Ben anajua kuwa vinne vimemuelekea. wasi wasi upo wapi.
  hicho ni kikao cha mafisadi tu na sio vyengine
   
 5. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapa Bangusilo umemsahau au?

  Well mi nafikiri huyu BWM amefanya mengi sana katika kuifikisha Tanzania hapa ilipo sasa!! Alikuja na sera nyingi akijidai yeye ni mtu wa UWAZI na UKWELI lakini sikuwahi kuona huo uwazi wala ukweli ukiwekwa wazi.

  kitakuwa ni matope tupu.

  Mkuu hapa nakuunga mkono ni kweli wezi hujiona wajanja na hapa tunachokitaka kwanza kabisa Ishu ya Richmond hiyo Tume ya Waziri Mkuu ihakikishe mapendekezo yote yanafanyiwa kazi kama ilivyopendekezwa na Tume teule na Bunge letu Tukufu. Pili turudi kwenye EPA nako mafisadi wote wapewe haki yao asibaki hata mmoja na kama wataongeza msongamano kwenye magreza ni bora Muungwana akatoa msamaha kwa wazee na wagonjwa walioko magerezani ili wawaachie nafasi hawa wafungwa wapya wa UFISADI....

  Tanzania bila ufisadi inawekekana..!
   
 6. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mafisadi ndani ya CCM ni wengi sana, lakini kikubwa ni viongozi wa juu kuwa mafisadi zaidi ya walioko chini yao. Kusaidia chama cha mapinduzi na kwa wale wanaokipenda ni kukiua na kuunda chama kingine kipya ambapo hakutakuwa na Mtu anajiita Mwenyekiti sijui msataafu, au Mwenyekiti wa sasa.

  Dawa ya moto ni Moto tu. baada ya yapo wale wana CCM wasiopenda UFISADI wataweza kuinua vichwa vyao na kuweza kuongea wakiwa kifua mbele. lakini sasa watakwenda Butiama, Sijui Vatican na kwingineko ile MIFISADI ikishatuna mbele itakuwa ni kazi kuisema wazi wazi.

  Hili Mkapa asijadiliwe atakwenda na anaweza kufika wa kwanza.
   
 7. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mkapa na wenzie mafisadi wakihudhuria NEC Butiama Itasikika sauti kutoka kaburi la Mwalimu ikitamka:

  "Wewe Ben ulikuwa chaguo langu nika zunguka nchi nzima kukunadi baada kufariki mie kumbe umekuwa FISADI MKUBWA!
  haya wewe na mafisadi wenzio ondekeni haraka Butiama sitaki muonakane hapa MAFISADI WAKUBA nyie"

  "Na wewe Lowasa unatafuta nini hapa Butiama umewafilisi Watanzania na mikataba yako mibovu ya Richmond ondoka haraka FISADI WAHEDI"

  "Na wewe Karamagi nini kimekuleta hapa Butiama unaitafuna nchi bila aibu kila scandal upo buzwagi upo,Richmond upo Tics upo!Potea haraka Butiama" FISADI USIYE KUWA NA HAYA"

  "Na wewe Bwana Mdogo Rostam BABA WA MAFISADI huna hata sura ya aibu kuja hapa Butiama?Umechota pesa za watanzania huko benki kuu bila aibu?Umeshirikiana na huyo FISADI mwenzio Lowasa kuingiza nchi kwenye mkataba ya Richmond"Haya nawe usionekane hapa Butiama tiimka haraka!

  "Na wewe Kijana Kikwete nitakuita Baadae nikueleze madhaifu yake"
   
 8. H

  Hussein Abdallah Member

  #8
  Mar 19, 2008
  Joined: Nov 1, 2006
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Umesahu na wewe JK unafiki na kula na mafisadi na kuogopa kua act kama Mkuu wa Nchi wote nyie mafisadi mmefuata nini hapa .
   
 9. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkapa anaweza kutoa makucha yake butiama na kumgeuzia kibao JK. Nadhani ana hasira naye sana kwa sababu inaonekana wazi kabisa kwamba mashambulizi yote kwake kupitia media yana baraka za JK.

  Halafu japokuwa sina takwimu lakini nadhani wajumbe kwenye vikao vyote viwili wakiwekwa kwenye makundi JK atakuwa na minority upande wake. Mkapa atakuwa na sauti zaidi kwa sababu ndani ya hivyo vikao majeruhi wa ufisadi ni wengi kuliko walio wasafi. JK atapewa onyo kali na kuambiwa asiendelee kamwe kukiweka chama kwenye vulnerable situation kama kilivyo sasa.

  Mkapa na mafisadi watatoka kifua mbele. JK ambaye tayari ameonesha udhaifu wa kuwashughulikia mafisadi kwa nguvu atatoka dhaifu zaidi na zaidi.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  You might have a point on this .Kweli umesema maneno akili imezunguka hapa .So watanzania wasitegemee lolote .
   
 11. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du Balahau. Hii kali. Ni ya kuitafakari.
   
 12. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45

  Hayo maneno niliyo-bold hapo juu.KWANI NI UONGO???
  Sisi waTZ ni wavivu sana wa kufikiri,sidhani kama tungekuwa tunafikiri kwa bidii leo tungekuwa tunaishaabikia CCM.Na kama tungekuwa tunafikiri kwa bidii sidhani kama watanzania wangemuona Mkapa ni mbaya.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli na kweli tupu. Zaidi ya hayo, tungekuwa na juhudi za kufikiri leo hii tusingeuona ufisadi kama zimwi tulilolishindwa, ingekuwa tumeshalimaliza.

  Huko Butiama wanakokwenda ni usanii mwingine unachorwa. Ngoja wakimaliza uone watakavyojitapa kwamba walikwenda kumuenzi nyerere kwa matendo! Lakini hawaujui mzimu wa yule mzee, utawamaliza
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Very strong na ni powerful analysis ya siasa ya bongo.
   
 15. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nurujamii:
  You are onto something here.
  Kikwete is very weak, and probably vulnerable. He has to tow the line or else, hapo 2010.

  And afteral, the bad guys know how deep his involvement in the various deals.

  Lakini, Kikwete akiamua kuwa na ubavu, he can redeem his name to the wananchi, better than anyone of those mafiosos.
  Sina shaka kabisa, leo hii Kikwete akisimama na kuomba msamaha kwa waTanzania, na kuwahakikishia kuwa tokea sasa anaachana na wapotevu hawa, wananchi watamkubali bila shaka.

  Kwa bahati mbaya, akili yake bado imo katika kufunika mambo akidhani watu ni wajinga.
   
 16. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I think using common sense we can all I agree that there is no way that BWM will show up in Butiama. Does this guy even attend CC meetings let alone NEC?? I doubt it.

  If I was betting I will bet on the side that he won't be there especially since it is in Butiama.
   
 17. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  JK the lonely card in the deck. There is no way in the earth JK will flip staff. JK yupo pekee asiye na nguvu, nchi inamuendea mrama. Strategic planner wake hawana experience na dirty politcs ya Tanzania.

  Maoni kwa JK ni amua kuwa chui kwamba hakuna kucheza na swala. Change the whole strategy and i believe the country will turn around.

  Mpe mwanansheria mkuu mafile ya EPA, Richmond and Buzwagi, hilo linaweza kubadili nchi kwenda kwenye mkondo safi.

  In a long run JK will be a looser if he will not turn those criminals into the hand of justice. One day JK will explain infronts of someone why he didn't turn them.

  I know JK pray five times, don't he feel guilt everytime when he set pray kwa Allah to forgive his sin? He should. How can you said, ewe molla naomba unisamehe makosa yangu, while unakwenda kurudia kosa lile lile la kutokumpeleka Lowassa, Karamangi, Yona, Mkapa, NK kwenye justice?
   
 18. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Majibu yangu naomba niyaelekeze kwa kichwa cha habari cha thread.


  Rais mstaafu. Mh. Benjamini William Mkapa anahudhuria kikao cha CC na then NEC kwa kuwa ni mjumbe wa vikao hivyo, period.

  Kikao hiki ni cha Kihistoria kwa sababu moja tu na ambayo imejileta yenyewe nayo ni issue ya Muafaka wa Zanzibar na Serikali ya Mseto.

  Mengine ya ufisadi hayatajadiliwa kwenye NEC, CC kwa kuwa kamati za Serikali zinazoendelea na mambo ya ufisadi hazijamaliza kazi zake... na Mwenyekiti atasema tunasubiri mapendekezo ya task force ya waziri mkuu.

  Mengine mtakayojadili ni marudio ya yale ambayo tumeshayasema kwa muda mrefu.
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna mjumbe mmoja toka visiwani, amenihakikishia kuwa wata-raise ishu ya Balali, alikuwa akiniomba nimsukumie hizo ishus toka hapa, maana nilipoongea naye mwanzoni alikuwa hajui lolote zaidi ya propaganda za magazeti ya bongo, ni mpaka nilipomsukumia za kutoka hapa Jf ndio akashituka, kwa hiyo la Balali na Richimonduli, yapo huko Butiama, nafikiri nilishasema toka miezi miwili iliyopita, tena kutawaka moto huko, kuhusu what to do na Lowassa, Msabaha, na Karamagi, maana wajumbe wengi wapya wamepania kama walivyompania Kingunge na kumpuzisha cc.
   
 20. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  jamani huyu Mzee wetu si alisema yeye mwenyewe kwamba ameshastaafu siasa? Au alinukuliwa vibaya? Tuelezeni jamani!
   
Loading...