Mjue Engineer wa Kitanzania aliyeipandisha chati Google!

Mkuu, nadhani siyo fair kumbagua mtu kwa sababu ya rangi ya ngozi yake, urefu wa pua yake, asili ya wazazi wake, au kitu kimgine chochote. Nadhani hii tabia ya kuangalia watu wa rangi au asili fulani kwa kudhani kwamba wote wa aina hiyo ni mafisadi haifai. Mbona tuna wahindi wengi tunaishi nao vizuri tu na wala siyo mafisadi? Anaweza kuwa ni raia tu mzuri wa nchi hii, na hajaifanyia ubaya wowote nchi hii, lakini wewe unambagua kwa kumtazama usoni tu! That's not fair.
Mkuu nadhani wewe ndo umesahau kwamba wao ndo wabaguzi wakubwa kwa watanzania weusi. Wengi wao (siyo wote) wanazo bado zile mentallity za during colonial era, za kujiona superior than black Tzs. Isingekuwa uvumilivu na upendo wa weusi, hali ingekuwa tofauti.
 
hivi kama hawa kweli ni watanzania na wana skill nzuri kiasi hiki wanapewa nafasi gani kwenye nchi hii?je hzi porojo za siasa za upuuzi zitawaruhusu watoe michango yao hapa tanzania??
 
Amezaliwa Tanzania... Hawajasema ni raia wa Tanzania au kasoma Tanzania. Mbona wengi wanazaliwa Tanzania lakini hawaishii kuwa watanzania. Labda alizaliwa Tanzania wakati wazazi wamekuja mapumziko mafupi...
 
Mtanzania kuwa pale siyo issue, swala ni anajivunia huo Utanzania? Na katika akili yake, huwa anakumbuka kuwa yeye ni Mtanzania? Labda mleta uzi angesema ni mambo mangapi kaifanyia Tz hapo google wakati mwenyewe hakumbuki kabisa kama aliwahi zaliwa Tanzania, zaidi ya kujiona Mtanzania.

Kwani kimsingi Tz imemwezeshaje kufika hapo?Isije ikawa ni mambo ya mtu anastruggle kivyake akitoboa watu mnaanza kummaindi na kuuliza kaifanyia nini TZ. Kwani ameombwa ashiriki nini akakataa? Mnataka aifanyie ufisadi sio ndo mjue kachangia?
Mbona wengi tu wameifnayia ufisadi tena baada ya wao kuwezeshwa na hata hatuandamani?

Isije ikawa kejeli za Mizengo kuwaambia watz walioko Ireland walete Matrekta wakati in return serikali inanunua mashangingi! Yaani watz walioko nje wajenge nchi wakati serikali yenye jukumu la kuijenga 'ikibomoa'

Nafikiri suala tu la yeye kustruggle kihalali(kama ni kweli) na kupata good job ni mchango tosha kwa taifa hata asipoleta hata kumi nyumbani!
 
Ben Gomes anaitangaza Tanzania, that is all!! Whether anajivunia, anatoa msaada, ni raia nafikiri hizo siyo issues cha msingi kutamka au kuandikwa kuwa alizaliwa Tanzania inatosha kabisa. Kuna mashirika yapo hapa nchini kwa ajili ya kuigangaza nchi kama vile Tanzania Tourist Board hawafanyi, basi ngoja mdosi atusaidie
 
yawezekana alizaliwa tzed lakin ameshaisahau au ajitambulishi nayo tena, jana nilikuwa najaribu ku-activate google adds a/c, ilikataa, sababu lugha ya kiswahili haitambuliki, lakin kuweka adds bila a/c activation its ok to them, blog inatumia lugha zote mbili, angekuwa mbongo anayejivunia nao au lugha hii angeshafanya jambo flan, naamini hivyo.
 
Jina kama asili ya mgoa. Wabongo bana, watu wasio wabantu tunawabagua/wanatubagua nchini.....wahindi wanaambiwa warudi kwao, kina Rostam warudi sijui Iran, Richa Adhia yule miss Tanzania alipondwa.....ila huyu kafanikiwa Google, basi ni Mtanzania. Kaaaaazi kweli kweli!
umeongea kweli mkuu imenigusa
 
yawezekana alizaliwa tzed lakin ameshaisahau au ajitambulishi nayo tena, jana nilikuwa najaribu ku-activate google adds a/c, ilikataa, sababu lugha ya kiswahili haitambuliki, lakin kuweka adds bila a/c activation its ok to them, blog inatumia lugha zote mbili, angekuwa mbongo anayejivunia nao au lugha hii angeshafanya jambo flan, naamini hivyo.
sema mkuu ni kweli lkn....heb niambie mkuu kwann unajiita next millionare?
 
Kwa nini aufikirie Utanzania wake wakati Watanzania wameshembagua sana na kumtaka 'arudi kwao' !

Gaijin, Segment ya ubaguzi iko katika kila society, some just exhibit a lot more than others. Only thing one can do is rise beyond ubaguzi na kuutukuza uzalendo wake kwa Taifa lake alilochagua, be USA or Tanzania.

Ninachoweza kupingana nacho hapa ni ile tabia ya wengi kuona mtu kafanikiwa kwa jambo fulani hivi ndiyo mnaanza kujipendekeza kwake. Mara huyu wa kwetu kabisa, ooh huyu wa nyumbani, huyu ni Mtanzania na mengine kama hayo. Hali mwenyewe keshasahau kabisa na kukata ties zote.
 
Mmhh...chukulia mtu aliyeanza kazi ya kubeba maboksi Walmart na baada ya miaka 30 of blood, sweat, and tears (pamoja na top-notch grades and accolades from "Walmart University" and whatnot) tuseme kabahatika kuwa Store Manager kwenye Walmart Superstore fulani somewhere, jee ana chance gani ya ku-influence overall corporate policies za Walmart kuhusu msimamo wa Walmart Corp kuhusu Tanzania?

Kama kuwa store manager ni kitu kikubwa kama unavyo elezea...anaweza ku-influence kwa ku-suggest majaribio ya kuuza Konyagi, Africafe, Chaibora n.k. kutoka Tanzania na si kutoka Kenya pekee kwenye shelves zao za fairtrade products!!

Kama ana suggest na kukukubaliwa then that is success, kama wanamkatalia, basi keshaonesha uzalendo wake kwa kujaribu. Na suppliers wa Bongo wakim-let down kwa kushindwa ku-supply, walau yeye atakuwa ameondokana na lawama for trying his/her best kupromote Utanzania wake.
 
kwahiyo wahindi siku hizi ni watanzania! Lol.Halafu huyo hapo chini jirani yako sijui muhindi mwenzie. Hebu kwanza nitafsirie alichoandika maana kidhungu not richabo.
Kweli not richabo. Hujawaona wahindi popote Tanzania? Unafikiri wote wametoka India jana? Wakati mwingine ni afadhali kunyamamza kuliko kuonyesha umbumbu wako tena kwa kujisifu.
 
I am proud of him, but is he a proud tanzanian?? maana kuzaliwa tanzania ni issue moja na pia gomes ni jina tata kwetu

anyway congrats
 
jina kama asili ya mgoa. Wabongo bana, watu wasio wabantu tunawabagua/wanatubagua nchini.....wahindi wanaambiwa warudi kwao, kina rostam warudi sijui iran, richa adhia yule miss tanzania alipondwa.....ila huyu kafanikiwa google, basi ni mtanzania. Kaaaaazi kweli kweli!



nakuambia wanamatatizo sana sana.......si umeona hapo kwenye mambo ya jimbo la igunga wanasema kama sio ngozi nyeupe huwezi kupita? Sasa hayo si mambo ya kinafiki kabisa jamani? Kwnini tusijifunze kwa wenzetu....obama katoka kenya sasa anaiongoza dunia.......angekuwa tanzania ndio anagombea uraisi wala kura moja asingepata watu walivyo na akili duni...tunatakiwa kufikia hatua tuache mambo ya kibaguzi.......pia tujue kwamba mtu unaweza kubadili uraia wako muda wowote utakapo na kuingia kwenye uraia wa nchi unayo ishi........hapa wabeba box ni wengi sana wanapiga tumba wakati wao wenye walisha badili uraia huko walipo.........
 
Hivi kweli dunia ya leo kuna mtanzania asiye wajua watanzania? Jamani tuwe makini kweli huyo ni mtanzania au na wewe muandika thread hii unafanana na mtanzania huyu unayesema ni mtanzania, acha kututania kabisa, heshima iwe mbele utani nyuma.
 
Hivi kweli dunia ya leo kuna mtanzania asiye wajua watanzania? Jamani tuwe makini kweli huyo ni mtanzania au na wewe muandika thread hii unafanana na mtanzania huyu unayesema ni mtanzania, acha kututania kabisa, heshima iwe mbele utani nyuma.
Wewe unafanyakazi immigration nini, kitengo cha passport.

Unawajuwa Watanzania wote.
 
What about Prof. Issa shivji, Aamir Jamal, mzee Sabodo, Kassim Dewji, Manji, Shamim Khan, Dereck Bryson, Salim Ahmed Salim, Hussein Bashe, Rostam, Kinana, Rage, Prof. Mascarenas, SS Bakhressa, Zungu etc. je hawa nao ni watanzania ama sio watanzania? Acheni ubaguzi
umemsahau Jetul Patel
 
Back
Top Bottom