Mji umepoa sana, sababu ni nini?

Mji umepoa sana, sababu ni nini?

LiFe 2-point-0

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2024
Posts
4,253
Reaction score
11,621
Wakuu na wanabodi habari zenu!. Za masiku mengi?

Ni muda mrefu sana toka nimeondoka rasmi jijini Dar es salam, na japo huwa nakuja kuja one time huwa inakua ni kwa specific task so naonana na specific people at specific one area.

Huwa sipati muda wa kuzunguka sana ,then naondoka.
But this time imekua tofauti. Shughuli zangu zimenielekeza sana kutembelea ofisi kadhaa za binafsi na serikali zilizopo mjini kati, posta.

Haya maeneo nayajua sana maana since 12 years ago nikiwa naingia mjini hapa kama mwanafunzi wa IFM haya ndio yalikua maeneo yetu ya kuzurura kwakua chuo kiko centre kabisa.

Mbali na chuo, kaz yangu ya kwanza na ya pili nimefanya hapa hapa posta na kuzungukia maeneo ya jiran kama kariakoo na other areas around.
Moja ya vitu nilishavikariri ni u busy wa haya maeneo. Watu wengi. Na kubwa zaidi kwa wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari, haya maeneo huwa ni changamoto sana kwa habari ya parking hasa unapochelewa kuingia city centre.

Hali niliokuana nayo hizi siku nimekua around hapa ni experience ya tofauti sanaa.
Mji umepwayaa, watu si wengi kama nilivyokua na ile picha ya posta tokea naijua.

Nimeingia saa 3 asubuh lakin parking lots zipo za kutoshaa kama zoote, koote huku kuanzia samora street, billicanas ya zaman , maeneo ya rita yan parking zipo kama zoote.

Hiki kitu sikuzoea namna hii.
Ikabidi niongee na jamaa mmoja mahala nilipokua ofisin kwake ,nikauliza kuhusu hii hali, akanambia mambo yamekua machache sasa hiv posta. Hata biashara pia zimeshuka sana kwa wauzaji wa bidhaa mbali mbali labda vyakula. Maofisi pia mengi yamehama.

Hata wenye ofis zao mjini siku hiz wanachelewa kuingia maana bussiness ime drop mnoo.

Basi nikakubali kuwa hakika mambo yame change.

Anyways, ndio maisha. Acha nimalize ishu zangu nirudi mkoa.
Kila lakheri wakuu
 
Jibu ni moja tu bro.

Mji umetanuka.
Posta zimesalia taasisi na ofisi za Serikali. Na Kuna huduma utaambiwa uende ofisi kuu Dodoma.

Na hivi Private zina branches nying pembezoni.
Hasa hasa Kinondoni, Mikocheni na Kijitonyama.

Kwahiyo watu weng shida za kiofisi wanamalizia nje ya Posta. Unless ni serikali. Na Serikal shida nyingne wanamalizia Dodoma.
 
Inawezekana chief. Kumepooza sana
 
Write your reply...shughuli za serikali nyingi zimehamia dodoma pia mambo ya online na brunch nyingi za taasisi zilizokua posta sasa zinapatika kwenye kiganya na mawilayani
 
Waliokua wanatishia kuandamana wamekimbilia vijijini kwao kujificha hadi tarehe ipite.
 
Write your reply...shughuli za serikali nyingi zimehamia dodoma pia mambo ya online na brunch nyingi za taasisi zilizokua posta sasa zinapatika kwenye kiganya na mawilayani
Hii ina make sense. Ndio maana SGR iko full booked 24/7 watu wanakwemda sana na kurud toka dodoma. Kuna jamaa kanambia jana kuwa Dom kwasasa hata mzunguko wa pesa upo, sina uhakika though
 
Askari ndio watafanya miji kukimbiwa hata na wapiga kura wasiotaka vurugu
You are right. Nimewasikia wengi wakisema hawataki tar 29 iwakute Dar. Sasa najiuliza mtu umejiandiksha Dar halaf hutaki siku ikikute Dar, nani ata vote? Au ndio connection ya CCM+NIDA×NEC 😂
 
wasije wakambebesha Lissu wa watu mikesi mingi baba wa watu kumbe maandamano si ya chama chake.
Hawana akili wala utu, kipimo mambo ya kipuuzi wanayofanya. Ila safari hii wataonja joto la jiwe kutoka kwa wananchi. Nakuambia mwaka huu hakuna uchaguzi.. Na wote wanapaswa kufungwa waliongiza inchi kwenye hasara kubwa namna hii ya uchaguzi
 
Natamani sana iwe hivi ila nasita but ikitokea nadhan nitakua na furaha sanA
 
Back
Top Bottom