Mkanganyiko kuhusu kashfa ya Richmond

Mkanganyiko kuhusu kashfa ya Richmond

pepsin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
3,486
Reaction score
6,172
Wanajukwaa,salam,
Baada ya kumsikia waziri Mkuu wa zamani,ndugu Edward Lowassa na baada ya kusoma michango mbalimbali humu ukumbini kutoka kwa wanaomuunga mkono na wanaompinga kuhusu ''safari ya matumaini'' nahisi mkanganyiko,
1.Inasemwa kashfa ya Richmondi ilitungwa tu na akina Sitta na Dr Mwakyembe ili ku muangusha Kwenye uwaziri mkuu.Hivyo hapakuwa na kitu halisia kama Richmond scandel,ilibuniwa tu,
2.Lowassa kasema hakufanya kitu chochote kuhusu Richmond bila kumshirikisha mh.Rais.Hata alifikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba ila hakukubaliwa.Hapa,je,huo mkataba aliotaka kuuvunja ni upi kama Richmondi ilikuwa ni kitu ya kubuni? Ina maana angevunja mkataba dhahania?
3. Ndg Lowassa anasema alikaa kimya kwa muda mrefu wa takribani miaka saba ili kuilinda Serikali (rais) na chama! Kwa hiyo hapa rais mtarajiwa anakiri kuwa mradi wa Richmond ulikuwa ni ufisadi mkubwa hata wa kuiangusha serikali! Na hivyo,je,tujue lipi,kwamba ni rais pekee ndio alikuwa mhusika wa Richmondi au Rais na Waziri mkuu wake(Lowassa) walihusika pamoja ila yeye alikaa kimya ili bosi mwingine apone(Hapa kama ndio hivyo maana yake uzalendo wake ni kwa mtu na siyo nchi?)
4.Ripoti ya kamati ya Dr.Mwakyembe ilionesha vimemo kutoka kwa PM kwenda kwa mawaziri na mpaka wabunge wa ccm wakashawishika kumhusisha Lowassa na Richmond.Ina maana hawa walikuwa hawaelewi mtego wa Sitta na Dr Mwakyembe,walikuwa wamehongwa au kipi kilitokea?
(Akina ole Sendeka,Kilango Malecela et a' nasikia wameshaungama)
Yote kwa yote,Richmondi ilikuwa kitu REAL au FAKE?
Kama ilikuwa real,Lowassa hakushiriki kabisa au alishiriki pamoja na mh.Rais ila baadae akatolewa sadaka kwa niaba ya mkuu?
Na kama alishiriki pamoja na mkuu wake kwa nafasi yake kunamfanya asiwe fisadi?
Karibuni Wajuaji,mtufumbue wengine macho.
 
Kama ndivyo,basi anatudanganyia nini anavyosema Aliundiwa kashfa? Anapaswa kuadhibiwa kwa ulaghai huu?

Alitakiwa aseme kipi kilianza tume ya sita na Mwakyembe au richmond? Na aseme je ni chini ya uwaziri wake mkuu ndio tulikuwa giza ?

Na aseme je ndiye yeye aliyeshikiri mzabuni wa Richmond kupewa tender na kunyimwa kampuni mahiri kama GE?

Na aseme je ulikuwa mpango wake na swahiba wake Rasta aziza kuingiza Richmond nchini na Generoator za GE alizotumia Gire wakuijua ni nzima na kutumia wafanyakazi wa tanesco ku zi sabbotage ili zisiwake, kwa deal la kumkimbiza gire ilimwisho ama wazitaifishe ama wazinunue ili wao ndio wazalishe umeme kama ilivyotokea kwenda Dowans??

Aseme je deal zima lilinzia wapi?

Na aje aseme kwanini alikaa kimya muda wote huo. Na kama ni kulinda serikali za uhujumu je mangapi bado anayalinda wakati nchi inahujumiwa na kuporwa?

Kama kaweza kulinda uozo akiwa waziri atafanyaje akiwa raisi si atauza nchi kisha kulinda wahujumu??
 
mpaka anaondoka pale ilikua haijalipwa hata senti tano shahidi zakia meghji shemeji yake kikwete alikua waziri wa fedha kipindi hicho
 
Waandishi wa habari aliokuwa anawasimulia haya mambo wooote walikuwa wamekula maharage ya wapi hata kushindwa kumwuliza maswali ya msingi kama hayo?
 
mpaka anaondoka pale ilikua haijalipwa hata senti tano shahidi zakia meghji shemeji yake kikwete alikua waziri wa fedha kipindi hicho
Huyu bwana alikuwa na project nyingine ya ulaji pia:mvua ya kutengeneza. Je alifanikiwa kutengeneza mvua ya kuweza kujaza mtera?
 
Mkuu samahani sana,Hizi fallacy mnazotumia kushambulia watu hazijibu hoja na maswali.
Kwa kifupi hazina msaada kwake wala kwenu.Bora uelimishe na uheshimike.
Kuna mtandao unatoa MIMINA I guess ww ni member wa huo mtandao wa kumimi.....wa
 
Well said Chief.
Alitakiwa aseme kipi kilianza tume ya sita na Mwakyembe au richmond? Na aseme je ni chini ya uwaziri wake mkuu ndio tulikuwa giza ?

Na aseme je ndiye yeye aliyeshikiri mzabuni wa Richmond kupewa tender na kunyimwa kampuni mahiri kama GE?

Na aseme je ulikuwa mpango wake na swahiba wake Rasta aziza kuingiza Richmond nchini na Generoator za GE alizotumia Gire wakuijua ni nzima na kutumia wafanyakazi wa tanesco ku zi sabbotage ili zisiwake, kwa deal la kumkimbiza gire ilimwisho ama wazitaifishe ama wazinunue ili wao ndio wazalishe umeme kama ilivyotokea kwenda Dowans??

Aseme je deal zima lilinzia wapi?

Na aje aseme kwanini alikaa kimya muda wote huo. Na kama ni kulinda serikali za uhujumu je mangapi bado anayalinda wakati nchi inahujumiwa na kuporwa?

Kama kaweza kulinda uozo akiwa waziri atafanyaje akiwa raisi si atauza nchi kisha kulinda wahujumu??
 
Samahani jamani mbona mimi sioni kitu kabisa ndani ya EL, kila ninapomsikiliza sioni chochote ninachoona zaidi ni mikakati, harakati sioni kitu special kabisa Iam sorry!
 
Wameungama?!!

Anyway,ukweli kuhusu Richmond utakuja julikana siku CCM wakitoka madarakani na si vinginevyo.
 
Mkuu,Sendeka alikuwa ni mmoja ya wabunge waliochangia kwa hisia Lowassa ajiuzulu.Kwa sasa anataka Lowassa asafishwe!
Ukweli tunaweza kuujua mapema zaidi.Wakipambana vizuri,silaha zote zitatumika na hapohapo sisi kuziona '''live''
Wameungama?!!

Anyway,ukweli kuhusu Richmond utakuja julikana siku CCM wakitoka madarakani na si vinginevyo.
 
ilikua fake,ila kina mwak,walicheza na lugha.
ishu ya umeme ilikua ni ya dharura,na hivyo taratibu zikaenda kidharura ili watu wapate umeme,,Nadhani baadhi ya taratibu za zabuni zikarukwa ili ipatikane kampuni itakayoleta mashine.
huwa nashindwa kuelewa wanaodai pesa za richmond ziliibiwa ni zipi hizo
 
Sawa mkuu.
Ebu niweke sawia hapa,
1.Mkataba ambao Lowassa alitaka kuuvunja ila akauiwa na mwenyekiti ulikuwa baina ya TANESCO na RIchmond ipi kama hii ilikuwa feki?
2.Kitu alichokificha Lowassa kwa heshima ya serikali yake na chama chake(kumb.tamko la kung'atuka bungeni) kilikuwa kipi ambacho kingeiangusha serikali yote kama sio ufisadi wa Richmondi?
3.Kama hamna wizi uliotokea kwa nini alikubali kufanya MAAMUZI MEPESI ya kujiuzulu kwa ajili ya kashfa ya kutunga? Karibu mkuu.

ISHU YA UMEME ilikua ni dharura,na kelele zilikua nyingi sana toka kwa watu,nadhani huyo lowasa akafanya pupa kuipa ok richmond bila kufuata utaratibu kipengele kwa kipengele.
sasa kina mwak waliposanua kuwa taratibu zilikiukwa,watu walikua washasau msoto uliokuwapo kuhusu tatizo la umeme kipindi kile.wakakomaa sasa kufuatilia vipengele mpaka nukta.

moja ya vigezo vya kuichagua richmond ilikua ni bei nafuu kuliko makampuni yote yalokuwa yakiwania tenda.
pengine lowasa alitoa ok kwa nia nzuri ukichukulia hali ya kipindi kile.
nadhani walitaka kuvunja mkataba baada ya richmond kuchelewa kuleta magenereta
 
Wanajukwaa,salam,
Baada ya kumsikia waziri Mkuu wa zamani,ndugu Edward Lowassa na baada ya kusoma michango mbalimbali humu ukumbini kutoka kwa wanaomuunga mkono na wanaompinga kuhusu ''safari ya matumaini'' nahisi mkanganyiko,
1.Inasemwa kashfa ya Richmondi ilitungwa tu na akina Sitta na Dr Mwakyembe ili ku muangusha Kwenye uwaziri mkuu.Hivyo hapakuwa na kitu halisia kama Richmond scandel,ilibuniwa tu,
2.Lowassa kasema hakufanya kitu chochote kuhusu Richmond bila kumshirikisha mh.Rais.Hata alifikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba ila hakukubaliwa.Hapa,je,huo mkataba aliotaka kuuvunja ni upi kama Richmondi ilikuwa ni kitu ya kubuni? Ina maana angevunja mkataba dhahania?
3. Ndg Lowassa anasema alikaa kimya kwa muda mrefu wa takribani miaka saba ili kuilinda Serikali (rais) na chama! Kwa hiyo hapa rais mtarajiwa anakiri kuwa mradi wa Richmond ulikuwa ni ufisadi mkubwa hata wa kuiangusha serikali! Na hivyo,je,tujue lipi,kwamba ni rais pekee ndio alikuwa mhusika wa Richmondi au Rais na Waziri mkuu wake(Lowassa) walihusika pamoja ila yeye alikaa kimya ili bosi mwingine apone(Hapa kama ndio hivyo maana yake uzalendo wake ni kwa mtu na siyo nchi?)
4.Ripoti ya kamati ya Dr.Mwakyembe ilionesha vimemo kutoka kwa PM kwenda kwa mawaziri na mpaka wabunge wa ccm wakashawishika kumhusisha Lowassa na Richmond.Ina maana hawa walikuwa hawaelewi mtego wa Sitta na Dr Mwakyembe,walikuwa wamehongwa au kipi kilitokea?
(Akina ole Sendeka,Kilango Malecela et a' nasikia wameshaungama)
Yote kwa yote,Richmondi ilikuwa kitu REAL au FAKE?
Kama ilikuwa real,Lowassa hakushiriki kabisa au alishiriki pamoja na mh.Rais ila baadae akatolewa sadaka kwa niaba ya mkuu?
Na kama alishiriki pamoja na mkuu wake kwa nafasi yake kunamfanya asiwe fisadi?
Karibuni Wajuaji,mtufumbue wengine macho.

Hayo yote sawa lkn ile mitambo ya richmond/dowans ilinunuliwa na symbion tena obama na hillary wakaja ifungua je naanza kupata waswas wake je bwana mkubwa alikuwa hajui mpk kukana kwmba hajui wamiliki wa dowans
 
Unajua waziri mkuu ana-reort kwa nani? huyo anaye m-report- ndo alimshinikiza, ingawa bado si uadilifu

suala lilikua umeme upatikane haraka,hata kama lowasa alishinikiza.
na hakuna pesa yeyote walilipwa hao richmond mpaka wanahamishia kwa dowans ambao walileta mitambo na kuzalisha umeme.
 
Hayo yote sawa lkn ile mitambo ya richmond/dowans ilinunuliwa na symbion tena obama na hillary wakaja ifungua je naanza kupata waswas wake je bwana mkubwa alikuwa hajui mpk kukana kwmba hajui wamiliki wa dowans

dowans alitaka kutuuzia mitambo ile,ila wabunge wakaikataa kuwa ni mibovu,kwamba wakiinunua watakiuka sheria ya manunuzi.ikabidi mwenyewe aiuze symbion,na sasa inaendelea kupiga kazi huku tukiilipa
 
Back
Top Bottom