Mjomba Hana Lolote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjomba Hana Lolote

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Mar 2, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Mjomba Hana Lolote


  Nina sehemu ya kuishi kwenye mwili, wakati mwingine naishi kwenye hotel inayoitwa damu; kila mmoja ananijua mimi ndiyo naitwa Kirusi mtoto wa UKIMWI, na nilizaliwa kwenye mwili wa binadamu kutokana na vitendo ZINAA.

  Mama nisikilize, baba nisikilize, kaka nisikilize, dada nisikilize, wewe uliye mwerevu nisikilize, hata wewe mwehu nisikilize, uliye mtii nisikilize, mwenye kiburi pia nisikilize, msomi nisikilize, usiye na elimu nisikilize, sina urafiki na mtu yeyote.


  Tunazaliana kama mchwa unaweza ukawauliza matajiri, maskini, weupe, weusi, wanawake, wanaume, madaktari na waganga wa kienyeji wote wananijua vizuri sana, hata kaka yangu STD ananifahamu nashambulia maelfu ya watu kila siku inayoenda duniani.


  Sikiliza!

  Na wewe nitakubeba na hasa kama unachukia kuwa mwaminifu kwa mke wako au mume wako.

  Nawabeba wote wanaokataa kusubiri na kuwa waaminifu ili wakapambe makaburi.

  Utakufa bado kijana!

  Afrika wananijua, Ulaya wananijua, Amerika wananijua, dunia nzima wananijua kwamba mimi ni KIRUSI, mtoto wa kiume wa Mzee Ukimwi.


  Kawaida natembelea baa, vilabu vya pombe, kumbi za disko na siogopi umri wa mtu, najificha kwenye maumbile ya miguu inavyovutia, makalio makubwa, mapaja yanayovutia.


  Wengine huniita mimi NGOMA, UMEME, wengine wananiita JULIANA, na wengine wananiita MDUDU wengine huniita MIWAYA, na wengine TRANSFORMER, wengine wananiita mimi Nambari ONE, na wengine MANYONYOBA na majina mengine mabaya mabaya kwani jina langu ni KIRUSI mtoto wa Ukimwi wala sina urafiki na mtu yeyote wala simuogopi mtu yeyote.


  Nawauwa Madaktari, Wauguzi, Wanasheria, Walimu, Maprofesa, Mawaziri, Wachungaji na wafagiaji barabara wala sina aibu.

  Nitakunywa damu yako na nyama nyama zote hadi ubaki mifupa na baadaye nakupiga teke kwenda kaburini.


  Nakushauri wewe mwanaume ukaze vizuri mkanda wa suruali yako na wewe mwanamke tunza nguo yako ya ndani kwa sababu ninakuangalia.


  Njia kamili ya kunishinda ni wewe kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako mmoja ambaye naye ni salama.

  Ukikubali kuwa rafiki na mjomba wangu (Condom) hutakuwa na nafasi ya kunikimbia kwani kazi ya mjomba ni kwa ajili ya uzazi wa mpango, huwezi kumtumia mjomba na ukanishinda mimi.


  Baada ya kusoma fahamu kwamba nipo nimekaa pembeni yako kosa moja tuu nakumaliza mzima mzima.

  Nani anajua! inawezekana tayari nipo kwenye mfumo wako wa damu nenda kapime, ila kama wewe ni mwaminifu haina haja ya kuwa na hofu. Naitwa KIRUSI mtoto wa Ukimwi sina urafiki na mtu.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Duh! Hii imeniacha hoi japo ni ukweli mtupu. Asante Mwanahalisi kwa bandiko hili ambalo limekaa kishairi lakini linazungumza kinagaubaga juu ya huyo jamaa asiye na urafiki na yeyote. Hakika lazima tujihadhari kwani daima anatufuata kila tulipo. Mungu tusaidie tuwe waaminifu katika maagano yetu
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Mungu tusaidie tuwe waaminifu katika maagano yetu

  amen mpendwa iwe kwako in jesus name
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  haya sasa, tungoje uende studio na tuisikie, la sivyo, Mjomba bado ngangari
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimependa utunzi wako ila kuna wengine wanaupata kwa njia tofauti sio zinaa peke ake!
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Tehe tehe! Kuna wengine.
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Shairi zuri na limebeba ujumbe sawasawa lkn hebu edit topic ya sredi kama inamkebehi mtu flan hivi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...