Yahya Mohamed
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 270
- 317
Safari kuelekea umoja wa vyama vya siasa vya upinzani kwa masilahi ya umma bado ni ndefu. Nini mtazamo wenu wanaJF na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwa vyama vya upinzani nchini.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki mzuri sana wiki iliyopita.
Hivyo vyama vingine sijui ni vyama vya upinzani au ndo kuganga njaa badala ya kupingana na chama tawala wao wanapingana na chama cha upinzani hapo hakuna haja ya kuwa na umoja na chama kinacho pinga mpinzani na kuacha chama tawala kikineemeka.
hivi huwa ni CHADEMA kinapingana na vyama vya upinzani au ni vyama vya upinzani ndio vinaipinga CHADEMA? nadhani pamoja na ushabiki ni bora pia tungeangalia na mwenendo wa CDM kwani haiwezekani leo hii akina mdee wapande jukwaani kuanza kuwatukana akina mbatia kesho tuamke tuseme NCCR wana matatizo, nadhani kuna tatizo la msingi halijadiliwi maana mtu kama slaa anaposhindwa kumkemea mgombea ubunge wa chama chake anapotoa matusi mbele yake nani ataweza? hata kama hakuna haja ya kuungana kwa sasa lakini heshima ya CDM mbele ya wapiga kura na mbele ya vyama vingine lazima iwe ajenda ya muhimu.
Umesomeka mkuu. nadhani katika kujadili waliotoa matusi vile vile tusisahau wastaafu wetu pale Jangwani.hivi huwa ni CHADEMA kinapingana na vyama vya upinzani au ni vyama vya upinzani ndio vinaipinga CHADEMA? nadhani pamoja na ushabiki ni bora pia tungeangalia na mwenendo wa CDM kwani haiwezekani leo hii akina mdee wapande jukwaani kuanza kuwatukana akina mbatia kesho tuamke tuseme NCCR wana matatizo, nadhani kuna tatizo la msingi halijadiliwi maana mtu kama slaa anaposhindwa kumkemea mgombea ubunge wa chama chake anapotoa matusi mbele yake nani ataweza? hata kama hakuna haja ya kuungana kwa sasa lakini heshima ya CDM mbele ya wapiga kura na mbele ya vyama vingine lazima iwe ajenda ya muhimu.
Yahaya umemtafuta Mbowe amekataa kuja ingekuwa vizuri kama ungempata Mbowe