Mjomba wangu sitakusahau

Mjomba wangu sitakusahau

Lasaba gani anaandika vizuri hivyo? Wakati kuna watu wamemaliza chuo wakiandika ni majanga
 
Wewe jamaa unamuonea mjomba.
Kwanza wewe ni kituko na kichekesho:

Yani unaomba kuwa Daktari?

Unaomba kuwa mtanesco?
Pamoja na kubeba nguzo huko tanesco ila hamkufundishwa safety?
Yani wewe jamaa ni mburula na kiazi sana.
Labda kama hii thread ni ya kutunga
Khaaaaa
 
Ku
Huyu jamaa ni comedian
Ana post nyingene, anahitaji kukodi mbwa wa3 kwa sababu mbwa wake aina Germany Shepard walimezwa na chatu, na hiyo chatu alimeza mifugo yake Kama mbuzi kuku na ngombe, Ila hao mbwa watatu wakimezwa itabidi mkodishaji wakae Tena mezani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ndio huyu! Naukumbuka huo uzi
 
We mleta mada ni boya kinyama dah. Nimecheka kiwaki mpaka masela hapa ghetto wameamka nikauchuka kama naota vile.
 
naomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira.

Hapa sijaelewa, kwani una taaluma hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu nimesoma nikaishia katikati maana nilikuwa kama nachanganyikiwa vile. Hebu naomba kuelewa kidogo. Wewe darasa la saba ila ukaomba kazi ya udakitari? Halafu pia ukaomba kazi ya TANESCO?

Kwa hyo ukadhani udaktari ni makalio kila mtu anayo?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona kama ulikuwa na kiherehere sana Mkuu... Ulitaka kazi ya udaktari wakati hukuwa na taalumu mara utanesco ... Nadhani hata rafiki wa mjomba wako alikuzingua tu baada ya kukusoma!

Tena anasema amtafutie kazi HATA YA UDAKITARI. Ina maana angeweza kupata zaidi ya hiyo ila kwa vile ni msaada hata udakitari sio mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu unataka kuwa dakitare wakati haujasomea?au sijasoma vizuri uzi wako

Aisee! Huyu mkuu nadhani ameandika comedy hapa. Mwanzoni nilisoma nikashindwa kumaliza nikaishia katikati maana nilikuwa kama nachanganyikiwa vile. Nimetulia nikaamua kuisoma mpaka mwisho nimecheka sana. Hii ni comedy kabisa.

Aisee Lasaba aruke akawe dactari ? wenzake tulishadisect sana michura na mipanya ila tukakimbia mbaya kabisa, huyu jamaa akili zinafanya kazi good au corona imepanda kichwani ? We are not late tunaweza kumsaidia aisee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi nimeishia hapo "HATA KAZI YA UDAKITARI" yaani simpo tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Dunia ina mambo, naweka akiba ya maneno

Hii kazi ya udaktari na darasa la saba

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mimi nilivyofika tu hapo kwenye swala la udaktari nikagundua nimeingizwa mkenge ikabidi nirudi juu kusoma jina la mleta mada.

Sent using Jamii Forums mobile app

At least kuna mtu amenisahaulisha Corona. Mleta mada usitufanyie hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijawah kucheka kama leo recently daaah huyu jamaa kiboko 🤣🤣🤣🤣

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kazi ya udaktari alimaanisha nafasi yoyote ya hospital na kazi ya uTanesco ni kazi yoyote ktk shirika hilo.
 
naomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira.

Hapa sijaelewa, kwani una taaluma hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
JF ni sawa na Nchi moja hapa duniani inaitwa, Marekani. Nasikia waliowahi kufika kule wanasema, kule kila kabila lililopo hapa duniani utalikuta kule; hata kama ni mwakilishi mmoja wa hilo kabila. Ndio JF sasa, kuna sampuli za watu wa kila aina.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😎😎😎😎😎 aisee
 
Darasa la saba..unaomba kazi ya utabibu.. mjomba hakuwa mjinga kuipotezea hiyo nafasi sababu alikujua huna hiyo taaluma .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa dada alikuwa daktari baada ya mjomba kumpeleka kwa Jamaa mwingine anajuana naye.
Neno hilindaktari ni pana kidogo, maana hata wa jadi nao wanajiita hivyo.
Wa mifugo pia hujiita hivyo na hata wa kule wanapohifadhia miili ya waliokwisha fariki huitwa/hujiita hivyo 'madaktari'

Ungefafanua vizuri, unamaanisha daktari yupi.?
 
Naomba leo nielezee kidogo kuhusu huyu mjomba wangu ambaye alikuwa tegemeo langu kipindi fulani ila alishindwa kunisaidia na nikajikuta nakuwa na maisha magumu sana huko jijini Dar es Salaam.

Mwaka 2004 niliondoka nyumbani kwenda Dar es Salaam kwa mjomba wangu nikiwa na miaka 22, nilikuwa kijana mwenye nguvu na nidhamu kwa watu wote. Ila sikuweza kuendelea na masomo kwa sababu nyumbani hali ilikuwa mbaya sana hivyo baada ya kuhitimu darasa la saba nikawa ni mtu wa kupambana kusaka riziki huku na kule ila sikuweza kufanikiwa kikubwa nilivyotegemea.

Mama yangu akampigia Mjomba simu na kuomba anichukue nikakae Dar es Salaam ili anisaidie kupata kazi. Kwa kweli mjomba alikuwa na uwezo na alifahamiana na watu wengi serikalini na katika sekta binafsi hivyo nilijua ataweza kunisaidia kupata kazi.

Mjomba yeye alikuwa ana duka kubwa la kuuza vifaa vya umeme pale Kariakoo na hakutaka kufanya kazi na mimi kwa kigezo kuwa ni mtu mzima sana hawezi kugombezana na mimi tena mbele za watu (mjomba ni mkali) basi tukazunguka huku na kule hakuna ajira na alipopata zaidi ni viwandani ila akataka nijitegemee nauli hivyo nikashindwa kuendelea.

Ila kinachouma ni kuwa Mjomba alikuwa na marafiki kila kona siku moja alikuja rafiki yake akajitambulisha alikuwa ni daktari hospitali moja maeneo ya Temeke basi wakaongea hapo muda mrefu wakati anaondoka nikawawahi na kuwaomba samahani na kumwambia mjomba tumehangaika sana kutafuta kazi naomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira. Mjomba akasema sawa nitaongea naye na yule daktari akasema akipata nafasi ataniambia.

Zikapita siku nyingi kimya hakuna jibu nikakutana na yule rafiki siku moja na kumkumbushia akadai alipata nafasi ila mjomba akakataa kuwa siwezi kuwa daktari atanitafutia kazi sehemu nyingine. Niliumia sana siku ile niliumia na kuona kama nimebeba dunia na mhimili wake mgongoni kwangu bila msaada wa mtu yeyote. Kweli kazi ya udaktari ilipatikana ila mjomba akakataa kweli? Nikamwambia mama na mama akalaani sana kile kitendo alichofanya mjomba ila tukasamehe.

Zikapita siku nikapata rafiki mmoja akaniambia kazi kwenye Shirika la Umeme na nikamwambia mjomba basi anisaidie nipate kata kazi ya utanesco akasema sawa nikajua ni zake zile ila kweli mjomba akanitafutia kazi na nikawa nafanya kazi ya utanesco. Siku moja isiyo na jina nilikutana na kisa kibaya zaidi niliporudi nyumbani usiku. Mjomba alikuwa anataka tufanye marekebisho ya umeme ndani na akasema wewe Mtanesco si utaweza au?

Nikasema nitaweza ila sikuwa najua chochote kuhusu umeme nilikuwa nachimba tu mashimo kazini na kubeba nguzo ila kufunga umeme walikuwa wanafunga wenzangu mimi nilikuwa sijawahi. Basi mjomba akasema chukua sijui huu waya ukate na uunge kwenye soketi ya nje. Nikasema sawa na nikaanza kazi ya kukata waya kumbe mjomba hakusema kuwa umeme ni hatari nakumbuka nilirushwa ukutani nikaanguka na kupoteza fahamu na siku napata fahamu niko hospitali na mama yupo kitandani sijui kuna nini wananishangaa na mimi nawashangaa tu. Nikatibiwa siku kadhaa nikapona.

Baada ya kupona mjomba akaninunulia nguo na viatu na kuniambia kesho utaondoka na mama kurudi kijijini. Nikamuuliza kuna nini na kwanini niondoke wakati niko kazini? Akasema tumeshauriana na mama yako urudi nyumbani kwa muda.

Sawa kwa shingo upande bila kujua sababu ya kurudi nyumbani nikarudi na mama. Nikafika kijijini watu wananiita fundi wengine daktari wengi Mtanesco mimi sielewi nani kawaambia kazi zangu hizo. Nikaanza kilimo taratibu na kuanza kupata tenda ya kupeleka ulezi Mwanza na hatimaye nikajenga na maisha yakawa yanategemea kilimo hadi sasa.

Mjomba nikawa nawasiliana naye na muda mwingine namtumia ulezi huku nikisema moyoni "Tenda wema nenda zako"

Siwezi kusahau kwa kweli..

Sent using Jamii Forums mobile app
hahahahahahahaha pole sana ila ni vizuri kuwa mkweli kwa mambo ambayo huwezi, hata kama mtu anataka kukusaidia ni vyema kuwa mkweli wakati mwingine usiweke maisha yako hatarini kisa kujiona unahitaji msaada tu.
 
eti unajiita daktari wa meno si utamng'oa mgonjwa mpaka ulimi kwa ulivyo daktari uchwara ?
 
unafikiri kazi ya udaktari ina dei waka kama kuchimba mashimo ya nguzo za umeme ?
 
Back
Top Bottom