Mjue Mama Thabita Siwale

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
TABITHA SIWALE: MWANAMKE JEMBE LA KINYAKYUSA. Tabitha Ijumba Mwambenja, mke wa Marehemu Mzee Siwale alizaliwa Mkoani Mbeya, wilayani Rungwe kwenye Ukoo wa Mwambenja na damu yake inasemekana kuwa na mahusiano ya karibu na Ukoo wa Chifu Mwakatumbula wa huko Kijiji Kitulivu Kyimo almaarufu kama KKK.

Ila kiasili huyu Tabitha ni mzaliwa wa maeneo ya Katumba hukohuko Tukuyu wilayani Rungwe, kwenye kaeneo fulani maarufu kwa wakazi wa Katumba na Tukuyu kwa ujumla panapojulikana kama "kwa Mwambenja".

Kutokana na kuolewa na kuwa mke wa Mzee Siwale amekuja kujulikana sana kwa jina la "Mama Siwale", Alianza kupenda siasa akiwa mtoto kabla ya Uhuru wa Tanganyika, akijipenyeza katika mikutano ya TANU kusikia yanayozungumzwa, ingawa baba yake alikuwa akimkataza kujihusisha na siasa na kumtaka asome kwanza, lakini yeye hakuacha siasa.

Aidha,Mama Siwale alipenda pia shughuli za Mahakama, kwa vile Baba yake alikuwa Ofisa wa mahakama.

Hivyo alivutiwa zaidi na kazi hizo, Alipata mafunzo ya Maarifa ya Jamii katika Shule ya Wasichana ya Geita na alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mpwapwa Dodoma na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi kwa miaka mitatu alikopata Shahada ya Juu ya Ualimu.

Alianza kufundisha mwaka 1961, katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bwiru huko Mwanza akiwa Mwalimu Mkuu; Aidha, alikuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wanawake ya Korogwe ambapo baadhi ya Wanafunzi wake ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,(UN) Dkt.

Asha -Rose Migiro ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria cha Haki za Binadamu,(HLRC) Bi. Helen Kijo-Bisimba.

Alipata mafunzo ya Siasa katika Chuo cha Siasa cha Kivukoni chini ya Mpango wa Taifa wa kuwafanya Watanzania waijue siasa ya Tanzania. Mnamo mwaka 1975 Mama Peruzi Butiku, mke wa Joseph Butiku, alitumwa na Rais Mwalimu Julius Nyerere amchukue na kumpeleka Ikulu, hapo ndipo Mwalimu Nyerere alimwambia kuwa, amemteua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu vya Rais.

Alikuwa Mbunge wa Taifa (wa kuchaguliwa na Raisi) wa kwanza Mwanamke na Waziri wa Elimu ya Taifa wa kwanza Mwanamke kuanzia mwaka 1975 hadi 1980 ambapo Bajeti yake kwa mwaka ilikuwa wastani wa Shs 216,049,000 kwa kipindi kilichoishia 1980 na aliweza kuingiza Wanafunzi shule ya Msingi kwa kasi wenye Umri kati ya Miaka 7 hadi 12.

Katika kipindi hiki watoto wa kike wengi waliozaliwa Tukuyu Rungwe walipewa majina ya Tabitha Wazazi wao wakihusudu wawe kama Mama Siwale.

Mama Siwale aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini tarehe 9 Novemba, 1975. Aidha, aliwahi kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchunguzi wa Ardhi (National Commission on Land Inquiry).

Mnamo mwaka 1977 chama cha TANU na ASP viliunganishwa na uchaguzi ulifanywa wa Baraza la Mawaziri wa Kwanza wa CCM ambapo Thabita Ijumba Siwale aliteuliwa tena Tarehe 14 Februari, 1977 kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini.

Mama Thabita Siwale mwaka 1980 aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Elimu ya Taifa hadi mwaka 1982 akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Padri Simon Chiwanga.

Mnamo mwaka 1984 alirudi tena Wizara ya Elimu kuwa Waziri na alimwachia Wizara hiyo Profesa Phillimon Sarungi. Alibaki na Ubunge hadi mwaka 2000. Aidha, alipata kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO. Pia mnamo mwaka 1989 alianzisha Taasisi ya Wanawake na Makazi (WAT-Human Settlement) na kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Akiwa Bungeni alipenda kupigania mambo mawili, Haki na nafasi ya mwanamke katika jamii na Umiliki wa ardhi na makazi. Alitetea hoja hadi kufanikiwa kuundwa kwa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999.

Akiwa katika Kamati ya kuandaa Mswada wa Sheria ya Ardhi alikuwa Mhimili Mkubwa wa kuwasilisha Mapendekezo kwenye Vifungu vya Sheria na Kutetea Wanawake katika haki ya kumiliki, kuuza na kutumia ardhi kama ilivyo kwa mwanaume.

Kwa wale wafuatiliaji wa Siasa za kiharakati nadhani mumewahi kusikia stori za lile kundi la G-55.

Huyu mama alikuwa ni Mmoja ya Wabunge kati ya Wabunge 55 waliounda kundi la G55 katika kutetea Uwepo wa Tanganyika wakati huo Waziri Mkuu akiwa Mhe John Samuel Malecela na Kundi hilo liliongozwa na Mheshimiwa Njelu Kasaka mbunge wa Chunya.

Mama Siwale aliwahi kutunukiwa Tuzo ya Mwanamke Mahiri wa Karne ya 21 mnamo Mwaka 2000 na Taasisi ya Kimarekani na Mwaka 2008, alipata Tuzo ya Mwanamke wa mwaka kutoka taasisi hiyo hiyo.

Mwaka 2001 alikuwa ni mmoja ya Wajumbe waliounda Kampuni ya NICO inayojihusisha na Uuzaji wa Hisa kwa lengo la kuondoa Vihatarishi vya kifedha katika Uwekezaji kupitia Mlundikano wa Hisa kibiashara (Mutual Fund) chini ya Mwenyekiti wake Felix Mosha na Makamu Mwenyekiti Jaji Mark Bomani.

Amewahi pia kushika nyadhifa kadhaa ikiwemo Uenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uvunaji wa Maziwa (DAFCO) na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wakati huo, likiitwa (NPF) chini ya Uenyekiti wa Mzee Peter Ngumbullu.

Mama Siwale ni Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wanawake na Mtandao wa Makazi (HIC-WAS). Pia amekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).

Kwa undani wa habari zaidi juu ya mmama huyu wa Kinyakyusa, tumwombe Mungu atupe uzima na kuniwezesha kukiandika kitabu cha "WANYAKYUSA MASHUHURI".

Kama hili la kuandika Kitabu likiwezekana, basi huko ndo kutakuwa na masimulizi mengi ya Wanyakyusa walio na waliopata kuwa maarufu ndani ya Mbeya, Tanzania na duniani kokote waliko au walikokuweko, Kwa sasa niwatakieni Jioni njema na maandalio mema ya maombolezo ya kifo cha Yesu Kristo hapo kesho.

Na zaidi niwatakieni maandalio mema ya Sikukuu ya Kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) siku ya Jumapili. Mungu awabariki, Kyala abasajege. © Lusako
 
17796581_1346307102082892_2289366681063184765_n.jpg
 
I know her. Nishakutana na picha zake pale Wat Saccos Kinondoni Bihafra zikimuelezea kama muasisi wa taasisi ile
 
Huyu mama alifanya maisha ya waseminari waliomaliza form four yawe magumu kosa lao ni kufanya vizuri ama kufaulu vizuri kidato cha nne. Alipitisha mswada bungeni kwamba wanafunzi wa seminari hawatachaguliwa kuingia A Level katika shule za sekondari za serikali. Kosa letu kubwa lilikua tulizuia nafasi kwa madhehebu mengine sababu ya ufaulu wetu. Hii Tanzania mambo ya ajabu ajabu yalianza zamani.

Kwasababu shule nyingi za seminari zilikua zinashika nafasi 10 bora katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne hivyo nafasi nyingi za kidato cha tano zilijazwa na watu wa dini moja hivyo katika kuleta usawa walianza kuzikandamiza shule za misheni badala ya kuboresha elimu katika shule zilizokua zinafanya vibaya.

Kwahiyo waseminari wakabaki kuishi maisha ya kinafiki hata kama hawakua na wito ili wabaki na wamalize form six.

Nina classmates wengi waliofaulu vizuri lakini waliishia form four sababu wazazi hawakuwa na uwezo wa kuwapeleka private school.

Kwasasa nikiangalia nyuma tulikotoka sishangai kwanini hili Taifa lina wasomi wengi lakini mambo wayafanyayo hayaendani na usomi wao.
 
Uzi wako una ukakasi na uwongo baadhi ya sehemu: Kwanza Chuo Kikuu cha Nairobi kilianza miaka ya karibu na ya 70 na mama Siwale unadai alianza kazi mwaka 1961. Kabla ya uhuru wa nchi za Afrika mashariki chuo kikuu kilikuwa Makerere peke yake, kikafuata chuo kikuu cha DSM kwa degree ya sheria mwaka 1962, na baadaye kilifuata chuo kikuu cha Nairobi.
Pili Siwale alidumu uwaziri wa elimu kwa miaka miwili tu na kufyatuliwa na Mwalimu. Alikuwa waziri wa elimu 1978-1980. Kabla ya hapo 1975-1977 waziri wa elimu alikuwa Nicholas Kuhanga, na kabla ya Kuhanga alikuwa Chediel Mgonja. Kwa kifupi huyu mama unayempamba na kumsifia kwa sababu wewe mwenyewe ni mnyakyusa, hakuimudu kabisa wizara ya elimu na kusababisha Mwalimu kumfyatua chapu chapu. Miaka hiyo mimi nilikuwa mwalimu hadi katikati ya miaka ya 2000 ndipo nikastaafu. Kwa hiyo usilishe watu matango pori hapa. Ni masahihisho hayo tu, mengine endelea na mapambio.
 
TABITHA SIWALE: MWANAMKE JEMBE LA KINYAKYUSA. Tabitha Ijumba Mwambenja, mke wa Marehemu Mzee Siwale alizaliwa Mkoani Mbeya, wilayani Rungwe kwenye Ukoo wa Mwambenja na damu yake inasemekana kuwa na mahusiano ya karibu na Ukoo wa Chifu Mwakatumbula wa huko Kijiji Kitulivu Kyimo almaarufu kama KKK.

Ila kiasili huyu Tabitha ni mzaliwa wa maeneo ya Katumba hukohuko Tukuyu wilayani Rungwe, kwenye kaeneo fulani maarufu kwa wakazi wa Katumba na Tukuyu kwa ujumla panapojulikana kama "kwa Mwambenja".

Kutokana na kuolewa na kuwa mke wa Mzee Siwale amekuja kujulikana sana kwa jina la "Mama Siwale", Alianza kupenda siasa akiwa mtoto kabla ya Uhuru wa Tanganyika, akijipenyeza katika mikutano ya TANU kusikia yanayozungumzwa, ingawa baba yake alikuwa akimkataza kujihusisha na siasa na kumtaka asome kwanza, lakini yeye hakuacha siasa.

Aidha,Mama Siwale alipenda pia shughuli za Mahakama, kwa vile Baba yake alikuwa Ofisa wa mahakama.

Hivyo alivutiwa zaidi na kazi hizo, Alipata mafunzo ya Maarifa ya Jamii katika Shule ya Wasichana ya Geita na alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mpwapwa Dodoma na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi kwa miaka mitatu alikopata Shahada ya Juu ya Ualimu.

Alianza kufundisha mwaka 1961, katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bwiru huko Mwanza akiwa Mwalimu Mkuu; Aidha, alikuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wanawake ya Korogwe ambapo baadhi ya Wanafunzi wake ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,(UN) Dkt.

Asha -Rose Migiro ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria cha Haki za Binadamu,(HLRC) Bi. Helen Kijo-Bisimba.

Alipata mafunzo ya Siasa katika Chuo cha Siasa cha Kivukoni chini ya Mpango wa Taifa wa kuwafanya Watanzania waijue siasa ya Tanzania. Mnamo mwaka 1975 Mama Peruzi Butiku, mke wa Joseph Butiku, alitumwa na Rais Mwalimu Julius Nyerere amchukue na kumpeleka Ikulu, hapo ndipo Mwalimu Nyerere alimwambia kuwa, amemteua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu vya Rais.

Alikuwa Mbunge wa Taifa (wa kuchaguliwa na Raisi) wa kwanza Mwanamke na Waziri wa Elimu ya Taifa wa kwanza Mwanamke kuanzia mwaka 1975 hadi 1980 ambapo Bajeti yake kwa mwaka ilikuwa wastani wa Shs 216,049,000 kwa kipindi kilichoishia 1980 na aliweza kuingiza Wanafunzi shule ya Msingi kwa kasi wenye Umri kati ya Miaka 7 hadi 12.

Katika kipindi hiki watoto wa kike wengi waliozaliwa Tukuyu Rungwe walipewa majina ya Tabitha Wazazi wao wakihusudu wawe kama Mama Siwale.

Mama Siwale aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini tarehe 9 Novemba, 1975. Aidha, aliwahi kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchunguzi wa Ardhi (National Commission on Land Inquiry).

Mnamo mwaka 1977 chama cha TANU na ASP viliunganishwa na uchaguzi ulifanywa wa Baraza la Mawaziri wa Kwanza wa CCM ambapo Thabita Ijumba Siwale aliteuliwa tena Tarehe 14 Februari, 1977 kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini.

Mama Thabita Siwale mwaka 1980 aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Elimu ya Taifa hadi mwaka 1982 akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Padri Simon Chiwanga.

Mnamo mwaka 1984 alirudi tena Wizara ya Elimu kuwa Waziri na alimwachia Wizara hiyo Profesa Phillimon Sarungi. Alibaki na Ubunge hadi mwaka 2000. Aidha, alipata kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO. Pia mnamo mwaka 1989 alianzisha Taasisi ya Wanawake na Makazi (WAT-Human Settlement) na kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Akiwa Bungeni alipenda kupigania mambo mawili, Haki na nafasi ya mwanamke katika jamii na Umiliki wa ardhi na makazi. Alitetea hoja hadi kufanikiwa kuundwa kwa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999.

Akiwa katika Kamati ya kuandaa Mswada wa Sheria ya Ardhi alikuwa Mhimili Mkubwa wa kuwasilisha Mapendekezo kwenye Vifungu vya Sheria na Kutetea Wanawake katika haki ya kumiliki, kuuza na kutumia ardhi kama ilivyo kwa mwanaume.

Kwa wale wafuatiliaji wa Siasa za kiharakati nadhani mumewahi kusikia stori za lile kundi la G-55.

Huyu mama alikuwa ni Mmoja ya Wabunge kati ya Wabunge 55 waliounda kundi la G55 katika kutetea Uwepo wa Tanganyika wakati huo Waziri Mkuu akiwa Mhe John Samuel Malecela na Kundi hilo liliongozwa na Mheshimiwa Njelu Kasaka mbunge wa Chunya.

Mama Siwale aliwahi kutunukiwa Tuzo ya Mwanamke Mahiri wa Karne ya 21 mnamo Mwaka 2000 na Taasisi ya Kimarekani na Mwaka 2008, alipata Tuzo ya Mwanamke wa mwaka kutoka taasisi hiyo hiyo.

Mwaka 2001 alikuwa ni mmoja ya Wajumbe waliounda Kampuni ya NICO inayojihusisha na Uuzaji wa Hisa kwa lengo la kuondoa Vihatarishi vya kifedha katika Uwekezaji kupitia Mlundikano wa Hisa kibiashara (Mutual Fund) chini ya Mwenyekiti wake Felix Mosha na Makamu Mwenyekiti Jaji Mark Bomani.

Amewahi pia kushika nyadhifa kadhaa ikiwemo Uenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uvunaji wa Maziwa (DAFCO) na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wakati huo, likiitwa (NPF) chini ya Uenyekiti wa Mzee Peter Ngumbullu.

Mama Siwale ni Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wanawake na Mtandao wa Makazi (HIC-WAS). Pia amekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).

Kwa undani wa habari zaidi juu ya mmama huyu wa Kinyakyusa, tumwombe Mungu atupe uzima na kuniwezesha kukiandika kitabu cha "WANYAKYUSA MASHUHURI".

Kama hili la kuandika Kitabu likiwezekana, basi huko ndo kutakuwa na masimulizi mengi ya Wanyakyusa walio na waliopata kuwa maarufu ndani ya Mbeya, Tanzania na duniani kokote waliko au walikokuweko, Kwa sasa niwatakieni Jioni njema na maandalio mema ya maombolezo ya kifo cha Yesu Kristo hapo kesho.

Na zaidi niwatakieni maandalio mema ya Sikukuu ya Kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) siku ya Jumapili. Mungu awabariki, Kyala abasajege. © Lusako
Flashback: 1973
Mama Siwale ni Mwalimu Mkuu Korogwe Girls.
wanafunzi(shule siitaji) tumeenda shuleni tumealikwa kwa sicial evining.
Wasichana walifurahi sana na tumeenda na bendi yetu ya mziki.
Mziki umeanza saa 11 kwa shingo upande.
Baada ya nusu saa umeme umezimwa, tukauliza vipi, tukaambiwa headmistress anasema muongoke.

Turaudi shuleni over300km away tukiwa tumesononeka sana.
Mama Siwale=Iron Lady.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom