Poppy Hatonn
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 2,102
- 2,718
Maziko yamekwisha kwa amani tunashukuru.
Kwanza tulikuwa Shinyanga tukamwita paroko kufanya ibada. Paroko hakuongea chochote zaidi ya kumgombeza maiti kwa tabia yake ya kutopenda kwenda kanisani alipokuwa hai.
Tukaenda Butiama ikafanyika misa, lakini hotuba ya paroko ilikuwa inaonyesha ulikuwepo mgogoro na kwamba ile misa kidogo isifanyike.
Hata hivyo, tumefanya misa na tumezika. Baada ya hapo mtu akatoa tangazo wanaukoo tukutane baada ya watu kutawanyika.
Tukafanya mkutano wa ukoo. Mtu akatoa hoja pale:"Mwalimu Nyerere amekufa, hakutuachia hela. Lakini, alikuwa anaheshimika, na yeye hayupo sasa, kwa hiyo ile heshima yake, yote ni yetu. Lakini watu wengine hapa wanafanya mambo ya ovyo. Kwa hiyo wachapwe viboko."
Baada ya mabishano ya muda mrefu, watu pale wamechapwa viboko.