Mkakati wa Kuwafelisha Waislam Kidato Cha Sita Wabainika

Status
Not open for further replies.
Waislam wanafeli sana kuliko wakristo ni kweli. Sasa utafananisha shule ya jabal hila ile ya kiislam pale moro na marian jamani. shule mbovu, elimu mbovu, misingi ya elimu mibovu, utafauluje? Jipangeni bwana muache udiniudini hapa, JK kajitahidi sana kuwabeba lkn hamna shukrani.
 
Mungu alimwambia Ibrahim, Isaka atarithi na atakuwa mfalme. Sasa Ishimael hakupewa hayo jamani!
Na mke wa Ibrahim akasema mtoto wangu wa pekee Isaka hatakaa pamoja na Ishimael. Tatizo la kuona nyinyi waislam mnaonewa na wakristo si kweli, mfano wapemba wanavyozaa bila mpangilio mtu mmoja hana elimu, hana hela, ila ana watoto 20! Matokeo yake watoto wanakosa elimu nzuri wanaishia la 7 wote!. Sasa unalaumu serikali!
Acheni kukimbili kusoma qruan someni vyote!
Kwa taarifa yako Wapemba wanazaana wengi na wanasomesha sana kama hilo haulijui nenda UD utaona,pia Waislam kusoma ni jambo la lazima kwetu kama tulivyoamuliwa na Mwenyezi Mungu hivyo wewe ukisema Waislam hawasomi sijui unatoa wapi hizo taarifa zako tunakushangaa! Jambo lolote kwetu sie Waislam ukiambiwa ni FARDH ni kuwa hauna wajibu wa kuliacha na ukiliacha basi unapata dhambi ndivyo lilivyo suala la Elimu kwetu ila nyie msio Waislam mnatutangazia kuwa sie ni VILAZA hatuna elimu nawaomba muelewe kuwa hizo falsafa zenu haziko sahihi!
 
mods hizi thread za udini zimezidi tumezichokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

khaaaaaa
 
Hakika Dhambi ya udini itatuuwa woote kwa pamoja!
Yaani kila kitu ni udini, natamani san wote tungesikiliza hotuma ya mwalimu nyerere ya tarehe 9. Dec 1962. Mwaka mmoja baada ya Uhuru
 
ni rahisi sana kupata A ktk Divinity lakini kwa ISLAMIC KNOWLEDGE sahau,why?huwanyanyua sana seminary za katoliki
 
Hapa wanafunzi wanapofeli kuusingizia kuwa ni juu ya dini zao mimi napinga kwa nguvu moja! tena napinga kabisa, dhana hii ilikuwapo wakati wa marehemu Kighoma Ali Malima alipokuwa waziri wa elimu, na ili kuondoa dhana hii ukaletwa mfumo wa wanafunzi kuandika namba badala ya majina yao na walipendekeza mfumo huu ni waislam sasa iweje tena tunalalamika, na pia wasahishaji wa mitihani hii ni walimu wa shule zetu ina maana wao hawaoni haya na kusema! msiulaumu uislam, maana kati ya dini sinazosisitiza suala la elimu ni uislamu, Muhammad ( rehema za Mungu ziwe juu yake) kabla ya kupewa utume kitu cha kwanza aliambiwa "soma, soma kwa jina la mola wako" hakuambiwa achague elimu ya kusoma, ndio maana hata wakati wake alisisitiza" Itafuteni sana elimu hata kama ni uchina", so kosa sio uislam, kosa ni waislam wenyewe na hapa ni wale wachache wasiojali mbona kuna waislam wengi tu wamesoma na wanafanya vizuri mfano ni Prof. maghembe, Marehemu Haroub Othman, Prof Issa Shivji, Mwanaid Maajar na wengine tuache visingizio na kuutukanisha uislam!
 
Kwa taarifa yako Wapemba wanazaana wengi na wanasomesha sana kama hilo haulijui nenda UD utaona,pia Waislam kusoma ni jambo la lazima kwetu kama tulivyoamuliwa na Mwenyezi Mungu hivyo wewe ukisema Waislam hawasomi sijui unatoa wapi hizo taarifa zako tunakushangaa! Jambo lolote kwetu sie Waislam ukiambiwa ni FARDH ni kuwa hauna wajibu wa kuliacha na ukiliacha basi unapata dhambi ndivyo lilivyo suala la Elimu kwetu ila nyie msio Waislam mnatutangazia kuwa sie ni VILAZA hatuna elimu nawaomba muelewe kuwa hizo falsafa zenu haziko sahihi!

Nakupongeza kwa kumjibu huyo jamaa kwa busara japo kauli zake zinakera,angejibiwa na ally kombo angeipata,big up mkuu
 
Zanzibar tunaambiwa kuna wanafunzi wengi majibu ya mitihani yao ilibadilishwa. walipata B lkn wakaambulia F. baada ya kufatilia ndipo walipogundua kwamba matokeo yao sio halali.
Hii pia imetokea mwaka huu kwa upande wa tanzania baram kwa uapnde wa shule za waislam. ipo mifano mingi kama utafatilia na kuondoa jazba za kidini utapata maelezo na walioathirika na matokeo. jee kuna komputa za waislam na wasiokuwa waislam?
Kwanini NECTA ikosee kwa wanafunzi wa kiislam tu. au hata madhe

Unazungumza kwa hisia au kwa utafiti? Ni wanafunzi gani Wazanzibar waliopata B halafu wakawekewa F? Huo ni uwongo mkubwa. Malalamiko ya Wazanzibari ilikuwa ni kuhusu wanafunzi wao wengi kufutiwa matokeo ya mtihani na kutoruhusiwa kufanya mtihani tena baada ya kugundulika kufanya udanganyifu. Wazanzibari hawakukana watoto wao kufanya udanganyifu bali malalamiko yao ilikuwa ni kuhusu adhabu waliyopewa kuwa ilikuwa kubwa mno.

Kwa huku bara tatizo lilikuwa ni kwenye somo la dini ya kiislam wala siyo kwenye masomo ya 'elimu dunia' kama mnavyoyaita. Mtu akufelishi kwa makusudi kwenye somo la dini ili iweje? Somo hilo ukifaulu au ukafeli halina athari yeyote juu ya nafasi yako ya kuendelea na masomo au kutoendelea, linaweza tu kuchangia kwenye daraja la ufaulu, na si vinginevyo. Unaposema Wakristo wamewafelisha wanafunzi wa kiislam kwenye somo la dini ya kiislam, ina maana wakifeli waislam, wakristo ndiyo wataenda kusomea uislam? No reasoning! Somo la dini ya kiislam linasahihishwa na walimu wa dini ya kiislam, na makosa yalitokea kwa mtu aliyekuwa akiingiza kumbukumbu kwenye database ya NECTA, na ni kosa ambalo lilifanywa na idara ya IT, siyo ukristo. Kama wanataka kuidhibu au kuitaka kuiwajibisha NECTA kwa kosa hilo wafanye hivyo kwa sababu tu NECTA na Wizara ya Elimu wameshindwa kusimamia mitihani siyo kwaajili ya ukristo wa mkurugenzi wa NECTA. Hivi Waislam wanataka wasio waislam wamhukumu Kikwete kwa kushindwa kusimamia uchumi wa nchi kwaajili ya Uislam wake au kwaajili ya utendaji wake kama Rais aliyechaguliwa na Watanzania mbalimbali wenye matarajio mbalimbali? Ndugu zetu 'Waislam Mufilisi wa Mawazo' msiturudishe kwenye karne 4. Sauti za Waislam Mufilisi Wachache zinawaabisha Waislam makini wa nchi hii ambao majina yao ni makubwa katika ujenzi wa amani na umoja wa Watanzania.
 
Huu nao ni upuuzi mwingine...Hao wengine wanafanya Islamic Knowledge??.

Na mimi nilikua na wazo kama lako...lakini kwa kuongezea wanafunzi waislamu inabidi muwakabe na kuwashutumu waalimu wenu waliotengeneza marking schemes zisizo sahihi hata ikatokea mitihani yenu ikasahihishwa vibaya
 
Hivi hata kwa kutizama namba tu ya mtahiniwa unawezajua dini yake? Naweza kuelewa kama kuna systematic error ambayo imetokea kwa shule fulani ambayo kwa bahati mbaya ni shule ya kiisilamu au kwa somo fulani ambalo linawahusu waisilamu pekee. Lakini tuhuma kuwa ni wanafunzi waisilamu pekee ndio wamekuwa targeted, hii sioni kama ina ukweli wowote. Labda kama kuna mtu anaweza kutuletea ushahidi hapa kuwa katika shule fulani ya mchanganyiko (waislamu na wasio waislamu) na katika somo ambalo ni wote waislamu na wasio waislamu walifanyia mtihani ikatokea kuwa katika shule hiyo na somo hilo ni waislamu pekee ndio matekeo yao yalikosewa! Kinyume na hapo tunaweza kujikuta tunaendeleza udini na hatimaye chuki ambazo baade zitatugharimu sote bila kujali tutakuwa na imani gani kwa wakati huo.
 
Hapa wanafunzi wanapofeli kuusingizia kuwa ni juu ya dini zao mimi napinga kwa nguvu moja! tena napinga kabisa, dhana hii ilikuwapo wakati wa marehemu Kighoma Ali Malima alipokuwa waziri wa elimu, na ili kuondoa dhana hii ukaletwa mfumo wa wanafunzi kuandika namba badala ya majina yao na walipendekeza mfumo huu ni waislam sasa iweje tena tunalalamika, na pia wasahishaji wa mitihani hii ni walimu wa shule zetu ina maana wao hawaoni haya na kusema! msiulaumu uislam, maana kati ya dini sinazosisitiza suala la elimu ni uislamu, Muhammad ( rehema za Mungu ziwe juu yake) kabla ya kupewa utume kitu cha kwanza aliambiwa "soma, soma kwa jina la mola wako" hakuambiwa achague elimu ya kusoma, ndio maana hata wakati wake alisisitiza" Itafuteni sana elimu hata kama ni uchina", so kosa sio uislam, kosa ni waislam wenyewe na hapa ni wale wachache wasiojali mbona kuna waislam wengi tu wamesoma na wanafanya vizuri mfano ni Prof. maghembe, Marehemu Haroub Othman, Prof Issa Shivji, Mwanaid Maajar na wengine tuache visingizio na kuutukanisha uislam!

Well said mkuu!
 
Kuna dharau kuhusu malalamiko ya Waislamu katika hili. Soma uelewe kabla ya kutupa matusi.
- Wanafunzi walifanya mitihani
- Mitihani yao ilisahihishwa na walimu wa kiislamu hivyo walijua wastani ya waliopasi
- Matoleo yaliyowekwa kwenye "database" yalikuwa tofauti na yale kwenye karatasi
 
Kuna dharau kuhusu malalamiko ya Waislamu katika hili. Soma uelewe kabla ya kutupa matusi.
- Wanafunzi walifanya mitihani
- Mitihani yao ilisahihishwa na walimu wa kiislamu hivyo walijua wastani ya waliopasi
- Matokeo yaliyowekwa kwenye "database" yalikuwa tofauti na alama za kwenye karatasi
- Shule ziliandika barua ya pamoja kuhoji hili
- NECTA ikabadilisha matokeo kinyemela bila kujibu barua na kuyaweka katika mtandao.
- Waislamu wakalalamikia hili
- Wajinga na Wadini wakawatukana
- Magazeti yakakausha

Sasa nani wa kuwajibishwa hapa?

yalikuwa tofauti na yale kwenye karatasi
 
Na mimi nilikua na wazo kama lako...lakini kwa kuongezea wanafunzi waislamu inabidi muwakabe na kuwashutumu waalimu wenu waliotengeneza marking schemes zisizo sahihi hata ikatokea mitihani yenu ikasahihishwa vibaya
Wakati wanatengeneza marking scheme, wewe ulikuwepo !? Au unaropokwa tuu ?
 
sijui kwa nini Tanzania tunakuwa na mawazo mabaya sana ya udini..katika hali ya kawaida mtu anafikiria kwamba mtu nafelishwa kwa sababu ya dini yake..nachelewa kuamini katika hili coz kwanza watahiniwa wanatumia number badala ya jina sasa sijui huyo anayefelisha Waislamu anawaona kwa kutumia nini na malengo yake nini!..! lakini ndugu zangu mkiruhusu haya mawazo yaingie kwenye vichwa vya watoto wetu hakika wataendelea kufeli kwa kusingizia wanaonewa. Tunampa stress Mama wa Watu bure pale baraza la mitihani. Kweli tunaelekea pabaya kama hatutakuwa makini katika hili. Eee Mungu tuokoe watu wako wanaangamia kwa kukosa maarifa..
 
Kina Ponda wamesema ni somo la Kiarabu na Knowledge ya dini ya Kiislamu ndio hao watoto wame fail na wakawa wanafananisha na somo la Biblia kwamaba watoto wanafaulu sana somo hili, lakini Waislamu wanafelishwa lao!

USHAURI; Kiarabu ni Lugha ngumu wafundisheni watoto wenu somo hilo kwa Kiswahili na hawato fail vinginevyo mtatoka mapovu mpaka utimilifu wa dahari! Shuleni mtoto masomo yake anaandika toka kushoto kwenda kulia ninyi mnawalazimisha kuandika toka kulia hii ni ajabu sana!
hoja sio ugumu wa somo au lugha, issue ni kwanini matokeo yabadilike baada ya kulalamikiwa?? na NECTA wenyewe wamekiri kuwa watu wao wa IT walikosea ktk kuyaingiza kwn system!!?? Na kama imewezekana kwa somo moja iweje ishindikane kwa masomo mengine??
 
Mizimu ya waarabu huwachanganya sana waislamu wanapofanya mitihani kwasababu wakati wenzao walikuwa madarasani wao walikuwa madrasani...vitu viwili tofauti.......msilaumu mtu ila muilaumu dini yenu ambayo haiwafanyi muwe na uwezo wa kushindana kielimu na wakristo.
Wewe akili yako ni mbovu una takwim ya waislam wangapi wamesoma na wakristo wangapi wamesoma? ngoja nikusaidie waislam wengi wameenda shule isipokuwa tokea uhuru walikuwa hawapewi kuongoza sekta muhimu kwasababu ya ubaguzi wa kidini na ndo maana mnalalamika sasa hv baada ya wasio wabaguzi kuwapa angalau nafasi nyeti cjui hao wazee maprofesa na madokta wakiislam hizo awam nyingine walikuwa ugaibun?
 
Waislam wanafeli sana kuliko wakristo ni kweli. Sasa utafananisha shule ya jabal hila ile ya kiislam pale moro na marian jamani. shule mbovu, elimu mbovu, misingi ya elimu mibovu, utafauluje? Jipangeni bwana muache udiniudini hapa, JK kajitahidi sana kuwabeba lkn hamna shukrani.

Sasa hivi mko bize kuua shule za serikali, zifanye vizuri zenu tu za Kanisa !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom