Mji Wa Kigamboni Warejeshwa Temeke

Mji Wa Kigamboni Warejeshwa Temeke

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,425
Reaction score
3,300
Baada ya malalamiko ya Wananchi na Madiwani pamoja na Wadau mbalimbali hatimae Serikali kwa kupitia kwa Waziri wake Anna Tibaijuka imeurudisha mji wa Kigamboni Chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke.
Ametoa ufafanuzi ya kuwa kitengo cha kuuboresha mji huo kitabaki kikijitegemea ila shughuli nyingine zitakuwa chini ya mkuu wa Wilaya kama mwanzo.

Huu utaratibu wa serikali kujiamulia mambo yake kienyeji bila kushirikisha washikadau wakubwa ambao ni Wananchi si mzuri umepitwa na wakati na zaidi huchochea Vurugu.
Chanzo. StarTv
 
ha ha ha ha serikali itajitekenya na kucheka yenyewe hakuna aliyejuu ya sheria Mtwara hoyeeeeeeeeeee wakikumbuka tuu nguvu ya wananchi wa Mtwara inabidi lugha zibadirike na ziwe lugha za upole tuliuliza hapa Proffessor amepata wapi nguvu ya kuamua hata bila bunge kupitia hiyo sheria
 
Kumbe nguvu ya Umma ina nguvu sana
 
Kiukweli kabisa, siasa wanayotaka kuileta Kigamboni itakuja kuiangamiza serikali ya Dar, hasa viongozi wanaofikiria kuwa wananchi si lolote si chochote katika maamuzi, suala la hili eneo limekuwa mtambuka baada ya kuanza kukuwa kiuchumi na kupendeza kimiundombinu, sasa kila mwenye mamlaka yake anataka kufanya ndio kichaka cha kujinufaisha, kwa karne hii sisi wananchi tumechoka sana, wao waendelee tu kutuburuza ila mwisho wa matamanio ya nafsi zao itageuka majuto na vilio visivyo na mwisho! Wawaulize waarabu wana taarifa ya nguvu za wananchi!
 
Baada ya malalamiko ya Wananchi na Madiwani pamoja na Wadau mbalimbali hatimae Serikali kwa kupitia kwa Waziri wake Anna Tibaijuka imeurudisha mji wa Kigamboni Chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke.
Ametoa ufafanuzi ya kuwa kitengo cha kuuboresha mji huo kitabaki kikijitegemea ila shughuli nyingine zitakuwa chini ya mkuu wa Wilaya kama mwanzo.

Huu utaratibu wa serikali kujiamulia mambo yake kienyeji bila kushirikisha washikadau wakubwa ambao ni Wananchi si mzuri umepitwa na wakati na zaidi huchochea Vurugu.
Chanzo. StarTv

It doesnt matter. Whether Kigamboni ipo temeke, mbagala, ilala, keko or Lindi region, we dont care. Haituhusu. Tunachotaka kuona sisi ni maendeleo. Mji safi, barabara, hospitali, umeme, masoko ya kisasa, shule za sekondari, vyuo nk. nk.
 
Wanaogopa kilichowapata viongozi wenzao kule Mtwara
 
Walikuwa wanauandaa mgogoro pengine zaidi ya ule wa Mtwara.
 
It doesnt matter. Whether Kigamboni ipo temeke, mbagala, ilala, keko or Lindi region, we dont care. Haituhusu. Tunachotaka kuona sisi ni maendeleo. Mji safi, barabara, hospitali, umeme, masoko ya kisasa, shule za sekondari, vyuo nk. nk.

yote hayo yatafanikiwa kwa kuwashirikisha wananchi.
 
It doesnt matter. Whether Kigamboni ipo temeke, mbagala, ilala, keko or Lindi region, we dont care. Haituhusu. Tunachotaka kuona sisi ni maendeleo. Mji safi, barabara, hospitali, umeme, masoko ya kisasa, shule za sekondari, vyuo nk. nk.

Kwa hiyo ushirikishwaji wa wananchi si muhimu.
Kumbuka CDA PALE Dodoma na sakata la kuuza Loliondo achilia mbali hiyo migodi ambavyo haisaidii hayo maendeleo. Tuliwaachia wakashindwa sasa ni zamu ya wananchi kuwapangia nini cha kufanya.
 
Hilo ni la Tibaijuka na madiwani, siyo la wananchi. Madiwani ndio waliodhurika kwa Kigamboni kutolewa Temeke, siyo wananchi. Amegundua bado anawahitaji ili ashirikiane nao kuendeleza utapeli, uongo na dhuluma zake. Kwa pamoja yeye na madiwani njaa wataendelea sasa na KDA.

Wananchi bado wanalilia hawakushirikishwa katika maamuzi ya mji mpya. Kule Mtwara wabunge na madiwani walipelekwa hadi ulaya (hongo), lakini ilipofika zamu ya wananchi hata hao wabunge na madiwani hawakufaa kitu. Ndicho Tibaijuka anatakiwa kujifunza. Anapoteza muda na pesa za serikali bure, mwishoni atapata presha.

Hiyo KDA alianzisha kwa ridhaa ya nani? anaropoka sana kwamba wananchi walishirikiswa. Lini? Mwaka jana alipanga kufanya mikutano kila kata ikatangazwa hadi kwenye vyombo vya habari na tovuti ya wizara. Alipofanya mkutano wa kwanza tu na kuulizwa maswali magumu hakurudi tena na wala hakutoa taarifa kwamba hataendelea na mikutano yake. Badala yake akaanza kuwahonga baadhi ya madiwani na wenyeviti wa mitaa. Hivyo anafanya kazi nao na ndio wanaohalalisha utapeli na uongo wa Tibaijuka. Wanamchuna tu, wainga ndio waliwao!

Kwamba kila mwananchi atalipwa fidia stahiki. Fidia stahiki ni nini? Atalipa nini na kwa kipimo gani? Atalipa kuanzia 2008, au analipa tu vinavyoonekana kwa macho wakati wa tathmini?

Tibaijuka kaingia makubaliano na wachina na waOman bila ridhaa ya wananchi. Aweke hayo mawasiliano yake yote na Wawekezaji (wote, waliokubali kuwekeza na waliokataa) hadharani ili wananchi wayajadili. Amehongwa bei gani na hao wachina na waarabu hadi akawakubalia wao ndio wawekezaji wa Kigamboni? Maafisa wake wamehongwa bei gani?
 
It doesnt matter. Whether Kigamboni ipo temeke, mbagala, ilala, keko or Lindi region, we dont care. Haituhusu. Tunachotaka kuona sisi ni maendeleo. Mji safi, barabara, hospitali, umeme, masoko ya kisasa, shule za sekondari, vyuo nk. nk.
hahahaahahahh Mwanamalundi hhaahahahaha
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni la Tibaijuka na madiwani, siyo la wananchi. Madiwani ndio waliodhurika kwa Kigamboni kutolewa Temeke, siyo wananchi. Amegundua bado anawahitaji ili ashirikiane nao kuendeleza utapeli, uongo na dhuluma zake. Kwa pamoja yeye na madiwani njaa wataendelea sasa na KDA.

Wananchi bado wanalilia hawakushirikishwa katika maamuzi ya mji mpya. Kule Mtwara wabunge na madiwani walipelekwa hadi ulaya (hongo), lakini ilipofika zamu ya wananchi hata hao wabunge na madiwani hawakufaa kitu. Ndicho Tibaijuka anatakiwa kujifunza. Anapoteza muda na pesa za serikali bure, mwishoni atapata presha.

Hiyo KDA alianzisha kwa ridhaa ya nani? anaropoka sana kwamba wananchi walishirikiswa. Lini? Mwaka jana alipanga kufanya mikutano kila kata ikatangazwa hadi kwenye vyombo vya habari na tovuti ya wizara. Alipofanya mkutano wa kwanza tu na kuulizwa maswali magumu hakurudi tena na wala hakutoa taarifa kwamba hataendelea na mikutano yake. Badala yake akaanza kuwahonga baadhi ya madiwani na wenyeviti wa mitaa. Hivyo anafanya kazi nao na ndio wanaohalalisha utapeli na uongo wa Tibaijuka. Wanamchuna tu, wainga ndio waliwao!

Kwamba kila mwananchi atalipwa fidia stahiki. Fidia stahiki ni nini? Atalipa nini na kwa kipimo gani? Atalipa kuanzia 2008, au analipa tu vinavyoonekana kwa macho wakati wa tathmini?

Tibaijuka kaingia makubaliano na wachina na waOman bila ridhaa ya wananchi. Aweke hayo mawasiliano yake yote na Wawekezaji (wote, waliokubali kuwekeza na waliokataa) hadharani ili wananchi wayajadili. Amehongwa bei gani na hao wachina na waarabu hadi akawakubalia wao ndio wawekezaji wa Kigamboni? Maafisa wake wamehongwa bei gani?
dawa nikuwachomea nyumba tu hamna lolote
 
Mji mpya wa wakazi wa Kigamboni ndio GESI yao hivyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kunufaika na mradi huo kupitia Manispaa ya Temeke.

Kuwapa Wakala (KIGAMBONI DEVELOPMENT AGENCY- KDA) nguvu kubwa kwenye mradi huo BADALA ya Manispaa ya Temeke ni sawa na kujenga kiwanda cha kusafisha GESI Kinyerezi - Dar esalaam badala ya Mtwara.

Temeke ni Wilaya iliyo nyuma kuliko zote Dar es salaam imesahaulika kama watu wa mtwara. Ni wakati wao kupata faida kupitia mradi wa Kigamboni.

Dar es salaam inataka kufaidika kwanza na GESI ya Mtwara kabla ya WanaMtwara. Wizara ya Ardhi inataka kufaidika kwanza na mradi wa Kigamboni kabla ya wanakigamboni kupitia Manispaa ya Temeke (madiwani wao).
 
Hii nchi siwaamini kabsa viongozi wetu,wamegeuka kuwa madalali na wafanyabishara wa ardhi yetu, wanalipa fidia halafu ardhi hiyohiyo wanaiuza kwa wageni thamani mara mia ya ile waliofidia.
 
Waende wakatafute eneo jingine si Kigamboni

Mkuu hawa viongozi wetu wakiona mnabana sana utasikia kigamboni inakuwa wilaya mpya. Chezea mafisadi uone ila Mtwara da wameamsha waliolala.
 
Back
Top Bottom