serikali ya sasa kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali iliwekwa hapo kwa nguvu ya vikundi. Na Mkapa hakuwa upande wa jk. Muulize lowassa ilikuwaje jk yuko madarakani.
Uliisikiliza kwa makini hotuba ya Mkapa siku ya Mkutano Mkuu wa Kuchagua mgombea wa urais kupitia CCM pale Chimwaga, Dodoma mwaka 2005?
Philip Mangula [Katibu Mkuu aliyemtangulia Makamba] aliandaa dose ya "rafu" za JK kwenye kusaka wadhamini na jinsi fedha zilivyotumika, report hiyo mpaka sasa iko kapuni na ndio maana Mangula alizimika ghafla bin vuu. Nilishangaa kumuona juzi kwenye kampeni za Igunga.
Magazeti juzi yaliandika Lowassa jinsi alivyomkumbusha JK namna watu wa maadili walimvyom-deal JK na kwamba ni "busara" za Mkapa ndizo ambazo zilimwokoa JK, kama si hivyo asingekuwa Rais.
Kama kweli Mkapa hakushiriki kumweka JK hapo Ikulu, ni kwanini alimpigia debe siku ya kuchagua mgombea? Kama Mkapa hakumweka hapo, kwanini hakufanyia kazi tuhuma za JK ambazo zilipelekwa kwenye kikao na watu wa maadili? Kama kweli Mkapa hakumweka hapo, kwanini hakukemea matumizi ya hongo kwenye Mkutano Mkuu wa 2005 wa kumteua JK? Mzee Butiku aliandika barua kwa Mkapa mara baada ya mkutano ule, mzee wa watu mpaka anaenda kwenye public barua ile haikuwa na mjibu na ninadhani iko hapa hapa JF maana nakumbuka iliandikwa kwenye magazeti kama ilivyo.
Ukishaona Top wa TISS zama hizo ni mwana mtandao, then lazima uweke maswali mengi sana. TISS inatakiwa kuwa neutral ili iweze kufanya kazi bila upendeleo wowote kwa yeyote yule.
Mwisho, Tanzania kuwa omba omba na yeye Mkapa ameshiriki katika kutuingiza kwenye huo mkenge, ametuachia mikataba mibovu ya madini, ambayo badala ya kunufaisha nchi imekuwa inanufaisha wageni. Ukisoma report za BoT wanaonyesha Tanzania tunapata dollar kibao za mauzo ya dhahabu, lakini shilingi yetu inazidi kuporomoka siku hadi siku. Hizo dollar ziko kwenye makaratasi tu kwa sababu ubovu wa mikataba na incentive packages ambazo makampuni ya kuchimba madini wamepewa.