Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
na Asha Bani, Lushoto
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amedaiwa kuwa ni mnyonyaji kutokana na kuhodhi eneo kubwa la ardhi katika Kijiji cha Mkuzi, wilayani Lushoto, Tanga.
Madai hayo yametolewa na wakazi wa kijiji hicho mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika kijijini hapo.
Wananchi hao walieleza kuwa wamefikia hatua ya kutoa kauli hiyo kwa maelezo kwamba kila eneo wanalotaka kugusa kwa ajili ya kilimo wanaaambiwa kuwa ni la Mkapa.
Wakizungumza katika mkutano huo, walisema wameamua kusema hayo huku wakifahamu kwamba baadaye watapata matatizo ya kiusalama.
Mmoja wa wananchi hao, Hussein Jumaa, alidai kuwa Mkapa amekuwa akiwanyonya kutokana na kuhodhi maeneo mengi na makubwa katika eneo hilo.
Alisema maeneo ambayo yanahodhiwa na rais huyo mstaafu ni zaidi ya lile alilojenga nyumba kubwa ya kifahari ambako anaishi baada ya kustaafu.
Sisi jamani hatuna ardhi ya kulima hapa, kila unapogusa unaambiwa kwa Mkapa na pia tunasikitika kutokana na wakati huo tulikuwa tunajilimia mazao ya chakula, lakini tangu aamie amekuwa hatusaidii kitu badala yake kila eneo anachukua yeye, alisema Jumaa.
Wananachi hao wametoa malalamiko hayo ikiwa ni miezi michache tangu wananchi wa Mvomero, mkoani Morogoro kumlalamikia rais huyo mstaafu na Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, kumiliki eneo kubwa la ardhi wilayani humo, hali inayosababisha wakose maeneo ya kulima.
Wananchi hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa wapo katika mchakato wa kwenda mahakamani kudai ardhi yao, ili waweze kupata eneo kwa ajili ya kilimo.
Walieleza kuwa Mkapa anamiliki eneo lenye ukubwa wa hekta 3,000 na Sumaye 600.
Katika hatua nyingine, wananchi hao wa Lushoto wanamlalamikia rais huyo kutokana na kuwatumikisha katika mashamba yake na kuwalipa ujira mdogo tofauti na kazi wanazofanya.
Walisema mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi kama punda kutokana na shida zao, lakini amekuwa akiwalipa ujira wa sh 2,000 kwa kutwa.
Tumekuwa tukifanya kazi kwa kutwa nzima eneo kubwa kuanzia asubuhi hadi jioni, lakini pia tumekuwa tukilipwa ujira mdogo wa sh 2000, lakini hii ni kutokana na shida ambazo tunazipata na kutokana na kukosa maeneo ya kulima, alisema mkulima mmoja ambaye alikataa kutaja jina.
Kutokana na kauli za wananchi hao, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema kuwa hayo ndiyo matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na viongozi wake wengi kujilimbikizia mali na kuwanyonya wananchi ambao ni wanyonge.
Alisema katika utawala wake, Mkapa alifanya mambo mengi maovu likiwamo la kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.
Tumbo alisema kutokana na hali iliyojitokeza Lushoto na sehemu nyingine za Mkoa wa Tanga, wananchi wana uwezo wa kuamua nini cha kufanya, ili kuweza pia kuiondoa CCM madarakani na kutafuta chama mbadala ambacho ni CHADEMA.
Hilo ndilo fundisho, ndani ya CCM kumejaa ufisaidi mtupu, yeye si mtu wa huku, lakini amestaafu akaja kuwanyonya kwa kuchukua eneo kubwa la ardhi, ingoeni CCM madarakani ikafie mbele, alisema Tumbo.
Wakati huohuo, Rais Mkapa akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alisema ingawa Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili yakiwemo madini, bado utajiri huo hauwezi kuinua uchumi wa nchi.
Alisema hali hiyo haitatoweka hadi pale nchi itakapojizatiti katika kuimarisha maeneo yanayogusa sekta husika za maliasili hizo.
Mkapa alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia unaohusu uhandisi wa madini.
Alisema Tanzania imekuwa ikizungumzia suala la umasikini wa wananchi wake huku ukweli ukifahamika kuwa imebarikiwa kwa utajiri wa rasilimali hasa zile za asili.
Kwa sasa vipo vikwazo vingi na sababu nyingi zinazochangia maliasili isiwe chanzo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu; kwa mfano Azimio la Arusha limekuwa likijadili juu ya maendeleo kupitia ujamaa, kwa bahati mbaya katika maudhui ya azimio hilo, maadili ya uongozi ndiyo yamepewa kipaumbele, alisema Mkapa.
Alisema ili kufikia malengo ni lazima kutimiza masharti manne ambayo yatagusa watu, ardhi, sera nzuri na uongozi bora ambapo kwa upande wa watu ni lazima wawe na elimu bora.
Aliongeza kuwa Watanzania ni lazima wawe na ubunifu na elimu ya kutosha kuwaandaa kutumia ujuzi wao huo katika kazi za kujenga taifa ikiwemo kutumia taaluma walizonazo, kutafuta na kuhakikisha wanafanikisha malengo yao kwa faida ya nchi yao.
Aidha, Mkapa alisema suala la mtaji linapaswa kupewa umuhimu hasa katika sekta ya madini inayohitaji uwekezaji mkubwa ili kutoa matokeo mazuri tofauti na sasa ambapo teknolojia inayotumika ni ndogo na hivyo kufanya kazi hiyo kuwa na tija kidogo kwa taifa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko akizungumza katika mkutano huo, alishauri serikali kuwatumia wataalamu wa madini nchini, ili kuliletea taifa tija kupitia sekta husika.
Naishauri serikali kuwatumia wataalamu wa fani hii ya madini, ili waweze kuliletea taifa tija inayokusudiwa kupitia elimu waliyonayo, alisema Naiko.
Aidha, aliwashauri wataalamu wa madini nchini kuishauri serikali kutumia rasilimali hiyo, ili kuliletea taifa tija. Aliongeza kuwa, serikali inatakiwa kuwathamini wataalamu wa fani hiyo, ili waweze kutumia taaluma yao kwenye suala zima la madini. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhandisi na sehemu ya Wahandisi wa Madini, Assah Mwaipopo, alisema lengo la mkutano huo ni namna ya kukiamsha chama cha wahandisi wa madini ambacho pamoja na kuwepo, lakini utendaji wake ulikuwa hafifu.