That shows umemsikia huyu jamaa majuzi tu na labda hujawahi kumsikiliza kwenye ile debate au katika hotuba zake za kampeni. Usiimbishwe nyimbo, jiridhishe kwa kuchunguza habari zinazosemwa. Je, ulisikia juu ya kesi yake ya kuzuia watu ambao si wazungu wasikodi nyumba zake? Je, ulipata kusikia juu ya kesi ya Central Park 5? Je, ulipata kusikia matusi ya nguoni aliyotoa dhidi ya Megyn Kelley mwaka jana. Je, uliwahi kusikia juu ya utapeli wake wa Trump University? Je, ulipata kusikia mzozo wa mwaka huu alipomkataa jaji kwa misingi ya kwamba si mzungu na kwamba wazazi wake walikuwa na asili ya Mexico? Unajua Trump alianza kupata umaarufu kisiasa kwa nini? Jibu: kwa sababu ya kudai hadharani kwamba Obama hakuzaliwa Marekani. Je, hivi hata unajua kwamba nchi ya Marekani ilikuwa na watu wa asili kabla ya wazungu na kwamba hao watu wa asili wapo lakini wamepokwa kila kitu, na sasa wazungu kama Trump wanadai nchi ni yao tu? Jiridhishe kwa ku-google hata kidogo tu.
Kingine ni kwamba ametengeneza mazingira ambapo wabaguzi kama KKK ndiyo wanamuona kuwa ni mtu atakayeendeleza sera zao. Umeshawahi kumsikia akisema "enzi zile watu hao wangebebwa na kutupwa nje." Umewahi kujiuliza ni enzi gani hizo anazozisema? Basi nikujuze ni wakati wazungu walipokuwa na sheria za kibaguzi. Waliopinga sheria hizo hasa watu weusi walifanyiwa vibaya sana. Yeyote anayepata umaarufu kwa kuwagawa watu wa nchi, hafai kuwa kiongozi.
Historia inatufundisha kwamba demagogues wa namna hiyo wanaweza kuwa na sera mbaya kabisa na wakakubalika kabisa kwa sababu wamechochea emotions na the bad side of humanity. Angalia historia ya Ujerumani jinsi walivyokuwa wanamwabudu Hitler. Na watu wanaona mambo yanayoshabihiana naya yale. Mtu anadai ni yeye tu ndiyo anaweza kurekebisha mambo. Tunawajua ma-genius wengi duniani. Lakini huwasikii wakijidai kwamba ni ma-genius. Trump tu anatamba hivyo. Kwa lipi la maana? Utapeli na kukwepa kodi kama alivyokiri?
Nataka nimtetee Bibi Clinton kuhusu server kuwa nyumbani. Kwanza kafanya vibaya na amekiri kwamba ulikuwa uamuzi mbaya. Lakini hili halikutoka tu kichwani mwake. Alishauriwa na watangulizi wake. Sasa kuna emails kama 31,000 zimepotea. Ni tatizo. Lakini uzito wa tatizo hili inaonekana ni mkubwa hata kuliko utawala wa kabla ya Obama ambao ulipoteza kama emails 40,000. Hapakuwa na kelele kutoka kwa republicans kama ilivyo sasa. Clinton ameanza kuandamwa toka mwaka 2000 na ikawa mbaya zaidi mumewe alipompa kazi ya kujaribu kubuni sera ya afya. We need to look at some of these things in a proper perspective. Kwamba amekubalika na section fulani ya watu si ushahidi kwamba ndiyo anafaa. Ingawa democrasia ndivyo inataka.
Sasa huo ubaguzi Una effect gani kwa legal citizens wa US? Nchi kuwa position ya kuitwa super power ni strategic mission and ops,
Na Trump anawaumiza zaidi raia wa nje ya mipaka ya US. Na akipata ndio hivyo hakuna atakaepeleka pua ovyo kwenye nchi yao au kugusa maslai yao. Wameshamfanyia image laundering aogopwe na mataifa ya nje. Akishakaa white house tayari ata create fear na US kuendelea kutawala tu vinchi vidogo.
Tunaimbishwa nyimbo ya ubaguzi tu bila kujua motives behind. Sera za Trump zimesimama kuiongoza na kuisimamisha US on top as always. Na ndio kitu bora kwa wamarekani. Maslahi ya nchi yao kwanza.
Sasa mbaguzi name mtu ambae haaminiki unadhani atachaguliwa nani? Bora huyo ambae ame reveal his true colors. Kuliko alieweka server nyumbani name kufanya take kwa usiri mkubwa bila kujali confidentiality ya national security.