Mkapa awaliza wanakijiji Lushoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa awaliza wanakijiji Lushoto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Dec 21, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Asha Bani, Lushoto


  [​IMG]
  RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amedaiwa kuwa ni mnyonyaji kutokana na kuhodhi eneo kubwa la ardhi katika Kijiji cha Mkuzi, wilayani Lushoto, Tanga.
  Madai hayo yametolewa na wakazi wa kijiji hicho mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika kijijini hapo.
  Wananchi hao walieleza kuwa wamefikia hatua ya kutoa kauli hiyo kwa maelezo kwamba kila eneo wanalotaka kugusa kwa ajili ya kilimo wanaaambiwa kuwa ni la Mkapa.
  Wakizungumza katika mkutano huo, walisema wameamua kusema hayo huku wakifahamu kwamba baadaye watapata matatizo ya kiusalama.
  Mmoja wa wananchi hao, Hussein Jumaa, alidai kuwa Mkapa amekuwa akiwanyonya kutokana na kuhodhi maeneo mengi na makubwa katika eneo hilo.
  Alisema maeneo ambayo yanahodhiwa na rais huyo mstaafu ni zaidi ya lile alilojenga nyumba kubwa ya kifahari ambako anaishi baada ya kustaafu.
  “Sisi jamani hatuna ardhi ya kulima hapa, kila unapogusa unaambiwa kwa Mkapa na pia tunasikitika kutokana na wakati huo tulikuwa tunajilimia mazao ya chakula, lakini tangu aamie amekuwa hatusaidii kitu badala yake kila eneo anachukua yeye,” alisema Jumaa.
  Wananachi hao wametoa malalamiko hayo ikiwa ni miezi michache tangu wananchi wa Mvomero, mkoani Morogoro kumlalamikia rais huyo mstaafu na Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, kumiliki eneo kubwa la ardhi wilayani humo, hali inayosababisha wakose maeneo ya kulima.
  Wananchi hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa wapo katika mchakato wa kwenda mahakamani kudai ardhi yao, ili waweze kupata eneo kwa ajili ya kilimo.
  Walieleza kuwa Mkapa anamiliki eneo lenye ukubwa wa hekta 3,000 na Sumaye 600.
  Katika hatua nyingine, wananchi hao wa Lushoto wanamlalamikia rais huyo kutokana na kuwatumikisha katika mashamba yake na kuwalipa ujira mdogo tofauti na kazi wanazofanya.
  Walisema mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi kama punda kutokana na shida zao, lakini amekuwa akiwalipa ujira wa sh 2,000 kwa kutwa.
  “Tumekuwa tukifanya kazi kwa kutwa nzima eneo kubwa kuanzia asubuhi hadi jioni, lakini pia tumekuwa tukilipwa ujira mdogo wa sh 2000, lakini hii ni kutokana na shida ambazo tunazipata na kutokana na kukosa maeneo ya kulima,” alisema mkulima mmoja ambaye alikataa kutaja jina.
  Kutokana na kauli za wananchi hao, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema kuwa hayo ndiyo matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na viongozi wake wengi kujilimbikizia mali na kuwanyonya wananchi ambao ni wanyonge.
  Alisema katika utawala wake, Mkapa alifanya mambo mengi maovu likiwamo la kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.
  Tumbo alisema kutokana na hali iliyojitokeza Lushoto na sehemu nyingine za Mkoa wa Tanga, wananchi wana uwezo wa kuamua nini cha kufanya, ili kuweza pia kuiondoa CCM madarakani na kutafuta chama mbadala ambacho ni CHADEMA.
  “Hilo ndilo fundisho, ndani ya CCM kumejaa ufisaidi mtupu, yeye si mtu wa huku, lakini amestaafu akaja kuwanyonya kwa kuchukua eneo kubwa la ardhi, ing’oeni CCM madarakani ikafie mbele,” alisema Tumbo.
  Wakati huohuo, Rais Mkapa akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alisema ingawa Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili yakiwemo madini, bado utajiri huo hauwezi kuinua uchumi wa nchi.
  Alisema hali hiyo haitatoweka hadi pale nchi itakapojizatiti katika kuimarisha maeneo yanayogusa sekta husika za maliasili hizo.
  Mkapa alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia unaohusu uhandisi wa madini.
  Alisema Tanzania imekuwa ikizungumzia suala la umasikini wa wananchi wake huku ukweli ukifahamika kuwa imebarikiwa kwa utajiri wa rasilimali hasa zile za asili.
  “Kwa sasa vipo vikwazo vingi na sababu nyingi zinazochangia maliasili isiwe chanzo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu; kwa mfano Azimio la Arusha limekuwa likijadili juu ya maendeleo kupitia ujamaa, kwa bahati mbaya katika maudhui ya azimio hilo, maadili ya uongozi ndiyo yamepewa kipaumbele,” alisema Mkapa.
  Alisema ili kufikia malengo ni lazima kutimiza masharti manne ambayo yatagusa watu, ardhi, sera nzuri na uongozi bora ambapo kwa upande wa watu ni lazima wawe na elimu bora.
  Aliongeza kuwa Watanzania ni lazima wawe na ubunifu na elimu ya kutosha kuwaandaa kutumia ujuzi wao huo katika kazi za kujenga taifa ikiwemo kutumia taaluma walizonazo, kutafuta na kuhakikisha wanafanikisha malengo yao kwa faida ya nchi yao.
  Aidha, Mkapa alisema suala la mtaji linapaswa kupewa umuhimu hasa katika sekta ya madini inayohitaji uwekezaji mkubwa ili kutoa matokeo mazuri tofauti na sasa ambapo teknolojia inayotumika ni ndogo na hivyo kufanya kazi hiyo kuwa na tija kidogo kwa taifa.
  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko akizungumza katika mkutano huo, alishauri serikali kuwatumia wataalamu wa madini nchini, ili kuliletea taifa tija kupitia sekta husika.
  “Naishauri serikali kuwatumia wataalamu wa fani hii ya madini, ili waweze kuliletea taifa tija inayokusudiwa kupitia elimu waliyonayo,” alisema Naiko.
  Aidha, aliwashauri wataalamu wa madini nchini kuishauri serikali kutumia rasilimali hiyo, ili kuliletea taifa tija. Aliongeza kuwa, serikali inatakiwa kuwathamini wataalamu wa fani hiyo, ili waweze kutumia taaluma yao kwenye suala zima la madini. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhandisi na sehemu ya Wahandisi wa Madini, Assah Mwaipopo, alisema lengo la mkutano huo ni namna ya kukiamsha chama cha wahandisi wa madini ambacho pamoja na kuwepo, lakini utendaji wake ulikuwa hafifu.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkapa heri AKAJIFICHE umakondeni kwao.

  Au Mapadri wamchukue wamlee tena ili AMRUDIE BWANA.
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wabongo bwana, yaani tumesahau yote aliyofanya Mkapa kwa nchi yetu. barabara zote alizojenga, Dar - Mwanza sasa hivi ni safari ya masaa tu ukilinganisha na siku za nyuma ambapo tulikuwa tunakwenda kwa siku mbili. uwanja wa taifa, madaraja, alivyoinua uchumi nchi yetu ikaanza kupata heshima kimataifa, tumesahau kwamba aliikuta nchi ikiwa imekwisha kabisa.
  Tumesahau kazi ngumu aliyoifanya ya kulipa madeni aliyokopa Mwinyi na kuirudisha nchi kwenye mstari, tumesahau pia kazi ngumu aliyoifanya mkapa ya kurudisha heshima ya mfanyakazi ambaye wakati wa mwinyi alipoteza kabisa thamani, tumesahau alivyofuta kodi ya kichwa, alivyofuta ada za shule ili kuwezesha wengi waende shule na mengine mengi ambayo hatuwezi kuyahesabu. Leo tunamdhihaki na kumnyanyasa namna hii. Kwakweli binadamu hatuna wema jamani. Muacheni mzee wa watu apumzike. kaifanyia makubwa nchi yetu. hata kama aliiba, alichokifanya pia kinaonekana. Hawa wapinzani wanapewa ruzuku kila siku, hatujawasikia hata wamesaidia kusomesha watoto yatima. Waende zao huko bwana. Mwacheni Mkapa wetu.
   
 4. s

  smalnama Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leta hoja usilete ukabila hapa
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ukisema Umakondeni maana yake ni sehemu wanayotoka Wamakonde. Narudia tena ni SEHEMU wanayotoka Wamakonde na si UKABILA.

  Na wewe ni Makonde nini? Inabidi Wanyamwezi tushike nchi na tuwatie adabu Makonde nyie. Sasa ndiyo nimeleta ukabila, now what?
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wajinga ndio waliwao...
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Vangi,
  Ni kweli tumesahau. Lakini nakuhakikishia hatutasahau jinsi alivyoanzisha biashara akiwa Ikulu. Hatutasahau jinsi alivyouza NBC kwa bei chee kwa Makaburu kwa kupewa kitita cha hongo. Hatutasahau jinsi alivyojimegea mgodi wa Kawira. Hatutasahau jinsi alivyoingiza kampuni ya ndugu zake kwa mabavu ya Ikulu kutusimamia TANESCO. Hatutasahau jinsi alivyojinunulia dege la fahari kwa hela zilizojaa rushwa. Hatutasahau jinsi alivyotuwekea mazingira ya kumpata Kikwete kuwa rais wetu mpya. Hatutasahau, na ukitaka ninaweza kuendelea tena na tena........
   
 8. mkongo

  mkongo Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vangi... hayo yote uliyoyataja alitakiwa kuyafanya. Si aligombea Urais mwenyewe na kuahidi kuwatumikia wananchi? Kwa kupewa nafasi ile alitakiwa ayafanye hayo yote... tena inawezekana kuna sehemu nyingine amezembea. Lakini ukiangalia upande wa pili wa shilingi alienda kufanya pia na yale ambayo hakuruhusiwa kufanya. Kiongozi huyu (Mkapa) alifaa atiwe ndani na kunyang'anywa mali zote ambazo hakuzipata kihalali. Tunamuheshika kama Mzee lakini heshima yake imeshachuja... aliyoyafanya ni yakutia aibu. Hata huyu aliyepo madarakani sasa hivi... eti amejenga chuo cha Dodoma, shule zisizo na walimu na zahanati zisizo na madaktari kama kweli ni wajibu wake na sio kumuomba au kwamba anatufanyia hisani. Kwa miaka mitano anayokaribia kumaliza amefanikiwa kutembea nchi nyingi za kutosha na fedha aliyoitumia kwa safari hizo ingetosha kabisa kuongeza walimu. Kujenga vyuo vingine zaidi lakini alichagua kutumia nchi za nje. Sasa basi tunataka mwingine mwenye kuwajibika kwaajili yetu.
   
 9. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mina shauri hao wanakijiji wajichangishe watafute wakili wampeleke mkapa mahakamani!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mahakama ipi? Hizi mahakama za Kikwete zinazosema "muacheni mzee apumzike"? Au wameanzisha mpya?
   
 11. L

  Lampart Senior Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa huyo Mwinyi unaemsakama sio ndie aliyekupa mdomo leo wa kusema????????
   
 12. L

  Lampart Senior Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ushahidi kamili vipi??????????????
  Tunataka ushahidi kamili kwanza kabla hamjawatia adabu!!!!!
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkapa hana tofauti na Mobutu seseseko wa zabanga
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hata Mkapa kasahau yote hayo, anakumbuka haya na yale aliyomuachia Mungu:

  "We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us " - Mkapa
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  1. Mkapa kwa nini ulijiuzia mgodi?
  2. Mkapa kwa nini uliiuza NBC kwa marafiki zako kwa bei chee?
  3. Mkapa kwa nini ulianzisha meremeta na deep green?
  4. Mkapa lakini ulijitahidi kukusanya kodi
  5. Mkapa kwa nini uligawa chuo cha TANESCO kwa waislam?
  6. Mkapa kwa nini ulimuua Gen. Imrani Kombe?
  .
  .
  .
  .
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  weka para kwenye bandiko lako linachosha kusoma
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Pamoja na kukumbuka mazuri aliyofanya basi ni vile vile lazima asahihishwe mabaya aliyofanya. Overal a president is elected and paid for an Excellent Job; not for stealing. Ni vizuri kumwajibisha Mr. President all the time ajue "to do the right thing"
   
 18. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii taarifa imeandikwa ki-Chuki-chuki.
  Hizi chuki binafsi zinaendelea kuwatafuna WaTanzania
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kituko sasa si ahame Lushoto na ile nyumba aiuze
   
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  This is almost nonsensical propaganda.
  The author should get his facts correct before putting pen to paper.
  3000 Hectares in Lushoto?
  Come on give me a break!!
  I dont see that area in Lushoto, Mombo probably yes.

  Halafu kijijini, mtu analipwa kiasi gani-kibarua to be exact.
  The author should find comparable rates from other areas.
  Ama sivyo kwa tunaoelewa rates hii inaonekana upuuzi mtupu.
  Na nasema hivyo si kwa ajili ya kusapoti Mkapa , la hasha, ila makala hii imejaa propaganda zaidi kuliko facts.
   
Loading...