Mjihadhari na huyu tapeli wa JF

Nimesoma mkuu kila kitu! Mi nimestik hapo kwanza...

Na mbaya zaidi wewe nimeona ndie ulieanza kumwita mwenzio tapeli... bila ya kupima kama jamaa nayeye ana imani kiasi gani kwako... ulikurupuka
Huenda alikua muoga hata hiyo nauli kutuma.
Kuana vitu hutakiwi kujihusisha kabisaa kama huna imani.

Yeye ndo mtakaji halafu anataka kuaminiwa dah.
 
Hivi na yeye angetuma hao Vifaranga sijui 100 kwako wewe ambae hakujui, usingeweza na wewe kumtapeli??
Mkuu....
Kwenye mazungumzo ya sim tulikubaliana kwamba atamkabidhi msafirishaji anae mfaham, kisha baada ya kuuona mzigo nilipaswa kutoa cash kabla sijauchukua
 
Hivi unatumaje nauli kwa mtu usiemjua?

Hivi inawezekana kweli kutuma mzigo bila hata advance yeyote?

Hivi hapo ni nani alitakiwa kua na khofu ya kupoteza anaetaka mzigo au mwenye mzigo?
 
Mwandiko wake tu unajua hamnazo
Ila siamini kama kweli mtu unaweza kufanya kitu serious humu na mtu usiemjua, wakati tunatumia majina fake na avatar fake
Wacha muingizwe mjini tu
Teh teh
 
Huenda alikua muoga hata hiyo nauli kutuma.
Kuana vitu hutakiwi kujihusisha kabisaa kama huna imani.

Yeye ndo mtakaji halafu anataka kuaminiwa dah.

Izi mambo kwa kweli zinahitaji uwe na imani haijalishi ww ni mnunuzi au mnunuaji, pengine jamaa wa watu nae alihisi kwamba mwana bodi hapa anataka amtapeli kwa 17 ndio maana akaomba na yeye alipe ya kuku 20 au 10
 
Mimi Jiwedogo ndo na mlaumu si huyu.
Ukiingia vibaya lazima utapeliwe katuma nauli kwa uhakikagani wa kuletewa mzigo hapo tu kanikera?
 
Kweli kabisa...
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
Nimetoa tahadhari tu mkuu, kwani sioni ubaya kuwatahadharisha wengi kupitia mimi
Pole sana, tushamjuwa huyo, maana sisi tumo huko huko kwenye ufugaji, ngoja tumtangaze aisumize wengine...
Zuzu tu hilo, halijajuwa bahatai yake, lingeweza tengeneza pesa ya ukweli..
 
Ni sa hihi.
Jamaa hajataka hata kujua mzigo wake utafikia wapi hadi alipie hiyo nauli kakurupushwa tu akatuma nauli kakosea
 
Ujue ni ujinga tu na upumbaf wa watu wachache kuwaharibia wengi...siku izi mambo kidigital just mawasiliano then mzigo unakufikia sema kupitia expansion joint huo wengne wanapiga deal.....mtu nipo Tanzania naagiza simu ya Lenovo naipata sembuse vifaranga, akichomwa moto huyo akili itamkaa sawa huko atakapokuwa anaishi kiroho.
 
Mimi Jiwedogo ndo na mlaumu si huyu.
Ukiingia vibaya lazima utapeliwe katuma nauli kwa uhakikagani wa kuletewa mzigo hapo tu kanikera?
Ruhsa kunilaumu mkuu, na ninapo kosea sioni ubaya kukubali kosa.
Kikubwa hapa nimeleta tahadhari ili nawengine wasikosee kama mimi
 
Izi mambo kwa kweli zinahitaji uwe na imani haijalishi ww ni mnunuzi au mnunuaji, pengine jamaa wa watu nae alihisi kwamba mwana bodi hapa anataka amtapeli kwa 17 ndio maana akaomba na yeye alipe ya kuku 20 au 10
Inawezekana mkuu
 
Ruhsa kunilaumu mkuu, na ninapo kosea sioni ubaya kukubali kosa.
Kikubwa hapa nimeleta tahadhari ili nawengine wasikosee kama mimi
Nimekusoma mkuu.

Kuna swali nilikuuliza huko juu hujajibu ila lipo nje ya mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…