Mkapa aomba suluhu kwa Nyerere

Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa amemuomba mjane wa Mwalimu Juliua nyerere ampatanishe na Mbunge wa Msoma mjini Vicent Nyerere. Akiongea na Gazeti la Mtanzania Jana msaidizi wa Mkapa alikiri Mkapa kusema kwamba Hajawahi kutambulishwa kama Vivent ni mtoto wa nyerere. Mtoto mkubwa wa mwalimu MADARAKA Nyerere amekaririwa akisema Vicent ni ndugu yao mtoto wa baba yao mdogo. Kauli hiyo ya Rais mstaafu inakuja mara baada ya Vicent kumjibu Mkapa kuwa ndiye alihusika na kifo cha mwalimu.
Chanzo:gazeti la mtanzania
Jana niliapa hakutakuwa na press conference ya Mkapa kujiosha! Sasa sijui ni suluhu gani anayotafuta! Jitu zima linajiaibisha!
 
mkapa hakuna mahali amekana kuwa hakumua nyerere! Kimya pia ni jibu

wapi slaa/mbowe wamekana kufanya ufisadi 300ml za visima toka kwa sabodo? Mbona mmekurupuka na kudai ushahidi bila kujibu hoja? Mkapa ndio wa kujibu bila ushahidi kwa maneno tu ya kwenye majukwaa? Huu kama si uchizi basi hakuna chizi duniani!
 
BMT kwa akili zako ulizopewa na Maulana unaona wana JF chadema wakae wajadili Milioni 300 zilizonunua nyumba Dubai, Zilizomjengea Jumba Slaa Kunduchi na zilizokarabati Billicanas? Labda mwana chadema mwehu lakini kila mwenye akili anajua from the start kuwa ile thread ni mav.i
wewe ndo ujibu hapa Mkapa anaomba Suluhu ya nini? Si anaijua vizuri familia ya Mwalimu?

Tehe......Tehe....Kwii.....Kwiiiiiiii.....!!!!!!
 
wapi slaa/mbowe wamekana kufanya ufisadi 300ml za visima toka kwa sabodo? Mbona mmekurupuka na kudai ushahidi bila kujibu hoja? Mkapa ndio wa kujibu bila ushahidi kwa maneno tu ya kwenye majukwaa? Huu kama si uchizi basi hakuna chizi duniani!

Pole Kibwetere
 
mkapa hakuna mahali amekana kuwa hakumua nyerere! Kimya pia ni jibu

wapi slaa/mbowe wamekana kufanya ufisadi 300ml za visima toka kwa sabodo? Mbona mmekurupuka na kudai ushahidi bila kujibu hoja? Mkapa ndio wa kujibu bila ushahidi kwa maneno tu ya kwenye majukwaa? Kimya chao (slaa & mbowe) nao kichukuliwe kuwa kweli 300ml zimeliwa? Huu kama si uchizi basi hakuna chizi duniani!
 
Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa amemuomba mjane wa Mwalimu Julius Nyerere ampatanishe na Mbunge wa Msoma mjini Vicent Nyerere. Akiongea na Gazeti la Mtanzania Jana msaidizi wa Mkapa alikiri Mkapa kusema kwamba Hajawahi kutambulishwa kama Vivent ni mtoto wa nyerere. Mtoto mkubwa wa mwalimu MADARAKA Nyerere amekaririwa akisema Vicent ni ndugu yao mtoto wa baba yao mdogo. Kauli hiyo ya Rais mstaafu inakuja mara baada ya Vicent kumjibu Mkapa kuwa ndiye alihusika na kifo cha mwalimu. Chanzo:gazeti la mtanzania
we unadhani alikua hajui? Alikua anataka kuwachanganya Wameru akakutana na rungu la uso toka kwa vicent sasa anahaha kujaribu kufiacha maovu yake kwa kuomba suluhu la haraka kabla siri nyingine hazijafumuka.
 
Rejao jibu hoja au na wewe umefuata nyayo za mzee uchwara?? kujichimbia mchangani kama mbuni sio suluhu...
 
Mkapa anaomba suluhu na Vicent kwa upatanishi wa mama Maria Nyerere, kwani Vincent ana uhusiano gani na mama Maria Nyerere hadi ahusike kuwasuluhisha? Kwani kuna ugomvi baina yao (Vincent na Mkapa) hadi wahitaji kusuluhishwa?

Je Mkapa kwa kuomba suluhu na Vincent Nyerere ni kusema kwamba sasa ametambua kwamba Vincent ni mwanafamilia ya baba wa taifa?

Hili litakuwa fundisho kwa mkapa siku nyengine asithubutu kuongea utumbo na kujishushia hadhi kiasi hiki.

Ninapenda siasa za Zambia.Rais mstaafu ni marufuku kuongelea siasa akiwa amestaafu.Serikali ya Zambia sasa inapanga kumnyang'anya Rais wa Zamani Rupia Banda marupurupu yote anayopewa baada ya kuendelea kufanyia kampeni chama chake.Nadhani Katiba mpya hapa kwetu iweke hii sheria.Laiti tungekuwa na utaratibu huu hapa kwetu aibu inayomkuta Mkapa sasa isingekuwepo.
 
cdm cdm cdm!kule ameguswa slaa na mbowe mumekuwa mbogo sana,halfu mnakurupuka tu,kwl watu kama nyie mpewe nchi,dr slaa angekuwa na akil finyu kama zenu leo hii cdm isingekuwa hapo.Jaribuni kujheshmu muwe fair pia
Sasa anayetakiwa awe fair ninani? Si dubwashika lenu liliamua kuanzisha siasa za majitaka likapewa kitu cha ukweli! Anatafuta pa kutokea hapati weeee patamu hapo!
 
pole kibwetere

tumia neno lolote unaloona linakufaa kuondosha heshima yangu ila tetea hoja! Tatizo lenu mnatumia fimbo kuwachapa wenzenu kwa makosa fulani, fimbo hiyo hiyo ikitumika kuwachapa nyie kwa makosa yale yale, mnaona mwaonewa na maneno meeengi!
 
Vincent Kwenye Mkutano wa Ufunguzi alitahadharisha kuwa ni Mpole na Si Mnyonge,mkapa hakuwa ameelewa
 
cdm cdm cdm!kule ameguswa slaa na mbowe mumekuwa mbogo sana,halfu mnakurupuka tu,kwl watu kama nyie mpewe nchi,dr slaa angekuwa na akil finyu kama zenu leo hii cdm isingekuwa hapo.Jaribuni kujheshmu muwe fair pia
Mkuu unataka fairness kwenye nini? Unataka upewe ushahidi kama Mkapa ni fisadi ama sio fisadi?
Unataka tuthibitishe kama Nyerere kifo chake hakikuharakishwa na Mkapa?
Mbona vyote vipo wazi ushahidi gani ambao wewe huuoni?
Na kuhusu Sabodo na kina Mbowe, unaweza kunipa mchanganuo kuwa nyumba Dubai,Billicanas na Nyumba ya Slaa vyote vyaweza kununuliwa, kukarabatiwa na kujengwa kwa shilingi Mil 700? Unadhani Dubai ni Chalinze eeh? Sasa kama hoja sio logical (hatusemi ni hoja ya uongo) kwa nini tusiombe ushahidi? Maana sio kila ambacho sio Logical ni cha Uongo vingine havina Logic lakini vya ukweli, sasa aliyetoa mada atupe japo muhtasari tu wa kikao kilichoketi kutoa hizo pesa
 
Back
Top Bottom