Mjini kumejaa wahuni na matapeli. Jamaa yangu alisingiziwa kumvunjia mtu iPhone 13 Pro Max

Mjini kumejaa wahuni na matapeli. Jamaa yangu alisingiziwa kumvunjia mtu iPhone 13 Pro Max

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
2,266
Reaction score
4,427
Siku moja jamaa yangu mmoja kutoka kijijini alinipigia simu akaniambia, "Kaka, nimefika mjini!" Nikamuuliza, "Umefika wapi?" Akasema, "Posta, daraja la Salender Bridge." Nikashangaa, maana sikuwahi kumwambia aje huko. Nikamuuliza tena, "Nani amekuambia ushuke huko?" Akajibu, "Konda wa daladala, aliniambia nishuke hapa ndo mjini kabisa!" Nikamwambia asisogee popote, nakuja.
Nilipofika, nikamkuta jamaa ameshikwa na watu watatu, mmoja akisema, "Huyu jamaa kanivunjia simu yangu iPhone 13 Pro Max, sasa anidai." Jamaa yangu alikuwa anatetemeka, hajui hata kilichotokea. Bahati nzuri niliwahi kabla hawajamchukua mbali. Nilivyoongea na wale jamaa, nikagundua ni wahuni wa kawaida wa mjini mtu anakushtaki kwa kitu ambacho hakijatokea, ili akuchune hela. Niliwatishia polisi, wakakata kona.

Jamaa yangu alibaki ameduwaa. Nikamwambia, "Mjini kuna wahuni, ukiingia bila maarifa, wanakutafuna mzima mzima!" Leo nimewaletea darasa la ukwl, ili msije mkaingia mjini mkadhani kila mtu ni mwema. Ukitaka kusurvive mjini, jifunze haya kabla hujajuta!

1. MATAPELI WANA MIKAKATI YA KUKUMALIZA
Matapeli wa mjini si watu wa mchezo. Wanavaa sura za watu wema, wanakukaribisha kwa upole, lakn wanalenga mfuko wako. Hawa watu wako kila sehemu kwenye daladala, kwenye ATM, kwenye mitaa yenye pilika nyingi, na hata mitandaoni.
Mfano,
Mtu anakufuata kwa stori tamu "Mzee, kuna mzigo wa viatu umetoka Dubai, tunauza bei ya hasara, 100,000 unapata pea tatu. Ila hela tunataka cash, hapa hapa." Ukiingia kichwa kichwa, unalizwa. Ukifika nyumbani, unafungua box, unakuta viatu ni vya plastic, havifai hata kwa mtoto wa chekechea.

Usiamini dili za haraka haraka. Mjini hakuna cha bure wala cha bei rahisi bila sababu. Think twice!

2. WAHUNI WA USAFIRI DALADALA, BODABODA, BAJAJI
Hapa ndipo akili zako zinapimwa. Konda wa daladala anajua sana kucheza na akili za abiria. Bajaji na bodaboda wanajua mchezo wa bei.
Unapanda daladala, unampa hela, konda anasema "sina chenji, shuka kituo kinachofuata uchukue." Ukishuka, daladala inapaa kama F-16, huku umepigwa mizinga ya chenji yako.
Au unapanda bodaboda, unamuuliza, "Mzee, ni shilingi ngapi mpaka Kariakoo?" Anakujibu, "Ni elfu mbili tu, kaka." Mkifika, anakwambia, "Aisee, ulivyosema Kariakoo nilidhani unapanda mtu mmoja, kumbe na mzigo! Hii sasa ni elfu tano."

Mjini, kabla hujapanda usafiri, hakikisha unajua bei sahihi. Pia, ukitoa hela kubwa, usubiri chenji yako kabla hujasogea!

3. WAHUNI WA MIKOPO WEWE NDIO MDHAMINI USIYETEGEMEA

Hili ni janga kubwa. Kuna watu wanakutumia kama mdhamini pasipo hata kukujulisha.
Unakutana na mshikaji wa zamani anakwambia, "Dah, kaka nipo kwenye shida, naomba nishike pesa kidogo kwa simu yako, nipe namba ya akaunti yako niweke hela halafu nikitoa nakuachia elfu kumi yako." Ukiingia mkenge, kesho unakuta umedaiwa mkopo wa milioni mbili, huku huelewi hata hela ilivyotoka.

Usikubali kushikilia pesa za mtu usiyemjua vizuri. Pia, usiwe mdhamini wa mkopo kama huna uhakika na mtu huyo.

4. WAUZA BIASHARA ZA UONGO UNAUZIWA HEWA
Mjini kuna watu wanaweza kukuuzia hata jengo la NMB ukikosa akili timamu. Wengine wanakupa bidhaa bandia kwa bei ya OG
Mfano:
Unanunua "iPhone mpya" kwa bei ya ofa. Ukifika nyumbani unafungua box, unakuta ndani ni mawe au kifaa cha kuchezea watoto.
Au wale wanaokupa "perfume original" kutoka Paris, unafungua baada ya siku mbili, inageuka kuwa maji ya kuoshea vyombo.

Nunua bidhaa kwenye maduka halali, siyo kwa watu wa vichochoroni au mitaani.

5. WAHUNI WA MITANDAO: UNAPOKEA SIMU UKAPOTEZA HELA
Hawa ni wa kisasa. Wanakupigia simu, wakijifanya ni huduma kwa wateja wa benki au mitandao ya simu, ili wakuibie.
Unapokea simu: "Habari kaka, mimi ni mfanyakazi wa Vodacom, tunafanya uhakiki wa akaunti yako. Tafadhali nisaidie kutoa PIN yako ili tukamilishe mchakato." Ukijibu, dakika tano baadaye unakuta akaunti yako imelambwa.

Benki au mitandao ya simu haikupi simu kukuomba PIN. Ukiombwa taarifa zako binafsi, jua umekutana na tapeli.

6. WAHUNI WA RAMANI: WANAKUONGOZA KWA HASARA
Hawa ni wale jamaa waliopo kwenye kona za mitaa, kazi yao ni kuwapoteza wageni kwa makusudi ili wawapige mizinga.

Unamwuliza mtu, "Mzee, njia ya kwenda Ubungo Terminal ni ipi?" Anakujibu, "Acha nikusindikize, mi ni mkazi wa hapa." Ukienda naye, anakufikisha sehemu tofauti na anakwambia, "Hapa ndo karibu, lakini kuna tozo ya kufika huku. Lipa elfu tano tu!"

Tumia Google Maps au uliza polisi au wenye maduka makubwa. Usimuamini kila mtu wa barabarani!

Mwisho:
Mji siyo sehemu ya watu wapole na waaminifu tu. Kama una tabia ya kuamini kila mtu, basi pole. Wanaokutana na wahuni wa mjini bila elimu hii wanajuta vibaya.
Leo umepewa darasa, ukilizwa tena, ujue ulitaka mwenyewe! Kama una jamaa anapanga kuja mjini, mshirikishe huu uzi, usimwache apotee.

Je, wewe umewahi kukutana na wahuni wa mjini?
 
Mjini kuna watu wanaweza kukuuzia hata jengo la NMB ukikosa akili timamu.
Hii hatari sana, nimekumbuka habari ya huyu jamaa hapa kwa video: Scammer Sold FAKE Airport for $242,000,000
1742537563426.png


View: https://www.youtube.com/watch?v=3RG7gfIur5M
 
Back
Top Bottom