Mjue fisadi wa enzi za mwalimu

Hakuwa Gasper Mwingira alikuwa anaitwa Augustin Mwingira, alizidiwa ujanja na mlebanon mmoja akiitwa George Hallack, sifikirii kama yeye alipata mgao wake.Na kwa kweli alikuwa na bahati mbaya tu wengineo walikuwa wanahamishwa wizara yeye tu alitolewa kazi. Siku hizi yupo Kigamboni anahubiri neno la Bwana

Mambo yote yanapokataa linalobaki ni kujisalimisha kwa bwana
 
Mzee Augustine Mwingira aliingizwa mjini na wakuu wa Air Tanzania. Meneja Mkuu wa Air Tanzania enzi hizo (1982) alikuwa Lawrence mmasi ambaye alifukuzwa kazi.

Watu wengi wanafikiri mambo ya ufisadi yameanza miaka hii. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na miradi mingi tu iliyoliwa na wajanja. Tofauti na siku hizi ilikuwa ni vigumu kujua kinachoendelea kwani watu walikuwa wanajificha sana au kutumia jina la chama kuhujumu nchi.

Lakini si afadhali enzi za Mwalimu? Si mnasema wenywe kuwa wahusika walifukuzwa kazi? Na kwamba watu wakati huo walifanya ufisadi kwa kujificha sana.

Hebu linganisha na ufisadi wa sasa. Viongozi wanafisadi bila aibu wala kificho. Ni wangapi wamefukuzwa kazi au hata kushtakiwa kwa ufisadi? Ukweli ni wachache sana tena ni kama watawala wanasema funika kombe mwanahamu apite.
 
Back
Top Bottom