Mkanganyiko kuhusu kashfa ya Richmond

Mkanganyiko kuhusu kashfa ya Richmond

Wanajukwaa,salam,
Baada ya kumsikia waziri Mkuu wa zamani,ndugu Edward Lowassa na baada ya kusoma michango mbalimbali humu ukumbini kutoka kwa wanaomuunga mkono na wanaompinga kuhusu ''safari ya matumaini'' nahisi mkanganyiko,
1.Inasemwa kashfa ya Richmondi ilitungwa tu na akina Sitta na Dr Mwakyembe ili ku muangusha Kwenye uwaziri mkuu.Hivyo hapakuwa na kitu halisia kama Richmond scandel,ilibuniwa tu,
2.Lowassa kasema hakufanya kitu chochote kuhusu Richmond bila kumshirikisha mh.Rais.Hata alifikia hatua ya kutaka kuvunja mkataba ila hakukubaliwa.Hapa,je,huo mkataba aliotaka kuuvunja ni upi kama Richmondi ilikuwa ni kitu ya kubuni? Ina maana angevunja mkataba dhahania?
3. Ndg Lowassa anasema alikaa kimya kwa muda mrefu wa takribani miaka saba ili kuilinda Serikali (rais) na chama! Kwa hiyo hapa rais mtarajiwa anakiri kuwa mradi wa Richmond ulikuwa ni ufisadi mkubwa hata wa kuiangusha serikali! Na hivyo,je,tujue lipi,kwamba ni rais pekee ndio alikuwa mhusika wa Richmondi au Rais na Waziri mkuu wake(Lowassa) walihusika pamoja ila yeye alikaa kimya ili bosi mwingine apone(Hapa kama ndio hivyo maana yake uzalendo wake ni kwa mtu na siyo nchi?)
4.Ripoti ya kamati ya Dr.Mwakyembe ilionesha vimemo kutoka kwa PM kwenda kwa mawaziri na mpaka wabunge wa ccm wakashawishika kumhusisha Lowassa na Richmond.Ina maana hawa walikuwa hawaelewi mtego wa Sitta na Dr Mwakyembe,walikuwa wamehongwa au kipi kilitokea?
(Akina ole Sendeka,Kilango Malecela et a' nasikia wameshaungama)
Yote kwa yote,Richmondi ilikuwa kitu REAL au FAKE?
Kama ilikuwa real,Lowassa hakushiriki kabisa au alishiriki pamoja na mh.Rais ila baadae akatolewa sadaka kwa niaba ya mkuu?
Na kama alishiriki pamoja na mkuu wake kwa nafasi yake kunamfanya asiwe fisadi?
Karibuni Wajuaji,mtufumbue wengine macho.
Lowasa anasema alikaa Kimya kwa miaka saba kwa kuwa alikuwa analinda serikali na Rais Kikwete asianguke ina maana sasa hivi ameamua kuongea kwa kuwa lengo lake sasa ni kumwangusha Rais Kikwete na Serikali yake???
 
Ukweli kuhusu Richmond utaendelea kubaki kuwa siri ya Baraza la Mawaziri la kipindi hicho cha Lowasa. Hakuna mkataba wowote unaoingiwa bila kujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri. Hivyo, sisi Raia wa kawaida (layman) tunaijadili RICHMOND kijuu juu tu, ukweli wanaujua mawaziri waliokuwepo.
Kuhusu kujiuzulu kwa Lowasa, aliwajibika ili kuinusuru serikali. Kumbuka kuwa kama richmond ilikuwa inaihusu serikali, ilikuwa mkuu wa serikali ndiye awajibike ambaye ni rais. Hivyo ili kuondoa ile total collapse of Government ambayo ingetokea kwa rais kujiuzulu, ikabidi Waziri mkuu awajibike kwa nafasi yake (Uwaziri mkuu), ili kuvunja baraza la mawaziri liundwe upya. Hivyo, issue si Lowasa kama mtu binafsi. Issue ni waziri mkuu ajiuzulu ili kumnusuru Rais asijiuzulu. Kwa maana nyingine ni kwamba, hata kama waziri mkuu wa wakati huo angekuwa Pinda, au Mwakyembe au Sumaye, lazima angewajibika ili kumlinda rais. Ndo maana jamaa alisema tatizo ni uwaziri mkuu.
Pia hata kama asingejiuzulu, bado asingeendelea kuwa waziri mkuu maana baraza la mawaziri lingevunjika kwa president kujiuzulu.
NOTE: Simtetei lowassa kwa nafsi yake, ila ninazungumza kile kilichotakiwa kutokea.
Mikakati yote na hatua zote za kuipata RICHMOND rais alikuwa na taarifa, na naamini alitoa go ahead, baada ya kujadiliwa kwenye Cabinet wakuu.

Tusiwe soft minded kihivyo
 
Tusiwe soft minded kihivyo[/QUOTE

. Msaidizi Mkuu wa Lowassa, Ole Kuyan, katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anasema, “…Endelea kusaini mkataba kati ya Richmond na serikali, maana Waziri Mkuu, Edward Lowassa tayari ameridhika kwamba Richmond ipewe mkataba Kauli kwamba Waziri Mkuu Lowassa “ameridhika” inafunga mjadala na inadhirisha kwamba Lowassa alijua kila hatua katika kufanikisha mkataba huu. Aidha, kauli ya Kuyan, kwamba Waziri Mkuu ameridhika na hivyo mkataba kati ya serikali na Richmond usainiwe, inaonyesha wazi kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa anasimamia jambo hili. Vilevile, ni Lowassa ambaye anatajwa kushinikiza upokonywaji Bodi ya Tenda ya Tanesco kazi ya kutafuta mzabuni, baada ya Bodi hiyo kukataa kuipa kazi ya kufua umeme wa dharula kampuni ya Richmond.

Ni Lowassa yuleyule anayetajwa kushinikiza kupunguzwa kwa vigezo ili kufanikisha azima ya kuipa kazi kampuni hiyo ya kitapeli. Lowassa na wenzake walijua, pasipo na shaka kuwa Richmond ni kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa, wala uwezo wa kufanya kazi iliyotaka kupewa.

Hili linathibitishwa na barua ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha kwenda kwa Lowassa, ambayo watetezi na wafuasi wa Lowassa wanaitumia kutaka kumsafisha. Barua hiyo yenye Kumb. Na. CDB 286/397/01 ya 17 Juni, 2006 inasema, “…Nakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Majadiliano ya Serikali (GNT) ya kuteua Richmond na naomba kuwasilisha kwako, kwa uamuzi na maelekezo.” jamani hapa hakuna namna lowasa anaweza mwingiza kikwete kwenye uchafu wake.ila tunajua mfa maji haachi kutapa tapa.chamuhimu hapa ni kujua suala la richmond lilikwisha lowasa aliwajibika kwa makosa yake mwenyewe na si kwa kuiokoa serikali au kwa makosa ya waliyo chini yake.naneno yote niliyo andika hapa yametoka kwenye ripoti ya mwakyembe,ripoti iliandikwa kitaalam kwa miaka saba mnatafuta pakutokea hampaoni ,viva mwakyembe msomi bingwa wa sheria alieitendea haki taaluma yake
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Msaidizi Mkuu wa Lowassa, Ole Kuyan, katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anasema, “…Endelea kusaini mkataba kati ya Richmond na serikali, maana Waziri Mkuu, Edward Lowassa tayari ameridhika kwamba Richmond ipewe mkataba Kauli kwamba Waziri Mkuu Lowassa “ameridhika” inafunga mjadala na inadhirisha kwamba Lowassa alijua kila hatua katika kufanikisha mkataba huu. Aidha, kauli ya Kuyan, kwamba Waziri Mkuu ameridhika na hivyo mkataba kati ya serikali na Richmond usainiwe, inaonyesha wazi kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa anasimamia jambo hili. Vilevile, ni Lowassa ambaye anatajwa kushinikiza upokonywaji Bodi ya Tenda ya Tanesco kazi ya kutafuta mzabuni, baada ya Bodi hiyo kukataa kuipa kazi ya kufua umeme wa dharula kampuni ya Richmond.

Ni Lowassa yuleyule anayetajwa kushinikiza kupunguzwa kwa vigezo ili kufanikisha azima ya kuipa kazi kampuni hiyo ya kitapeli. Lowassa na wenzake walijua, pasipo na shaka kuwa Richmond ni kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa, wala uwezo wa kufanya kazi iliyotaka kupewa.

Hili linathibitishwa na barua ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha kwenda kwa Lowassa, ambayo watetezi na wafuasi wa Lowassa wanaitumia kutaka kumsafisha. Barua hiyo yenye Kumb. Na. CDB 286/397/01 ya 17 Juni, 2006 inasema, “…Nakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Majadiliano ya Serikali (GNT) ya kuteua Richmond na naomba kuwasilisha kwako, kwa uamuzi na maelekezo.” jamani hapa hakuna namna lowasa anaweza mwingiza kikwete kwenye uchafu wake.ila tunajua mfa maji haachi kutapa tapa.chamuhimu hapa ni kujua suala la richmond lilikwisha lowasa aliwajibika kwa makosa yake mwenyewe na si kwa kuiokoa serikali au kwa makosa ya waliyo chini yake.naneno yote niliyo andika hapa yametoka kwenye ripoti ya mwakyembe,ripoti iliandikwa kitaalam kwa miaka saba mnatafuta pakutokea hampaoni ,viva mwakyembe msomi bingwa wa sheria alieitendea haki taaluma yake
 
Hapa kiini cha richmond ni raisi kikwete himself.Tuache unafikina tuseme ukweli.
 
EL hakujua kuwa ni kosa uaminifu wake uko wapi wewe, mlinda mwizi umpe ofisi. Kwa kulinda ufisadi watu wangapi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma za hospitali. Usiwe hivyo mtz amka mlinda mwizi ndye mwizi mkuu
 
ilikua fake,ila kina mwak,walicheza na lugha.
ishu ya umeme ilikua ni ya dharura,na hivyo taratibu zikaenda kidharura ili watu wapate umeme,,Nadhani baadhi ya taratibu za zabuni zikarukwa ili ipatikane kampuni itakayoleta mashine.
huwa nashindwa kuelewa wanaodai pesa za richmond ziliibiwa ni zipi hizo

Umeme ulizalishwa huo wa dharula? Huelewi hata unachosema pesa ilipwa kwa richmund kwa muda gani soma uelewe siyo ushabiki mwakyembe na kamati yake walitoa kila kitu hujui hata unamshabikia
 
Waadau nadhani majibu umeyaona.. na labda nichangie hili, maamuzi ya kuipa richmond tender hiyo yalitoka kwa namba moja. Na hata nilishawahi ona picha wakati karamagi ana sign mkataba wa dowans uingereza if not mistaken. JK was on that pic standin behind karamagi. Sasa kama lowassa alimuuliza mwenyekiti kwaanini unawaruhusu hawa kunisema hivi wakati ukweli wote kuhusu hili swala unaujua na sihusiki na ndo mkapa kuingilia kati kwa maana ingeleta mtafaruku mwenye ule mkutano wa ccm dodoma waa mwezi Nov 2011. Basi hapa nadhani tumeona ukweli kuwa jk ndo muhusika na ndo pia alipanga escrow since 1994 akiwa waziri wa nishati na madini na ndo mwaka jana(20yrs later) akatupiga hela za escrow na kutotaka majina ya wenye account stanbic waliolipwa yajulikane. Na pia kama ndo hivyo basi pia waziri mkuu huyu na wengine ukifata ile trend ya wakati ule wangejiuzuru pia. But nothin happened na pesa iliyopea escrow ukilinganisha naa na ya kununua zile generators kuna tofauti kubwa sana. Escrow is big big money stolen. Haya bado wabunge hawa hawa ambao wanajidai wanapenda maendeleo ya taifa hili ukichanganya na wapinzani wameshindwa kupigania serikali kutowalipa ongezoko la asilimia 250 ya hela zao. Nikimaanisha hizo milioni 230 kwa kila mbunge.. wakati mahabara za shule tu za sekondari walitukomalia sisi wananchi tuchangie. Wangepambana na hilo pia tungeona ni wenzetu ila ndo hivyo tena wapo wenye nia nzuri ila ndo hao mnawasemaa ni mafisadi with no proof. Kwa mtazamo wangu. Lowassa anafaa sana na ni kiongozi mahiri. Apewe nidhaa ya kutuongoza. Tutafika mbali sana.
 
Aya nenda ukachukie buku 10 yako kwa kutetea!!
 
Ukweli kuhusu Richmond utaendelea kubaki kuwa siri ya Baraza la Mawaziri la kipindi hicho cha Lowasa. Hakuna mkataba wowote unaoingiwa bila kujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri. Hivyo, sisi Raia wa kawaida (layman) tunaijadili RICHMOND kijuu juu tu, ukweli wanaujua mawaziri waliokuwepo.
Kuhusu kujiuzulu kwa Lowasa, aliwajibika ili kuinusuru serikali. Kumbuka kuwa kama richmond ilikuwa inaihusu serikali, ilikuwa mkuu wa serikali ndiye awajibike ambaye ni rais. Hivyo ili kuondoa ile total collapse of Government ambayo ingetokea kwa rais kujiuzulu, ikabidi Waziri mkuu awajibike kwa nafasi yake (Uwaziri mkuu), ili kuvunja baraza la mawaziri liundwe upya. Hivyo, issue si Lowasa kama mtu binafsi. Issue ni waziri mkuu ajiuzulu ili kumnusuru Rais asijiuzulu. Kwa maana nyingine ni kwamba, hata kama waziri mkuu wa wakati huo angekuwa Pinda, au Mwakyembe au Sumaye, lazima angewajibika ili kumlinda rais. Ndo maana jamaa alisema tatizo ni uwaziri mkuu.
Pia hata kama asingejiuzulu, bado asingeendelea kuwa waziri mkuu maana baraza la mawaziri lingevunjika kwa president kujiuzulu.
NOTE: Simtetei lowassa kwa nafsi yake, ila ninazungumza kile kilichotakiwa kutokea.
Mikakati yote na hatua zote za kuipata RICHMOND rais alikuwa na taarifa, na naamini alitoa go ahead, baada ya kujadiliwa kwenye Cabinet wakuu.

Tusiwe soft minded kihivyo

NAFARIJIKA WATANZANIA WAMEANZA KULIFAHAMU SUALA HILI/ii
 
lowasa ni fisadi mkubwa yeye ndiye aliyeunda kundi la matapeli na kuiibia nchi

naona unatetea ili ile baishara yako haramu ipate wa kuilinda,lowassa anakwenda kufumuwa mabaishara yote yasiyokuwa halali,ndio maana mnaona nikikwazo kwenu
 
lowasa ni jambazi mkubwa toka angali tumboni.El ni mwizi na tamaa za tumbo
 
Samahani jamani mbona mimi sioni kitu kabisa ndani ya EL, kila ninapomsikiliza sioni chochote ninachoona zaidi ni mikakati, harakati sioni kitu special kabisa Iam sorry!

Nawa maji usoni una tongotongo wewe, mara sioni....mara naona....
 
Lakini kama usafi wako una walakini kwa nini kujisafisha kwa Dodoki?ina maana lazima wewe?bila wewe basi hakuna mwingine?
 
Ukweli kuhusu Richmond utaendelea kubaki kuwa siri ya Baraza la Mawaziri la kipindi hicho cha Lowasa. Hakuna mkataba wowote unaoingiwa bila kujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri. Hivyo, sisi Raia wa kawaida (layman) tunaijadili RICHMOND kijuu juu tu, ukweli wanaujua mawaziri waliokuwepo.
Kuhusu kujiuzulu kwa Lowasa, aliwajibika ili kuinusuru serikali. Kumbuka kuwa kama richmond ilikuwa inaihusu serikali, ilikuwa mkuu wa serikali ndiye awajibike ambaye ni rais. Hivyo ili kuondoa ile total collapse of Government ambayo ingetokea kwa rais kujiuzulu, ikabidi Waziri mkuu awajibike kwa nafasi yake (Uwaziri mkuu), ili kuvunja baraza la mawaziri liundwe upya. Hivyo, issue si Lowasa kama mtu binafsi. Issue ni waziri mkuu ajiuzulu ili kumnusuru Rais asijiuzulu. Kwa maana nyingine ni kwamba, hata kama waziri mkuu wa wakati huo angekuwa Pinda, au Mwakyembe au Sumaye, lazima angewajibika ili kumlinda rais. Ndo maana jamaa alisema tatizo ni uwaziri mkuu.
Pia hata kama asingejiuzulu, bado asingeendelea kuwa waziri mkuu maana baraza la mawaziri lingevunjika kwa president kujiuzulu.
NOTE: Simtetei lowassa kwa nafsi yake, ila ninazungumza kile kilichotakiwa kutokea.
Mikakati yote na hatua zote za kuipata RICHMOND rais alikuwa na taarifa, na naamini alitoa go ahead, baada ya kujadiliwa kwenye Cabinet wakuu.

Tusiwe soft minded kihivyo
Hill in saw a kabisa.ufafanuzi mzuri.
 
Sakata la Richmond linaeleweka vzr isipokuwa kwa mtu asiyetaka kuelewa tu na aliyegoma kuelewa na kujua kwa sababu zake binafsi na mapenzi yake kwa Wezi na Mafisadi wa nchi hii.Lowasa na serikali ya chama chake ni WEZI WALIOKUBUHU.na yeyote anayetetea ni mjinga na mpu.mbavu
 
waadau nadhani majibu umeyaona.. Na labda nichangie hili, maamuzi ya kuipa richmond tender hiyo yalitoka kwa namba moja. Na hata nilishawahi ona picha wakati karamagi ana sign mkataba wa dowans uingereza if not mistaken. Jk was on that pic standin behind karamagi. Sasa kama lowassa alimuuliza mwenyekiti kwaanini unawaruhusu hawa kunisema hivi wakati ukweli wote kuhusu hili swala unaujua na sihusiki na ndo mkapa kuingilia kati kwa maana ingeleta mtafaruku mwenye ule mkutano wa ccm dodoma waa mwezi nov 2011. Basi hapa nadhani tumeona ukweli kuwa jk ndo muhusika na ndo pia alipanga escrow since 1994 akiwa waziri wa nishati na madini na ndo mwaka jana(20yrs later) akatupiga hela za escrow na kutotaka majina ya wenye account stanbic waliolipwa yajulikane. Na pia kama ndo hivyo basi pia waziri mkuu huyu na wengine ukifata ile trend ya wakati ule wangejiuzuru pia. But nothin happened na pesa iliyopea escrow ukilinganisha naa na ya kununua zile generators kuna tofauti kubwa sana. Escrow is big big money stolen. Haya bado wabunge hawa hawa ambao wanajidai wanapenda maendeleo ya taifa hili ukichanganya na wapinzani wameshindwa kupigania serikali kutowalipa ongezoko la asilimia 250 ya hela zao. Nikimaanisha hizo milioni 230 kwa kila mbunge.. Wakati mahabara za shule tu za sekondari walitukomalia sisi wananchi tuchangie. Wangepambana na hilo pia tungeona ni wenzetu ila ndo hivyo tena wapo wenye nia nzuri ila ndo hao mnawasemaa ni mafisadi with no proof. Kwa mtazamo wangu. Lowassa anafaa sana na ni kiongozi mahiri. Apewe nidhaa ya kutuongoza. Tutafika mbali sana.

huyo lowassa nae amelipwa 230
 
Kama ndivyo,basi anatudanganyia nini anavyosema Aliundiwa kashfa? Anapaswa kuadhibiwa kwa ulaghai huu?
Anajua vizuri kuwa Watanzania ni WAJINGA hivyo hawatakumbuka chochote. Kwa Watanzania wiki tu ni kubwa kusahau mabaya yote...sasa huyu miaka saba?
 
Back
Top Bottom