Tukiweka ushabiki pembeni na akili za ajabu ajabu za wamarekani (maana unaweza kukuta wanamchagua), Trump hana sifa ya kuwa Rais wa Marekani. Hata wanasiasa wa kawaida tu hapa kwetu Tanzania wanaweza kumpita kwa mbali kung'amua lipi la kuzungumza na lipi la kuacha. Aaaaah! mama Clinton ana bahati kujipatia mteremko
Hizi ni hisia za kipuuzi. Unachotakiwa kujiuliza:
1) Hivi ndani ya Republican hakuna watu wenye uwezo wa kisiasa kuwazidi hawa wa kwetu?
2) Mpaka pale alipofikia hatua ya kuwa mteule wa Chama alijifikisha mwenyewe au watu walimchagua?
3) Kuna wakati mpaka kwenye kura za maoni Trump amekuwa akimzidi Hilary Clinton, ina maana hizo kura za maoni anajipa mwenyewe?
4) Hivi wanaomjua mtu atakayeiongoza Marekani vizuri ni Watanzania au Wamarekani?
Mimi ninaamini kuwa kwa Marekani, mpaka alipofikia huyu Trump ni lazima ana uwezo katika maeneo mengi ambayo Wamarekani wengi hawana. Trump anaweza kushinda uchaguzi wa Marekani kama alivyoshinda Obama (wengi walisema Obama asingeshinda). Na hata akishindwa, mpishano wa kura hautakuwa mkubwa. Hiyo inaonesha kuwa Wamarekani wengi, kwa ulinganisho, wanaona wagombea hawa wawili wanakaribiana sana.
Kwenye ubaguzi sina uhakika kama Trump ni mbaguzi. Marekani ni ya Wamarekani, siyo Wanigeria au Wasaudia au Watanzania. Nchi ya Marekani ambayo watu wake wamewahi kuuwa na magaidi mara kadhaa, magaidi wote wakiwa ni wageni, hata ningekuwa mimi, kwa usalama wa watu wangu ningependekeza hatua kali za udhibiti wa wageni kwaajili ya usalama wa watu wengi.
Trump ameongelea zaidi udhibiti wa wageni, na bahati mbaya wageni hao ni Waarabu, Waafrika na Walatino. Huku hawa wote wakiwa na rekodi mbaya ya matukio ya uhalifu nchini Marekani.
Tujenge nchi zetu ili ziwe ni mahali pazuri pa kuishi kuliko kukimbilia nchi za wengine, tukiamini tunaweza kudictate sera na sheria za ugenini.