warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,213
- 18,466
Yamenikuta, nani anaukumbuka huu wimbo?
Nimeingia saluni kutengeneza nywele , si
unajua kuweka blaki .Basi nimeingia saluni ,
kwanza mambo siyo kama enzi zilee,
nimepokelewa na wadada wawili wamevaa
suruali zimebana hao, sijui walizivaaje ,
masikioni wana hedfoni mdomoni chingam .
Karibu mzee , karibu kiti Haya mapya, enzi
zile vinyozi wote walikuwa wababa tu hukuti
mdada kwa kinyozi, kwanza tulikuwa
hatusemi tunaenda saluni , tulikuwa tunaenda
kwa kinyozi; bei zimeandikwa, kwenye kibao
wazi, kunyoa kipara 500/, Amigo 700/,
Madilu 800/.
Sasa mambo tofauti kabisa , saluni ina TV,
muziki toka kwenye sabufa , wadada kibao,
viti vya makochi dah . Haya nikakaa kwenye
kochi la kifahari , mdada mwenye suruali
imebana akaja, Unanyoa nywele ? Nikasema
hapana napaka rangi tu .
Kanishikashika kichwa na masikio
akaniambia , ingekuwa vizuri upunguze kidogo
ndiyo rangi itapendeza, mtu ukishikwa
masikio akili inasimama , bila kufikiri nikajibu
ndiyo.
Akaitwa mkaka mmoja akachukua mashine
na kuanza kupunguza nywele zangu, naye
akauliza , Vipi mustach ? Itafaa upunguzwe
kidogo Nikajibu sawa na kwa kweli niliwasifu
hawa vijana wanajali mteja .
Baada ya mkaka kupunguza nywele na
mustach , akaja mdada mwingine naye kavaa
kisuruali cha kubana, mkononi kashika
kibakuli cha rangi ya nywele , akaanza
taratibu kunipaka kwa uangalifu sana, huku
ananiongelesha kwa sauti yenye mvuto, vipi
skrab?
Nikamuuliza ndo nini? Akaniambia ni
kusafisha uso, na itakuwa vizuri kama nifanye
na skrab maana nitapendeza , tena akausifu
uso wangu kuwa hauna vichunusi , nikakubali
skrab, ilikuwa pia nataka kujua ndiyo nini.
Nikaamia chumba kingine kuoshwa nywele ,
nikakuta mdada mwingine kaniambia nivue
shati, nywele zikaoshwa vizuri, wakawa
wadada wawili mwingine kaanza kunipaka
mafuta ya nywele kisha nikaanza kusafishwa
uso na maji ya moto , ikaanza hiyo skrabu.
Nikaanza kufikiria kuwa nilitoka kwangu kuja
hapa kupaka rangi nywele tu , hawa watoto
wamenipenda wamenipunguza nywele na
mustach , wamenifanyia skrab, hapa ndio pa
kuja kila wikiendi. Hatimae nikaambiwa
tayari, nilipojiangalia kwenye kioo nimekuwa
mpyaaa , nikauliza bei , naambia elfu ishirini
na tano!
Akili ikasimama kwa sekunde, kidogo nizimie .
Nikaja juu, Kupaka rangi nywele shilingi alfu
ishirini na tano toka lini ? Mzee si umenyoa
nywele , mustach , umefanya scrab , umesema
tukupake mafuta yale expensive jumla ndio
hiyo mzee .
Mfukoni nilikuwa na hizo hizo ambazo
zilikuwa bajeti ya usafiri wa kwenda kazini
wiki nzima . Nikazitoa na kukumbuka neno
nililiona limeandikwa kwenye gari
fulani .Mjini cha bure salamu tu !