Mjue Vladmir llyich Lenin - Sehemu ya 01

Mjue Vladmir llyich Lenin - Sehemu ya 01

Maisha ya awali ya V.I Lenin...................
View attachment 1209039

Maisha ya utotoni: 1870 - 1887

Vladmir llyich lenin kama tunavomjua wengi amezaliwa tarehe 22/04/1870 , katika mji wa Ulyanovisk,Russia. Baba yake na vladmir aliyejulikana kama Llya Nikolayevich Ulyanov, kutoka kwenye familia ya wakulima wadogowadogo na wafugaji pia, ingawaje kabila lake halikujulikana vizuri kwani kuna watu waliomdhania kama mrussia, mchuvash, mmordvin au mkalymik.

Ukiachana na maisha yake ya nyuma llyich alikulia kwenye maisha ya watu wa kawaida(middle-class), na alifanikiwa kusoma masomo ya fizikia(physics) pamoja na hesabu(mathematics) katika chuo kikuu cha Kazan Imperial kablahajaanza kufundisha Penza Institute for Nobility.

Llyich alimuoa mama yake Vladmir Maria Alexandrovina Blank katikati ya mwaka 1863, aliyekuwa anatokea kwenye familia ya kitajiri mama yake akiwa ni mjerumani na baba yake akiwa ni mrussia. Baada ya kuoana llyich alipata kazi Nizhny Novgorod akiwa kama Director wa shule zote za praimary katika mji wa Simbirsk.

Lenin alizaliwa baadae katika mji huo wa Simbirsk tarehe 22/04/1870 na kubatizwa siku 6 baadae, akiwa kama mtoto aliitwa "voladya" . Lenin alizaliwa akiwa ni mtoto wa 3 akiwafata Anna(aliyezaliwa 1864) na Alexander(aliyezaliwa 1866), akifatiwa na wadogo zake watatu; Olga(aliyezaliwa 1871), Dmitry(aliyezaliwa 1874) na Maria(aliyezaliwa 1878). kati ya ndugu zake wote lenin alipenda kukaa na dada yake Olga ambaye walipenda kuongozana kila mahali, lenin alipendelea kucheza mpira wa miguu na kucheza mchezo wa chess.

Mwaka 1886, wakati lenin akiwa na umri wa miaka 15 baba yake alifariki kwa ugonjwa wa ubongo(Brain haemorrhage). Katika kipindi hicho kaka yake mkubwa Alexander alikuwa anasomea chuo kikuu cha St.Petersburg huku akiziusisha na mambo ya kisiasa huku akikipinga chama cha siasa cha mapinduzi kilichoongozwa na Tsar Alexander III.

Alexander alijiunga na chama kingine cha siasa kilichoandaa mipango ya kumuua Tsar Alexander III kwa bomu, ila kabla ya kutekeleza azima yao walikamatwa na Alexander akahukumiwa kunyongwa. Licha ya mawazo mengi kuhusu vifo vya Baba na Kaka, Lenin aliendelea kusoma na akamaliza akiwa na daraja la juu(high-class) na akzawadiwa medali ya dhahabu, na hapo ndipo alipoamua kujiunga na chuo kikuu cha Kazan kwa ajili ya kusoma sheria.


Maisha ya chuoni na harakati : 1887 - 1893

A
ugust 1887, Lenin aliingia chuoni Kazan na kujiunga na kikundi cha watu wa jamii moja kilichojiita zemlyachestvo na akachaguliwa kuwa mwakilishi wa kikundi hicho kwenye baraza kuu la chuo, Disemba 1887, Lenin aliongoza maandamano dhidi ya serikali kufungia vikundi vya wanfunzi katika chuo alichosoma. Lenin alikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuongoza maandamano hayo na kusimamishwa masomo huku akifukuzwa katika mji huo wa Kazan.

Baada ya mama yake Lenin kupata taarifa alijitahidi kuiomba serikali ili Lenin arudishwe mjini Kazan bila hata kurudi chuo. Baada ya kurudi Lenin alijiunga na kikundi kingine cha mapinduzi kilichojulikana kama Nikolai Fedoseev's revolutionary circle , hapo ndipo alifanikiwa kusoma kitabu cha Karl Max kilichoandikwa mwaka 1867, na kuchochea hali ya kisiasa iliyokuwa ndani yake. Mama yake Lenin alitafuta ardhi katika kijiji cha Alakaevka(Samara oblast), akiamini kuwa mwanaye atakuja kulima lakini ilikuwa sivyo kwani baadae alikuja kuuza ardhi hiyo kwani Lenin alikataa.



Uzi unaendelea..................
usisahau kunitag mkuu
 
Back
Top Bottom