Mjane...

Wanawake wengi hata kama hawataki ..wanaujua ukweli kuwa ni nadra sana kwa mwanaume aliyefiwa na mke kubaki mjane

Wanawake wengi huwa hawapendi kuolewa tena na mifano imejaa tele hata mkijaribu kufikiria wanawake wajane walioolewa mtaona idadi ni ndogo sana.QUOTE]

Hiyo bold una full support from Chris. Jitahidi usife kabla ya mumeo, lazima atavuta chombo kipya ndani.

Hiyo red umechemka. Njoo mitaa ya kwetu nikuonyeshe wajane wawili watatu ufanye utafiti upya.

WAWILI WA TATU BADO INABAKIA NI IDADI NDOGO vinginevyo nionyeshe nimechemka kivipi.
Hiyo bold ndugu yangu hakuna kujitahidi..... ukiitwa unaitika tu hata kama hutaki.
 
nikifa leo. aoe tu ila asubiri watoto wakue angalau kidogo, sio vitoto viduchu hata kabla havija changanyikiwa vizuri na msiba wa mama yao avichanganye zaidi kwa kuleta mama wa kambo!
akifa yeye leo mimi siolewi, nasubiri kwanza mpaka watoto wakikua,
 
Hahaha! Akifa muzee yako usisahau kuniPM. Napenda sana wajane.
 
Hahaha! Akifa muzee yako usisahau kuniPM. Napenda sana wajane.

Bila kujali ugonjwa? unatutisha mpwa..unajua tunakutegemea sana hapa wewe umeoa wanawake 2/5 humu jamvini tuta waacomodate vp???
 
Bila kujali ugonjwa? unatutisha mpwa..unajua tunakutegemea sana hapa wewe umeoa wanawake 2/5 humu jamvini tuta waacomodate vp???

Hahaha! Binamu bana. Hata Jizaz si alisema tuwasaidie wajane? Ugonjwa nao ni issue. Na prefer zaidi wajane wa mihanga ya ajali. Hahaha!

Lol! Hiyo red hiyo! Mpwa umenipandisha chati kinoma. Wananipendaga wenyewe bana. Sa mi nifanyeje?
 
Nasikia kuna wanawake wa kabila fulani hapa Tz huwa wanajisababishia ujane ili waweze ku-qualify kwa miradi ya pesa inayohusu wajane!

Na wengine, kabila hiyohiyo, hujisababishia ujane ili warithi mali ya marehemu, watanulie na 'serengeti boys' ambazo wanazibadilisha wanavyotaka. Hao utasikia wanajitapa mume kafa lakini sijaolewa, kumbe wanajipoza na serengeti boys.
 
Hahaha! Binamu bana. Hata Jizaz si alisema tuwasaidie wajane? Ugonjwa nao ni issue. Na prefer zaidi wajane wa mihanga ya ajali. Hahaha!

Lol! Hiyo red hiyo! Mpwa umenipandisha chati kinoma. Wananipendaga wenyewe bana. Sa mi nifanyeje?

Shauri ya AVATAR yako they like people who athletics on the bed...who take busines serious!
 
...inaonekana wengi wenu mnasubiria kwa hamu 'mpaka kifo kitapowatenganisha', Interesting!

Kuna rafiki yangu alifariki November mwaka jana, ameacha mjane na mabinti wadogo wawili. Kuna jamaa aliyekuwa heshi kujipitisha pitisha nyumbani kwao, (japo marehemu alikuwa hawivi nae kihivyo huyo jamaa) ndio yumo mbioni kumuoa huyo mjane...

Binafsi roho haipendi ila ndio hivyo tena, heri yake (*bi mjane) akistirika kuliko kuonekana anahaha,...

kuolewa majaaliwa.
 
Wanawake wengi wanaweza kukaa muda mrefu baada ya kufiwa na ndipo wakaamua kuolewa, na wengine wanaweza wasiolewe kabisa. Lakini yote haya yanategemea hali ya uchumi ya huyo mama, baba wa familia kabla hajafa je aliacha uchumi imara wa familia? je, ndugu wa mume wanaingilia namna ya ku-run mali alizoacha marehemu? na pia je mjane ana mahusiano mazuri ama mabaya na ndugu wa marehemu mume wake?

Pia umri wa mjane inaweza kuwa factor kubwa sana, suppose kama hajafikisha miaka 30? Wengi wakifiwa wakiwa na umri mdogo hutamani kuolewa tena, na wengi wakiwafiwa wakiwa na umri mkubwa huamua kubaki single na kuamua kumegwa kisiri siri pale anapohitahitaji huduma.

Kwa upande wa wanaume, wengi huoa haraka/mapema mara baada ya kufiwa, nadhani hili halina uhusiano na mambo ya kumega, bali ni swala zima kwamba nyumba ni mke. Nyumba anayoisha mwanaume single haiwezi ikawa as neat as nyumba inayokaliwa na wana ndoa. Na pia haiwezi kuwa organised (mpangilio wa vitu ndani ya nyumba) na ratiba ya milo inayoeleweka. Akina baba wa kibantu, tumezowea kupikiwa, kufuliwa na wakati mwingine kulelewa kama watoto wadogo.

Mke akifariki, nyumba lazima ikumbwe na matatizo ya usafi, hata kama familia ina msichana wa kazi lakini hawezi kuwajibika ipasavyo ikilinganishwa na mama mwenye nyumba anapokuwepo.

Personally siwezi kumpangia aolewe lini in case ikitokea nimefariki, hayo ni maamuzi yake, maana inawezekana anaweza kuwa anamegwa hata ukiwa hai, sasa je ukifa si ndio atamegwa vizuri tena kwa nafasi. Muhimu ni kwamba ahakikishe anatunza watoto kama tutakuwa tumejaaliwa kuwa na watoto, maana wengine wakioa/olewa wanasahau watoto kabisa.
 
Kuna rafiki yangu alifariki November mwaka jana, ameacha mjane na mabinti wadogo wawili. Kuna jamaa aliyekuwa heshi kujipitisha pitisha nyumbani kwao, (japo marehemu alikuwa hawivi nae kihivyo huyo jamaa) ndio yumo mbioni kumuoa huyo mjane...

Hii scenario inatia mashaka sana kwamba inawezeka marehemu alikuwa anajua kilichokuwa kinaendelea gizani kati ya huyo bwana harusi mtarajiwa na mjane.
 
Naomba kuuliza kitu......
Inakuwaje mnafikiria kuwa mwanaume tu ndio anaacha mali? au kwamba mwanaume akifa basi assumption ni kuwa mali iliyopo ilikuwa yake.Hamjui kuna wanawake wana mali zao?
 
...kinachosumbua kwenye hizi jamii zetu za kiafrika ni midomo ya watu bana.

Huenda hata jamaa alikuwa si mbaya kihivyo kwa marehemu lakini madhali hawakuwa wakiwiva sana, bi mjane atasingiziwa alikuwa keshabaini nia ya jamaa tangu awali...

Namhurumia sana bi mjane kwa hili, lakini kama nilivyosema... Madhali mfiwa kaachwa na watoto wadogo, naye ndio kwanza hata 30yrs hajavukka si vibaya kuolewa mapema, na kama majaaliwa yake ndio huyo jamaa, hata kama palitokea dosari wakati wa uhai wa mumewe... ndio imetoka hivyo.

Najaribu kui picture scenario ambapo mke anafariki halafu mume bila kukawia anamuoa shoga-besti wa marehemu... lazima kina mama waje juu!
 
Naomba kuuliza kitu......
Inakuwaje mnafikiria kuwa mwanaume tu ndio anaacha mali? au kwamba mwanaume akifa basi assumption ni kuwa mali iliyopo ilikuwa yake.Hamjui kuna wanawake wana mali zao?

Ni mapokeo ya mfumo dume ....

Ulishawahi kusikia mke kafa halafu kukawa na mgogoro wa mirathi? Hata kama bread winner wa familia alikuwa ni Mama, huwezi kusikia kuna kasheshe ya kugawana mali ama ndugu wa mke wakija kudai kwamba mali iliyopo ni jasho ya ndugu yao.
 
Back
Top Bottom