Mjadala wa Umoja wa Upinzani StarTV Dec 5, 2010

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Safari kuelekea umoja wa vyama vya siasa vya upinzani kwa masilahi ya umma bado ni ndefu. Nini mtazamo wenu wanaJF na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwa vyama vya upinzani nchini.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki mzuri sana wiki iliyopita.
 
Yahya asante kwa taarifa hii.

Nadhani inatupasa tukubali kwamba uwezekano wa vyama vya siasa hususani upinzani kwa Tz haiwezekani kutokana na matakwa ya sheria za msajili wa vyama na hila za chama tawala. Wakati mwingine tukubali kwamba jeshi dogo lenye ufanisi linafaa kuliko jeshi kubwa lisilo na ufanisi.
 
Muungano wa vyama vya upinzani ni jambo la kusahau kwa sasa. Ni zoezi lililoonekana kushindwa tangu awali. Vyama vitaungana bila kupenda ikiwa mazingira kama yaliyotokea uk yatajitokeza hapa
 
Safari kuelekea umoja wa vyama vya siasa vya upinzani kwa masilahi ya umma bado ni ndefu. Nini mtazamo wenu wanaJF na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwa vyama vya upinzani nchini.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki mzuri sana wiki iliyopita.

Yahya,

Wageni watakuwa kina nani?
 
Live calls zinaruhusiwa mzee Mwanakijiji ila vema kama unahitaji kupiga simu nikupe namba ucall mapema, maana unapowadia muda wa calls kwa ujumla line huwa tabu kupata
 
Yes Nicky
Tunategemea kuwa na MWEKWABE WAITARA - CHADEMA, JAMES MBATIA AMA DAVID KAFULILA - NCCR na Tunasubiri Conformation ya HAMAD RASHID - CUF
 
Inaonekena wengi wenu mnaamini muungano wa vyama vya upinzani ni kwa manufaa ya watz. Hatuoneshi ni kwa namna gani muungano huo unaleta tija kwa vyama husika na wananchi wote. Pia kutoungana hakijachambuliwa vema tija yake. Tuondokane na fikra za mkumbo, tuchambue manufaa na hasara za kunngana au kutoungana kwa vyama husika na kwa wananchi.
 
Gurudumu
Kama mada inavyosomeka nilitegemea uaanze kuonyesha njia sasa kwa kujenga hoja ambazo zitasaidia kutoa dira na si kupuuza mawazo mema ya waliotangulia hapo juu.
Lete hoja sasa ya msingi...kama mada inavyosomeka.
Thanks
 
Kutokana na mkanganyiko wa kiitikadi na matukio yaliyotekea hivi karibuni kikatiba kwa mfano chama kimoja kuwa kwenye serikali upande mmoja wa muungano ni vizuri chama kilichopata uwezo wa kuunda upinzani bungeni ki kanuni kikaendelea na mipango ya upinzani,hawatakuwa wa kwanza duniani ili kuepusha mipasho na manyanyaso kutoka kwa muungano wa upinzani
 
Mpaka sasa tulipo CDM ndicho chama cha upinzani
Hivyo vyama vingine sijui ni vyama vya upinzani au ndo kuganga njaa badala ya kupingana na chama tawala wao wanapingana na chama cha upinzani hapo hakuna haja ya kuwa na umoja na chama kinacho pinga mpinzani na kuacha chama tawala kikineemeka.
 
wapinzani waungane sasa ili kiwe nini? Tangu 1995 hawajaungana; hoja zitakazotolewa sasa zimetolewa tangu mwanzo wa upinzani. Muungano wa upinzani kwa ufupi hauwezekani, hauitajiki na kiakili kabisa hauna sababu; at least siyo kwa wapinzani walivyo sasa.
 
Kwani tanzania kuna vyama vingapi vya upinzani? Mi nakijua kimoja tu CHADEMA naomba mnisaidie nivijue vingine.
 
Yahaya umemtafuta Mbowe amekataa kuja ingekuwa vizuri kama ungempata Mbowe
 
Vingine huwa navisikia wakati wa uchaguzi tu, tena wakati mwingine dakika ya lala salama vina jitoa na kuunga mkono chama Tawala! Vyama vya namna hiyo huwezi kuviweka kundi moja na chama cha upinzani lazima kitawavuruga tu. Vyama hivyo vya msimu huwa ni makando kando ya chama tawala ili kuwachakachua kimawazo wapiga kura na kuchukua ruzuku ya kampeni. Kwa watu makini vyama vya namna hiyo ni kuvikwepa kama ukoma.
 
Hivyo vyama vingine sijui ni vyama vya upinzani au ndo kuganga njaa badala ya kupingana na chama tawala wao wanapingana na chama cha upinzani hapo hakuna haja ya kuwa na umoja na chama kinacho pinga mpinzani na kuacha chama tawala kikineemeka.

hivi huwa ni CHADEMA kinapingana na vyama vya upinzani au ni vyama vya upinzani ndio vinaipinga CHADEMA? nadhani pamoja na ushabiki ni bora pia tungeangalia na mwenendo wa CDM kwani haiwezekani leo hii akina mdee wapande jukwaani kuanza kuwatukana akina mbatia kesho tuamke tuseme NCCR wana matatizo, nadhani kuna tatizo la msingi halijadiliwi maana mtu kama slaa anaposhindwa kumkemea mgombea ubunge wa chama chake anapotoa matusi mbele yake nani ataweza? hata kama hakuna haja ya kuungana kwa sasa lakini heshima ya CDM mbele ya wapiga kura na mbele ya vyama vingine lazima iwe ajenda ya muhimu.
 
Mchango wako umepokelewa Mjepu

Umesomeka mkuu. nadhani katika kujadili waliotoa matusi vile vile tusisahau wastaafu wetu pale Jangwani.
 
Yahaya umemtafuta Mbowe amekataa kuja ingekuwa vizuri kama ungempata Mbowe

Hatukupenda kufanya Duplication ya ITV ila kwa kuwa mjadala bado utaendelea tutajitahidi katika wikiend zijazo kuwa nae katika Studio
Thanks kwa angalizo FROIDA
 
Back
Top Bottom