Mkakati wa Freeman Mbowe kugombea urais utaangamiza CHADEMA kama utaendelea anavojipanga

Kwani sifa mgombea kiti cha urais CDM lazima awe mwenyekiti? au mdoa fununu unampango wa kuwagombanisha maswahiba.
 
Time will tell lakini kuna jembe shibuda,huyu anakubalika kwa jamii yote kanda ya ziwa na upeo wake ni mzuri.
 
Tufanye kazi za maendeleo,wagombea urais tumeshawajua ni mbowe ,slaa,zito,na shibuda.hadi sasa hakuna zaidi ya hawa alieonyesha nia japo wazee wa chama hawataki zito na shibuda wagombee
 
Hakuna hata mmoja mwenye sifa hata muelekeo pia siuoni ,hawa wanafikiri ubabe wao ndio vigezo vya kuwa Raisi wa Tz ,watu wengine mnaona ni rahisi kuwa raisi wa tz yaani ukiweza kuzua longolongo basi mnakimbilia kuwania uraisi.
 
Nani asiyejua kwamba Urais ni mtamu? Nani asiyeutaka? Watu wanajipanga wanapanga mitandao yao ndani ya vyama ndio maana hakuna chama ambacho tayari kimeishamtaja mgombea Urais wake. Ndani ya CDM kuna mitandao ya Urais halikadhalika CCM kuna mitandao ya Urais. Watu wanajipanga kimya kimya wakiviziana. Mbowe ana karata ya kuwa KUB na pia Mwenyekiti wa Chama kwa sasa na Dr. Slaa ana karata ya kuwa Katibu Mkuu wa Chama nasi kila mmoja anajipanga kivyake.
 
Mkuu hebu tudadafulie basi. CCM tunayafahamu makundi na wafuasi wa baadhi wanaosemekana kutaka kuwania urais. Wengine wameshaanza kupigana vikumbo kwenye uongozi wa Uvccm. Lakini binafsi sijasikia makundi ambayo yameanza kujidhatiti kwa CDM zaidi ya Zitto kusikika/kusemwa kuwa anafikiria hivyo lakini hakuna uthibitisho wa makundi na jitihada zake (kama sijakosea). Kama unafahamu chochote juu ya makundi na mitandao yao na jinsi wanavyojipanga kimya kimya basi tuwekee mkuu.
 
BUSARA ZITATUMIKA AU UCHAGA UTATUMIKA VIP?WEKA WAZI BWANA maana cdm kwa wachaga sindio nyumbani

Kwa wale wote waciojua aina za comments zinatumwa na binadamu mwenye ubongo wenye matundu.. Hiyo juu ni mojawapo..

Sent from Tora Bora..
 
Najua lengo lako ulitaka kuweka thread hii kwenye forum ya jokes, ila umejichanganya tu! Usiwaze tumekusamehe bure!
 
Mkuu hebu tudadafulie basi. CCM tunayafahamu makundi na wafuasi wa baadhi wanaosemekana kutaka kuwania urais. Wengine wameshaanza kupigana vikumbo kwenye uongozi wa Uvccm. Lakini binafsi sijasikia makundi ambayo yameanza kujidhatiti kwa CDM zaidi ya Zitto kusikika/kusemwa kuwa anafikiria hivyo lakini hakuna uthibitisho wa makundi na jitihada zake (kama sijakosea). Kama unafahamu chochote juu ya makundi na mitandao yao na jinsi wanavyojipanga kimya kimya basi tuwekee mkuu.

Mkuu hujasikia kuna mama anapitapita huku na huku kusafisha njia? Zitto ana kundi la vijana, Dr. Slaa ana kundi la wakereketwa na Freeman Aikael Mbowe ana kundi la wahafidhima ndani ya chama! Unataka udadavuzi zaidi? Mkuu siasa ni kujipanga na siasa ni makundi hakuna siri yoyote na asikudanganye mtu kwamba kuna mwanasiasa ambaye anataka uongozi lakini hana kundi hasa akiwa anataka uongozi huo kupitia jumuiya fulani kama chama cha siasa.

Kwa sasa CDM hakuna mgombea Urais kwa hiyo nafasi ipo kwa yeyote atakayemzidi mwenzake kwenye uamuzi ndani ya chama. Hivyo basi watu wanajenga ngome zao. Ingekuwa hakuna shida basi ingekuwa wazi kwamba Dr. anapewa nafasi nyingine ya kujaribu lakini kwa kuwa si hivyo basi uamuzi wa wanachama au wazee (kumbuka uenyekiti na Zitto) utachukua nafsi.
 
Nyie ndo mnafikiria makundi ndani ya cdm kwenye vibaraza vyenu vya magamba..CDM HATUNA VITA VYA URAIS.
 
Freeman Alkaeli Mbowe anaamini kuwa fursa ya CHADEMA kuchukua nchi ni 2015,hivyo ni fursa muhimu kwake kugombea urais kupitia CHARDEMA,ili afanikiwe ameamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA mwakani ili ajiweke katika nafasi nzuri kinyume na kauli yake kuwa hatagombea uenyekiti tena.

Ili kufanikiwa kwa sasa mkakati unaoratibiwa na wafanyakazi wa CHADEMA ndani ya chama ni kuandaa na kuratibu mapambano dhidi ya Dr.Slaa anaeonekana kuwa kikwazo kikuu na kisiki cha mpingo kwake,hofu juu ya zitto inazidi kupungua kutokana na umri,kasha zinazozidi kumuandama Kabwe.

Wapenda haki na mabadiliko ndani ya nchi hii,mwambieni Freeman Mbowe kuwa kwa sasa Dr.Slaa anafaa kwa vigezo vyote japo anamadhaifu mengi kama wanadamu wengine lakini ukimlinganisha na Mbowe utajua umuhimu wa Dr. Slaa.

Naomba kusema haya kwa kuwa napenda mabadiliko yatakayohakisi maisha ya watanzania na si vinginevyo

Matatizo ya kula ugali jioni..tumbo linakuwa busy kudigest kwa ivo damu safi yote inaelekea tumboni
 
Ni mapema kuongelea mwasala ya nani atagombea tusubiri 2015 isitoshe chama ndio kitafanya maamuzi nani agombee lakin swala la nani tumpe urais litafanywa na watanzania wapiga kura ambao wengi si wanachama wa chama chochote
 
Mkuu hujasikia kuna mama anapitapita huku na huku kusafisha njia? Zitto ana kundi la vijana, Dr. Slaa ana kundi la wakereketwa na Freeman Aikael Mbowe ana kundi la wahafidhima ndani ya chama! Unataka udadavuzi zaidi? Mkuu siasa ni kujipanga na siasa ni makundi hakuna siri yoyote na asikudanganye mtu kwamba kuna mwanasiasa ambaye anataka uongozi lakini hana kundi hasa akiwa anataka uongozi huo kupitia jumuiya fulani kama chama cha siasa.

Kwa sasa CDM hakuna mgombea Urais kwa hiyo nafasi ipo kwa yeyote atakayemzidi mwenzake kwenye uamuzi ndani ya chama. Hivyo basi watu wanajenga ngome zao. Ingekuwa hakuna shida basi ingekuwa wazi kwamba Dr. anapewa nafasi nyingine ya kujaribu lakini kwa kuwa si hivyo basi uamuzi wa wanachama au wazee (kumbuka uenyekiti na Zitto) utachukua nafsi.

Mkuu kwenye thread za Tuntemeke hukosekani......Zitto ana kundi la vijana gani? Wa CCM? Unaonaje kura ya maoni hapa JF? Siyo vijana wanapiga hizi kura? Achana na cheap politics mkuu....
 
Back
Top Bottom