Asalam alaikum,
Habari za masiku ndugu zanguni.
Naanza kwa jina la Mwenyezimungu muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake! mwenye kujua ya dhahiri na ya siri (yaliyo mioyoni mwetu) na rehma zimfikie kipenzi chetu Muhammad SAW.
Je Ponda ni nani?
Mimi awali nilikuwa najua Ponda na Kundecha kuwa ni wanaharakati wenye kupigania haki za waislamu lakini imeniuma sana kujua undani wa hawa watu! Mimi ni mwislamu na siku zote nilikuwa naona jamaa wanafanya kazi kwa maslahi ya umma wa kiislamu lakini kumbe kuna mambo nyuma ya pazia.
Manji Vs Ponda & Co
Kuna uwanja ambao ulikuwa mali ya East African Muslim Welfare Society na kurithishwa kwa bakwata sehemu ya eneo lile ambalo lipo maeneo ya chang'ombe bakwatwa ililiuza/gawa kwa jumuia ya shia ismailia ambao na wao walikuwa wana hisa kwenye East African Muslim Welfare Society na Ismailia wakamuuzia Manji.
Mkiangalia hapo juu hakuna mgogoro wowote wa kati ya Manji na Waislamu ila kina Ponda inavyoonyesha walikodiwa ili kuweka mazingira ya kumfrastrate manji apauze kwa bei poa.
Leo tumuulize Ponda alilipwa kiasi gani kuhakikisha Manji hapamiliki pale? na kwanini walinyamaza baada ya manji kukitema kiwanja kile? Kwa akili ndogo ya kuzaliwa utajua kuwa Ponda & Co walitumika kufanya umafia ili kiwanja kipatikane kirahisi.
Kukamatwa kwa Ponda.
Kuna eneo ambalo limebakia kwenye kiwanja cha East African Muslim Welfare Society ambacho kinasemekana kuuzwa miaka minne au mitano iliyopita Ponda na group lake walivamia siku ya Ijumaa na kujenga msikiti wa muda na kuweka mabaunsa na baadhi ya waumini kwa madai kuwa kiwanja ni cha waislamu! yale yale yaliyomkuta Manji! na habari za chini ya kapeti ni kuwa Ponda na watu wake wamelipwa 15 Mil kumobilize uvamizi ule!
Huyu jamaa anatumiwa kwa kuwa anaushawishi kwenye jamii yetu ya waislam lakini leo hii kama Mungu atadhihirisha kuwa anayoyafanya hayafanyi kwa ajili ya waislamu ila kwa maslahi ya mabwana zake basi nadhani shingo yake itakuwa halali ya Waislamu. Kwani wale waliokamatwa jana usiku pale Chang'ombe wengi wao hakupata mgao wa tajiri anaepataka pale zaidi ya chai ya asubuhi chakula cha mchana na maji ya chupa!
Najua kuna wanahabari humu jamvini mkimuhoji jaribuni kumhoji issue ya manji iliishaje? je walilipwa nini baada ya kufanikisha zoezi lile?
Narudia waislamu ifike muda tuchukue muda wa kufikiria tusikubali kuburuzwa na viongozi wanaoangalia matumbo yao na kusababisha matatizo kwa waislamu wasiojua set up ya matukio husika.
Ahsanteni sana na ni matumaini yangu mmepata kitu juu ya mada hii.
muongo na mnafiki mkubwa wewe!!!