Mjema: Maendeleo yote nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM anayesimamia Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Ndugu Sophia Edward Mjema amesema Serikali ya Tanzania inayoongozwa na CCM imefanya makubwa sana na kwamba maendeleo yote yanayoonekana kwasasa kwenye Taifa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mjema amezungumza hayo leo Alhamisi tarehe 15 Juni, 2023 kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

"Maendeleo yote ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, llani inatekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan." Alisema.

"Tusibabaishwe na yeyote, tuendelee kumpongeza na kuunga mkono juhudi kubwa za Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania na Taifa kwa ujumla." Alisisitiza Mwenezi Mjema.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Godfrey Chongolo leo ameanza ziara ya takribani siku 8 mkoani Dodoma ambapo ameambatana na Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi pamoja na Katibu wa Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi Gavu.

Ziara yao imeanzia wilaya ya Mpwapwa ambapo ina majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Mpwapwa mjini pamoja na Kibakwe.

Ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo wa CCM mkoani Dodoma pamoja na mambo mengine imelenga kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho, kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina ikiwemo kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

IMG-20230615-WA0045.jpg
IMG-20230615-WA0049.jpg
IMG-20230615-WA0048.jpg
FB_IMG_1686817735233.jpg
 
Back
Top Bottom