Mkakati huu wa CCM pia Utashindwa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Kakobe: Upole wa JK hatari

• Asema viongozi wa dini ndio chanzo cha ufisadi

na Sophia Maghembe na Anitha Mkude

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amesema ameshtushwa na ukimya wa Rais Jakaya Kikwete kushindwa kukemea nyaraka zinazotolewa na madhehebu ya dini, hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama haitadhibitiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema tamko la Rais Kikwete lina uzito kuliko kiongozi yeyote nchini.

Alimtaka Rais Kikwete asikae kimya, kwani kufanya hivyo kutaonekana kama ni kutaka kumfurahisha kila mtu.

Alisema kama hali hiyo ikiendelea, inaweza kuligawa taifa ambalo limekuwa na misingi ya amani, umoja na utulivu tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.
“Rais Kikwete anapaswa kutoa tamko juu ya viongozi wa dini, ambao sasa wanatoa nyaraka mbalimbali… tunaamini kauli yake itakuwa nzito kuliko kiongozi yeyote,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema Rais Kikwete ni mpole, lakini anapaswa kuonyesha ujasiri wake ili taifa lisipoteze amani iliyojengeka muda mrefu isitoweke.

Akionekana dhahiri kutoridhishwa na nyaraka hizo za kidini, alisema umefika wakati uhuru wa kutoa maoni utumiwe kwa mipaka, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa maoni yanayotolewa hayasababishi kwa namna yoyote ile taifa kugawanyika.

Alisema moja ya jukumu kubwa la viongozi wa dini, ni kuilinda serikali kwa manufaa ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya dini fulani.

“Mtu kama anataka kutoa maoni yake atoe kama yeye na si kushirikisha dhehebu zima, na aangalie kitu gani anachozungumza si kama walivyofanya Wakatoliki na Waislamu kwa kusema kuwa ‘huu ni waraka wa Wakirsto’ na ‘huu ni muongozo wa Waislamu’,” alisema Askofu Kakobe.

Sababu kubwa ya viongozi wa madhehebu ya dini kutoa waraka na mwongozo, ni kuwataka wafuasi wa dini hizo na Watanzania kwa ujumla kuchagua viongozi wanaofaa.

Alisema viongozi wa dini hawatakiwi kutoa waraka unaohusu siasa na kuwahimiza waumini wao kuchagua viongozi wa dini zao kwani katika uchaguzi mkuu wa mwakani watatakiwa kuchagua viongozi wa serikali na wala si wa dini.

“Kiongozi akienda kuomba kura, haendi kama muumini wa dhehebu fulani, bali anaenda kama mfuasi wa chama fulani. Sijawahi kusikia mbunge wa dini fulani, ila ni mbunge wa Watanzania wote. Kinachotuunganisha ni Utanzania si dini wala ukabila,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema nyaraka zilizotolewa na Wakristu na Waislamu, zimejaa maneno ya kichochezi ambayo yanatumika kama miongozo kwa waumini wa dini hizo na Watanzania kwa ujumla.

“Waislamu walipozindua waraka wao, walisema; ‘Wakatoliki wamemwaga ugali na sisi tunamwaga mboga. Kama Wakatoliki wangezingatia ushauri huenda tusingefika huku sisi Waislamu’. Kauli hizi ni za hatari, zinaweza kuleta vita,” alisema Kakobe.

Kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, Askofu Kakobe alisema hali hii inaonyesha mpasuko kwani kila dhehebu linataka mfuasi achague kiongozi kutoka kwenye dini husika.

Akitoa mfano wa maneno yanayoashiria mpasuko katika waraka wa Kanisa Katoliki, Kakobe alinukuu kifungu kinachosema; “wagombea wanavyotawaliwa na dini yao ni muhimu kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa kwa jumuia za kanisa ili tunu za Kikirsto zionekane katika sera na uongozi.”

Katika hatua nyingine, Kakobe alikemea kauli iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Antony Mayalla, kwamba wanasiasa hawana haki ya kuwafundisha viongozi wa dini kama walivyofanya mara baada ya kanisa hilo kutoa waraka wake.

Alisema, Pengo alionyesha jeuri na utovu mkubwa wa nidhamu kwa kiongozi wa nchi, kwa kutoa kauli hiyo mbele ya Rais Jakaya Kikwete.

“Nikemee vikali tamko la kiongozi mmoja wa dini aliyesema ‘wanasiasa wasitufundishe’. Kauli ile aliitoa mbele ya rais, ule ulikuwa ni utovu wa nidhamu. Ilionyesha jinsi alivyo jeuri na asivyotaka kushaurika. Sisi kama viongozi wa dini, tunapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu,” alisema Kakobe huku akiepuka kutaja jina la Pengo ingawa baadaye alijisahau na kumtaja.

Alisema kawaida waraka hutolewa na viongozi wa vyama vya siasa wakati wa kampeni kwa ajili ya kujinadi mbele ya wananchi.

“Dini inapotoa waraka, inamaanisha inataka kushika madaraka kama vyama vya siasa… wote tunaamini kwamba dini inafanya kazi kama ilivyosajiliwa,” alisema Askofu Kakobe.

“Unajua kama DECI ilisajiliwa na kufanya shughuli zake, lakini ilivyogundulika kwenda kinyume cha sheria, ilifungiwa na kushuhudia inafikishwa mahakamani. Hivyo dini hizi zinapaswa kufunguliwa mashitaka kwa kwenda kunyume na usajili,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema anawashangaa viongozi wa dini na watu wanaoshabikia waraka huo wa Kanisa Katoliki, kwamba unapinga viongozi mafisadi wasichaguliwe, ilhali chanzo kikuu cha kuwepo kwa mafisadi ni viongozi wa dini kushindwa kuwajibika na kuwaelimisha waumini wao hadi wakajiingiza kwenye ufisadi.

“Mafisadi wana dini na wamelelewa katika dini hizi hizi, sasa iweje wao wawasemee mafisadi? Ina maana wamekuwa wazembe katika kukemea na kujenga maadili. Kwa hiyo wao ndio wanaotengeneza mafisadi,” alisema Askofu Kakobe. Aliwataka wananchi kutoshabikia nyaraka zinazotolewa na viongozi wa dini na waziogope kama ukoma kwani vita ikitokea, hakuna fidia watakayopata wananchi kama walivyopata wahanga wa matukio ya milipuko ya mabomu Mbagala. Alishauri viongozi wa madhehebu ya dini, wanasiasa na viongozi wa kiserikali wakutane na kujadili mustakabali wa umoja na amani ya taifa, ikiwa ni pamoja na athari za dini au dhehebu kutoa waraka unaowaandaa wananchi kwa ajili ya chaguzi za kisiasa.
 
Jamani hivi Kakobe anastahili kusema haya ? Ama toka awe mzee wa CCM ndiyo anataka kudhani anajua vyema zaidi ya wengine ?
 
Kakobe amesahau alitabiri Mrema angekuwa Rais baada ya kuwa anasali kwenye kanisa lake, na hayo hayakuwa hivyo. Kwangu mimi naona hana jipya. Anatafuta namna ya kutoka na kujipatia umaarufu. Ntawashangaa CCM wakiindandia meli ambayo kapteni ni Kakobe...sijui wapi itaishia ila naona mwisho wa mashaka
 
Nadhani ameshaona mahali anapoweza kuzoa umaarufu. Anajua kabisa kuwa atapongezwa na watawala kwa kuokoa jahazi. Ila hajui kuwa anaanza kukaribisha mafisadi kanisani kwake na hivyo kumuondoa kwenye njia. Labda kama ameshapigia mahesabu ya namna ya kuwakabili wakimfuata. Maana nae ni mtaalamu wa kunusa pesa.
 
Full Gospel Bible Fellowship ni sawa na CCM tu kwa sababu wanategemea ujinga wa waumini wao ili kuendelea kujiimarisha.
 
Tunaweza kusema Kakobe amemlipuwa Pengo na sasa si Pengo tena ni kibogoyo ,apo juu wacheni Jazba mlokole amesema kweli kabisa ,mpeni haki yake.na waacheni ushabiki ,hivi mtapungua kitu gani kama mkikubali kuwa aliyoyasema yana ukweli mtupu.
 
Jamani hivi Kakobe anastahili kusema haya ? Ama toka awe mzee wa CCM ndiyo anataka kudhani anajua vyema zaidi ya wengine ?

- Ndugu yangu Lunyungu, haya niliyasema siku nyingi kuwepo kwa power vacuum kwenye uongozi wa taifa letu unaruhusu kila mtu ku-act as a policy maker, au atleast mshauri wa taifa, usishangae yanakuja mengi sana ya ajabu mpaka wabongo tutakapoamka na kuchagua viongozi wanaofaaa.

Respect.

FMEs!
 
- Ndugu yangu Lunyungu, haya niliyasema siku nyingi kuwepo kwa power vacuum kwenye uongozi wa taifa letu unaruhusu kila mtu ku-act as a policy maker, au atleast mshauri wa taifa, usishangae yanakuja mengi sana ya ajabu mpaka wabongo tutakapoamka na kuchagua viongozi wanaofaaa.

Respect.

FMEs!


Mwingira na Upako , Kakobe mzee wa CCM sote tulimuona pale mbele kabisa leo anajifanya anaongelea nafasi gani ? Kesha wafanya watu wengin kuwa masikini wakubwa .Mawazo yake ni sawa na ya wale wanao pingana na Kanisa kwa ajili ya waraka ila hawaoni ubaya wa Mafisadi .Kakobe nadhani hajui kwamba wale jamaa walikaa wakatulia na shule iko pale hawajasema lolote la udini wala nini .Angoje wanyolewe huko Kanisa linaendelea kupambana na nakala zinatakiwa kwa nguvu .
 
Lakini jamani sii viongozi waliopitisha waraka wa kanisa walishauri dini nyingine nazo ziandike waraka wao?..sasa imekuwaje tena wanaanza kutofautiana!. Huko kwa Waislaam nako vurugu tupu Bakwata haikubaliani na waraka yaani vichekesho ktk nchi ya Wagagagigikoko..
Ngoja nijikumbushe zile nyimbo za halaiki wakati wa Nyerere - KUPE kupe - kata miirija!
 
CCM inatakiwa ijibu mapigo ya waraka moja kwa moja bila ya kuwatumia wapuuzi kama hawa .Will not help anything .Wababaishaji kama akina Mwingira na Kakobe wanatumika hovyo wao wana own makanisa nk .Mkakati huu ni wa kijinga for sure .CCM wajifunze walimtuja Kingunge kaleta balaa zaidi .

Hivi kweli hadhi ya Kakobe na Pengo ni sawa ? Kwa maneno ya Kakobe anategemea akisema kwamba serikali ichukue ifanyeje ? Imkamate Pengo kwa kusema aliyo yasema yasema ? Kweli the man an ashort brain sana .NO wonder anawavua watu chain kanisani .
 
I dont see anything new from this man of mazingaombwe, they call him kakobe.Waache wafu wazike wafu wenzao kama ambavyo kakobe anafanya,tunasubiri atabiri tena uongo wake kama alivofanya mwaka 1995.
 
Kakobe ni mganga wa kienyeji kama akina Prof maji marefu mwenue uaskofu wa kujipa na mtafuta chapaa akama wakikuyu wenzake walivyo .Analia lia NGO yake isifungwe .
 
Back
Top Bottom