Mkandarasi atishia kusitisha ujenzi terminal 3

MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,318
6,391
Siku za hapo nyuma tulielezwa kuwa mkuu baada ya kufanya ziara ya gafla na kumtumbua yule mama wa hazina alitoa maagizo madai ya kampuni ya bam yalipwe. Sasa mbona leo kwenye taarifa ya habari saa mbili azam tv, kuna habari kuwa mkandarasi ametoa notisi ya kusitisha ujenzi. Swali la kujiuliza ni kuwa hakukuwa na mawasaliano kati ya mkulu na hazina kama fedha zipo?
 
Hahahahaaa mbwembwe zote zile? nakumbuka katibu mkuu fedha alithibitisha madai yao kulipwa yote tena akabeua lingine ati serikali imekamilisha malipo ya awali ya bilioni 300 kwaajili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha kisasa!!! yetu macho na masikio.... huyu mtu mikono yake ina balaa tu kote alikowahi pita ni nuksi.
 
Mkuu mbona nimesikia Mkandarasi kalipwa pesa zote na hadai chochote labda akitoa certificate nyingine. Nimesikia kwamba Consultant yaani msimamizi wa Mkandarasi ndiye katoa notisi kwa kuwa hajalipwa. Nimemuona Katibu Mkuu akisema hiyo ni kawaida katika mambo ya ujenzi na haiwezi kuzuia ujenzi.

Jambo moja muhimu ni vyema kufahamu kati ya Consultant na Contractor kwenye construction project ili tusiwe tunachanganya mambo.
 
Nafikiri idadi kubwa ya miradi ilioanza itakwama na hata hii mipya sijui, maana hata hiyo fly over ya Mandela road mpaka leo hakuna hata nguzo iliokamilika.
 
nijuaavyo mimi certificate inapotoka wanalipwa wote consultants na contractor, plz dadavua
 
Ha ha ha ha ha......hii ndio awamu ya tano bwana........nimeangalia nikabaki nashangaa, Mh Rais aliposema walipwe maana hela zipo alikuwa anamuagiza nani, Leo kamati ya bunge inasema vingine......awamu hii ni vituko.
 
Siku za hapo nyuma tulielezwa kuwa mkuu baada ya kufanya ziara ya gafla na kumtumbua yule mama wa hazina alitoa maagizo madai ya kampuni ya bam yalipwe. Sasa mbona leo kwenye taarifa ya habari saa mbili azam tv, kuna habari kuwa mkandarasi ametoa notisi ya kusitisha ujenzi. Swali la kujiuliza ni kuwa hakukuwa na mawasaliano kati ya mkulu na hazina kama fedha zipo?
Si aliwapa hela mbele ya vyombo vya habari?
Au ilikuwa zake za kuuza sura tu. Maana utasikia kesho natoa hela unafikiri anatoa mfukoni mwake. Waziri wa Fedha hana kazi.
 
Nafikiri idadi kubwa ya miradi ilioanza itakwama na hata hii mipya sijui, maana hata hiyo fly over ya Mandela road mpaka leo hakuna hata nguzo iliokamilika.
are u sure hakuna nguzo iliyokamilika?
 
Nafikiri idadi kubwa ya miradi ilioanza itakwama na hata hii mipya sijui, maana hata hiyo fly over ya Mandela road mpaka leo hakuna hata nguzo iliokamilika.
Wataalam wa kuponda kila kitu, hadi mnaonekana zero brain. Tazara hakuna hata nguzo moja iliyosimama? Halafu mnasema Bashite alizungusha form iv, Kumbe idadi ya waliozungusha ni kubwa tu.

Pita Tazara kesho uhesabu nguzo ngapi zipo juu.
 
nijuaavyo mimi certificate inapotoka wanalipwa wote consultants na contractor, plz dadavua
Contractor huwa anatoa Interim Payment Certificate ambayo inakuwa certified na Consultant ili Client/employer alipe. Kwa upande wake Consultant hutoa Fee Note ili alipwe na Employer/Client. Ni vitu viwili tofauti
 
Huyu Bashite mnamsingizia tu, nadhani ma-bashite tumejaa Tanzania nzima. Kamati ya kudumu ya bunge imesema mkandarasi amelipwa pesa zake zote hadi next phase, lakini kwa sasa haidai serikali, ambaye hajalipwa na anadai sehemu ya pesa zake ni mhandisi mwelekezi.

Ndio maana wengi tulifeli form iv, tusimcheke Bashite coz asilimia kubwa tuna vielement vya jamaa.
 
Wataalam wa kuponda kila kitu, hadi mnaonekana zero brain. Tazara hakuna hata nguzo moja iliyosimama? Halafu mnasema Bashite alizungusha form iv, Kumbe idadi ya waliozungusha ni kubwa tu.

Pita Tazara kesho uhesabu nguzo ngapi zipo juu.
Achana naye huyo jamaa kwa kuwa hajui Tazara ipo wapi. Tunaishi naye huku kisiwani Lyakanyasi. Serikali imezuia uvuvi haramu huku basi wote tunatapatapa.
 
Nafikiri idadi kubwa ya miradi ilioanza itakwama na hata hii mipya sijui, maana hata hiyo fly over ya Mandela road mpaka leo hakuna hata nguzo iliokamilika.
Mandera road ipi unayoiongelea wewe?
 
Wataalam wa kuponda kila kitu, hadi mnaonekana zero brain. Tazara hakuna hata nguzo moja iliyosimama? Halafu mnasema Bashite alizungusha form iv, Kumbe idadi ya waliozungusha ni kubwa tu.

Pita Tazara kesho uhesabu nguzo ngapi zipo juu.
Rudia kusoma nilichoandika nimesema haijakamilika au unataka kusema urefu ule ndio mwisho.
 
Kua mzalendo wacha unafiki au ulipopata habari ulikua na ngada kichwani kama hujaelewa tafuta vyanzo sio ujinga tu na hao wanaokusapoti na uzwazwa wako huo fahamu mkandarasi hadai hata shilingi ila mshauri wa mkandarasi ndo anaedai na taarifa wametoa kamati ya bunge ya ujenzi na miundo mbingu.
Ndo nyie munaombea taifa njaa wakati familia yako yote iko kijijini.
Wacha ushabiki wakiboya.
Ova
 
Back
Top Bottom