Mjadala wa Katibu mkuu mpya CHADEMA wateka nchi

Mjadala wa Katibu mkuu mpya CHADEMA wateka nchi

Ni ukweli uliodhahiri kwamba kwa sasa mjadala ulioteka kila kona ya nchi ni jina la Katibu mkuu mpya CHADEMA.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza jina la Katibu mkuu na hatimaye kupigiwa kura na Baraza Kuu.

Jumamosi ya wiki hii nchi inatarajiwa kutikisika kwa tukio linalosubiriwa na mamilioni ya wafuasi wa Chadema kote nchini ambapo kutokea jijini Mwanza moshi mweupe utaonekana pale Freeman Mbowe atakapoibua jina la Katibu Mkuu.

Shauku ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kikiwa na mashabiki kila kona ya nchi.

Pia sababu nyingine ni kutokana na mazingira aliyoacha Katibu mkuu wa zamani Wilbroad Slaa ya kususia uongozi baada ya kukosa fursa ya kugombea Urais.Ususiaji ambao unadaiwa ulisababishwa na mkewe Josephine Mushumbusi.

Pia chama hicho kinajaza nafasi hiyo huku kikiwa na hazina kubwa ya wanachama maarufu wakiwemo mawaziri wakuu wawili wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

Yote kwa yote Freeman Mbowe ndiye anatarajiwa kutegua kitendawili hiki huku wafuasi wake wakimpa jina la utani..' mzee wa kubadili gear angani..''

Tusuburi tuone...
Labda nchi ya moshi....! Kwanza Chadema si chama bali ni saccoss ya Lowasa na Mbowe....
 
mjadala umetekaje nchi, mim sijausikia kabisa asee, saiv nasikia mambo ya bei elekezi ya sukari, Magufuli kumtembelea Seif, hayo mengine ya Katibu ndio nimeyasikia kwako asee, ivi CHADEMA kumbe bado wapo? dah hii serikali itawapa shida sana kupata kiki
 
Alishinda Magufuli....kama mlishinda si mngeingia barabarani km mlivyokuwa mnadai mwanzo......
Ndio kilichowafanya mshindwe kuwachimbia Watanzania visima vya maji safi na salama mkaenda kuwaletea Magari ya Maji ya kuwasha ili muwaumize?
 
Mkuu Kimbunga habari za siku nyingi sana Sheikh. Usiyempenda kaja...Mnyika amepata ridhaa ya wananchi kwa miaka mingine Mitano...this time around I hope hutakuwa unampigia ramli ya kutorudi bungeni.

Anyway, tuyaache hayo yameshapita. Molemo sio Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kwahiyo humtendei haki kwa kujaribu kumpa majukumu yasiyo yake.
Lakini kwakuwa Mbowe ni Jemedari tunaamini kuwa atatuletea Katibu Mkuu ambaye ni Jemedari kama yeye.

Asante kamanda Maranya kwa kunisaidia.

Kimbunga hapa amedhihirisha mjadala kwa sasa ulioteka nchi ni Katibu mkuu mpya Chadema.Ndiyo maana yuko hapa akitia neno
 
mjadala umetekaje nchi, mim sijausikia kabisa asee, saiv nasikia mambo ya bei elekezi ya sukari, Magufuli kumtembelea Seif, hayo mengine ya Katibu ndio nimeyasikia kwako asee, ivi CHADEMA kumbe bado wapo? dah hii serikali itawapa shida sana kupata kiki
Kwahiyo unachosikia sasa hivi nimaigizo tu? Hapa tufanye ujasikia unaona kabisa mambo ya chadema no maigizo
 
Back
Top Bottom