Dar: Waziri Mbarawa atoa maagizo matatu, mradi wa mwendokasi kutoka Gongo la Mboto hadi Mjini km 23.3

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara Mabasi yaendayo haraka awamu ya tatu (BRT-3) ambapo amemuagiza Mkandarasi SINOHYDRO Cooperation Ltd anayejenga mradi huo kuongeza kasi katika utekelezaji wake pamoja na kuhakikisha mradi unakamilika vizuri na kwa wakati.
IMG-20230807-WA0027.jpg

Pia amemuagiza Mhandisi Mshauri na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kuusimamia mradi huo ambao umefikia asilimia 12 kikamilifu ili tuweze kupata barabara yenye viwango vinavyostahili kama usanifu unavyoeleleza.
IMG-20230807-WA0028.jpg

Waziri Prof. Mbarawa ametoa maagizo hayo leo tarehe 7 Agost 2023, Jijini Dar- es Salaam baada ya kutembelea na kukagua mradi wa barabara hiyo inayoanzia Posta ya zamani, barabara ya Nyerere kuelekea Gongo la mboto yenye urefu wa kilometa 23.3 kwa gharama ya shilingi bilioni 231.

‘’Mkandasari amechelewesha mradi kwa asilimia 2 lakini sasa anafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi huu unakamilika, tunapenda kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Ramia Suluhu Hassan kutuwezesha kuhakikisha kuwa tunajenga barabara hii ambayo ni muhimu kwa uchumi wa Nchi yetu kwa sababu inaenda maeneo ya Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Julius Nyerere na Maeneo yenye Wananchi wengi, naomba watu wa Dar-es Salaam wawe wavumilivu, tunataka kujenga barabara hii kwa viwango wakati huo huo tunaangalia usalama wa watu wanaopita’’ ameeleza Waziri Prof. Mbarawa.
IMG-20230807-WA0039.jpg

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa kuhakikisha asilimia 2 zilizocheleweshwa na mkandasi zinakuja kufidiwa wakati ujenzi ukiendelea katika hatua inayofuata huku akiihakikishia Serikali kwamba mradi huo utakwenda kwa haraka na kwa viwango vinavyokubalika.
IMG-20230807-WA0031.jpg
IMG-20230807-WA0034.jpg

Naye Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar-es Salaam Mhandisi Harun R. Senkuku
amesema licha ya mradi kuwa nyuma asilimia 2 lakini jinsi mkandarasi anavyoendelea kujenga mradi kasi nayo inaongezeka, huku Meneja wa Mradi wa BRT Mhandisi Frank Mbilinyi akisema ujenzi huo utaifanya barabara hiyo kuwa na jumla ya njia sita, mbili za mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) na mbili kila upande za magari ya kawaida hatua ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo.
IMG-20230807-WA0024.jpg

IMG-20230807-WA0033.jpg

Wakizungumza kwa niaba Wakuu wa Wilaya Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bi. Charangwe Seleman Makwiro ametoa wito kwa Mkandarasi kuongeza kasi katika ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa haraka ili kuwawezesha wananchi kuondokana na changamoto ya msongamano wa magari katika barabara hiyo na kufanya shughuli zao za usafiri na usafirishaji kwa haraka.
IMG-20230807-WA0030.jpg
IMG-20230807-WA0035.jpg

Huku Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Decodemas Tambo akimshukuru Dkt. Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambao amesema ni muhimu kwa Wananchi na wageni wanaotoka nje ya Nchi hasa kwa kuzingatia kuwa barabara hiyo inatumiwa pia na watu wengi wanaoruka na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar- es Salaam.

Ujenzi wa BRT awamu ya Tatu unahusisha Barabara ya Azikiwe, Bibi Titi Mohammed, Nkrumah na Nyerere hadi Gongo la mboto km 17.92, Barabara ya Shaurimoyo, Uhuru na Mandela hadi TAZARA km 4.49 na Barabara ya Lindi toka Shaurimoyo hadi BRT Terminal(Gerezani) km 0.95.

IMG-20230807-WA0037.jpg
IMG-20230807-WA0038.jpg
IMG-20230807-WA0026.jpg
IMG-20230807-WA0043.jpg
IMG-20230807-WA0041.jpg
IMG-20230807-WA0032.jpg
IMG-20230807-WA0026.jpg
IMG-20230807-WA0025.jpg
 
Mbarawa hana credibility ya kwenda popote na kutoa maagizo.
 
Back
Top Bottom