Mjue Mtemi Mkwawa wa uhehe na Wahehe

lole Gwagisa, Yericko Nyerere,

..napenda kujua Mkwawa alikuwa akipata wapi silaha za kivita?

..je, kuna ukweli wowote kuhusu tuhuma kwamba alikuwa akijihusisha na biashara wa WATUMWA??

..ugomvi wa Mkwawa na Wajerumani ulikuwa kuhusu nini haswa?
 
Last edited by a moderator:
lole Gwagisa, Yericko Nyerere,

..napenda kujua Mkwawa alikuwa akipata wapi silaha za kivita?

..je, kuna ukweli wowote kuhusu tuhuma kwamba alikuwa akijihusisha na biashara wa WATUMWA??

..ugomvi wa Mkwawa na Wajerumani ulikuwa kuhusu nini haswa?

Swali la nyongeza. Je Mkwawa Mwinyigumba alikuwa mhehe 100%?
 
lole Gwagisa, Yericko Nyerere,

..napenda kujua Mkwawa alikuwa akipata wapi silaha za kivita?

..je, kuna ukweli wowote kuhusu tuhuma kwamba alikuwa akijihusisha na biashara wa WATUMWA??

..ugomvi wa Mkwawa na Wajerumani ulikuwa kuhusu nini haswa?
mkwawa silaha za kivita alikuwa akitengeneza yeye mwenyewe baada ya kuuziwa bunduki ya kwanza na waarabu ndipo akadokolezea teknolojia hiyo na akafanikiwa kutengeneza ya kwake, ikumbukwe pia huyu jamaa alikuwa mwizi wa technolojia mpya ya mapambano kila alipoiona, ndo maana alikuwa akiwashinda sana maadui zake kama wangoni ambao aliiba mbinu za mapambano kwao na akatumia kuwapigia wao. ukienda kalenga utaiona hiyo buduki inyosemekana aliitengeneza yeye mwenyewe na sehemu ambayo lilikuwa ghala la silaha lililosheni baluti, lakini pia ikumbukwe kuwa alikuwa akiteka na kuwanyang'anya silaha maadui, mfano kwa mjerumani aliteka bunduki mi tatu na kumi pamoja na mizinga mitatu.
ugomvi kati ya mkwawa na wajerumani ulianzia pale mkwawa aliopowatoza wajerumani kodi kwa kupita kwenye himaya yake, lakini wajerumani walikataa ndipo mkwawa akaamua kufunga ile trade root ya kwenda kilwa ndipo uhasama ulipoaanza na kuzaa vita ya kwanza iliyopiganiwa lugalo ambayo alishinda kisha wajerumani wakajipanga tena kwa kushirikiana na makabila hasimu ya wahehe ndipo walipomshinda japo kwa tabu.
hakuna ushahidi wa wazi ambao unaonyesha mkwawa kuwa alijihusisha na biashara ya utumwa maana yeye mwenyewe alikuwa na tabia ya kuwakamata mateka na kuwatumikisha mwenyewe bila kuwauza na hili linathibitishwa na koo mbalimbali zinazopatikana kalenga kwenye ngome yake ambazo nyingi sio za kihehe bali ni za makabila mbalimbali na pia kuna maeneo kama ikonongo huko walikuwa wakiwekwa wageni wale wasio wahehe na mkwawa kwa ajiri ya kulima.

pa kuna swali kauliza zakimi kama mkwawa alikuwa mhehe 100% ukweli ni kwamba mkwawa ni mjuu wa aliyekuwa mfalme wa wahehe. baba ake mkwawa inasemekana alitokea huko ethiopia na ni mhabeshi ambaye alikuwa muwindaji sasa alipofika lilinga ndipo akakaribishwa na mfalme akaa kwake kwa siku kazaa na akampa binti wa huyo mfalme mimba kisiri baada ya kuona hivyo akakimbia na huyo binti ndipo alipomzaa mkwavinyika yaani mtwaa nchi ambaye anafahamika kama mkwawa.
 
Mkwawa au kwa jina defu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 Julai 1898[SUP]1[/SUP]) alikuwa chifu na kiongozi mkuu wa Wahehe katika Tanzania wakati wa upanuzi wa ukoloni wa Ujerumani wakati wa mwisho wa karne ya 19. Mkwawa aliongoza upinzani wa Wahehe dhidi ya Wajerumani.

Upanuzi wa Wahehe


Jina la Mkwawa ni kifupi cha Mukwava ambalo ni kifupi cha Mukwavinyika iliyokuwa jina lake la heshima likimaanisha “kiongozi aliyetwaa nchi nyingi”. Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 mahali palipoitwa Luhotakaribu na Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879.
Babake Munyingumba aliwahi kuunganisha temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwa dola moja. Aliiga mfumo wa kijeshi wa Wasangu waliowahi kuwa kabila lenye nguvu waliowahi kujifunza mfumo huu kutoka Wangoni na impi za Shaka Zulu. Hadi miaka ya 1870 eneo la Wahehe ilipanushwa mbali kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo.
Baada ya kifo cha chifu mzee watoto walishindana kati yao juu ya urithi wake huku mpwa wa Mkwa bwana Mwambambe Mwalunyungu aliyekuwa msaidizi na wa karibu wa Mnyigumba akikalia utawala huo kwa mabavu,
Msuguano huo ulimfanya Mkwawa kuitoroka Iringa na kwenda uhamishoni Morogoro ambako alikaa kwa takribani miaka miwili na kuhamia Mpwapwa Dodoma. Hali ya utawala wa Mwambambe Mwalunyungu haikuwavutia wazee wa kihehe ambapo waliandaa uasisi na wakatuma mmoja wa askari aende Mpwapwa akanuite Mkwawa arudi kuchukua himaya.
Jambo hilo lilimfanya mkwawa aingiwe na hofu kuwa angeuawa na Mwambambe, lakini wazee walimhakikishia kuwa watamuunga mkono, kweli Mkwawa alirudi na vita ikaanza ambapo katika mapigano askari wa Mwambambe walikuwa wakiasi kadiri mapigano yalivyosonga, na baadae Mwambambe akakimbia nakujificha kwenye kichaka kiitwacho (lugegele)
Ikumbukwe kuwa Mwambambe alikuwa na uwezo wa kudaka mkuki inayomlenga zaidi ya kumi, hivyo kila askari wakijaribu kumcho na mkuki alikuwa akidaka na kuwaua askari hao na mkuki huohuo, mwisho askari mmoja aliyeitwa Mwakilufi, aliushika mkuki nakujaribu kama anajichoma vile kisha akaufyatua kwa spidi ya hali ya juu na ukampata kifuani na kutokeza mgongoni Mwambmabe,
Hakika ilikuwa ni vita ya kimizimu, baada ya hapo Mwambe aliongea maneno haya “Be mnyakilambo, ndakulile kiki pe ukumbulaga de?” (kijana nilikulia nini unaponiua hivi?) Yule askari Mwakilufu alijibu, “Walye nda unoge be” (ulikula hivyohivyo bwana)
B
aada ya kumuua Mwambambe walimla nyama pale pale tena mbichi, Mkwawa alimwambia yule askari atambe kidogo kuonyesha ujasiri wake, hapo yule askali akaanza, vava mwakilufi,vasengidunda,vamaseto,vamwalumato, vamwaluhala, vamwamyinga, vasemdapo, vamwamgimwa, vamwachalamila, vamwachavala, vamwamalangalila, nk
Sasa Mkwawa akawa ameshinda na akawa kiongozi mpya wa Wahehe. Aliendelea kupanusha utawala wake. Hadi mwisho wa miaka ya 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika. Misafara hii iliyobeba bidhaa za nje kama kitambaa, visu na silaha kutoka pwani ikirudi na watumwa na pembe za ndovu ilipaswa kumlipia hongo ikanunua pia wafungwa wa vita zake. Hapo athiri na uwezo wake wa kulipa jeshi kubwa ikapanuka.
Mkwawa na upanuzi wa Wajerumani

Tangu miaka ya 1885 Wajerumani walianza kuunda koloni yao katika Tanzania bara. Mwaka 1888/89 utawala wao ulitikisihwa na vita ya Abushiri lakini baada ya kushinda upinzani wa Waafrika wa pwani Wajerumani walilenga kuimarisha utawala wao juu ya sehemu za bara.
Mkwawa aliwahi kusikia mapema habari za Wajerumani akajaribu kuwasiliana nao lakini bila kuelewana. Aliamua kujenga boma imara lenye kuta za mawe kwenye makao makuu yake huko Kalenga karibu na Iringa. Katika mwezi wa Februari 1891 alituma wajumbe kwa kambi la Wajerumani huko Mpwawa wakapokelewa na gavana Mjerumani. Wakati huohuo Mkwawa aliendelea kutuma askari zake hadi Usagara iliyotazamiwa na Wajerumani kama eneo lao. [SUP][1][/SUP] Katika kipindi hiki gavana mpya Julius von Soden alifika Dar es Salaam. Hakuwa na mamlaka juu ya mkuu mpya wa jeshi Emil von Zelewski aliyepokea amri zake kutoka Berlin moja kwa moja. Baada ya kusikia habari za mashambulio ya Mkwawa katika Usangara aliomba na kupata kibali cha “kuwaadhibu Wahehe”.
Mapigano ya Lugalo

Katika mwezi wa Julai 1891 von Zelewski aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 13 na askari Waafrika hasa kutoka Sudan 320, pamoja na wapagaji 113. Walikuwa na bunduki za kisasa, bunduki za mtombo na mizinga midogo. Zelewski aliwadharau Wahehe kama washenzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu. Kwa hiyo hakuuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali. Njiani aliangamiza vijiji alivyokuta na katika mwezi wa Agosti alipoona Wahehe 3 waliomkaribia aliagiza kuwaua bila kuongea nao. Kumbe walikuwa mabalozi wa Mkwawa aliyetaka kujadiliana na Wajerumani.
Tarehe 17 Agosti 1891 Zelewski na jeshi lake walipita kwenye manyasi marefu karibu na Lugalo. Mkwawa alikuwa alimsububiri na Wahehe 3,000 walionyamaza hadi Wajerumani waliotembea kwa umbo la safu ndefu walikuwa karibu kabisa wakawashambulia. Wajerumani walikosa muda kuandaa silaha zao wakashtushwa kabisa. Sehemu kubwa ya askari waliuawa katika muda wa dakika chache pamoja na jemadari von Zelewski. Sehemu ya kombania ya nyuma ilirudi nyuma na kusimama kwenye kilimo kidogo walipoweza kutumia bunduki la mtombo wakajitetea na kuua Wahehe wengi. Sehemu hii ilijumlisha maafisa 2 na maafande 2 Wajerumani waliweza kukimbia na kujiokoa pamoja na askari 62 na wapagaji 74.
Kipindi cha vita dogo

Baada ya mapigano Mkwawa alihesabu wafu wake waliokuwa wengi. Alikataza bada za kilio kwa sababu alitaka kuficha idadi ya askari waliokufa. Akaelewa sasa ya kwamba silaha za Wazungu zilikuwa hatari alituma tena mabalozi kwa gavana von Soden walioeleza ya kwamba Wahehe walikuwa walijitetea tu dhidi ya shambulio walitaka amani. Lakini madai ya Wajerumani yalikuwa magumu eti kuwaruhusu wafanyabiashara kupita bila matata na kutoshambulia majirani tena.
Mkwawa hakuwa tayari kuahidi yote akachelewesha mikutano. Wakati huu kamanda mpya Mjerumani Tom von Prince alijenga boma jipya la Wajerumani katika Uhehe na Mkwawa alijibu kwa kusambulia vikosi vidogo vya jeshi la kikoloni. Gavana Soden alidai kutoendelea na mapigano. [SUP][2][/SUP]. 1893 gavana von Soden aliondoka Afrika na gavana mpya von Schele alitaka kulipiza kisasi akaamuru mashambulio dhidi ya Mkwawa.
Anguko la Kalenga

Mwezi wa Oktoba 1894 von Schele aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 33 na askari Waafrika pamoja na wagajai zaidi ya 1000 kuelekea Kalenga. Walikuwa na mizinga 4 na bunduki bombomu. Walipofika mbele ya Kalenga Wahehe walijisikia salama kutokana na kuta imara lakini Wajerumani walijipanga kilomita kadhaa nje ya mji wakaanza kufyatulia mizinga yao na kuua watu ndani ya mji. Wakati wa giza kwenye asubuhi wa 30 Oktoba 1894 askari wa jeshi la Schutztruppe walipanda ukuta katika sehemu ulipodhoofishwa tayari na kuingia mjini. Hadi jioni walikuwa waliteka mji wote. Gombora na mikuki ya Wahehe hazikuweza kushindana na bombomu za Wajerumani. Mkwawa mwenyewe aliamua kukimbia pamoja na 2000 – 3000 askari lakini kabla ya kukimbia alimwua mganga mzee aliyewahi kutabiri ya kwamba atawashinda Wajerumani waliokuja. Gavana von Schele aliandika taarifa kwa serikali ya Ujerumani “tulizika maadui 250, wengine walichomwa katika nyumba zao, wanawake na watoto 1500 kutekwa nyara” [SUP][3][/SUP].
Mkwawa alijificha msituni pamoja na askari zake akasubiri. Gavana von Schele alishindwa kuendelea na mashambulio wa sababu gharama za vita zilishinda makaisio yake na wabunge wa upinzani katika Reichstag huko Berlin walipinga vita ya kikoloni; walikataa kuongeza makisio na kiongozi wa wasoshalisti August Bebel aliita mtindo wa kuchoma mji na kuteka nyara watoto na wanawake “ushenzi mkuu”.
Amani fupi

Baada ya kuondoka kwa Wajerumani Mkwawa aliweza kurudi na kujenga tena nyumba mahali pa Kalenga. Katika Septemba 1895 Mkwawa alikuwa tayari kujadiliana na Wajerumani na tar 12 Oktoba walipatana amani. Wajerumani walimkubali Mkwawa kama chifu wa Wahehe , Wahehe waliahidi kukabidhi gobori zote, kuonyesha bendera ya Kijerumani na kuwaruhusu wafanyabiashara na wasafiri kupita Uhehe. Mkwawa alimwagiza mjomba wake kutia sahihi akakataa mwenyewe akisema hii ingemwua. Hata hivyo miezi kadhaa baadaye alitafuta msaada wa Wajerumani kwa shambulio dhidi ya Wabena.
Afisa mmoja Mjerumani aliyefika Kalenga mpya alizuiliwa kuingia na kumwona chifu akaambiwa alipe hongo ya bundiki 5 wa kuingia katika eneo la Mkwawa. Hapo maafisa wa jeshi la Wajerumani waliolinda mpaka ambao bado walitafuta nafasi ya kulipiza kisasi kwa Lugalo waliamua chifu alivunja mkataba. Kapteni Tom von Prince alijenga boma jipya karibu na Kalenga alianza kuwasiliana na machifu wadogo wa Wahehe. Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani lakini Wabena na makabila mengine walikumbuka vita na mashambulio ya awali kutoka Uhehe walipendelea kushikamana na Wajerumani. Mkwawa aliwaua machifu wawili wahehe waliowahi kukaa na von Prince lakini aliona hawakuwa wa pekee waliosita kumtii tena. Alipata habari ya kwamba mdogo wake Mpangile alishikamana na Wajerumani. Wakati wa Septemba 1896 Wahehe waligawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliochoka vita ilikuwa tayari kuwakubali Wajerumani.[SUP][4][/SUP]. Wajerumani waligawa eneo lao. Wasangu walirudishwa katika eneo lao la awali wakarudi kutoka Usafwa katika mji mkuu wa Utengule Usangu. Mpangile alisimikwa kama kiongozi mpya wa Uhehe penyewe lakini baaa ya siku 50 alisimamishwa na kuuwa na Wajerumani waliomshtaki eti anamsaidia kakaye kisiri.
Mafichoni na kifo

Mkwawa alikuwa aliondoka sehemu za Iringa mwezi wa Agosti 1896 alipoona mgawanyiko. Alifuata mwendo wa mto Ruaha akilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliomtafuta. Disemba 1896 alihamia milima ya Uzungwa alipojificha. Kutoka hapa alitelemka mara kwa mara kwenye mabonde alipopata vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya askari vya Kijerumani.
Katika Julai 1897 kikosi kikubwa cha Wasangu pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta kambi la Mkwawa mlimani wakashambulia lakini Mkwawa aliweza kukimbia. Mwaka 1898 Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu akiongozana na watu wachache sana. Aliishi hasa kwa njia ya kuwinda. Wakati wa Julai 1898 aliongozana na wavulana 4 pekee halafu Wazungwa 2 mume na mke. Tarehe Julai 16 Wajeumani waliowahi kusikia habari zake walimkuta huyu mama Mzungwa alipotafuta chakula wakamkamata akawaambia Mkwawa alielekea kusini na alifika sehemu inaitwa Mrambarasi.. Wakamfuata na tar 18 Julai Mkwawa alimwua mume Mzungwa kwa hofu ya kusalitiwa. Aliendelea na wavulana 2 tu walioitwa Musigombo na Lifumika. Watoto waliogopa angeweza kuwaua pia. Hapo Lifumika aliamua kukimbia asubuhi ya tar 19 Julai. Lakini siku ileile alipotelemka kutoka mlimani alikutana na kikosi cha Wajerumani akakimbia lakini wakamshika wakamlazimisha kuwaambia habari za Mkwawa. Kijana alimwambia sajenti Mjerumani kuwa chifu alikaa mgonjwa mahali kwa umbali wa masaa 3.
Walimlazimisha kuwaongoza. Njiani walisikia kwa mbali sauti ya bunduki, risasi 1. Wakaendelea na baada ya masaa mawili walikuta maiti za Mkwawa na kijajana mwingine. Inaonekana waliwahi kujiua na sauti ya bunduki ilikuwa Mkwawa aliyejipigia risasi.[SUP][5][/SUP]
Fuvu la Mkwawa

Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen.
Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema. Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: “Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu … Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.”
Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.
Fuvu hii ilipelekwa Tanganyika tarehe 9 Julai 1954 na kuhifadhiwa katika jengo la makumbusho ya Mkwawa kwenye kijiji cha Kalenga
Marejeo
0. Kitabu kiitwacho Mtemi Mkwawa na wahehe. kiliandikwa na Wiliam Malangalila

  1. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 108
  2. ↑ Iliffe uk. 109-110
  3. ↑ David Pizzo, “To devour the land of Mkwawa”: Colonial violence and the German-Hehe War in East Africa, 2007, uk 173
  4. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 113 / 114
  5. ↑ John Iliffe, A modern history of Tanganyika, 1979, uk 115 /116
mkuu hapo naona fuatilia vizuri, mwambambe mwalunyungu hakuwa askari wa mnyigumba bali ndiye aliyekuwa jemedari mkuu wa mkwawa, baadaye akaja kumpindua mkwawa na mkwawa kufanikiwa kukimbilia dodoma na wala hayawahi kukimbilia morogoro na alifika dodoma huku akiwa amejipaka masizi na majivu kama mtumwa. morogoro ni sehemu ambayo dawa za kumrudisha mkwawa nyumbani zilipoenda kuchukuliwa sababu mizimu ya wahehe ilipatikana huko sehemu za lulanga. ikumbukwe kuwa huyu mwambambe ni shujaa ambaye alivunja rekodi ya kukimbia katika wanajeshi wa enzi hizi na alikuwa na nguvu za ajabu wao wanasema haijawahi tokea, hata mkwawa aliporudi walimfukuzia umbali mrefu mno mbaka alipoenda kujificha pale kichakani ambapo inasemekana walikuwa wakimpiga mikuki ila yeye aliidaka na kuirudisha ambapo aliwauwa askari wengi wa mkwawa mbaka alipochoka ndipo askari mmoja alipofanikiwa kumlenga kifuani na kumwua.
 
Yericko Nyerere

Nataka kujua wanyakyusa walitoka wapi na kwanini wanyakyusa hawana chifu wa aina ya Mkwawa katika historia ya makabila ya Tanzania? Halafu haya majina ya mwalunyungu mwambambe mbona kama ya kinyakyusa? hivi nani aliyeanza kuwepo maana naona mkwawa alikua na himaya kubwa mpaka mbeya inakuwaje hapo wanajamvi?
ni kweli himaya ya mkwawa ilikuwa ni kubwa sana maana tiyari alikuwa amefika mbeya, songea dodoma, tabora na morogoro kiasi kwamba utawala wake ungedumu mda mrefu zaidi basi nusu ya tanganyika ingekuwa ya uhehe maana wakati huo hakuna kabila lililokuwa na uwezo wa kuwadhibiti wahehe, na mkwawa inasemekana yeye alikuwa anajihami zaidi na wamasai ambao alisikia wana nguvu hivyo alianza kujiandaa kufanya vita nao.
 
mkwawa alikuwa ni zao kati ya muwindaji wa kihabeshi na binti wa mfalme wa wahehe wakati huo


Kwa hiyo unakubaliana kuwa hakuwa mhehe 100%. Na vilevile kutokana uhabeshi wake alifanana na tipu tipu na sio wahehe wengine.
 
Wakuu humu JF, this celebrated hero died 111 years ago,lest we forget his sacrifice and bravado.

Chief Mkwawa of the Hehe
This is a short history of Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855-19th July 1898)

The Tanganyikan interior in the latter half of the nineteenth century was in a state of chaotic flux. Incursions by Arab slave traders from the coast had disrupted the balance of power between clans and tribes, while the militaristic Ngoni tribe's invasion in the south had triggered several mass migrations. This uncertain climate provided ideal soil on which opportunistic leaders such as Chief Mirambo of the Nyamwezi could plant their own personal kingdoms.

Another leader who emerged triumphantly from this confusion was a Hehe chief named Mtwa Mkwawa Mwamnyika ("Conqueror of Many Lands"), better known as Chief Mkwawa. Born near Kalenga in 1855, Mkwawa's ambitious character was well suited to his time. By 1889, he had become undisputed leader of the Hehe, whom he made the region's dominant tribe by uniting – though force or diplomacy – more than one hundred clans and smaller tribes. It was not just numbers, but regimented military organization that formed the basis of Hehe power, and which gave Mkwawa the ability to stem the hitherto inexorable southward advance of the Maasai. Mkwawa also began to threaten Arab control over the lucrative slave and ivory-carrying caravan routes that passed through his territory, though declining Arab power meant that it was not against the sultans of Zanzibar that the showdown eventually came, but against the German colonial war machine.

At first, Mkwawa tried to secure treaties with the Germans, but when they refused, the Hehe turned their arms against the arrogant newcomers. On August 17, 1891, a year after the Germans had placed a garrison in Iringa, Mkwawa's troops surrounded and ambushed a German expeditionary force led by Lieutenant Emil von Zelewski in the Lugalo Hills east of Iringa, killing nearly five hundred soldiers and capturing a vast quantity of firearms and munitions. Only two German officers and fifteen men escaped.

This is one story that has not been properly retold.
Chief Mkwawa lured Zeweleskis troops that were advancing on Mkwawas villages, pillaging,torching village huts and killing resistant young warriors.

A perfect pincer movement, whereby a retreating warrior force attracted a well armed German regiment under Zeweleski.

To the surprise of the German force the warrior force as if by instinct came o a stand still and started to fight back while two flans of spear wielding warriors attacked on the main body of the German force. And it worked.

On the 17th August 1891 the German force was annihilated, ten German officers lay dead including the commanding officer Lt Emil von Zeweleski.

Mkwawas forces gave chase, about 300-400 crack warriors, and the Germans did not stop until after covering over 400km and rested at Kondoa.

Mkwawa was no fool, and anticipated German revenge – by building a thirteen-kilometre, four-metre high wall around his palace and military base at Kalenga. The Germans took their time to reorganize, and it wasn't until October 1894 that they made their move, establishing themselves on a hill overlooking Kalenga, now the site of Tosamaganga, and beginning a two-day bombardment of Kalenga (the name tosamaganga means to "throw stones"). On October 30, 1894, the Germans under Tom von Prince stormed and took Kalenga with relative ease. The extent of Mkwawa's wealth can be gauged by the fact that it took four hundred porters to carry all his ivory away. The Germans also found 30,000 pounds of gunpowder, which they used to level the town. For Mkwawa, the loss of Kalenga was a double tragedy, since his mother – who had been told that her son had been captured – committed suicide.

In fact, Mkwawa escaped into the forests west of Kalenga, from where he waged a four-year guerrilla war against the Germans. He was finally cornered in 1898, having been betrayed by informants attracted by a five-thousand-rupee reward. Rather than surrender, he shot his bodyguard, and then himself. The Germans, arriving on the scene shortly after, placed another shot into Mkwawa's head just to be sure, then severed it. The chief's headless body was buried by his family at Mlambalasi, 12km south of the road to Ruaha National Park, while his skull was sent on to Berlin and then on to the Bremen Anthropological Museum. There it remained until 1954, when it was finally returned to the Hehe – it's now the star exhibit of Kalenga's Mkwawa Memorial Museum.
Mkwawa's death marked the end of two decades of resistance to German rule across Tanganyika, and the end of the Hehe Empire, but the ensuing peace was short-lived. Seven years on, the Maji Maji Uprising erupted.

This year about 111 years ago, Mtwa Mkwawa must be remembered as a hero worth emulating.

Hiyo sehemu niliyo highlight nyekundu na kupigia mstari sahihi ni Mwamyinga
 
Kwa hiyo unakubaliana kuwa hakuwa mhehe 100%. Na vilevile kutokana uhabeshi wake alifanana na tipu tipu na sio wahehe wengine.
unachosema ni ukweli kabisa, lakini la kufanana na tipu tipu sina uhakika, ukimfuatilia sana umbo lake na tabia zake zilikuwa ni za kihehe kabisa, vyovyote itavyokuwa alikuwa na damu ya kihehe na uhehe kumbuka aliikuta ikiwa imara na yenye nguvu ye aliendeleza pale alipoishia mnyigumba ambaye alifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wahehe na kuliimarisha jeshi na kutanua hikaya ya mhehe
 
Pia naomba tuliweke wazi kuwa mkwawa hakuwa chief bali alikuwa king(mfalme), naona hili limepotoshwa kwa muda mrefu na watoto mashuleni wanafundishwa hivyo kitu ambacho ni uongo
 
unachosema ni ukweli kabisa, lakini la kufanana na tipu tipu sina uhakika, ukimfuatilia sana umbo lake na tabia zake zilikuwa ni za kihehe kabisa, vyovyote itavyokuwa alikuwa na damu ya kihehe na uhehe kumbuka aliikuta ikiwa imara na yenye nguvu ye aliendeleza pale alipoishia mnyigumba ambaye alifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wahehe na kuliimarisha jeshi na kutanua hikaya ya mhehe

Katika posti yako moja umesema kuwa Mkwawa alipata bunduki kutoka kwa waarabu na kuanza kutengeneza zake mwenyewe. Na unakanusha kuwa hakuusika na biashara ya watumwa.

Hili uweze kutengeneza bunduki ni lazima uwe na chuma. Kwa historia ninayojua mimi, wahehe hawakuwa na technologia ya chuma. Makabila yalikuwa na technologia ya kufua chuma ni wafipa, walogo, wahaya .....

Pili katika vita ya kwanza na wajerumani, jeshi la mkwawa ziliteka bunduki kama 300 kutoka kwa majeshi wa ujerumani. Bunduki hizi zilikuwa nzuri kuliko zile za waarabu. Kama wahehe walikuwa na utaalamu wa kutengeneza bunduki kwanini hawakukopi zile za mjerumani?

Tatu huwezi kutumia bunduki bila kuwa na risasi au baruti. Wakati wajerumani wanateka ngome ya Mkwawa walikuta hazina kubwa baruti na meno ya tembo. Kwa sababu uheheni hakuna baruti, je ni biashara gani alikuwa anafanya?

Nne Mwamubambe ambaye alikuwa ni shemeji ya Mkwawa ni mnyamwezi. Alichukuliwa utumwa na wahehe na kulelewa na baba yake Mkwawa. Kama Mkwawa au Baba yake hakujishughulisha na biashara ya utumwa huyu Mwamubambe alifikaje uheheni?
 
lole Gwagisa, Yericko Nyerere,

..napenda kujua Mkwawa alikuwa akipata wapi silaha za kivita?

..je, kuna ukweli wowote kuhusu tuhuma kwamba alikuwa akijihusisha na biashara wa WATUMWA??

..ugomvi wa Mkwawa na Wajerumani ulikuwa kuhusu nini haswa?


Swali la nyongeza. Je Mkwawa Mwinyigumba alikuwa mhehe 100%?

Wakuu, mniwie radhi kwa kutoonekana jukwaa hili la historia, hasa historia ya watukua wetu kama Mtwa Mkwavinyika Mnikungu (Mkwawa).
Namshukuru sana mkuu mnyikungu kwa kuendeleza historia ya Mtwa Mkwawa.
Mimi nitarudi na stories nyingine za ziada.
 
Katika posti yako moja umesema kuwa Mkwawa alipata bunduki kutoka kwa waarabu na kuanza kutengeneza zake mwenyewe. Na unakanusha kuwa hakuusika na biashara ya watumwa.

Hili uweze kutengeneza bunduki ni lazima uwe na chuma. Kwa historia ninayojua mimi, wahehe hawakuwa na technologia ya chuma. Makabila yalikuwa na technologia ya kufua chuma ni wafipa, walogo, wahaya .....

Pili katika vita ya kwanza na wajerumani, jeshi la mkwawa ziliteka bunduki kama 300 kutoka kwa majeshi wa ujerumani. Bunduki hizi zilikuwa nzuri kuliko zile za waarabu. Kama wahehe walikuwa na utaalamu wa kutengeneza bunduki kwanini hawakukopi zile za mjerumani?

Tatu huwezi kutumia bunduki bila kuwa na risasi au baruti. Wakati wajerumani wanateka ngome ya Mkwawa walikuta hazina kubwa baruti na meno ya tembo. Kwa sababu uheheni hakuna baruti, je ni biashara gani alikuwa anafanya?

Nne Mwamubambe ambaye alikuwa ni shemeji ya Mkwawa ni mnyamwezi. Alichukuliwa utumwa na wahehe na kulelewa na baba yake Mkwawa. Kama Mkwawa au Baba yake hakujishughulisha na biashara ya utumwa huyu Mwamubambe alifikaje uheheni?
kaka asante kwa changamoto zako, naomba nikujibu japo kidogo kama ifuatavyo, si kweli kama wahehe hawakua wafua chuma, wahehe ni wafua chuma wazuri tu, technolojia ya kufua chuma ilikuwepo toka enzi na enzi ndo maana vitu kama mikuki nyengo na vitu vingine vya chuma walitengenezea wao wenyewe, pia nikukumbushe kitu kimoja kulithibitisha hili. wahehe kila kitu hufanyika kulingana na koo husika, kuna koo za matabibu kama wakina nyenza na kina maliga na kulikuwepo na koo na wafua vyuma kama na watengenezaji wa bunduki kama kina nyakasonga, mbaka leo ukitafuta koo hizo bado zinatengeneza bunduki shotgun maarufu kama magobole.

pili umeuliza kwa nini wahehe hawakucopy bunduki za mjerumani, ndugu yangu bunduki za kipindi kile zote zilikuwa ni shotgun au magobole, liwe la mwarabu au mjerumani zote zilikuwa zinafana kabisa. kwahiyo asingeweza kuiga kitu ambacha tiyari alikuwa ameisha kiiga.

tatu umesema mwenyewe alikutwa ana hazina kubwa ya meno ya tembo na baruti. wingi wa meno ya tembo inadhihirisha kabisa kuwa huyu jamaa alikuwa akifanya biashara ya meno ya tembo hasa ukizingatia yeye alikuwa anapatikana kwenye mbuga ya wanyama inayofahamika kama ruaha sasa.kumbuka meno ya tembo ndo ilikuwa biashara kubwa sana wakati huo.

mwisho naomba kukanusha habari za kuwa mwambambe alichukuliwa mtumwa, mwambambe ni mhehe kabisa na anatokea ukoo wa kina mwalunyungu ambao ndo ulikuwa unatawala uhehe kabla ya mkwawa. labda wewe umesoma vitabu fulani vya wazungu vinavyosema mkwawa alipinduliwa na wangoni wakiongozwa na mwambambe kitu ambacho si cha kweli. hata sababu ya mwambambe kumpindua mkwawa ilikuwa hiyo kuwa aliona kama kapolwa ufalme na mkwawa. pia naomba utofautishe tofauti kati ya mateka na watumwa, mkwawa alikuwa na mateka wa vita alivyopigana na makabila mbalimbali kama wangoni, wasangu, wabena,wasafwa, wanyamwezi na mengine mengi ambao mwisho wa siku aliwafanya watumwa kwa kuwatumikisha yeye mwenyewe na sio kuwauza ndo maana irnga utakutana na koo nyingi za kingoni, kigogo na nyingine kutoka makabila mengine ambao ama watekwa na kubakishwa hapa kufanya kazi au waliletwa na wafalme wa makabila mengine kama hongo ili mkwawa asiende kuwashambulia.
 
Yale mafuvu 83 yaliyobakia ndo inakuwaje? Ngoja niende Bremen Museum kuwauliza.
Isike naye alijilipua. Ile yeye ni baruti nadhani hawakupata kitu. Kinjiketile ilikuwaje? Kaburi lake lipo?

ulivyoenda Bremen walisemaje mkuu zitto?
 
Wote tunatambua ushujaa wa Mtemi Mkwawa dhidi ya mkoloni Mjerumani. Mjerumani alipigwa round ya kwanza na mbabe Mkwawa akakimbia na kwenda kujipanga tena .

Aliporudi for second round, zikapigwa tena ila kidume Mkwawa aligoma kushikwa na Mjerumani na kwa ujasiri wa ajabu akaamua kujiua. Ukiachana na Wahehe, hakuna kabila lolote ambalo limeweza kuonesha ushujaa kama wa Wahehe.

Na ndio maana Mzungu alichukua fuvu la mbabe Mkwawa na kuondoka nalo ili kulichunguza zaidi kuhusiana na ushujaa wa huyu kidume. Wahehe ni mashujaa sana. Hata sasa hivi wapo hivyo hivyo tofauti na makabila mengine.
 
kwanza mkwawa hakua mhehe

ila ujasiri wa kujinyonga ndio ujasiri mkubwa zaidi duniani
 
kwanza mkwawa hakua mhehe

ila ujasiri wa kujinyonga ndio ujasiri mkubwa zaidi duniani

Pole sana mkuu nani aliye kudanganya kuwa mkwawa alijinyonga??

na kwa taarifa yako mkwawa hakujinyonga na lile fuvu la kichwa ni kanya boya tuu.soon nitakupa story kamili stay tuned.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom