Mjue mnyama Kobe

Mjue mnyama Kobe

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
kobe_c0c42.jpg

Kobe ni mnyama jamii ya Reptilia ambaye kwa kumtazama tu lazima ujiulize maswali mengi.Kitendo chake cha kuficha kichwa, mwendo wake na gamba lake gumu!!
moja unayotakiwa kuyajua kuhusiana na kobe!!!

[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] hawezi kuogelea kabisa lakini anaweza kubana pumzi zake kwa muda mrefu sana!! Ukimwondoa Nng’e kobe anafuata kwa uwezo wa kuishi muda mrefu bila kupumua!!!

[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wamekuwa ulimwenguni zaidi ya miaka milioni mia mbili iliyopita!!! Ni zaidi ya mijusi na wanyama wengine!!

[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wa sasa unaowafahamu wanaweza kuishi hadi miaka mia moja!!

[HASHTAG]#KOBE[/HASHTAG] wameweza kuishi kila bara kasoro bara moja tu Antarctica!!

[HASHTAG]#Gamba[/HASHTAG] la kobe limeundwa na mifupa 60 tofauti tofauti!! Na mifupa hii yote imeungana.

[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] wa kike hutaga kati ya mayai mawili hadi kumi na mawili na huchukua siku 90 hadi 120 kuyaatamia na hatimae kutotoa.

[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] wa kike ana uwezo wa kutaga kila baada ya miaka mitatu baada ya kukutana na kobe dume!!

[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] hana hata jino moja!!

[HASHTAG]#Licha[/HASHTAG] ya kuwa na gamba gumu sana, kobe akiguswa hata na unyoya wa kuku anatambua kuwa ameguswa!! Ana hisia kali sana!!

[HASHTAG]#Kobe[/HASHTAG] mkubwa kabisa duniani ana uzito wa kilogram mia saba.. hii inamfanya kuwa reptilia mzito kupita wote!!

[HASHTAG]#Kuna[/HASHTAG] aina 40 ya kobe!!!

Huyu ndiye kobe………
 
akainama ujue anatunga sheria
 
Kobe haatamii bali hufukia mayai yake kama mjusi kingine tambua kuna kobe wa majini na nchi kavu kama ilivyo kwa chura kobe ana meno madogomadogo kama mjusi anakula majani laini n k
 
Daah.. napenda kufuga sna kobe n other pets.
Miaka flan nliokota wawil enz izo mbez beach porin porin..nkafuga weee..
Baada ya kusafir a week,juat a week wahuni wakapita nao
 
Hapo kwenye miaka milioni miambili umetudanganya maana tangu Adam mpaka sasa ni miaka yapata Elfu 6 hivi haifiki hata elfu 10
Habari za Adam zipo kifikra zamwanadam,na habari ya Kobe ni ki sci ence usivilinganoshe
 
wakati nikiwa mdogo umri wa primary kwetu kulikuwa na shimo kubwa na hawa kobe wakubwa sana walikui..... wa wawili na walikuwa wakitoka shimoni tunapanda mgongoni kwao watoto wawili kila kobe halafu kobe wanatembea...... walikuwa wakubwa sana na nilipofika mkoa fulani nikakuta vikobe nikadhani ni vitoto kumbe eti ni wakubwa tayar .... ila hapo kwenye miaka umesema uongo mtakatifu.
 
Hapo kwenye miaka milioni miambili umetudanganya maana tangu Adam mpaka sasa ni miaka yapata Elfu 6 hivi haifiki hata elfu 10
Mwanadam ndio kiumbe wa mwisho kabisa kuumbwa.
Lakin pia umepata wapi kuwa kutoka Adam mpka sasa ni miaka 6000?
 
mhh mkuu kg 700 awe mzito kuliko rept, mamba zingine zinaua mpaka 800kg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom