Nani asiyejua kwamba Urais ni mtamu? Nani asiyeutaka? Watu wanajipanga wanapanga mitandao yao ndani ya vyama ndio maana hakuna chama ambacho tayari kimeishamtaja mgombea Urais wake. Ndani ya CDM kuna mitandao ya Urais halikadhalika CCM kuna mitandao ya Urais. Watu wanajipanga kimya kimya wakiviziana. Mbowe ana karata ya kuwa KUB na pia Mwenyekiti wa Chama kwa sasa na Dr. Slaa ana karata ya kuwa Katibu Mkuu wa Chama nasi kila mmoja anajipanga kivyake.
Nyie ndo mnafikiria makundi ndani ya cdm kwenye vibaraza vyenu vya magamba..CDM HATUNA VITA VYA URAIS.
Aliyegombea 2010 ni mchaga?
keep on dreaming! vita ipo kubwa tena ile ya kinafki! bora ccm wamejiweka wazi wazi ...
Freeman Alkaeli Mbowe anaamini kuwa fursa ya CHADEMA kuchukua nchi ni 2015,hivyo ni fursa muhimu kwake kugombea urais kupitia CHARDEMA,ili afanikiwe ameamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA mwakani ili ajiweke katika nafasi nzuri kinyume na kauli yake kuwa hatagombea uenyekiti tena.
Ili kufanikiwa kwa sasa mkakati unaoratibiwa na wafanyakazi wa CHADEMA ndani ya chama ni kuandaa na kuratibu mapambano dhidi ya Dr.Slaa anaeonekana kuwa kikwazo kikuu na kisiki cha mpingo kwake,hofu juu ya zitto inazidi kupungua kutokana na umri,kasha zinazozidi kumuandama Kabwe.
Wapenda haki na mabadiliko ndani ya nchi hii,mwambieni Freeman Mbowe kuwa kwa sasa Dr.Slaa anafaa kwa vigezo vyote japo anamadhaifu mengi kama wanadamu wengine lakini ukimlinganisha na Mbowe utajua umuhimu wa Dr. Slaa.
Naomba kusema haya kwa kuwa napenda mabadiliko yatakayohakisi maisha ya watanzania na si vinginevyo
Mkuu kwenye thread za Tuntemeke hukosekani......Zitto ana kundi la vijana gani? Wa CCM? Unaonaje kura ya maoni hapa JF? Siyo vijana wanapiga hizi kura? Achana na cheap politics mkuu....
Freeman Alkaeli Mbowe anaamini kuwa fursa ya CHADEMA kuchukua nchi ni 2015,hivyo ni fursa muhimu kwake kugombea urais kupitia CHARDEMA,ili afanikiwe ameamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA mwakani ili ajiweke katika nafasi nzuri kinyume na kauli yake kuwa hatagombea uenyekiti tena.
Ili kufanikiwa kwa sasa mkakati unaoratibiwa na wafanyakazi wa CHADEMA ndani ya chama ni kuandaa na kuratibu mapambano dhidi ya Dr.Slaa anaeonekana kuwa kikwazo kikuu na kisiki cha mpingo kwake,hofu juu ya zitto inazidi kupungua kutokana na umri,kasha zinazozidi kumuandama Kabwe.
Wapenda haki na mabadiliko ndani ya nchi hii,mwambieni Freeman Mbowe kuwa kwa sasa Dr.Slaa anafaa kwa vigezo vyote japo anamadhaifu mengi kama wanadamu wengine lakini ukimlinganisha na Mbowe utajua umuhimu wa Dr. Slaa.
Naomba kusema haya kwa kuwa napenda mabadiliko yatakayohakisi maisha ya watanzania na si vinginevyo
Mie naona kwanza wangejaribu kupata japo nusu kitu (uwakilishi) huko Zanzibar.
Sisi kama vuguvugu la madiliko hatuwatambui watu wa visiwani ( Zan & Pemb).
Zanzibar wana wa2 1.5 million ambao wanaingia mara mbili kwa mji mzima wa Mwanza na wanaingia mara 9 kwa kanda ya ziwa.
Chadema wanaitaji kushinda kwa kishindo KANDA YA ZIWA, KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, na KANDA YA KASKAZINI. Maeneo mengine ya nchi CDM watagawana kura na vyama vingine.
Zanzibar haina umuhimu.
Mkuu hujasikia kuna mama anapitapita huku na huku kusafisha njia? Zitto ana kundi la vijana, Dr. Slaa ana kundi la wakereketwa na Freeman Aikael Mbowe ana kundi la wahafidhima ndani ya chama! Unataka udadavuzi zaidi? Mkuu siasa ni kujipanga na siasa ni makundi hakuna siri yoyote na asikudanganye mtu kwamba kuna mwanasiasa ambaye anataka uongozi lakini hana kundi hasa akiwa anataka uongozi huo kupitia jumuiya fulani kama chama cha siasa.
Kwa sasa CDM hakuna mgombea Urais kwa hiyo nafasi ipo kwa yeyote atakayemzidi mwenzake kwenye uamuzi ndani ya chama. Hivyo basi watu wanajenga ngome zao. Ingekuwa hakuna shida basi ingekuwa wazi kwamba Dr. anapewa nafasi nyingine ya kujaribu lakini kwa kuwa si hivyo basi uamuzi wa wanachama au wazee (kumbuka uenyekiti na Zitto) utachukua nafsi.