Mjukuu wa Museveni,apandishwa cheo jeshini

Mjukuu wa Museveni,apandishwa cheo jeshini

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,488
Reaction score
5,981
Ruhamya Kainerugaba, mjukuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amepandishwa cheo na kuwa Luteni wa Pili katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), katika hafla iliyofanyika Chuo cha Kijeshi cha Kabamba, wilayani Mubende.

Ruhamya alikamilisha mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Kijeshi cha Sandhurst nchini Uingereza, Agosti 2026, baada ya mafunzo ya wiki 44, na kutunukiwa rasmi cheo hicho Agosti 7, 2026.

Safari yake jeshini ilianza Juni 2025 alipojiunga na UPDF kama mwanajeshi wa kawaida, kabla ya kuhudumu kwa muda mfupi katika kikosi maalumu cha ulinzi na kwenda Uingereza kwa mafunzo ya maafisa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Museveni aliwataka maafisa wapya kudumisha nidhamu na kulitumikia taifa kwa heshima, huku baba yake Ruhamya, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, akimpongeza kwa kupata cheo hicho.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
 
Back
Top Bottom