Mjue fisadi wa enzi za mwalimu

Tip Master

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
490
532
Nimekutana na mzee mmoja wa enzi hizo na kunijuza kuwa waziri wa mawasiliano wakati wa utawala wa Nyerere mh. AGUSTIN MWINGIRA aliwai kuliingizia hasara taifa letu kwa mara ya kwanza tangu lipate uhuru wake kwa kwenda kununua ndege mbili Lebanon.

Nasikia ndege hizo zilikuwa mikweche na tangu zilipotua DIA enzi hizo zikitokea Lebanon hazikuwai kuruka tena mpaka wa leo in short hazikufanya kazi kabisa.

Kama kuna mwenye habari yoyote kuhusiana na hilo naomba atujuze zaidi.
 
Dah.. Na kweli mtujuze,na aliishia wapi na ufisadi huo...

Ila kama sitaeleweka vibaya,naomba kujuzwa na matajiri wa enzi hizo.. Mfano,wafanyabiashara na watu wengine maarufu enzi za Mwalimu..
 
Nimekutana na mzee mmoja wa enzi hizo na kunijuza waziri wa mawasiliano mh GASPER MWINGIRA aliwai kuliingizia hasara taifa letu kwa mara ya kwanza tangu lipate uhuru wake kwa kwenda kununua ndege mbili lebanon.nasikia ndege hizo zilikua mikweche na tangu zilipotua DIA enzi hizo zikitokea lebanon hazikuwai kuruka tena mpk wa leo in short haztwa ikufanya kazi kabisa.kama kuna mwenye habari yoyote kuhusiana na hilo naomba atujuze zaidi
Hakuwa Gasper Mwingira alikuwa anaitwa Augustin Mwingira, alizidiwa ujanja na mlebanon mmoja akiitwa George Hallack, sifikirii kama yeye alipata mgao wake.Na kwa kweli alikuwa na bahati mbaya tu wengineo walikuwa wanahamishwa wizara yeye tu alitolewa kazi. Siku hizi yupo Kigamboni anahubiri neno la Bwana
 
Mzee Augustine Mwingira aliingizwa mjini na wakuu wa Air Tanzania. Meneja Mkuu wa Air Tanzania enzi hizo (1982) alikuwa Lawrence mmasi ambaye alifukuzwa kazi.

Watu wengi wanafikiri mambo ya ufisadi yameanza miaka hii. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na miradi mingi tu iliyoliwa na wajanja. Tofauti na siku hizi ilikuwa ni vigumu kujua kinachoendelea kwani watu walikuwa wanajificha sana au kutumia jina la chama kuhujumu nchi.
 
asante sana kwa kunikosoa jina mkuu,unaweza ukawa una orodha ya mafisadi wengine wa enzi za mwalimu
 
Mzee Augustine Mwingira aliingizwa mjini na wakuu wa Air Tanzania. Meneja Mkuu wa Air Tanzania enzi hizo (1982) alikuwa Lawrence mmasi ambaye alifukuzwa kazi.

Watu wengi wanafikiri mambo ya ufisadi yameanza miaka hii. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na miradi mingi tu iliyoliwa na wajanja. Tofauti na siku hizi ilikuwa ni vigumu kujua kinachoendelea kwani watu walikuwa wanajificha sana au kutumia jina la chama kuhujumu nchi.

nakubaliana na wewe mkuu yan watu wengi walineemeka uku wakiwa na uzio wa mfumo mbov wa habari na elimu duni ya watz,
 
Lakini yeye (Mwalimu) alikuwa anafanya maamuzi magumu ukilinganisha na waliomfuatia!

sawa alikua anafanya maamuzi magumu lakin naona hawa wakina jk jk wanakaudhaifu ka uswaiba,nasikia mwl akikupenda anakubeba mpk mbeleko inachanika lakini yeye alikua akuachii,mf kuwaamisha hamisha watumisha mikoa pmj na vitengo tofauti na walipokua wamebolonga,hv mkuu unaweza ukatueleza impact yoyote ya ustadh kawawa ?
 
[QUOTE said:
dony2680;3403206]sawa alikua anafanya maamuzi magumu lakin naona hawa wakina jk jk wanakaudhaifu ka uswaiba,nasikia mwl akikupenda anakubeba mpk mbeleko inachanika lakini yeye alikua akuachii,mf kuwaamisha hamisha watumisha mikoa pmj na vitengo tofauti na walipokua wamebolonga,hv mkuu unaweza ukatueleza impact yoyote ya ustadh kawawa
?

Agustin mwingira alikuwa mwanafunzi wa nyerere kule Pugu. Hivyo nyerere hakumfukuza kazi bali alimpeleka kuwa mkuu wa mkoa Arusha. kawawa naye nae aliweka ka Kigango kule sweeden baada ya kusikia sweeden inaisaidia tanzania 5% ya hela zao za walala hoi!
 
Mi napenda kusikia juu ya wale wafanyabiashara wakubwa wa enzi hizo.. Source ya ukwasi ilikuwa nini...
 
Enzi ya mwalimu akiwa Rais na Sekoine akiwa waziri mkuu wafanyabiashara wengi walitiwa ndani kwa kuhujumu uchumi;wahindi, waarabu na wabantu pia!!Walikuwa na special courts za kuwahukumu pia.
 
Nasikia kuna baadhi ya matajiri hata kwenye kipindi cha utaifishaji mali zao hazkuguswa kabisa,na hao matajiri nackia baadhi yao wanatoka mikoa ya kagera na kilimanjaro,nasikia hata babake mh mbowe akuguswa!
 
Nimekutana na mzee mmoja wa enzi hizo na kunijuza waziri wa mawasiliano mh AGUSTIN MWINGIRA aliwai kuliingizia hasara taifa letu kwa mara ya kwanza tangu lipate uhuru wake kwa kwenda kununua ndege mbili lebanon.nasikia ndege hizo zilikua mikweche na tangu zilipotua DIA enzi hizo zikitokea lebanon hazikuwai kuruka tena mpk wa leo in short hazikufanya kazi kabisa.kama kuna mwenye habari yoyote kuhusiana na hilo naomba atujuze zaidi
hivi ufisadi maana yake nini? incompetency ya mtu= Ufisadi vilevile? labda mimi silielewi vizuri ili neno naomba kujuzwa tafadhari!
 
Lakini yeye (Mwalimu) alikuwa anafanya maamuzi magumu ukilinganisha na waliomfuatia!
..Waliomfatia Mwl. wasingeweza kufanya maamuzi magumu kwa kuwa na wao walikuwa wanachotewa na hao mafisadi so si rahisi kumfunga paka mwizi kengere wakati ulimlengesha adokoe ili baadae mle wote...utauchuna tu..
 
kumbe safari moja uanzisha nyingine
 
Mzee Augustine Mwingira aliingizwa mjini na wakuu wa Air Tanzania. Meneja Mkuu wa Air Tanzania enzi hizo (1982) alikuwa Lawrence mmasi ambaye alifukuzwa kazi.

Watu wengi wanafikiri mambo ya ufisadi yameanza miaka hii. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na miradi mingi tu iliyoliwa na wajanja. Tofauti na siku hizi ilikuwa ni vigumu kujua kinachoendelea kwani watu walikuwa wanajificha sana au kutumia jina la chama kuhujumu nchi.

Je magnitude ya wakati huo inalingana na ya sasa.............I mean issue ya $94m wakati huo uliweza kuifanya?
 
Kulitokea ufisadi enzi ya mwalimu wizara ya usafirishaji wakati huo waziri wake alikuwa Mustapha Nyang'anyi; walinunua kivuko cha pale magogoni kilichokuwa kimetumika na kibovu kikitwa UNIFLOATE kwa bei ya kuruka!! Mwalimu alimpenda sana Mustapha kwahiyo hakuna lolote lilitendeka!! Kama sijakosea Sinde Warioba alikuwa waziri mkuu enzi hizo; Col.Kashmir ndio aliyekuwa dalali wa hiyo dili mbovu!!
 
Back
Top Bottom