- Source #1
- View Source #1
Kupitia mitandao ya kijamii,kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa Mogaj Kibabage, anayedaiwa kuwa kaka wa mchezaji wa Simba SC, Nickson Kibabage, ambaye anahudumu katika Jeshi la Marekani amepandishwa cheo kutoka Koplo (Corporal) hadi Sajenti (Sergeant) baada ya kufaulu kozi maalumu ya kijeshi iliyomwezesha kupata cheo hicho.
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii,kumekuwepo na chapisho linalodai kuwa Mogaj Kibabage, anayedaiwa kuwa kaka wa mchezaji wa Simba SC, Nickson Kibabage, ambaye anahudumu katika Jeshi la Marekani amepandishwa cheo kutoka Koplo (Corporal) hadi Sajenti (Sergeant) baada ya kufaulu kozi maalumu ya kijeshi iliyomwezesha kupata cheo hicho.
Ufuatiliji mtandao umebanisha kuwa jina Harafat Mogaji umeonesha kuwa mtu huyo ni mmoja wa Wanigeria wawili waliokuwa wakihudumu katika Jeshi la Anga la Marekani (US Air Force), ambao wamehukumiwa kifungo cha gerezani kutokana na kuhusika katika mtandao wa kimataifa wa ulaghai wa mtandaoni.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chombo cha habari cha kimataifa cha DW English, Chijioke Timothy Odimegwu alihukumiwa kifungo cha miezi 111 katika gereza la shirikisho, huku Harafat Mogaji akihukumiwa kifungo cha miezi 78.
Mtandao huo ulifanikiwa kuchukua takribani dola milioni 1.68 za Marekani kutoka kwa mwathirika mmoja katika jimbo la Iowa, Marekani, na zaidi ya dola 720,000 kutoka kwa mwathirika mwingine katika jimbo la Ohio.
Aidha, Odimegwu aliamriwa kulipa takribani dola 366,600 kama fidia, huku Mogaji akiamriwa kulipa takribani dola 995,700.
Hivyo kwa ufuatiliji huo unatamatisha kuwa taarifa zinazodai kuwa mogaj ni ndugu yake mchazeji wa simba Nickoson kibabage zinapotosha uhalisia wa tukio lenyewe.