Mjadala wa Katibu mkuu mpya CHADEMA wateka nchi

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,228
Ni ukweli uliodhahiri kwamba kwa sasa mjadala ulioteka kila kona ya nchi ni jina la Katibu mkuu mpya CHADEMA.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza jina la Katibu mkuu na hatimaye kupigiwa kura na Baraza Kuu.

Jumamosi ya wiki hii nchi inatarajiwa kutikisika kwa tukio linalosubiriwa na mamilioni ya wafuasi wa Chadema kote nchini ambapo kutokea jijini Mwanza moshi mweupe utaonekana pale Freeman Mbowe atakapoibua jina la Katibu Mkuu.

Shauku ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kikiwa na mashabiki kila kona ya nchi.

Pia sababu nyingine ni kutokana na mazingira aliyoacha Katibu mkuu wa zamani Wilbroad Slaa ya kususia uongozi baada ya kukosa fursa ya kugombea Urais.Ususiaji ambao unadaiwa ulisababishwa na mkewe Josephine Mushumbusi.

Pia chama hicho kinajaza nafasi hiyo huku kikiwa na hazina kubwa ya wanachama maarufu wakiwemo mawaziri wakuu wawili wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

Yote kwa yote Freeman Mbowe ndiye anatarajiwa kutegua kitendawili hiki huku wafuasi wake wakimpa jina la utani..' mzee wa kubadili gear angani..''

Tusuburi tuone...
 
Kumbe Marando alipona na akarudi nchini kutoka India! Maana nimesikia huenda akawa Katibu Mkuu.

Ila pia ilitajwa huenda Sumaye ndiye akawa Katibu Mkuu, na leo nimesikia Sumaye anataka kwenda kutibiwa India!
 
Ni ukweli uliodhahiri kwamba kwa sasa mjadala ulioteka kila kona ya nchi ni jina la Katibu mkuu mpya CHADEMA.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza jina la Katibu mkuu na hatimaye kupigiwa kura na Baraza Kuu.

Jumamosi ya wiki hii nchi inatarajiwa kutikisika kwa tukio linalosubiriwa na mamilioni ya wafuasi wa Chadema kote nchini ambapo kutokea jijini Mwanza moshi mweupe utaonekana pale Freeman Mbowe atakapoibua jina la Katibu Mkuu.

Shauku ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kikiwa na mashabiki kila kona ya nchi.

Pia sababu nyingine ni kutokana na mazingira aliyoacha Katibu mkuu wa zamani Wilbroad Slaa ya kususia uongozi baada ya kukosa fursa ya kugombea Urais.Ususiaji ambao unadaiwa ulisababishwa na mkewe Josephine Mushumbusi.

Pia chama hicho kinajaza nafasi hiyo huku kikiwa na hazina kubwa ya wanachama maarufu wakiwemo mawaziri wakuu wawili wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

Yote kwa yote Freeman Mbowe ndiye anatarajiwa kutegua kitendawili hiki huku wafuasi wake wakimpa jina la utani..' mzee wa kubadili gear angani..''

Tusuburi tuone...
mkuu Molemo salama lakini? Nilidhani unatupatia za ndani kumbe maneno matupu!

Au hiyo hazina ndio itatoa mmoja wao kuvivaa viatu ya Padre Dr. Slaa? Kila la kheri, hata ukiawa wewe nadhani una uzoefu mkubwa na ni hazina ya CDM hivyo unaweza pewa!
 
mkuu Molemo salama lakini? Nilidhani unatupatia za ndani kumbe maneno matupu! Au hiyo hazina ndio itatoa mmoja wao kuvivaa viatu ya Padre Dr. Slaa? Kila la kheri, hata ukiawa wewe nadhani una uzoefu mkubwa na ni hazina ya CDM hivyo unaweza pewa!
Nipo mkuu @Kimbunga.Tumsubiri Mwenyekiti kikatiba ndiye anapaswa kutangaza jina na siyo Molemo atangaze
 
Mkuu Kimbunga habari za siku nyingi sana Sheikh. Usiyempenda kaja...Mnyika amepata ridhaa ya wananchi kwa miaka mingine Mitano...this time around I hope hutakuwa unampigia ramli ya kutorudi bungeni.

Anyway, tuyaache hayo yameshapita. Molemo sio Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kwahiyo humtendei haki kwa kujaribu kumpa majukumu yasiyo yake.
Lakini kwakuwa Mbowe ni Jemedari tunaamini kuwa atatuletea Katibu Mkuu ambaye ni Jemedari kama yeye.

Back
Top Bottom